In DEFENCE of LOWASSA (Warioba & Butiku on it)

Unaweza ukaorodhesha mali au utajiri wa Lowassa? Ana mali kiasi gani? Je umeona kama amedeclare mali yake na ali declare nini na kuacha nini?
Kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu "usalama wa taifa" haujamfanyia kazi?
Lets not go by hearsay, we should have evidence ili kutenda haki, siyo tu kusema kwa sababu umesikia watu wakisema.
Nanu, Kuorodhesha mali za mwizi sio kazi ndogo maana ni wataalamu wa kuzificha. Ila hawa wote ni Makubwajinga katika show-off za matumizi yao. Lowassa ninayemfahamu mimi alipokuwa Arusha-AICC hakuwa na nyumba wala gari. Mara tu alipopewa uwaziri wa Ardhi kwa miaka miwili tu akawa na uwezo wa kujenga hekalu palw Masaki alilowapangisha ubalozi wa South Africa walipoanzisha ofisi Dar. Huu-huu ndio wakati alipokuwa anafukuza wafanyakazi wengine wa Wizara ya Ardhi kwa kuwashutumu kushiriki rushwa. Halafu 1995 akawa na uwezo wa kukodi ndege kwenda Dodoma kugombea urais, bahati mbaya akafungiwa na Nyerere kutokupata madaraka mpaka Mwalimu alipotutoka ndio wafujaji wenzake wakamrudisha. Hayo tu yanatosha kumfungia maisha kama Usalama wa Taifa wangekuwa kweli wanafanya kazi kwa maslahi ya nchi. Bahati mbaya hivi sasa wanafanya kazi ya umbea tu kwa maslahi ya kiongozi anayewatuma, in this case JK.
 
Akili ya Mdanganyika inaashiriwa wazi na anapoitazama saa...muulize mdanganyika yeyote jibu ni hilo hilo pasi kufikiria mara mbili.. Wakati mshale wa saa unaonyesha at three sisi (wadanganyika) husema ni saa tisa jioni/usiku, kiasi kwamba kwa fikra za kawaida binadam yeyote mwingine hawezi kuelewa inakuwaje kuwaje!..
Iweje mshale wa saa uwe ktk namba tatu isomeke kama saa tisa?.. haya ndio maswala ya Lowassa.
Mtajenga kila sababu kuhalalisha hata lile lisokuwa na logic, na mara zote utajiuliza kwa nini tusiziwee saa zetu mishale yake kulingana na namba za saa tunazosoma?..na hata kama utaweka - basi weka saa yako wewe, mwenye shida ya saa ama wakati ni wewe sii wote...Hivi kweli mwanao akikuuliza kwa nini mshale wa saa upo namba moja unasema ni saa sabaa..utamjibu nini?

Basi na tuelewe tu kwamba akili za mtumwa siku zote huchanganywa sana na fikra za utumwa kiasi kwamba tunashindwa kuchanganua mazuri toka ktk mabaya yetu wenyewe..
Kwa mdanganyika ni sawa na halali kwa mtu mweusi mwenziwe kuhodhi mali kama kaburu na akayafanya mabaya yote kama Kaburu na pengine zaidi ya kaburu atapata utetezi lakini sii mzungu ama kabila nyingine..
Hayo ya Lowassa na kundi lake ni sawa kabisa na makaburu ama wakoloni waliotutawala kwa karne..Bianfsi kilichobadilika leo ktk utawala wetu ni rangi ya ngozi ya Mtawala, laa sivyo hawa watu wamerithi mabaya yote ya mkoloni isipokuwa inasomeka tu kwamba mshale ukiwa ktk namba 3 isomoke kwa kiswahili kama ni saa tisa sio saa tatu..Na hunichosha sana kuona vijana wetu wakihalalisha mabaya ya viongozi wao kwa vigezo dhaifu kaa hivi..Its OK kwa Lowassa kuwa na mashamba makubwa sana akawalimisha wananchi lakini asiwe mzungu, mwarabu au mhindi watu wataingia na mikuki kumtoa lakini kifupi hakuna faida kwao ktk hali yeyote ile.iwe mtawala ni mweusi maadam kunakucha who cares!
 
Mheshimiwa Spika, wewe ni Mwanasheria unafahamu suala la Natural Justice. Kwamba Kamati Teule imesikiliza watu wengine wote pamoja na wanaoita minong'ono ya mitaani, wamesafiri mpaka Marekani kutafuta mashahidi, lakini mimi ambaye ni mmoja kati ya watuhumiwa mle hawakunihoji hata siku moja.

Mheshimiwa Spika, nimesimama kueleza masikitiko yangu. Ofisi ya Bunge mpaka ofisini kwangu hata kama wangeniita ningekwenda kwa miguu kama hamna gari na nilikuwa tayari kufanya hivyo.<font face="Georgia"><font size="3">
Mkuki kwa nguruwe; Lowasa anahitaji NATURAL JUSTICE, ilhali yeye hakupata kuwafanyia hivyo waliochini yake. Mhe. unakumbuka alikuwa akiwafokea kama watoto wadogo DCs na DEDs. Kama umesahau, unakumbuka kisa kati ya Lowasa na DC-Ilemela Col PETER MADAHA? Lowasa ni fisadi hata mkianzisha magazeti mia kidogo. Au unataka kutulatea kisa cha JIWE WALILOLIKATAA WAJENZI? Kukuche kusiche Lowasa wenu hainuki tena kisiasa kuja kutumaliza. Damu yetu aliyokunywaa inatosha.
 
Lowasa badala ya kulia na kulaumu angeomba muda kwa spika ili atoe ufafanuzi hakufanya hivyo. Badala yake aliamua kujiuzulu na aliyemteua akakubali. Hapo ndipo kuna maelezo ambaye wanayoyajua ni Rais, Lowasa na labda wakubwa wengine. Sisi watu wa kawaida tulitegemea angelijitetea kama kulikuwa na ulazima. Mbona hakufanya hivyo? Anajitetea kwa lipi ilihali kamati ya Mwakyembe haikuanika role yake kwenye saga hiyo? Kuna nini ambacho kimefichwa mpaka akaamua kujiuzulu? Ukisoma between the lines of his statement utaona uwaziri mkuu was on the line. Hapo pana jambo tumefichwa.
 
Go on Eddo... tell us the truh! only the truth will make u free n bcome new prezda 2015 or b4 kama mkuu ataamua kujiuzuru kwa ukweli utakao toa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom