In DEFENCE of LOWASSA (Warioba & Butiku on it)

Mzee ES,

Respect Mkuu. Hivi unataka kuniambia kuwa kwa kujiuzulu kwake basi asihojiwe tena na Bunge? Tunataka wakirudi, akalishwe kikao na ajieleze. Kama tutasema hamna sababu ya yeye kujieleza tena maana si Waziri Mkuu, basi ina maana Rais kakubali kuzimika kwa hoja na uchunguzi mzima ikiwa mtuhumiwa mkuu atapewa kinga ya kutotoa au kujibu tuhuma kwa kuwa kajiuzulu!

Hivyo basi, narudia kuwa Kikwete kwa kukubali kwa Lowassa kujiuzulu bila kujibu hoja au kumrudisha kujibu tuhuma kuna maanisha kazi ya Mwakyembe ilikuwa ina walakini tangu mwanzo na dhumuni halikuwa kuchunguza Uhujumu bali ni kuleta hoja za kumsakama Lowassa aishie kujiuzulu na kuachia ngazi.

No wonder alisema it is about Uwaziri Mkuu! He walks a free man, despite being disgraced politically!

Rev,

I bet you my bottom dollar that the issue is over and you will hear no more of it.

Kumshitaki Lowassa au kumbana bungeni maana yake itakuwa kumnyang'anya kila kitu, a man with nothing to lose is a dangerous man.Lowassa akiwekwa katika position hiyo anaweza kuwa a loose canon, judging from the jazba aliyoonyesha kwenye resignation speech Kikwete would not want Lowassa to go ogg on him and his IPTL deal and others issues kama campaign finances.

Kwa hiyo Lowassa is sadly, home free.
 
Pundit, Kipande hiki kimefunga mjadala..

Hata hivyo kamati teule imetimiza wajibu wake kwa uwazi na ukweli kama ilivyoagizwa na Bunge letu tukufu. Kwa kuzingatia umuhimu wa nafasi aliyonayo Mheshimiwa Waziri Mkuu katika uendeshaji wa shuguuli za serikali na uongozi wa nchi nzima kwa ujumla, ni wajibu wake yeye mwenyewe kupima uzito wa matokeo ya uchunguzi huuu na wajibu wake kikatiba ndani na nje ya bunge. Vile vile ni wajibu wa Bunge ambalo linathibitisha uteuzi wake kwa mujibu wa Ibara ya 51 inayothibitisha uteuzi wake. Kuangalia ikiwa matokeo ya uchunguzi huu hayajaathiri hadhi na uzito wake ndani ya bunge.

That was the next step!

Hii ndiyo sheria ya Bunge na hatuwezi kubeba sheria za mtaani na kuzifungia kirago zikubalike!


Watu wanaandikia mate wakati wino upo. Nashangaa hata wanasheria kama Warioba bado tu wanatumia mate wakati wino upo.

Na majibu yapo wazi hapo bolded. Kwamba next step ilikuwa EL kuelezea his part and then bunge liamue na kuhitimisha kazi waliyoipa commission.

Ila kutokana na usanii wake EL akakwepa na kutangaza ghafla kujiuzulu.
 
Watu wanaandikia mate wakati wino upo. Nashangaa hata wanasheria kama Warioba bado tu wanatumia mate wakati wino upo.

Na majibu yapo wazi hapo bolded. Kwamba next step ilikuwa EL kuelezea his part and then bunge liamue na kuhitimisha kazi waliyoipa commission.

Ila kutokana na usanii wake EL akakwepa na kutangaza ghafla kujiuzulu.

Labda ndio kitu wanaita "collective responsibility" we all sink and drown or we all swim free!
 
Watu wanaandikia mate wakati wino upo. Nashangaa hata wanasheria kama Warioba bado tu wanatumia mate wakati wino upo.

Na majibu yapo wazi hapo bolded. Kwamba next step ilikuwa EL kuelezea his part and then bunge liamue na kuhitimisha kazi waliyoipa commission.

Ila kutokana na usanii wake EL akakwepa na kutangaza ghafla kujiuzulu.


Nategemea a hot debate next week juu ya Richmond pamoja na kwamba kuna watu wamesha wajibika .Wabunge si wajinga waache kujadili hili .Labda lizimwe but am sure serikali lazima itoe majibu .Now Mwanyika anangoja nini kujiondoa ama anangoja huruma ?Mbona yuko kimya ?
 
