In DEFENCE of LOWASSA (Warioba & Butiku on it)

all in all haki haikutendeka, kama aliiba hakuiba Mwakyembe na timu yake walisukumwa zaidi na Agenda ya 2005 election na kusahau wananchi ambao walipaswa wapewe fact 100% ili waamue kusuka au kunyoa na si ku target some of people.

WaTz tumepata nini juu ya hili la Lowasa na Richmond Vs Mwakyembe's team.
 
Ukiachilia mbali haya yaliyomuondoa madarakani, Lowassa, je anaweza kutueleza ni wapi aliweza kujikusanyia utajiri mkubwa kupita kiasi kwa mtumishi wa serikali? Ukweli ni kuwa toka awali Lowassa hakupaswa kupewa wadhifa wowote serikalini, kama ilivyokuwa kabla ya Mwalimu kufariki, maana tayari alishakuwa ananuka rushwa. Kwa hiyo kwa yeye kutimuliwa kutokana na rushwa sio kitu cha ajabu kwani tayari alishafahamika kuwa ni mla rushwa.
 
Watz tumepata kitu kwa kweli, unafikiri bila kusakamwa na kamati angejiwajibisha! kama pesa ilikuwepo na umeme ulikuwa wa dharura na ukashindikana kupatikana simply kwa sababu walikuwa wakikumbatia richmond! acha wawajibike haina haja kutetea hapo.
 
Hii ndio Tanzania nchi yenye mito, milima na maziwa mazuri. Uoto wa asili, wanyama na utulivu uliopitiliza bila ya kuwa na amani.

Nchi yenye siri kali, maslahi ya chama na mtu binafsi ni bora kuliko maslahi ya nchi na wananchi wake.

Nchi ambayo kila kisa huundiwa Tume, ambayo hufanya uchunguzi kwa garama kubwa ila majibu na maamuzi ya tume hubaki mifukoni mwa waunda tume.

Nchi ambayo kwa wafalme wake kufoji vyeti ili waitwe madaktari na maprofesa ni kama padre au mchungaji kwenda kanisani.

Nchi ambayo kufanya lolote ikiwezekana hata kuwauza wananchi ilimradi chama na wafalme wasiondoke madarakani ndio kiapo.

Nchi ambayo wafalme wanawapenda sana wahalifu na kuwatelekeza walio wema, ilimradi mapenzi yao yatimizwe.

Nchi yangu Tanzania nguzo zimeoza, kuta zimetoa nyufa na paa zimeota kutu, tunamuomba Mwenyezi muumba atuepushe na tetemeko la ardhi isije nyumba yetu ikaanguka.

Nchi ambayo watu wake wameichoka sasa wanatamani kukimbilia nchi za wenzao eti kwa kingizio cha uraia wa nchi mbili.

_______________________________________________________________________
Ole wao wadhulumuo vipofu kwa maana siku wakiona hawatakuwa na huruma kwa yeyote.
 
TZ ni nchi ambayo watu wake ni waoooga kama kunguru wa zamani, wenye baka jeupe. Kura ni za siri lakini watu wanaichagua SISIEM wakidhani miandiko yao itakaguliwa na hivyo wapinga SISIEM kukamatwa baada ya uchaguzi..
 
Utajiri wa Lowasa unaweza kuwa umetokana na kuuza ng'ombe wake...kama ulivyo utajiri wa Chenge Tukumbuke wamasai na wasukuma ni wafugaji.
 
Utajiri wa Lowasa unaweza kuwa umetokana na kuuza ng'ombe wake...kama ulivyo utajiri wa Chenge Tukumbuke wamasai na wasukuma ni wafugaji.

Chenge aliuza ng'ombe wangapi each kuweza kuwa na $1m katika bank account moja(najua ana nyingi tu).Ng'ombe wa kienyeji anauzwa for around $100 mnadani so it means chenge aliuza ng'ombe 10,000!!!quite a sum...mfugaji mwenye ng'ombe kiasi hiki hata kwenye Google earth utaona zizi/boma lake na kila mtu atamjua.....sijawahi kusikia chenge akiwanao...
 
Utajiri wa Lowasa unaweza kuwa umetokana na kuuza ng'ombe wake...kama ulivyo utajiri wa Chenge Tukumbuke wamasai na wasukuma ni wafugaji.
Ng'ombe wepi walionao hawa wezi? Ranchi zao ziko wapi tusikokujua? Matajiri wote wa ng'ombe Arusha tunawajua ambao kazi yao ni ng'ombe tu, sasa Lowassa kaingia lini mmoja wao ilihali anaishi Dar na kuhangaika na majukumu ya serikali? Kama kauza ng'ombe wake wote ili awe na hayo mabilioni, iwapi kodi yetu kutokana na mapato yake? Tusiwatafutie visababu hawa wezi. Huwezi kuishi Dar ukalipwa TShs. 700,000 kama mshahara, ukaacha hiyo miradi unayodai inakuingizia zaidi ya $1,000,000 ili ishughulikiwe na wengine, hata kwenye enzi ya cellphone na internet haiwezekani. Mwizi tu ndie anayeweza kukupa sababu za aina hiyo.
 
Lowasa ana ranchi kubwa sana maeneo ya Handeni huko Tanga. Ina ukubwa wa hekta elfu tatu, na ana ng'ombe wengi sana.

