India: Mwanaume abeba mwili wa mkewe Km 12

H
View attachment 387846

Amang Majhi alifariki dunia kwa maradhi ya kifua kikuu Jumanne usiku
Mwanamume mmoja maskini nchini India alibebe maiti ya mkewe kwa zaidi ya kilomita 12 baada ya hospitali alimofariki kushindwa kumsafirisha kwa gari la kuwabebea wagonjwa hadi kijiji mwake.

Mke wa Dana Mjhi, Amang, mwenye umri wa 42, alifariki dunia baada ya kuugua maradhi ya kifua kikuu katika hospitali ya Ulaya, mji wa Bhawanipatna jimbo la Orissa.

Bwana Mahji alisema kijiji chake kilikuwa umbali wa kilimita 60 na hakuwa na uwezo wa kulipa gharama ya usafiri wa gari la kuwabebea wagonjwa.

Hospitali hiyo imekana madai hayo.
'Hakuna namna'
'Mwanamke huyo alilazwa hospitalini siku ya Jumanne na kufariki usiku huo huo.

Bwana yake alichukua maiti hiyo bila kuwafahamisha wahudumu wa hospitali hiyo,' afisa mkuu wa afya B Brahma alisema
Bwana Majhi, anadai mkewe alifariki siku ya Juma nne usiku na kuamua kubeba mwili wake siku ya Jumatano baada ya wahudumu wa hospitali hiyo kumsihi kuondoa mwili huo.
' Nilikuwa nikiwaomba wahudumu wa hospitali hiyo wanisaidie gari nimbebe mke wangu lakini nikaambulia patupu.

Kwa sababu mimi ni maskini na nisingeweza kukodisha gari la kibinafsi sikuwa na njia nyingine ila kumbeba mke wangu mabegani.'

Wakati akitembea , Bw Majhi alisindikizwa na mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 12 , Chaula
Mapema Jumatano , alisema alifunga mwili wa mkewe na nguo na kuanza safari hiyo ndefu ya kuelekea kijijini huko Melghar kwa mila na tamanduni za mwisho akiungana na mwanawe mwenye umri wa miaka 12 , Chaula.
Alitembea kwa takriban kilomita 12, ndipo watu walipoingilia kati na kumsaidia kwa gari la kubebea wagonjwa wakamfikisha hadi mwisho wa safari yake.

Shughuli ya kuchoma mwili wa mkewe ilifanyika siku ya Jumatano usiku.
Hao wahudumu waliomnyima gari huyo masikini hawatofautiani na wale matutusa wa muhimbili wanaopasua kichwa badala ya mguu na kubadilisha maiti.
 
acheni ujinga ninyi,dhambi mfanye ninyi adhabu apewe yesu,imeandikwa kila mtu ATABEBA MZIGO WAKE MWENYEWE
 
Daah huku kwetu wanazuia maiti siku hizi kama hukumaliza pesa ya matibabu..Gari hawatoi kabisaa!
 
Mimi mwanadamu ni nini hata nijidai?Kwani mimi nilieumbwa kwa mwili wa nyama na pumzi ya msaada ni nani hata nilewe madaraka?
Mimi ni msafiri,Mpita njia na mpangaji katika Ulimwengu huu uliojaaa dhiki na taabu.

Nina nini mimi?Eti nina jeshi na pesa?Hapana...Hivyo vyote havitanizuia kufa na kuoza na kuliwa na funza.
Nina magari na nyumba za kifahari kushinda wenzangu?Hapana...Hata moja sitazikwa nayo,Yote na ufahari wake nitaziacha nyuma.

Sasa mimi ni nani eti??Mimi si kitu,mimi si lolote...Nijapopita katikati ya majeshi yanayonitii na watu wanaoniogopa...bado mimi si lolote!!Mimi ni fukara na masikini wa mwili na roho.. kiburi na majivuno ya ubinadamu yananidanganya.

Mimi ni mavumbi,katika mavumbi nimetoka,na mavumbini nitarudi....Nitaoza kwa kuliwa na funza...Kilo kilicho changu katika mwili huu wa nyama ktapukutika...Utabaki unywele tu katika shimo la kaburi ili kutimiza hesabu mbele za yeye aliye mkuu kuliko wote.

