Wivu wa mapenzi wasababisha kumkata mkewe koromeo, na kisha kujinyonga mpaka kufa

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Mkazi wa Mtaa wa 14 Kambarage Mjini Geita, Martine John anadaiwa kujiua kwa kujinyonga baada ya kudaiwa kumjeruhi mkewe, Justina Paulo (34) kwa kitu chenye ncha kali kwa kile kinachodaiwa wivu wa mapenzi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Adam Maro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ingawa amesema hawezi kulizungumzia zaidi kwa kuwa yupo safarini.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Geita, Mfaume Salum akizungumza na waandishi wa habari leo, Novemba 23, 2023 amesema wamempokea mwanamke huyo ambaye amelazwa hospitalini hapo baada ya kukatwa sehemu ya koromeo, kichwani na mkononi na kitu chenye ncha kali.

“Novemba 22 saa tano asubuhi tulipokea mwanamke katika idara yetu ya dharura akiwa na majeraha kwenye shingo, mkono na kichwani. Majeraha haya yanaonyesha yamekatwa na kitu chenye ncha kali. Eneo la shingo jeraha ni kubwa, amekatwa sehemu ya koromeo na anaendelea na matibabu,” amesema Dk Salum.

Mama mzazi wa mwanamke aliyejeruhiwa, Anastazia Paulo akizungumzia maisha ya wanandoa hao, amesema wamekuwa na mgogoro wa mara kwa mara uliosababisha mwanae kurudi nyumbani, japo imeelezwa siku za karibuni mume wake alimfuata baada ya kusuluhishwa na kurudi kuendelea na maisha.

“Binti yangu ameishi na huyu mwanaume kwa miaka 10, Julai mwaka huu waligombana akarudi nyumbani, lakini baadaye mumewe alikuja wakasuluhisha wakasema wamesameheana, lakini jana saa nne nilipigiwa simu nikaambiwa mkwilima wangu amejinyonga na kumkata mapanga mkewe,” amesema mama huyo na kuongeza;

“Kipindi cha nyuma ugomvi wao ulikuwa ni kila mara mwanangu akienda kuimba kwaya, akirudi mumewe anadai anakwenda kwa wanaume wengine, sasa sijui hadi kufikia hapa walikosana nini maana mpaka sasa mwanangu hawezi kuongea.”

Balozi wa eneo hilo, Stephano Matata amesema Novemba 22 saa mbili asubuhi, alifika mtoto akieleza amegonga mlango wa baba yake mdogo haufunguki, lakini chini kumetapakaa damu na walipokwenda kufungua waliona mwili ukining’inia huku mkewe akiwa kitandani mwili ukiwa umetapakaa damu.

“Mwonekano wa tukio hili unaonyesha Martine ndiye aliyefanya tukio hili, kwa kuwa inaonyesha alijitahidi kufuta damu ndani ya nyumba. Tumekuta mikono yake ina damu, labda alipoona hali ya mkewe ni mbaya akaamua kujinyonga,” ameeleza Matata.

Akizungumzia maisha yao kabla ya tukio hilo, amesema kwa muonekano wa nje wanandoa hao walikua ni watu wenye upendo na hakuwahi kupokea malalamiko yoyote ya kutokea ugomvu kato yao.

Chanzo: Mwananchi
 
Sasa huyu jamaa.... Au basi ngoja niishie hapa mana bado sijafinyiwa kwa ndani vizuri mpaka nimwage ubongo na akili zake.
 
Mapenzi haya au ujinga?
 
Back
Top Bottom