Yes Mfwatiliaji,

....EL katimua mbio huku anajifanya kaonewa.....alishaona ngoma hii ni nzito na haiwezi na ndio maana kakimbilia kujiuzulu........hana lolote........kiogozi mzima kama Waziri mkuu kuonyesha majazba!!!........aaaaaggrr!!!!!
 
Naomba kuuliza, maana mimi siyo mtaalam wa sheria. Kuna paragraph moja kwenye report inasema kwamba iwapo Msabaha, Mwakapugi na Balozi Kazaura wangemtaja EL kwamba anahusika basi Kamati ingeweza kumhoji kwa kiapo.

Mheshimiwa Spika, ushiriki huu wa karibu wa Waziri Mkuu katika kila hatua ya zabuni ya umeme wa dharura, si lazima uwe ushahidi wa kwamba kiongozi huyo wa kitaifa alihusika katika kuibeba Richmond. Unaweza pia ukawa ushahidi wa staili yake ya kawaida kabisa ya uongozi katika kufuatilia masuala yote ya kitaifa kwa karibu sana tukizingatia kwamba nchi wakati huo ilikuwa katika kipindi kigumu sana cha ukosefu wa umeme. Watu pekee waliokuwa wanaujua ukweli wenyewe, ukweli ambao ungeipa Kamati Teule msingi wa kumhoji Waziri Mkuu kwa kiapo, walikuwa watatu: Waziri Dk. Msabaha (Mb), Katibu Mkuu Mwakapugi na Mwenyekiti wa Bodi Balozi Kazaura.

Juzi Dr. Mvungi alisema kwamba kitendo cha kamati kumhoji EL akiwa PM ilikuwa ina amount kwenye situation ya impeachment kitu ambacho ni cha kikatiba zaidi. Swala la kura ya kutokuwa na imani na PM lazima kuwe na grounds za kueleweka. Kwa hiyo Kamati haikuwa na nguvu ya kumwita kumhoji ili kupata maelezo ya upande wake. Hapa inabidi watu wajiulize, je, ni kwanini Msabaha na Balozi Kazaura walikubali kusema "bangusilo" wakiwa nje ya kiapo na hawakusema wakiwa kwenye kiapo? Nadhani hapa kuna fumbo kubwa sana na vigogo hao hawakutaka kuleta balaa ya impeachment na walidhani kwamba kwa kufanya hivyo wangekuwa wanamtetea PM!

Conclusion ya Kamati iko wazi, imesema ushahidi wa mazingira, mawasiliano, na kiburi cha Wizara ya Nishati na Madini vina m-implicate EL. Paragraph iko hapa:

Uhuru mkubwa ambao viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini waliutumia bila wasiwasi katika kuhakikisha kwamba kampuni waliyoitaka, Richmond Development Company LLC, inapewa zabuni ya umeme wa dharura; maelekezo ya mara kwa mara ya Waziri Mkuu kwa Wizara katika kila hatua ya mchakato huo; upendeleo wa dhahiri ambao Richmond Development Company LLC iliupata kutoka taasisi mbalimbali za Serikali k.m Kituo cha uwekezaji (TIC) ambacho kilifikia hatua ya kufumbia macho baadhi ya taratibu zake za msingi ili kuipa kampuni tanzu ya Richmond Development Company LLC cheti cha uwekezaji haraka iwezekanavyo; kutotimiza masharti ya Bodi za Makandarasi na Wahandisi na Wizara ya Nishati na Madini kuikingia kifua kampuni hiyo isichukuliwe hatua za kisheria; uteuzi wa mwisho wa Richmond Development Company LLC kuwa mkandarasi kufanywa na Waziri Mkuu mwenyewe tarehe 21 Juni 2006;uamuzi wa kuiteua Richmond Development Company LLC kuwa mkandarasi kusafishwa na TAKURU ( sasa TAKUKURU) kuwa ulikuwa wa wazi na wa haki; uamuzi wa Serikali kuizuia TANESCO isivunje mkataba na kampuni hiyo licha ya sababu zote kisheria kuwepo, ni baadhi tu ya viashiria vya nguvu kubwa iliyo juu ya Wizara ya Nishati na Madini kutumika katika suala hili na Kamati Teule kutokana na ushahidi wa kimaandishi, kimazingira na wa mdomo, inaiona nguvu hiyo kuwa ni Waziri Mkuu.

Kwa hiyo mimi naona tu kwamba Mzee EL alikuwa anatafuta mwanya wa kutokea ili aonekane ameonewa. Afterall atakuwa anaona amekufa kiume, lakini ningeona amekufa kiume zaidi iwapo angepangua hoja moja baada ya nyingine na finally akasema kwamba kwa kuwa amechafuliwa sana na report ya tume anaamua kubwaga manyanga. Hakujibu hata hoja moja na pia hata alipobanwa na Selelii akafuta claims nyingi na ikabaki moja kwamba ni mstari mmoja tu wa kwamba RDC ni mradi wa EL na RA. Lakini hao si maneno ya Kamati, bali ni maneno ya Balozi Kazaura na Mzee wa Bangusilo. Msabaha kwenye uteteji wake hakukanusha kutamka maneno hayo, so kuituhumu Kamati kwamba ilimsingizia bado naona ni kichekesho. Alitakiwa ambane Msabaha na Kazaura kama kweli RDC ni mali yake!
 
Nategemea a hot debate next week juu ya Richmond pamoja na kwamba kuna watu wamesha wajibika .Wabunge si wajinga waache kujadili hili .Labda lizimwe but am sure serikali lazima itoe majibu .Now Mwanyika anangoja nini kujiondoa ama anangoja huruma ?Mbona yuko kimya ?

.........huyu Mwanyika anajifanya kichwa ngumu....sasa wacha watu tumuendee msitu.................
 
Watu wanaandikia mate wakati wino upo. Nashangaa hata wanasheria kama Warioba bado tu wanatumia mate wakati wino upo.

Na majibu yapo wazi hapo bolded. Kwamba next step ilikuwa EL kuelezea his part and then bunge liamue na kuhitimisha kazi waliyoipa commission.

Ila kutokana na usanii wake EL akakwepa na kutangaza ghafla kujiuzulu.

Tatizo ni kuwa validity ya hiyo document (ripoti ya Mwakyembe) inakuwa reduced na the fact kuwa hawakupata side ya Lowassa na kumpa nafasi ya kujieleza.Huwezi kufanya fact finding yoyote valid kwa kuangalia upande mmoja tu.
 
Nimekaa muda mrefu na nimeshindwa kujizuia.

a. Kuna baadhi yetu humu wanaliangalia suala hili kwa mwanga wa mahakamani. Kwamba, Kamati ingefanya kama inavyofanyika mahakamani ambapo mtuhumiwa anaitwa, mashtaka yake yanasomewa, upande wa mashata unaleta ushahidi wake halafu upande wa utetezi unaleta mashahidi wake na hata mtuhumiwa anaweza kupewa nafasi ya kujitetea. Hili ni kosa.

b. Bunge haliongozwi na taratibu za kimahakama au utaratibu wa uendeshaji mashtaki, uletaji ushahidi, na cross examinations. Nimesema "Bunge" kwa sababu Nguvu iliyo kwenye Bunge by extension ni nguvu ya Kamati zake. Hivyo, taratibu za madaraka, kinga, na nguvu ya Bunge yanaongozwa na Sheria ya "Nguvu, Kinga, na Madaraka ya Bunge ya 2008" na mabadiliko yake ya 2004.

c. Sheria niliyotaja hapo juu (na nimeiambatanisha) inaelezea utaratibu wa Kamati Teule nguvu zake n.k Hakuna mahali ambapo sheria inasema Kamati lazima ipate maelezo toka kwa mtu yeyote yule awe anadaiwa au mdai. Hata hivyo, wana nguvu ya kumuita mtu yeyote yule wakitaka na mtu huyo ana kinga fulani fulani.

d. Kwa upande wa kumuondoa Waziri Mkuu au hata Rais sheria na Katiba havina kipengele cha "utetezi". Kwa mfano, Rais amembaka mtu na kwa vile nikosa la jinai na Rais hawezi kushtakiwa basi Bunge linaona amevunja maadili basi bunge linaanzisha utaratibu wa kumuondoa (impeach). Utaratibu huo ulioko kisheria haumpi nafasi Rais ya kuelezea "kubakwa" kulikuwaje.

e. Na tukumbuke kuwa Waziri Mkuu hakulazimishwa kujiuzulu na hakuna mbunge aliyetoa hoja ya Waziri Mkuu kujiuzulu. Hata kamati katika ripoti yake ingetaka Waziri Mkuu ajiuzulu wangesema kwa maneno hayo, wamesema apime uzito wa ripoti hiyo na aangalie wajibu wake wa kikatiba (kile kiapo) na aone kama anaweza kuendelea na kazi zake.

f. Waziri Mkuu akafikiria na kuona kuwa ripoti hiyo ni nzito na asingeweza kuendelea na wajibu wake akaamua kujiuzulu. Uamuzi wa kufanya hivyo umefanywa na yeye binafsi au na chama chake, lakini kwa vyovyyote vile haukufanywa kama hoja iliyomfungia Zitto. Lowassa angetaka angesimama na kusema hajiuzulu kwani hana sababu na hakuwa na ulazima wowote wa kuwa mtu wa kwanza kuzungumza siku ile.

Yeye mwenyewe kwa maneno yake alisema kuwa Spika alipomdokeza kuhusu kinachokuja alienda akampa ushahidi "tena kwa maandishi" wa kutokuhusika kwake na Richmond. Ushahidi huo uliletwa Januari 29 wakati ripoti ya Bunge ilikuwa imemaliza kazi yake Disemba 31.

Kama ushahidi wake ulikuwa una nguvu, angewaacha wabunge wapige kelele siku zote mbili na mwishoni anapopewa nafasi ya kusema kitu (siyo kujitetea) kama alivyopewa Zitto angesimama na ushahidi wake na kuichambua ripoti ile kipengele kwa kipengele (kanuni ya hoja hujibiwa kwa hoja). Wabungee waliompigia kelele wangeonekana wakuja, na asingejiuzulu na kina Mwakyembe wangetakiwa wajustify walichofanya.

Hakufanya hivyo, kwa sababu alijua kuwa preponderous of evidence was overwhelmingly against him. Ushahidi aliokuwa nao usingiweza kuushinda ushahidi wa Dr. Mwakyembe.

g. Inasikitisha wanasheria kama Warioba wanashinda kuelewa jambo la msingi kama uwezo na nguvu za Bunge. Kama Mahakama ingesikia kesi ya Lowassa, na Lowassa asingepewa nafasi ya kutoa ushahidi au utetezi wake, na ikamuhukumu kwa kumkuta na hatia hapo tunasema haki haikutendeka. Haki inatafutwa mahakamani, Kamati Teule haitafuti haki, inatafuta ukweli na kuacha mambo ya haki Mahakamani.

h. Hata hivyo, naamini ingekuwa vizuri kama Lowassa angeitwa na kutoa maelezo yake au kufafanua mambo fulani. Hilo ni suala la maoni siyo suala la lazima. Hivi mmejiuliza hii natural justice mbona inaliliwa kwa Lowassa? Balali katimuliwa Benki Kuu, nani alimpa nafasi ya kumsikiliza?

Yeye katimuliwa kwa ushahidi wa kampuni inayolipwa fedha! Talk about injustice! Mbona Warioba na wenginee hawajalilia haki ya Balali kusikilizwa kabla ya kufanywa fisadi numero uno, au kwenye hili shamba wanyama wengine ndio wana haki zaidi na wengine ndiyo kama kina Balali!?

Huyu Lowassa anayelilia haki ya kusikilizwa alipomtimua yule Mhandisi pale Dar kufuatia kuanguka kwa lile Ghorofa, nani alisimamia haki ya maelezo ya Mhandisi yule, kwanini asisubiri maelezo ya kitaalamu? Alifanya vile kwa vile ilikuwa ndani ya uwezo wake kumtimua na binafsi sina tatizo nalo hilo.

Nyinyi mnaofanya kazi kama Marekani na Uingereza hujawahi kusikia mtu anaingia ofisini na kuitwa na bosi na kuambiwa hana nafasi tena kwenye hiyo kampuni na anatakiwa arudishe ufunguo n.k na wanaleta security guard kusimama kumuangalia anavyoondoka? Si angepewa nafasi ya kujitetea na kuelezea "ilikuwaje". No, we can not run a governemnt like that.

i. Pia tukumbuke kitu kimoja, Kamati haikuundwa kumchunguza Lowassa, Msabaha, au Karamagi they WERE not the subject of the investigation. Naomba muangalie terms of reference. Walitakiwa kuchunguza Richmond, they did that na walienda kwa Richmond yenyewe, hawa wengine ni casualties wa uchunguzi huo.

j. Mwisho nielezee hili la watu kukataa kwenda kwenye Kamati. Kama mnakumbuka nilipozungumza na Dr. Mwakyembe nilimuuliza suala la nguvu zahiyo Kamati. Naomba mrudie Sheria niliyoiambatanisha kuanzia Kipengele cha 13 ambapo kinazungumzia ushahidi.

Niwahakikishie jambo moja na please mark my words, hili halijaisha. Yona na Rostam wasidhanie hata kidogo kuwa wamedodge bullet na msishangae kabla Bunge halijaisha watu wakatiwa pingu. Mimi nikiitwa na mahakama hata kama niko safari mbinguni aidha nitoe maelezo na kupangag siku nyingine au nikatishe safari na kurudi. Siwezi kuamua tu kwa vile niko kijijini basi siwezi kuja.

Kamati teule inafanana na mahakama kwenye nguvu hii ya kuita mashaidi na kutoa arrest warrant. Angalieni sana wanakokwenda unless waanze kusema "tuyaache yaliyopita tugange yajayo".

Haya nisiwachoshe, I hope I have been of help. Niende zangu kulala, I haven't slept for the past three days!!!
 

Attachments

  • Hakimadarakayabunge3-1988.pdf
    151.4 KB · Views: 55
Masanja, Kichuguu na Bi Mkubwa nawapa salute kwa mchango wenu bomba. Mimi nawaunga mkono moja kwa moja kwamba haki ilitendeka na EL hana cha kulalamikia katika hili.

Mimi ninavyofahamu, japo si mtaaalam sana wa sheria. tume ya Mwakyembe iliundwa na Bunge na hivyo kuitwa Parliamentary Select Committee ambayo kazi yake ilikuwa ni kuchunguza uhalali au vinginevyo au ukamilifu wa taratibu zilizopelekea Richmond kupata mkataba wa kufua umeme na kama walikuwa na sifa na kutekeleza majukumu waliyopewa. Walikuwa pia na jukumu la kuangalia uhalali wa kisheria wa kuwepo kwa Kampuni hii na kama serikali ilifuata taratibu zote. Tume ilikuwa na jukumu la kukusanya ushahidi kwa kuangalia nyaraka na kuhoji watu mbalimbali na katika hatua hii, hakukuwa na shutuma zozote ambazo mtu yeyote alitakiwa kuja mbele ya tume na kutoa utetezi na wala tume haikuwa na jukumu la kutoa hukumu dhidi ya mtu yeyote na kwa hiyo, tume ndiyo iliyokuwa na utashi wa kujua yupi ni shahidi muhimu wa kujibu issues ambazo walikwa wame-frame ili kujibu au kutimiza terms of reference walizopewa.

Bwana EL alikuwa na fursa, kama walivyo wengine kujibu tuhuma zinazotokana na ripoti pale ambapo hukumu hutolewa napo ni Bungeni. Tume ilikuwa ni mwendesha mashtaka ambaye alikuwa anatuhumu mbele ya chombo amabcho ndiyo kilikuwa kifikie uamuzi na hapa ndiyo principles of natural justice zilikuwa zi-apply na kutoruhusu kumhukumu mtu bila kumsikiliza. Bunge lilimpa nafasi ya yeye kujitetea na yeye badala ya kutumia nafasi hiyo kutujulisha usahihi wa tuhuma hizo kwa kutoa utetezi wake aka-short circuit utaratibu na akaanza kulalamika kwamba hajatendewa haki na amezushiwa uongo bila kusema uongo huo ni upi na ukweli hasa ni upi. Mimi nafikiri amechezea nafasi muhimu sana ambayo ingetupa ukweli wa 'usafi' wake katika hili. Kwa kukatiza mambo na 'kukubali yaishe' ameonyesha watu kwamba hiyo ndiyo exit passage ambayo angeitumia kuchomoka kwenye huu mtego ambao vinginevyo ungemuumbua zaidi.

Kwa hiyo mimi natofautiana na majibu ya Mheshimiwa Selelii kwamba kwa nafasi yake waliona si vema kumuita. Ukweli ni kwamba hakukuwa na haja ya kumuita kama tume iliona hana ushahidi wowote wa kuongezea au kujibu kile ambacho tume ilikuwa inakitafuta.

Kwa hapa Mzee EL na washauri wake wa kisheria walichemsha!
 
Tatizo ni kuwa validity ya hiyo document (ripoti ya Mwakyembe) inakuwa reduced na the fact kuwa hawakupata side ya Lowassa na kumpa nafasi ya kujieleza.Huwezi kufanya fact finding yoyote valid kwa kuangalia upande mmoja tu.
Report ilikuwa ikichunguza Richmond siyo ofisi ya waziri mkuu, waziri mkuu kajiingiza mwenyewe kwenye hiyo soo.Hakukuwa na ulazima wa kumwita ili kuthibitisha maovu ya Richmond na ndiyo maana report ilisema wazi kwamba hoja zote za walio hojiwa zinampoint yeye waziri mkuu kwa hiyo ni vema afikirie kwa makini.