Thamani yangu si lolote...Nisijivune,Nisijigambe,Nisinyanyase,Nisihusudu vilivyo vya ulimwengu na kuyaacha maisha yasiyo na kikomo.Eee Mungu unirehemu...Kwa kuwa mimi ni mdhambi.

Umeandika kwa hisia kali sana. Umenikumbusha kitu cha muhimu ambacho huwa namwomba Mungu azidi kuniepusha daima. Majivuno...Majivuni ni sumu ya utu
 
India kuna umasikini wa kutisha
hu wa kwetu afadhali mara 1000

kuna watoto wanazaliwa barabarani tu
hadi wanakuwa watu wazima hawajawahi kuishi ndani ya nyumba

Na hilo jimbo ni mojawapo ya majimbo yenye umaskini wa kutupa mkuu.
 
Mwanamume India abeba maiti ya mkewe 12km

_90922043_1ae6257b-169b-4718-b830-780cdca4e43e.jpg

Image captionAmang Majhi alifariki dunia kwa maradhi ya kifua kikuu Jumanne usiku
Mwanamume mmoja maskini nchini India alibebe maiti ya mkewe kwa zaidi ya kilomita 12 baada ya hospitali alimofariki kushindwa kumsafirisha kwa gari la kuwabebea wagonjwa hadi kijiji mwake.

Mke wa Dana Mjhi, Amang, mwenye umri wa 42, alifariki dunia baada ya kuugua maradhi ya kifua kikuu katika hospitali ya Ulaya, mji wa Bhawanipatna jimbo la Orissa.

Bwana Mahji alisema kijiji chake kilikuwa umbali wa kilimita 60 na hakuwa na uwezo wa kulipa gharama ya usafiri wa gari la kuwabebea wagonjwa.

Hospitali hiyo imekana madai hayo.

'Hakuna namna'
'Mwanamke huyo alilazwa hospitalini siku ya Jumanne na kufariki usiku huo huo.

Bwana yake alichukua maiti hiyo bila kuwafahamisha wahudumu wa hospitali hiyo,' afisa mkuu wa afya B Brahma alisema

Bwana Majhi, anadai mkewe alifariki siku ya Juma nne usiku na kuamua kubeba mwili wake siku ya Jumatano baada ya wahudumu wa hospitali hiyo kumsihi kuondoa mwili huo.

' Nilikuwa nikiwaomba wahudumu wa hospitali hiyo wanisaidie gari nimbebe mke wangu lakini nikaambulia patupu.

Kwa sababu mimi ni maskini na nisingeweza kukodisha gari la kibinafsi sikuwa na njia nyingine ila kumbeba mke wangu mabegani.'

_90922044_a9225ea5-7253-40b1-8d23-9194a7c8de95.jpg
Image copyrightGOOGLE
Image captionWakati akitembea , Bw Majhi alisindikizwa na mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 12 , Chaula
Mapema Jumatano , alisema alifunga mwili wa mkewe na nguo na kuanza safari hiyo ndefu ya kuelekea kijijini huko Melghar kwa mila na tamanduni za mwisho akiungana na mwanawe mwenye umri wa miaka 12 , Chaula.

Alitembea kwa takriban kilomita 12, ndipo watu walipoingilia kati na kumsaidia kwa gari la kubebea wagonjwa wakamfikisha hadi mwisho wa safari yake.

Shughuli ya kuchoma mwili wa mkewe ilifanyika siku ya Jumatano usiku.

BBC
1472214126925.jpg
Hii picha.......
Imeniumiza moyo.
 
Kweli hili picha la kihindi, kama walimpokea hapo hospital mgonjwa iweje wamruhusu aondoke na maiti, si kuna askari wa hapo hospital, kibali cha kutoka na maiti alipata wapi ? Hiyo hospital isikwepe lawama kabisa
 
Kwa umbali wote huo? wanajimii wengine walikuwa wapi kumsaidia, kama hospital inilikataa? Bila shaka ni matabaka na kubaguana kwao
 
Back
Top Bottom