Inatisha!

Sijaona kitu au nimeshindwa kufungua

Nilijua wengi wao watapata shida kufungua hiyo link jaribu kufungua kwa web browser tofauti kama Mozilla Firefox,Google chrome na kadharika


ila inatisha kweli kweli huko twatakiwa tumia diplomasia na si kutumia nguvu ya jeshi msilazimisha kuwaongoza watu kama hawataki kupelekwa mtakavyo
 
Kazi nzuri sana, Tarime ni mafano wa kuigwa, wananchi wanajua haki zao za msingi - Na ukiangalia vizuri kazi hii unaona kumbe Tarime si wakorofi, si wapenda vita bali ni wapenda haki, hawataki kuonewa, kukandamizwa, kudaganywa kwa namna yoyote ile.

Kazi hii kama ingeonyeshwa pia katika mikoa ya kati kama Singida, Tabora, Shinyanga, Dodoma na hata Morogoro ingesaidia kwani ni darasa tosha la elimu ya uraia kwa mwananchi kujua haki zake za msingi.
 
nimeona clip ya kwanza tu.........hata siamini macho yangu...............kilichoniaminisha kuwa ni Tanzania..........ni baada ya kuona kiswahili kinazungumzwa vizuri tu na wananchi wale................

Nimemsikiliza Bony Marwa/Chacha (Mkuria No.1)..................najisikia huzuni sana hivi sasa.................hata kama ni kutaka uongozi jamani si kwa nguvu za dola namna hiyo.............KWELI INATISHA SANA.................

Nashauri vyama vya upinzani watumie hizi clip kuelimisha wananchi juu ya utawala wa Kijambazi wa CCM...........muda upo wa kuleta mabadiliko.................tuweke ushabiki wa vyama vyetu kapuni jamani.................ule ni Unyama ambao mwanadamu yeyote hapaswi kuufurahia bali kuulaani.............

............I'm still puzzled kama kweli hii ninayoiona ni Tanzania................
 
Mmmh! si mchezo, huyu Bony Marwa/Chacha (Mkuria No.1) angefika chuo kikuu nadhani angekuwa mtu hatari sana! Hoja zake zimenigusa mno!
 
na kale ka wimbo kwenye clip ya tatu (mwishoni) kwenye hiyo documentary inabidi katumike sana kwenye kampeni za wapinzani
 
Aiseeeeee
Wakurya wote wanazaliwa wanajeshi kasoro magwanda.

Sasa wanachi wa tarime na wa dar wapi ni wasomi? ni wa wapi ni wajasiri. Ni wa wapi wana elimu zaidi?

Mbona Tarime wameamka kuliko dar ,mwanza, musoma, mbeya mjini?
 
Watanzania wote tungekuwa kama wana Tarime ufisadi na wizi wa CCM ungekwisha zamani sana. Wana Tarime wana ujasiri, wanajiamini na wamechoka na hali jinsi ilivyo.
Mwanakijiji katoa ombi tupige kura zetu za maoni kwa njia ya email, wengi wetu wameruka kimanga kwa ajili ya woga wa usalama wa taifa. Sasa kama tunaogopa kupiga kura za maoni kwa njia email, mbona wenzetu hawa wana Tarime wanaongea waziwazi na bila ya woga wowote?.

Wana JF ni kweli tuna nia ya kuikomboa Tanzania ama tunataka kuwa wasikilizaji wa harakati hizi za ukombozi?. Tusipofanya sisi nani atafanya?.
 
hivi wale polisi wko self conscious kweli? wa TZ hii mambo bado mtu una vaa kofia na t-shirt ya kijani? jamani nani anaenda msituni? recruit wa kwanza kesha nipata
 
DVD ZITENGEZWE wape raia, Mbulu wakiona watawaunga tarime asilimia 100%
 
Hii inatisha na hatutaki tufike hapa... Video kama hizi ni propaganda chafu sana za watu wasioitakia mema demokrasia.

Video vya namna hii vinapenyezwa na mafisadi ili uchaguzi wa 2010 usimamiwe na JWTZ na ili kura zichakachuliwe kulingana na matakwa ya watawala... hii ni njama ya CCM na wametumia nembo ya CHADEMA kwa makusudi, ili kusudi chadema kionekane chama cha fujo na kisichohubiri amani. Hakuna Mtanzania hata mmoja anayetamani maisha ya Tarime, ni maisha ya hofu na huu ni mtaji mkubwa wa mafisadi kubaki madarakani, wanaanza kuwahubili watanzania kuwa Chadema ni cha fujo na hakistahili! WASHINDWE na WALEGEEE

Usiwe mzembe wa kufikiri(Rangi nyekundu), documetary hii inaonesha chadema hawakufanya fujo, bali ni

  1. matumizi ya feza almost 1 bil (Kuhonga wapiga kura) kwa ccm huku polisi wakilipwa 1000 per day,
  2. mabavu ya kulazimisha watu waogope na kupigia ccm(mfano makamba anasema ccm ni chama tawala),
  3. Lugha zisizofaa kutoka kwa viongozi wa juu wa ccm (mfano vidole vitatu vimekunjwa na kimoja kuchomoza by Makamba),
  4. ..........................
  5. ......................
  6. .....................
  7. ......................
  8. .................. malizia kujaza, wewe je upo tayari kuendelea kuwa maskini? wakati nchi imejaa rasilimali kibao, wewe ukiambiwa mfano mmoja mdogo tu wa nchi moja ya afrika (Angola) ambapo unaweza kuwa sawa na TZ, Jamaa (Nchi moja ya ulaya) ilipata kama dola million 600 kutokana na shughuli za mafuta, na ikatoa kama mhisani dola 166mil kwa serikali ya Angola, basi tafakari utayaona mengi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom