India: Mwanaume abeba mwili wa mkewe Km 12

Binadamu buana, huyo aliepiga picha hii yeye alishindwaje kumsaidia? Aliona kupiga picha ni jambo la maana zaidi kuliko kumsaidia?? Na hapo panaonekana ni wilayani kabisa ameshindwaje hata kumkodishia Boda boda? Au alimpiga picha kwanza ndio akamsaidia?
 
Mwanamume India abeba maiti ya mkewe 12km

_90922043_1ae6257b-169b-4718-b830-780cdca4e43e.jpg

Image captionAmang Majhi alifariki dunia kwa maradhi ya kifua kikuu Jumanne usiku
Mwanamume mmoja maskini nchini India alibebe maiti ya mkewe kwa zaidi ya kilomita 12 baada ya hospitali alimofariki kushindwa kumsafirisha kwa gari la kuwabebea wagonjwa hadi kijiji mwake.

Mke wa Dana Mjhi, Amang, mwenye umri wa 42, alifariki dunia baada ya kuugua maradhi ya kifua kikuu katika hospitali ya Ulaya, mji wa Bhawanipatna jimbo la Orissa.

Bwana Mahji alisema kijiji chake kilikuwa umbali wa kilimita 60 na hakuwa na uwezo wa kulipa gharama ya usafiri wa gari la kuwabebea wagonjwa.

Hospitali hiyo imekana madai hayo.

'Hakuna namna'
'Mwanamke huyo alilazwa hospitalini siku ya Jumanne na kufariki usiku huo huo.

Bwana yake alichukua maiti hiyo bila kuwafahamisha wahudumu wa hospitali hiyo,' afisa mkuu wa afya B Brahma alisema

Bwana Majhi, anadai mkewe alifariki siku ya Juma nne usiku na kuamua kubeba mwili wake siku ya Jumatano baada ya wahudumu wa hospitali hiyo kumsihi kuondoa mwili huo.

' Nilikuwa nikiwaomba wahudumu wa hospitali hiyo wanisaidie gari nimbebe mke wangu lakini nikaambulia patupu.

Kwa sababu mimi ni maskini na nisingeweza kukodisha gari la kibinafsi sikuwa na njia nyingine ila kumbeba mke wangu mabegani.'

_90922044_a9225ea5-7253-40b1-8d23-9194a7c8de95.jpg
Image copyrightGOOGLE
Image captionWakati akitembea , Bw Majhi alisindikizwa na mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 12 , Chaula
Mapema Jumatano , alisema alifunga mwili wa mkewe na nguo na kuanza safari hiyo ndefu ya kuelekea kijijini huko Melghar kwa mila na tamanduni za mwisho akiungana na mwanawe mwenye umri wa miaka 12 , Chaula.

Alitembea kwa takriban kilomita 12, ndipo watu walipoingilia kati na kumsaidia kwa gari la kubebea wagonjwa wakamfikisha hadi mwisho wa safari yake.

Shughuli ya kuchoma mwili wa mkewe ilifanyika siku ya Jumatano usiku.

BBC
 
hizo picha alowapiga alisafiri nao au imekuwaje?
maana zimepigwa maeneo tofauti tofauti..
 
Jamani hata watu kumsaidia....!!! Naona katika picha kama watu wanamshangaa tu
 
Nawaambia jamani MUNGU MKUU MTAKATIFU ndio mwenye uvumilivu mkubwa sana sana kama angekuwa na Hasira nasisi asingebaki hata mmoja.MUNGU MKUU nakuomba utusamehe makosa yetu
 
Dah huyoo binti kitamuuma mpka siku atakapo kufa. Haki duniani imepotea. upendo kwisha, binadamu wamejawa na ukatili kutawaliwa na pesa, kujitukuza kujikweza.
 
