BICHWA KOMWE -
JF-Expert Member
- Jul 21, 2022
- 5,358
- 12,037
ANAANDIKA BICHWA KOMWE:-
Hizi shule zinazoitwa "international schools" zinafundisha nini cha ziada sana ambacho hakimo penginepo?
Ni kweli, shule zina mazingira mazuri na yanayofurahisha, lakini je, kile wanachofundishwa wale watoto kina hadhi gani ya kulipiwa mamilioni?
Hapa ieleweke vema kwamba siungi mkono mashule ya kata ambayo kimsingi ni mashule butu yasiyo na sifa wala vigezo vya kuwa shule. Mashule ya kata ni maeneo maalumu ambayo watoto wanaenda kujazwa ujinga na kupoteza wakati.
Hizi international schools pia ni kama mashule ya kata yaliyochangamka tu isipokuwa pale unaenda kununua KIINGEREZA kwa milioni hamsini kwa mwaka.
Zaidi sana mtoto atapewa midoli ya kuchezea na mabembea ya kuning'inia. Of course bila kusahau CHETI CHA KIINGEREZA.
Linapokuja swala la maarifa ni kitu kingine kabisa. Hawa watoto ni makanjanja tu kama watoto wengine wanaosoma kwenye mashule ya kata.
Mpaka sasa sijaona ni kwanini mtoto akanunue Kiingereza kwa shilingi milioni hamsini wakati mtu anaweza kujifunza Kiingereza hata chini ya mti na akabukua vema tu kama makanjanja wengine akina Dayamondi waliojifunza Vingereza magetoni.
Tukiwawezesha hawa walimu wetu uchwara wa shule za Kata wataweza kufundisha kizungu vizuri tu.
Tuanze kudahili walimu ambao wana ufaulu mkubwa badala ya kudahili vilaza wenye MADIVISHENI FOO ati ndio wakawe walimu!
Hili lizingatiwe sana.