Iringa kwachafuka: FFU watumia mabomu, waandishi wapigwa mawe

Haya haya,
Niliyasema haya miaka mitatu tu iliyopita, kwa kwamba maadam unemploymment inazidi kuongeza na vijana wengi wanakosa kazi itafikia wakati vijaa hao watachukua sheria mikononi na sasa wakati umewadia. Jambo dogo sana linaweza kukuzwa na likaleta machafuko makubwa kwa sababu serikali haikujali kukuza uchumi kwa lengo la kupunguza umaskni. Na huwezi kupunguza umaskini kwa mikataba na sera za umalaya bila kufikiria kwanza AJIRA kwa wananchi wako...Huu ni mwanzo tu.
 
Kwa kweli dini hizi zinazoingia sasa hivi sichunguzwe maana inaonekana wengi wamegeuza ndio kichaka au sehemu ya kuficha mambo maovu mengi na kuwaibia wajane ,yatima kwa jina utoe ili ubarikiwe tofauti na madhebu makubwa kama catholic.anglikana,lutherana.morovian.na mengine ya siku nyingi
 
Mkandara,

..lakini hapo tatizo ni imani za KISHIRIKINA!!

..yaani miaka 50 baada ya uhuru mambo haya yanatokea Tanzania.

..kwa upande mmoja wananchi wanatatizo la kutokuwa na elimu na kuamini mambo ya kishirikina.

..kwa upande mwingine polisi nao hawaelewi kazi yao, tatizo la elimu tena, na wanatumia nguvu zilizopitiliza kiasi.
 
Mkandara,

..lakini hapo tatizo ni imani za KISHIRIKINA!!

..yaani miaka 50 baada ya uhuru mambo haya yanatokea Tanzania.

..kwa upande mmoja wananchi wanatatizo la kutokuwa na elimu na kuamini mambo ya kishirikina.

jamaniiii jeshi la polisi linafanya kazi yake,ingekuwa wewe ndio uko humo ungesema hivyo.tatizo dini imeaachwa hulia kila mtu anasajiri,inawezekana hata al shababu imesajiriwa na wizara ya mambo ya ndani.tuache vyombo Vya usalama vifanye kazi yake
 
DSCF1673.JPG
DSCF1667.JPG
DSCF1666.JPG
DSCF1681.JPG
DSCF1643.JPG
DSCF1652.JPG


VURUGU ZA WANANCHI IRINGA,ASKARI NA WAANDISHI WAJERUHIWA VIBAYA

Zaidi ya watu 10 wakiwemo askari wanne na wanahabari wamejeruhiwa huku baadhi yao wakitibiwa na kuruhusiwa na wengine kulazwa katika Hospital ya mkoa wa Iringa baada ya kuibuka kwa mapigano hayo kati ya polisi na wananchi ,mapigano ambayo yametokana na imani potofu za wananchi katika kuamini ushirikina.Wananchi hao zaidi ya 200 walivamia nyumba ya mzee wa kanisa moja la kilokole katika mji wa Iringa eneo la Frelimo jina limehifadhiwa kwa sababu za kimaadili

Hata hivyo pona ya wanahabari na polisi waliokuwa wamefungiwa ndani ya nyumba hiyo na kushambuliwa kwa mawe na kunusurika kuteketezwa kwa moto wakiwa ndani ya nyumba hiyo ilionekana baada ya askari polisi wa FFU kutumia mbinu kubwa ya kulazimika kutumia risasi ya moto kumshambulia mguuni mmoja kati ya watu wanaodaiwa kutaka kuongoza wengine kuichoma moto nyumba hiyo iliyokuwa na wahahabari ndani ,polisi na mchungaji mmoja.

Baadhi ya wananchi wamelipongeza jeshi la polisi mkoa wa Iringa kwa kuokoa maisha ya wanahabari hao na watu wengine zaidi ya 10 ambao walipaswa kuuwawa na wananchi hao .

Wananchi hao walionekana kuongezeka idadi baada ya FFU kuwatisha kwa mabomu ya machozi huku wakidai kuwa mabomu hayo hayaui na bila polisi kupata mbinu ya haraka ya kutumia risasi ya moto zaidi ya watu hao 10 wakiwemo wanahabari waliokuwa ndani ya nyumba hiyo wangekuwa wameuwawa na wananchi hao ambao waliondoa imani na kikosi hicho kuwa wamehusika kuificha misukule hiyo.

Hapa tulipofika siyo. Leo walelenga miguu kesho watalenga kifua. Huu ujinga kuna mtu ipo siku atatakiwa kujibia haya.
 
Ujinga ni mzigo mkubwa sana. Wameamua kuuana kwa imani za kishirikina!.
 
Kila sehemu na karaha zake. Iringa misukule, kwetu Tanga ushoga na uchawi wa kitabuni, hovyo kabisa
 
Bomu limeanza kulipuka kama Lowasa alivyo tabiri? Watu hawana kazi, they have nothing to loose
 
Iringa kumechafuka, kisa? misukule, Arusha kumechafuka kisa? Kiongozi amekataa dhamana, Mbeya kumechafuka kisa? Machinga Dar kumechafuka kisa? Mafuriko. mwe hizi ni dalili za kukata tamaa. Poleni Watanzania kazeni butu safari ndo kwanza inaanza baada ya miaka 50
 
Back
Top Bottom