Laiti tungekuwa na kipimo kinachoweza kupima machungu aliyobeba huyo mtoto na baba yake labda kingepasuka bila kutoa majibu!
Kwel kabsa. Yan chuki alyojenga apo ata gaidi hawez fkia
 
MWANAUME mmoja kutoka katika familia maskini inayoishi mjini Bhawanipatna katika jimbo la Orissa nchini, amelazimika kuubeba mwili wa mkewe begani, baada ya hospitali kushindwa kutoa gari la kubebea mwili huo.

Dana Majhi alikutwa na masahibu hayo, baada ya aliyekuwa mke wake, Amang kufariki dunia katika hospitali ya wilaya, kutokana na kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa Kifua Kikuu.

Mara baada ya mkewe kufariki, Majhi (42) alianza taratibu zote za kusafirisha mwili wa mke wake, kwa kuulizia gari maalum lililotolewa na Serikali kwa ajili ya shughuli hizo.

Cha ajabu, uongozi wa hospitali hiyo ulimjibu kuwa gari hilo halipo hivyo kumlaimu Majhi kuuandaa mwili wa mkewe na kuanza kuubeba, kuelekea kijiji kwake ambako kuna umbali wa kilometa 60 kutoka hospitalini hapo.

Mara baada ya Majhi kukamilisha kuuandaa mwili wa mke wake, aliianza safari ya kuelekea kijijini kwake Melghar, huku akiwa ameubeba mwili huo begani pamoja na kusindikizwa na mwanae wa kike mwenye umri wa miaka 12, Chaula. Hata hivyo, uongozi wa hospitali hiyo, ulikana kumnyima gari la kubebea maiti mwanaume huyo maskini.

Akizungumza kuhusu hilo, Ofisa mmoja wa hospitali hiyo, B Brahma alisema mwanamke huyo alifikishwa hospitalini hapo Jumanne mchana na kufariki siku hiyo hiyo, na mume wake kuubeba mwili wa mkewe pasina kuutaarifu uongozi wa hospitali hiyo.

“Mwanamke huyo aliyekuwa akisumbuliwa na Kifua Kikuu (TB), alifikishwa hapa Jumanne mchana, na kufariki dunia siku hiyo hiyo. Cha ajabu, mumewe aliamua kuubeba mwili wa mkewe, pasipo kutoa taaria kwa uongozi wa hospitali,” alisema Brahma.

View attachment 387474

CRUEL WORLD
 
uploadfromtaptalk1472187295516.jpeg

Amang Majhi alifariki dunia kwa maradhi ya kifua kikuu Jumanne usiku
Mwanamume mmoja maskini nchini India alibebe maiti ya mkewe kwa zaidi ya kilomita 12 baada ya hospitali alimofariki kushindwa kumsafirisha kwa gari la kuwabebea wagonjwa hadi kijiji mwake.

Mke wa Dana Mjhi, Amang, mwenye umri wa 42, alifariki dunia baada ya kuugua maradhi ya kifua kikuu katika hospitali ya Ulaya, mji wa Bhawanipatna jimbo la Orissa.

Bwana Mahji alisema kijiji chake kilikuwa umbali wa kilimita 60 na hakuwa na uwezo wa kulipa gharama ya usafiri wa gari la kuwabebea wagonjwa.

Hospitali hiyo imekana madai hayo.
'Hakuna namna'
'Mwanamke huyo alilazwa hospitalini siku ya Jumanne na kufariki usiku huo huo.

Bwana yake alichukua maiti hiyo bila kuwafahamisha wahudumu wa hospitali hiyo,' afisa mkuu wa afya B Brahma alisema
Bwana Majhi, anadai mkewe alifariki siku ya Juma nne usiku na kuamua kubeba mwili wake siku ya Jumatano baada ya wahudumu wa hospitali hiyo kumsihi kuondoa mwili huo.
' Nilikuwa nikiwaomba wahudumu wa hospitali hiyo wanisaidie gari nimbebe mke wangu lakini nikaambulia patupu.

Kwa sababu mimi ni maskini na nisingeweza kukodisha gari la kibinafsi sikuwa na njia nyingine ila kumbeba mke wangu mabegani.'

Wakati akitembea , Bw Majhi alisindikizwa na mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 12 , Chaula

Back
Top Bottom