Du, wanadamu tuna matatizo. Kanywea tena. Wakati Vita bado haijaanza. Usiombe majibu ya Israel. Hali itakuwa mbaya. Pray for peace. Tutaathirika wote
Wakati kajificha nyuma ya marekani na uingereza, France,Hadi Jordan kamsaidia kutungua drones...hao wabwekaji tu wakimtegemea USA
 
Hayo yaliyopenya yameleta madhara gani ukilinganisha ni kile kilichofanywa na Israel pale ubalozini Damascus?
Yamepiga na kuharibu kambi kubwa ya jeshi la anga ,pia matokeo ya shambulizi hili yatadumu kwa muda mrefu kati ya hizo nchi mbili.

Na pia shambulizi hili litaifaidisha Iran kimkakati.

Kwa hili shambulizi litaifanya Israel ianze kujifikiria mara 2 kabla ya kushambulia masilahi ya Iran tofauti na mwanzo.
Kiufupi hili shambulizi litaifaidisha Iran kwa muda mrefu.
 
Vita si mpira wa miguu kwamba ukipigwa upande wako nawe unarudisha upande wa mpinzani, yumkini hata mpira wenyewe kuna wakati unaweza kuurudisha kwa golikipa ili mpange mashambulizi upya. HIvo mpaka hapa sijaona kuufyata
Danadana hizo hazikutarajiwa kuwa ni baina ya Israel na nchi yoyote nyengine duniani.
Wao tunavyojua ni kupiga tu kwani wana jeshi bora na teknolojia za hali ya juu duniani.
 
Military base imechakaa,haiwezi Fanya kazi Tena,cruise missiles 7 zimetua
Hahaha.....Wavaa kobazi mnajichekesha.🤣 na Mudy pia atakuwa amefurahi sana kule akhera
 
Attachments

  • 20240414_125315.jpg
    20240414_125315.jpg
    54.1 KB · Views: 2
Marekani wamesihi Israel isijaribu kulipa kisasi kwasababu wakifanya hivyo mzozo utakuwa mkubwa mashariki ya kati.. natamani hii vita iishe maana kama kutatokea malipizi dhidi ya Iran huku Africa ndiyo waathirika wa kilakitu kwenye vita hii
Jinga kabisa, Afrika tunahusika na tutaathirika vipi na huo upuuzi wao?
Magufuli alipowaambia muanze kujitegemea hamkumuelewa?
Mna sababu ipi muhimu inayowafanya kuwa tegemezi?
Acha Watwangane tu heshima iwepo maana kuna wanaojiona ni viranja na wamiliki wa dunia
 
We jamaa uelewa wako mdogo sana....Jamani wemgine someni tu comments za wajuvi wa mambo ili mpanue maoblangata yenu... Kwausichofahamu Israel na Syria ni km Namanga TZ na Namanga KE... Ata kwa mguu unafika....Pili Diplomatic premises (ubalozi) hua haushambuliwi lile ni jengo tu halina threat yoyote sasa Israel kushambulia Jengo nayo nimafanikio kwako kweli?? Ebu jaribu kupitia military blogs za kimataifa ujifunze kitu.... Israel analindwa kwa gharama kubwa sana na US...bila US/UK/France na Jordan leo ingekua ni kilio kikubwa kwa Israel.... Jiulize Iran imeishambulia Israel lakini US president na baraza lake la usalama wamekaa kujadili as if US ndo kashambuliwa....
Inaonekana wewe ni mgeni kwenye hii mijadala. Tumeujadili humu huo ubalozi hapo Damascus takribani wiki moja sasa.

Kilichoshambuliwa ni mkutano wa majenerali na maafisa wengine wa kijeshi katika maeneo ya ubalozi. Wewe unadai Israel imeshambulia jengo?!

Wanajeshi walikuwa wakifanya nini katika eneo la ubalozi unaopakana na nchi wanayoirushia maroketi mara kwa mara?

Wanajeshi ndio wamekuwa mabalozi ama wanadiplomasia siku hizi?!
 
Ubalozi huwa na waambata wa kijeshi,ni kawaida,ubalozi haushambuliwi kwa sheria za kimataifa,hapa umeendelea kuonesha ubongolala wako tena
 
Yamepiga na kuharibu kambi kubwa ya jeshi la anga ,pia matokeo ya shambulizi hili yatadumu kwa muda mrefu kati ya hizo nchi mbili.

Na pia shambulizi hili litaifaidisha Iran kimkakati.

Kwa hili shambulizi litaifanya Israel ianze kujifikiria mara 2 kabla ya kushambulia masilahi ya Iran tofauti na mwanzo.
Kiufupi hili shambulizi litaifaidisha Iran kwa muda mrefu.
Kambi ipi unayosema? Ni hiyo Nevatim Airbase ambayo media mbalimbali zinaonesha F-35s zikiendelea kutua na kupaa?

Israel inashambulia maslahi ya Iran hapo Lebanon wakati huu ninapoandika andiko hili.
 
Ujasiri wa Iran umeifanya Israel inywee kiaina tofauti na wengi tulivyotaraji kuwa ikipigwa kweli na Iran itarusha mvua ya makombora Tehran papo kwa papo.

Kitisho cha vita vikubwa zaidi kiko wazi baada ya Iran kuiambia Marekani ikae mbali katika vita vyake na Israel.

Baada ya mashambulio ya jana mpaka kwenye kambi za jeshi za Tel Aviv, Iran imesema mpaka hapo imefunga ukurasa wake wa mwanzo wa vita.

Inasubiri iwapo Israel itajibu na wao waendeleze ukurasa mwengine mpana zaidi
Busara inahitajika sana kumaliza mzozo huo.
Vita ni njia yenye madhara makubwa kwa jamii.
 
Ujasiri wa kurusha makombora hewa!! Wangetuma wanajeshi tuone huo ujasiri! Hatushabikii vita ila hawa waarabu na waajemi waliokuzwa ktk imani ya chuki ya kidini dhidi ya wanaowaita makafiri wanadekezwa sana na wayahudi na wazungu, dawa yao ingekuwa kuwajibu wanachokifanya kutofuata sheria za kivita ndiyo wataacha ujinga wa kubagua dini za wenzao na kuwaona wenye imani tofauti hawapaswi kuishi duniani au wakiishi wawe watumwa wao tu.
Mbona umeropoka sana!?
Kwani Israel alipolipua balozi ya Iran alituma askari!?
Kuanza aanze Israel Iran ikilipizwa isemwe ni udini!?
Wapi wamesema wanapigana dhidi ya uyahudi!?
Na wewe eti ni great thinker aisee hii hatari.
 
Kambi ipi unayosema? Ni hiyo Nevatim Airbase ambayo media mbalimbali zinaonesha F-35s zikiendelea kutua na kupaa?

Israel inashambulia maslahi ya Iran hapo Lebanon wakati huu ninapoandika andiko hili.
Wameonesha runway ya uwanja hawakuonesha airbase nzima.
Bali runway peke yake.
 
Ubalozi huwa na waambata wa kijeshi,ni kawaida,ubalozi haushambuliwi kwa sheria za kimataifa,hapa umeendelea kuonesha ubongolala wako tena
Soma vizuri sheria za kimataifa zinazohusu masuala ya vita (International Law). Ubalozi unaweza kupoteza kinga ya kutambulika kama eneo la kiraia endapo utatumika kijeshi na kwa maslahi ya jeshi.
 
Soma vizuri sheria za kimataifa zinazohusu masuala ya vita (International Law). Ubalozi unaweza kupoteza kinga ya kutambulika kama eneo la kiraia endapo utatumika kijeshi na kwa maslahi ya jeshi.
Nimekwambia ubalozini huwa Kuna waambata wa kijeshi,wanajeshi kufanya kikao ubalozini kwao siyo tatizo,acha ujinga
 
Inaonekana wewe ni mgeni kwenye hii mijadala. Tumeujadili humu huo ubalozi hapo Damascus takribani wiki moja sasa.

Kilichoshambuliwa ni mkutano wa majenerali na maafisa wengine wa kijeshi katika maeneo ya ubalozi. Wewe unadai Israel imeshambulia jengo?!

Wanajeshi walikuwa wakifanya nini katika eneo la ubalozi unaopakana na nchi wanayoirushia maroketi mara kwa mara?

Wanajeshi ndio wamekuwa mabalozi ama wanadiplomasia siku hizi?!
Kwa hiyo sasa hivi mkuu wa jeshi la Tz akienda Kenya haruhusiwi kwenda kwenye ubalozi wa Tz?
 
Kambi ipi unayosema? Ni hiyo Nevatim Airbase ambayo media mbalimbali zinaonesha F-35s zikiendelea kutua na kupaa?

Israel inashambulia maslahi ya Iran hapo Lebanon wakati huu ninapoandika andiko hili.
Masilahi ya Iran ndani ya Lebanon ni yapi?
Kitendo cha kuonesha video ili kuamisha watu kuwa unatumika ni kucheza na saikolojia ya watu.
 
Back
Top Bottom