Inatia Hasira!

mcfm40

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,452
3,150
Ndugu zangu wanaJF,
Nipo hapo Afrika kusini kwa muda sasa. Huwa najiuliza maswali mengi bila kupata majibu ninapokuwa nakatiza mitaa hasa ya Capetown. Miundo mbinu yao hasa barabara flyovers utashangaa.

Najua makaburu wamefanya kazi kubwa hapa lakini najaribu kulinganisha na kujifargua kwa makufuli na km 11,000 za barabara. Kusema ukweli tanzania hatuna barabara, ni mzaha mtupu!! yaani miaka hamsini ya uhuru tumeshindwa kuweka hata kaflyover kamoja hapo ubungo? miaka hamsini..! Kaflyover Kamoja tu! imekuwa ni siasa tuuu...!

Fikiria labda kila baada ya miaka kumi tungekuwa tunajenga kaflyover kamoja kwenye makutano ya barabara zetu, tungekuwa mbali sana? Inatia hasira na ni aibu kujisifia bila kufanya ulinganisho hata wa mbali tu na wenzetu! Hata Ethiopia wanatushinda? Kwanza kusema awamu ya nne wamejenga km11,000 kulinganisha na awamu nyingine, ina maana hizo awamu nyingine waliokuwepo madarakani ni CUF au CHADEMA? Si ni nyie nyie CCM? Au mnakubali sera zenu za huko nyuma hazikuwa na mashiko? Tunapoitazama CCM tunaitazama kwa ujumla wake tangu uhuru sio katika vipindivipindi.

Tunaangalia continuity ya sera na mipango ya CCM katika kutufikisha hapa tulipo! We cannot compartmentalize development! Mawaziri wa Kikwete wanajua udhaifu wake ndio maana kila wanapozungumza wanasisitiza yale yaliyoyofanywa na serikali ya awamu ya nne kwa kumtaja Kikwete, bila kuzungumzia yana connection gani na yaliyofanywa na awamu nyingine! Kwa sababu wanajua mengi yaliyoahidiwa hayakutelezwa.

Kwa hiyo ni muda muafaka sasa CCM na serikali yake iache kujilinganisha na awamu zilizotangulia (thye are the same people) bali wajilinganishe na majirani zetu na nchi nyingine tulizopata uhuru pamoja. Kwamba wao wako wapi na sisi tupo wapi! Hapo ndipo wanaweza kujifaragua kwamba tunaongoza kwa miundo ya barabara. Sio kumlinganisha Kiwete na Mkapa au mwinyi huo ni upuuzi na udhaifu!
 
Hata CCM wakitawala miaka 1000 hakuna jipya watakolotuletea waizi tu ndiyo wamejaa humo solution ni kuwapiga chini tujaribu mkondo mwingine.
 
nchi ngumu sana hii, maana kila kinchoahidiwa ni uongo lakini wananchi tunawashanilia na kuwapa tena kura, kama hatutaungana kwa pamoja kuleta mabadiliko ya kweli, tutaishia kuwa maskini ombaomba siku zote, na kitakachofuata baada ya hapo watakuja kututawala tena maana hatutaweza kulilipa deni lao wanalotudai'
 
Back
Top Bottom