Ila simaanishi kwamba utajiri wake unatokana na kuuza ng'ombe. Ila mkumbuke uchaguzi wa mwaka huu unaruhusu mgombea binafsi. Morani wana asili ya ujasiri, msishangae jamaa akaingiza timu kama mgombe urais kwa tiketi binafsi.
 
Ni fitina tu, si unajua Lowasa alivyo na nguvu CCM?
Hizo zilikuwa mbio za urais 2015.

Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni, EL alikuwa mkali sana kwa watumishi wa umma na mambo yalikuwa yanakwenda. Huyu wa sasa hivi ni mpole kupita kiasi.
 
Jamani tusimeze matapishi yetu tena.
Lowassa ni mfanyakazi lakini pia ni FISADI, ili tuendelee mbele ebu tuachane na mafisadi kwanza kwa muda.
Hawa wezi wezi wana bahati sanaaaa hawako China, vichwa vyao ingekuwa halali ya mbwa wa polisi siku nyingi vimeishachemshwa na kupewa chakula wale mbwa wa polisi hakuna mjadala.
 
Lowasa ana ranchi kubwa sana maeneo ya Handeni huko Tanga. Ina ukubwa wa hekta elfu tatu, na ana ng'ombe wengi sana.

Ila simaanishi kwamba utajiri wake unatokana na kuuza ng'ombe. Ila mkumbuke uchaguzi wa mwaka huu unaruhusu mgombea binafsi. Morani wana asili ya ujasiri, msishangae jamaa akaingiza timu kama mgombe urais kwa tiketi binafsi.

Je hii ranchi alirithi au aliipata toka kwenye mshahara wake akama mtumishi wa umma?Hekta moja ya ardhi ni kama 1,000,000 kwa hizo 3,000 fanya mahesabu yako.Bado hiyo mifugo....
 
Bugurunkwamnyamani,

Jamaa ni mwizi, period! Haitaji hata kulizwa this is now general knowledge to everybody in TZ. Kama ana cha kujitetea si angesema pale bungeni kila mtu akasikia na kujisafisha. Hotuba yake haina hata chembe ya kujitetea ukichulia kuwa alishaona ripoti tofauti na wenzake waliohojiwa kichwakichwa. Yeye kutuambia kuwa hakutendewa haki kwa kutokuhojiwa haitusaidii sisi wala yeye mwenyewe. Anachotakiwa kufanya ni kujisafisha kitu ambacho ameshindwa. Naomba majibu ya maswali yafuatayo:
1. Mbona sasa alikuwa kimbelembele kujaribu kuzuia ripoti isiwasilishwe bungeni?
2. Mbona alijaribu kuwatisha mawaziri na kuwanga'ang'aniza waitetee ripoti ambayo hata hawajaiona.
3. Mbona alitamka hadharani kuwa serikali ilikuwa ina nia nzuri kwenye swala la Richmond.
4. Atwambie kama ni kweli ripoti hii aliisikia na kuiona siku ile iliposomwa.

wenye wivu mtajinyonga mwaka huu.kama EL ni mwizi why kamati haikumhoji??waliogopa nini?he has a point na hapo ndo napoona mwakyembe na wenzie maboga
 
Ukiachilia mbali haya yaliyomuondoa madarakani, Lowassa, je anaweza kutueleza ni wapi aliweza kujikusanyia utajiri mkubwa kupita kiasi kwa mtumishi wa serikali? Ukweli ni kuwa toka awali Lowassa hakupaswa kupewa wadhifa wowote serikalini, kama ilivyokuwa kabla ya Mwalimu kufariki, maana tayari alishakuwa ananuka rushwa. Kwa hiyo kwa yeye kutimuliwa kutokana na rushwa sio kitu cha ajabu kwani tayari alishafahamika kuwa ni mla rushwa.
Unaweza ukaorodhesha mali au utajiri wa Lowassa? Ana mali kiasi gani? Je umeona kama amedeclare mali yake na ali declare nini na kuacha nini?
Kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu "usalama wa taifa" haujamfanyia kazi?
Lets not go by hearsay, we should have evidence ili kutenda haki, siyo tu kusema kwa sababu umesikia watu wakisema.
 
wenye wivu mtajinyonga mwaka huu.kama EL ni mwizi why kamati haikumhoji??waliogopa nini?he has a point na hapo ndo napoona mwakyembe na wenzie maboga
You are correct and very correct. alitakiwa ahojiwe na waseme walipomhoji alisema.......na hii inathibitisha kuwa Report Mwakyembe it had an agenda hidden againts this. Na ndiyo mpaka leo hata mapendekezo yao mengine ya watu kufutwa kazi hayajafanyika maana report ilikuwa na unafiki ndani yake.
 
Nadhani repoti ya REPOA iliyosema Lowassa ni maarufu kuliko JK na mke wa EL ni mchapa kazi kuliko mke wa JK, ndiyo msingi wa haya yote!!!!!!!!!!!!!!!!!! Kumbuka Ouko na Moi!!!!!!!!!!!!
 
Je hii ranchi alirithi au aliipata toka kwenye mshahara wake akama mtumishi wa umma?Hekta moja ya ardhi ni kama 1,000,000 kwa hizo 3,000 fanya mahesabu yako.Bado hiyo mifugo....
Mbona hata wafanyakazi wana maranchi na mifugo mingi tu. Kwa wamasai mifugo ni desturi yao na ni utajiri wao. Ng'ombe anazaa mara moja kwa mwaka!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom