In DEFENCE of LOWASSA (Warioba & Butiku on it)

Nategemea a hot debate next week juu ya Richmond pamoja na kwamba kuna watu wamesha wajibika .Wabunge si wajinga waache kujadili hili .Labda lizimwe but am sure serikali lazima itoe majibu .Now Mwanyika anangoja nini kujiondoa ama anangoja huruma ?Mbona yuko kimya ?

Hot debate in which direction? I am sure kuna wabunge watataka kuifufua lakini wabunge wa CCM wote watalimwa vimemo alivyovisema Mama Kilango na wabunge wa upinzani watazimwa kama wanavyozimwa kila siku.

Lowassa kajiuzulu and that is the best you can get out of this system.Ushamsikia Mizengo Pinda anasema "yaliyopita si ndwele tugange yajayo"

Lowassa was privy to many of Kikwete's deals na kum corner kunaweza kusababisha a mess on Kikwete's hands.He does not want that.

Next week kila mtu atakuw kwenye euphoria ya serikali mpya.
 
Naomba kuuliza, maana mimi siyo mtaalam wa sheria. Kuna paragraph moja kwenye report inasema kwamba iwapo Msabaha, Mwakapugi na Balozi Kazaura wangemtaja EL kwamba anahusika basi Kamati ingeweza kumhoji kwa kiapo.

Juzi Dr. Mvungi alisema kwamba kitendo cha kamati kumhoji EL akiwa PM ilikuwa ina amount kwenye situation ya impeachment kitu ambacho ni cha kikatiba zaidi. Swala la kura ya kutokuwa na imani na PM lazima kuwe na grounds za kueleweka. Kwa hiyo Kamati haikuwa na nguvu ya kumwita kumhoji ili kupata maelezo ya upande wake. Hapa inabidi watu wajiulize, je, ni kwanini Msabaha na Balozi Kazaura walikubali kusema "bangusilo" wakiwa nje ya kiapo na hawakusema wakiwa kwenye kiapo? Nadhani hapa kuna fumbo kubwa sana na vigogo hao hawakutaka kuleta balaa ya impeachment na walidhani kwamba kwa kufanya hivyo wangekuwa wanamtetea PM!

Conclusion ya Kamati iko wazi, imesema ushahidi wa mazingira, mawasiliano, na kiburi cha Wizara ya Nishati na Madini vina m-implicate EL. Paragraph iko hapa:

Kwa hiyo mimi naona tu kwamba Mzee EL alikuwa anatafuta mwanya wa kutokea ili aonekane ameonewa. Afterall atakuwa anaona amekufa kiume, lakini ningeona amekufa kiume zaidi iwapo angepangua hoja moja baada ya nyingine na finally akasema kwamba kwa kuwa amechafuliwa sana na report ya tume anaamua kubwaga manyanga. Hakujibu hata hoja moja na pia hata alipobanwa na Selelii akafuta claims nyingi na ikabaki moja kwamba ni mstari mmoja tu wa kwamba RDC ni mradi wa EL na RA. Lakini hao si maneno ya Kamati, bali ni maneno ya Balozi Kazaura na Mzee wa Bangusilo. Msabaha kwenye uteteji wake hakukanusha kutamka maneno hayo, so kuituhumu Kamati kwamba ilimsingizia bado naona ni kichekesho. Alitakiwa ambane Msabaha na Kazaura kama kweli RDC ni mali yake!

Keil,

Of course EL alikuwa anatafuta pa kutokea, my thing is, hawa wajinga kina Msabaha Kazaura na Karamagi waliotoa ushahidi wa half truth undr oath na kutoa ushahidi mwingine nje ya kiapo, inabidi watafutiwe mashtaka ya obstruction of justice kwa sababu hawakuipa kamati "the truth and the whole truth" under oath.Otherwise oath yetu inakuwa bonge la joke.Unless walikula deal fulani la kutoa info outside of oath without repercussions.Ndiyo maana ES anasema hii ni "rule of politics" wala siyo "rule of law".

My thing siyo kwamba nalaumu tume ilimsingizia.My thing ni kwamba regardless ya walichosema Kazaura, Msabaha na Karamagi, Kamati ilikuwa na ushahidi mkubwa tu wa kumuhoji Lowassa, bila ya kuwa na issue ya impeachment kwa sabau unapomuhoji kuna outcomes mbili, moja ya yeye kuweza kuyaexplain vizuri maswali yote na nyingine ya yeye kushindwa kuya explain.Sijui issue ya impeachment inatoka wapi?
 
Kwa hiyo kesho na keshokutwa tukikuundia a witchhunt committee itakayoku frame na kukusomea a summary execution report bila kukupa nafasi ya kujitetea itakuwa poa tu.Au siyo?

Kama ningekuwa mimi ndio Lowassa na ripoti imenitaja bila kuhojiwa huku nikijua sina hatia yoyote, nisingejiuzulu bali ningei-challenge bungeni hiyo ripoti katika mjadala. Na ningeleta ushahidi wote wa kuwaumbua wanaonipakazia, na mwishowe tungempata anayesema uongo. Na kama kamati ya kina Mwakyembe ingekuwa imesema uongo kwa nia ya kumdhalilisha waziri mkuu, ambacho kingefuata baada ya bunge kuridhika kuwa Mwakyembe na wenzie ndio waongo, Mudhihir angetoa hoja kuwa wapewe adhabu kama ile ya Zitto Kabwe! Sasa kinyume chake Lowassa kajiuzulu badala ya kujitetea, bado mnasema kaonewa wakuu? Nafasi ya kujitetea mbona ndio hiyo hapo bungeni, au alitaka asikilizwe wapi? Na huo uamuzi wa kujiuzulu ninyi mnaona ametekeleza mapendekezo ya kamati au ya utashi wake? Kamati haikupendekeza waziri mkuu ajiuzulu, awajibike au awajibishwe. Pendekezo linalomhusu waziri mkuu katika ripoti ya kamati teule ni lile la 16, ambako sehemu iliyoelekezwa kwake moja kwa moja ni ile inayosema (nanukuu): "Kwa kuzingatia umuhimu wa nafasi aliyonayo Mhe. Waziri Mkuu katika uendeshaji wa shughuli za Serikali na uongozi wa nchi kwa ujumla, ni wajibu wake yeye mwenyewe kupima uzito wa matokeo ya uchunguzi huu na wajibu wake kikatiba ndani na nje ya Bunge" (uk.48). Hawakusema ajiuzulu, tofauti na mapendekezo waliyotoa kwa wengine ambapo walitamka waziwazi kuwa "wawajibishwe" na kina Msabaha na Mwakapugi "wachukuliwe hatua kali za kinidhamu" (uk 47). Kwa hiyo Lowassa alipewa nafasi ya pekee, ya kupima uzito wa matokeo hayo na kuchukua hatua mwenyewe, na hatua aliyoona inamstahili ni kujiuzulu, sasa uonevu uko wapi hapa?

Nina uhakika hatua aliyojichukulia ni ndogo kuliko adhabu anayojua anastahili kwa makosa yake. Hii ni kutokana na uzoefu wangu wa kuwafahamu binadamu katika kujihukumu wenyewe, huwa wanachagua adhabu iliyo nafuu. Nilipokuwa mwalimu shuleni, mwanafunzi akikosa nikimwambia achague adhabu aliniambia "nisamehe mwalimu!" Na nikimsisitizia kuwa nimeamua atandikwe viboko na hivyo nikimtuma akalete fimbo, atakuja na kafimbo kadogo alikokachomoa kwenye ufagio wa "chelewa!" Na hata ninapopata ile fimbo ninayotaka kutumia nikimuuliza "nikuchape viboko vingapi?" anajibu "kimoja!" au akiona aibu kidogo "viwili" bila kujali ukubwa wa kosa. Kwa hiyo Lowassa amejikadiria mwenyewe anachostahili, lakini bado ni kidogo sana kilichomkuta, tunapaswa tumwongezee: tumshtaki mahakamani na arudishe yote aliyokwiba hadi sasa.
 
Watu tushamsema sana Lowassa kabla na baada ya ripoti, ukweli ni kwamba Mwakyembe na tume yake waliogopa kumuhoji Lowassa,wakapindisha the basic pinciples za fairness, rule of law na due process.

You appear to be adept at throwing around bombastic, technical terms without understanding their true meaning within the legal context.

That said, why don't you tell us what you understand by "basic pinciples za fairness", "rule of law" and "due process", and how each of these relates to the contents of the Mwakyembe Commission report and subsequent resignation of Lowassa and his sidekicks.
 
Pundit,

Nadhani report ilishasema kuwa kulingana na sheria ya Bunge hiyo ilikuwa kazi ya Waziri mkuu mwenyewe na Bunge..
Kuna sheria ambazo zinamlinda Rais, Makamu wa rais na Waziri mkuu ambazo kwa heshima ya wadhifa wao hupelekwa kama walivyozipokea, unless ziwe ni tetesi na hiyo ni kazi ya Paparazi kuhoji vitu kama hivyo...Wao ni wachunguzi na nafasi ya Waziri mkuu kujieleza ilikuwa Bungeni ama kwa mkuu wake JK.

Kifupi nitakubaliana nawe ukisema Lowassa hakutendewa haki pale rais alipokubali barua yake ya kujiuzuru... haikutakiwa kabisa aikubali na kuacha swala hili linaelea.. so kama kuna mtu alompa nafasi Lowassa ya kuanza tunga visingizio ni rais mwenyewe ambaye Lowassa alimfuata na kulia swala hili lisifike bungeni. Kukubali kwa rais ombi la waziri mkuu kujizuru ndilo limeondoa nafasi ya Waziri mkuu kuhojiwa, mbona nasikia rais alikataa ombi la Balali?... ilikuwaje iwe rais ndiye kamsimamisha kazi hali Balali iliwakilisha ombi lake... kisheria kuna kitu gani hapo ambacho rais alijaribu kuepuka barua ya awali ya Balali?... think about that brother!
Pili ni wananchi hatukutendewa haki ktk sakata hili kwani viongozi wote wamejiuzuru sasa kilichobaki ni tetesi na kuomba Mungu mapendekezo ya kamati hiyo yafanyiwe kazi..

Labda cha muhimu zaidi ni sisi sote tusonge mbele, Lowassa hajashtakiwa bado kwa hiyo, hiyo sheria na upuuzi mwingine utakuja hapo tutakapo mvuta mahakamani, bila shaka ataipata haki yake kabla ya kufikishwa rumande.
 
Sasa kinyume chake Lowassa kajiuzulu badala ya kujitetea, bado mnasema kaonewa wakuu?

Kithuku,

Nani kasema Lowassa kaonewa? Tatizo ni kwamba kwenye sheria, haki si muhimu tu kupatikana, bali pia ni muhimu haki kuonekana kuwa imepatikana.Beef yangu siyo juu ya incident, it is more about the process and principle.

Kwa hiyo ukifanya kazi na kutoa ripoti ya haki, lakini ambayo inaweza kuwa spinned kuwa haki haikutendeka, unaweza kuleta grounds za watu ku question kama haki imetendeka.

Ndiyo maana Lowassa anapata msemo hajahojiwa, kwa sababu kwa kutohojiwa amepewa nafasi ya ku-spin mambo kwamba hajatendewa haki.

Nilitaka Lowassa abanwe akose hata pa kutokea kirahisi rahisi kama hivyo.Ingewezekana kabisa speech ya kujiuzulu ya Waziri Mkuu ingekuwa ya kuwaomba msamaha Watanzania kwa ubadhirifu wake (kwa kukosa cha kutokea), au kungekuwa na perjury charges against Lowassa kwa kudanganya under oath.Mwakyembe kwa kutomhoji Lowassa amewanyima Watanzania any of those teo outcomes, instead Lowassa sasa yuko huru kama mbunge na mfanyabiashara.
 
Pili ni wananchi hatukutendewa haki ktk sakata hili kwani viongozi wote wamejiuzuru sasa kilichobaki ni tetesi na kuomba Mungu mapendekezo ya kamati hiyo yafanyiwe kazi..

Labda cha muhimu zaidi ni sisi sote tusonge mbele, Lowassa hajashtakiwa bado kwa hiyo hiyo sheria na upuuzi mwingine utakuja hapo tutakapo mvuta mahakamani, bila shaka ataipata haki yake kabla ya kufikishwa rumande.

Mkandara,

Do you seriously believe Lowassa will be dragged to court under the current settings?
 
Ndio maana nimesema tuombe Mungu!..... what else mkuu wangu hatuwezi shindana na dola. Kifupi mimi nasema kama kuna watu ambao hawakutendewa haki basi ni sisi wananchi!.. sababu nimezieleza hapo juu na kuna uwezekano mchezo umekwisha!..

Wamejiuzuru na ndio kuwajibika kwenyewe..
 
You appear to be adept at throwing around bombastic, technical terms without understanding their true meaning within the legal context.

That said, why don't you tell us what you understand by "basic pinciples za fairness", "rule of law" and "due process", and how each of these relates to the contents of the Mwakyembe Commission report and subsequent resignation of Lowassa and his sidekicks.

If this appear to be bombastic according to your level I cannot help you.

Basic principles za fairness ni kuwa baba mwenye watoto wawili akiletewa shauri la food fight kati ya watoto wake, au accusation ya mtoto mmoja kaiba hela, kabla ya kuhukumu au kumpeleka polisi mtoto inabidi a establish validity ya claims za side zote kwa kuwahoji wote.Huhitaji kuwa mahakamani ili upate a fair hearing hii hata the ancients walifahamu ndiyo maana hata mfalme Suleiman alipoletewa case ya wanawake wawili waliogombea mtoto mmoja hakutoa ruling mpaka aliposikia sides zote.

Rule of law, due process na principles za fairness zote zinakumbatia fair hearing.

Tatizo ni kuwa unataka kutuambia kuwa kuna legal context katika concept za common sense, kama vile common sense, the bigger set, is drawing from the legal frame of reference, wakati in actual fact the legal frame of reference is drawn from common sense.
 
E Lowassa.............kama mwenyewe ulivyosema kuwa tatizo hapa ni "UWAZIRI MKUU"..............tulio wengi tunasema NO.........Uwaziri Mkuu si Hoja.......tunataka ujitetee kwa hoja na sio kwa KILIO tunataka pia utueleze mali zako umezipataje............WE ARE NOT DONE WITH YOU YET!!
 
Mjomba, Hapa aliyeletwa mashtaka ni Bunge ndiye nabii Suleiman. Na mtoto kisha kubali makosa hata kabla hajasikiwa kachuma kiboko mwenyewe!
 
Huu mjadala ni mzuri na unaonyesha ni jinsi gani watu tulivyo na njia mbali mbali za kupambanua mambo.

Mi nadhani wengi humu hatujaisoma na kuichanganua hii report kwa vile ni ndefu. Kifupi report ilisema, watu ambao wangeipa basis ya kumhoji PM ni Waziri Msabaha, Kazaura na Mwakapugi. Sasa hawa jamaa waliogopa kumtaja PM directly! (wangemwaga unga) na badala yake wakasema kwamba waliyoyafanya PM hakuhusika (nidhanu za woga na maslahi!!) lakini wakaamua kukubali uhusika wa PM nje ya kiapo! simply put it, evidence was too much for Edward to be spared...So what we see here, Harrison and his committee walikuwa very brave! kutoa evidence ambazo wahusika kama waziri na katibu mkuu waliogopa kuzitaja kwenye kiapo! Na kama Msabaha na Mwakapugi wangetoa evidence dhidi ya PM chini ya kiapo, then tume inge-recommend hatua dhidi ya PM!! lakini kwa vile hawakufanya hivyo, ndo maana na wao tume hawaku-recommend chochote dhidi ya Edward! Tukubali, kitendo cha mwakyembe to expose such damning evidence against the most powerful and manipulative man in the country is just examplary na kitendo cha kizalendo mno. Ni wachache sana wanaoweza kufanya hivyo! Watanzania wengi sisi tuna nidhamu za woga hata Mwakyembe alisema. Hata hao akina warioba na Butiku wamechair tume ngapi? what have we seen from their commissions? Simply put it, tume ya Harrison ilifanya kitu ambacho kwa Tanzania hakijawahi kutokea na niwachache wangeweka kukifikiria kwamba kinaweza kutokea...kumwanika kiongozi wa ngazi za juu kama Lowassa..it takes courage na patriotism ya hali ya juu..

Mi ni katika wale wanaoamini kwa dhati kwamba kitendo cha Harrison et al kuexpose maovu ya Edward walisukumwa na uzalendo kwa nchi yetu, wanaona akina yakhe wanavyohangaika na huu umeme kila siku...Jamani ni uzalendo, hata kama wengi watataka kuitafsiri in either way..

Iweje Lowassa atangaze nia ya kujiuzulu wakati hata hiyo report haijajadiliwa? Ni kwa misingi ipi jamaa alimwambia Rais nia yake ya kujiuzuru hata wakati report haijaletwa bungeni? Nadhani Tanzanians we are better than this. Lowassa wants to fool us. Kwa nini hakujitetea wakati alipopewa nafasi na badala yake akaitumia nafasi hiyo kuwaaga wabunge kwamba ameshajiuzuru? Alikuwa ameshachukua uamuzi wakati report haijasomwa! Yes, even the speech was already prepared!! what a coincidence!!

Iam sure now people especially in government will be more alert because they know that when you do cover up.......ultimately it will be known and the price is high.
 
E Lowassa.............kama mwenyewe ulivyosema kuwa tatizo hapa ni "UWAZIRI MKUU"..............tulio wengi tunasema NO.........Uwaziri Mkuu si Hoja.......tunataka ujitetee kwa hoja na sio kwa KILIO tunataka pia utueleze mali zako umezipataje............WE ARE NOT DONE WITH YOU YET!!

Kwa nini ajieleze Lowassa tu? Kwa nini wote wasijieleze mali zao wamezipata wapi? Kwani fisadi katika Tanzania ni Lowassa peke yake?
 
If this appear to be bombastic according to your level I cannot help you.

Basic principles za fairness ni kuwa baba mwenye watoto wawili akiletewa shauri la food fight kati ya watoto wake, au accusation ya mtoto mmoja kaiba hela, kabla ya kuhukumu au kumpeleka polisi mtoto inabidi a establish validity ya claims za side zote kwa kuwahoji wote.Huhitaji kuwa mahakamani ili upate a fair hearing hii hata the ancients walifahamu ndiyo maana hata mfalme Suleiman alipoletewa case ya wanawake wawili waliogombea mtoto mmoja hakutoa ruling mpaka aliposikia sides zote.

Rule of law, due process na principles za fairness zote zinakumbatia fair hearing.

Tatizo ni kuwa unataka kutuambia kuwa kuna legal context katika concept za common sense, kama vile common sense, the bigger set, is drawing from the legal frame of reference, wakati in actual fact the legal frame of reference is drawn from common sense.

I can see you are introducing yet another piece of legal jargon, namely "fair hearing". Sijaona umetoa jibu kuhusu jinsi hizo dhana ulizozitaja zinahusiana au zina-apply vipi na kazi ya tume kama ile ya Mwakyembe. Jee unajua maana na kazi ya tume vis-a-vis mahakama? Pia isingekuwa vibaya kama ungetuambia mandate waliopewa tume ya Mwakyembe.
 
Masanja,
Maneno yako kweli tupu ndio maana mwanzo wa mada hii nilisema kama wangekwenda kwa Lowassa na he said/she said kinda of evidence angewauliza kitu kimoja tu - who said that?..Hivi kweli mnakuja ofisini kwangu kuniuliza vitu ambavyo mtuhumiwa fulani kasema ati mimi ni mmiliki wa Richmond?...can you prove that?..wote wangeonekana wajinga.
Leo hii tungekuwa tumelala kizani kwani ktk hatua zote za upatikanaji wa Tender hiyo ofisi ya waziri mkuu kisheria haikutakiwa kuingilia hata kidogo na kifupi haimo.. Sasa cha kujiuliza sisi ni hizi nguvu za cheo hiki!.. na tumejifunza nini.
 
jamani sasa naona tufikie mwisho wa mjadala huu.
let me create a scenario, then we will see what is what;;;;;

pundit ni kibaraka wa lowassa. ndio nimesema na ninapendekeza hajitoe humu ndani kwa kuangalia namna mwendo wake uko gizani.

watch what happens next ;;;;;;;; tik tak tik tak
 
Kithuku,

Nani kasema Lowassa kaonewa? Tatizo ni kwamba kwenye sheria, haki si muhimu tu kupatikana, bali pia ni muhimu haki kuonekana kuwa imepatikana.Beef yangu siyo juu ya incident, it is more about the process and principle.

Kwa hiyo ukifanya kazi na kutoa ripoti ya haki, lakini ambayo inaweza kuwa spinned kuwa haki haikutendeka, unaweza kuleta grounds za watu ku question kama haki imetendeka.

Ndiyo maana Lowassa anapata msemo hajahojiwa, kwa sababu kwa kutohojiwa amepewa nafasi ya ku-spin mambo kwamba hajatendewa haki.

Nilitaka Lowassa abanwe akose hata pa kutokea kirahisi rahisi kama hivyo.Ingewezekana kabisa speech ya kujiuzulu ya Waziri Mkuu ingekuwa ya kuwaomba msamaha Watanzania kwa ubadhirifu wake (kwa kukosa cha kutokea), au kungekuwa na perjury charges against Lowassa kwa kudanganya under oath.Mwakyembe kwa kutomhoji Lowassa amewanyima Watanzania any of those teo outcomes, instead Lowassa sasa yuko huru kama mbunge na mfanyabiashara.

Mahali pa Lowassa kuonesha innocence yake palikuwa pale bungeni, kwani alikuwa hajahukumiwa bado. Wenzie wote hukumu zilipendekezwa dhidi yao, yeye akaachwa. Baada ya kusikia yaliyosemwa kwenye ripoti, hakupaswa tu kusema "sikuhojiwa" na kuishia "najiuzulu". Angesema "sikuhojiwa, na ukweli ni huu hapa" halafu aweke ukweli wote mezani ujadiliwe dhidi ya hiyo ripoti, au angesema kwa kuwa hajahojiwa naye pia anaomba muda ahojiwe kama wenzie! Kwani aliyasema hayo akakataliwa? Hakuna haki yoyote iliyokiukwa hapa, maana hadi sasa tunavyojadili hapa hakuna hatua hata moja iliyochukuliwa na bunge kutokana na ripoti ya Kamati teule, watu wamejiuzulu wakati bado mjadala unaendelea. Kwa kuwa mjadala wa ripoti bungeni haujahitimishwa na bunge halijatoa maazimio yoyote kuhusu ripoti hiyo, hadi sasa hakuna yeyote aliyenyimwa haki.
 
.......................Nilitaka Lowassa abanwe akose hata pa kutokea kirahisi rahisi kama hivyo.Ingewezekana kabisa speech ya kujiuzulu ya Waziri Mkuu ingekuwa ya kuwaomba msamaha Watanzania kwa ubadhirifu wake (kwa kukosa cha kutokea), au kungekuwa na perjury charges against Lowassa kwa kudanganya under oath.Mwakyembe kwa kutomhoji Lowassa amewanyima Watanzania any of those teo outcomes, instead Lowassa sasa yuko huru kama mbunge na mfanyabiashara.

....hiyo quote imetulia Mkuu Pundit.......ngoja nizame tena kwenye ripoti........je ishu ni yeye kuhojiwa tu au ni EL kutakiwa kutoa ushirikiano in whatever way.....unajua wakti mwingine unaweza ukawa umetoa maelezo kwa maandishi na kusiwe na umuhimu wa kuhojiwa.....kama maandishi yamejitosheleza......na wakti mwingine unaweza ukatakiwa/ukaombwa utoe maelezo kwa maandishi..........kuna mawili kujibu au kutojibu.....vyote hivyo vinaweza visijenge hoja ya fulani kuhojiwa
 
If this appear to be bombastic according to your level I cannot help you.

Basic principles za fairness ni kuwa baba mwenye watoto wawili akiletewa shauri la food fight kati ya watoto wake, au accusation ya mtoto mmoja kaiba hela, kabla ya kuhukumu au kumpeleka polisi mtoto inabidi a establish validity ya claims za side zote kwa kuwahoji wote.Huhitaji kuwa mahakamani ili upate a fair hearing hii hata the ancients walifahamu ndiyo maana hata mfalme Suleiman alipoletewa case ya wanawake wawili waliogombea mtoto mmoja hakutoa ruling mpaka aliposikia sides zote.Rule of law, due process na principles za fairness zote zinakumbatia fair hearing.

Tatizo ni kuwa unataka kutuambia kuwa kuna legal context katika concept za common sense, kama vile common sense, the bigger set, is drawing from the legal frame of reference, wakati in actual fact the legal frame of reference is drawn from common sense.

Bunge ndilo lililoletewa hiyo ripoti, wakati bado linajadili (ambapo ndio nafasi ya Lowassa kueleza his side of the story), yeye akaamua kukatisha kwa kusema anajiuzulu. Nadhani inafaa wakati mjadala wa ripoti hii utakapoendelea huko bungeni, Lowassa abanwe ajibu tuhuma hizi, maana amekwepa kuzijibu.
 
Back
Top Bottom