Fact zote walizozitaka kuhusu richmond walizapata, mengine yaliyo zuka ndiyo yamemwingiza PM kwenye soo.

Kimsingi kamati ilifanya kazi iliyotumwa kwa ufanisi mkubwa Waziri mkuu kulaumiwa ni by product ya uchunguzi na siyo main product.

Kugeuza yatokanayo na hoja kuu kuwa ndiyo centre ya mazungumzo ni kuturudisha nyuma hatua millioni.

Sijui kwa nini watu wana uchungu na wakisemacho ni dosari ya kamati, wakati huo huo hawasikitiki na kumlaani mtu aliyesababisha watanzania kuongezewa gharama ya kila kilowatt ya umeme, hata kama huyo mtu wanadhani si Lowassa.
 
Report ilikuwa ikichunguza Richmond siyo ofisi ya waziri mkuu, waziri mkuu kajiingiza mwenyewe kwenye hiyo soo.Hakukuwa na ulazima wa kumwita ili kuthibitisha maovu ya Richmond na ndiyo maana report ilisema wazi kwamba hoja zote za walio hojiwa zinampoint yeye waziri mkuu kwa hiyo ni vema afikirie kwa makini.

Fact zote walizozitaka kuhusu richmond walizapata, mengine yaliyo zuka ndiyo yamemwingiza PM kwenye soo.

Kimsingi kamati ilifanya kazi iliyotumwa kwa ufanisi mkubwa Waziri mkuu kulaumiwa ni by product ya uchunguzi na siyo main product.

Kugeuza yatokanayo na hoja kuu kuwa ndiyo centre ya mazungumzo ni kuturudisha nyuma hatua millioni.

Sijui kwa nini watu wana uchungu na wakisemacho ni dosari ya kamati, wakati huo huo hawasikitiki na kumlaani mtu aliyesababisha watanzania kuongezewa gharama ya kila kilowatt ya umeme, hata kama huyo mtu wanadhani si Lowassa.

Watu tushamsema sana Lowassa kabla na baada ya ripoti, ukweli ni kwamba Mwakyembe na tume yake waliogopa kumuhoji Lowassa,wakapindisha the basic pinciples za fairness, rule of law na due process.
 
Watu tushamsema sana Lowassa kabla na baada ya ripoti, ukweli ni kwamba Mwakyembe na tume yake waliogopa kumuhoji Lowassa,wakapindisha the basic pinciples za fairness, rule of law na due process.

Kama dr Mwakyembe na tume yake wangemwogopa sana Lowassa wangeshindwa kabisa kuisoma ile report.

Kitendo cha kuisoma ripoti kindadhihirisha kwamba Lowassa hakuwa tishio kwao jana wala kesho.
 
Kama dr Mwakyembe na tume yake wangemwogopa sana Lowassa wangeshindwa kabisa kuisoma ile report.

Kitendo cha kuisoma ripoti kindadhihirisha kwamba Lowassa hakuwa tishio kwao jana wala kesho.

Sikusema wamemwogopa sana nimesema wameogopa kumuhoji.Ukisoma sababu zao za kutomuhoji utaona walikuwa wanajinyeanyea tumuhoji tusimuhoji, wakaamua wasimuhoji kwa kuogopa wakaamjua kuleta mambo ya kuheshimu ofisi ya Waziri Mkuu, mtu aki violate principles hata akiwa rais mnamuhoji tu.

Sasa kwa sababu hawakumuhoji Lowassa tumemkosa kwa perjury! Ingetakiwa wamfuate kabla ushahidi haujajulikana, awadanganye under kiapo, halafu on top ya ma issue yote kuwe na perjury.

Hapo ndipo pangekuwa patamu, kwa maana ingekuwa clear kwamba Lowassa angetakiwa kufungwa kwa perjury alone, tungeona JK na usanii wake angefanyaje.

Sasa hivi utaona Lowassa ataendelea kutesa kama kazi.Halafu mnasema kutomhoji Lowassa haikuwa muhimu?
 
Watu tushamsema sana Lowassa kabla na baada ya ripoti, ukweli ni kwamba Mwakyembe na tume yake waliogopa kumuhoji Lowassa,wakapindisha the basic pinciples za fairness, rule of law na due process.

Pundit, hawakupindisha vitu hivyo, walifanya kile ambacho wanaweza kufanya ndani ya sheria. Lowassa, Karamagi and Msabaha were not the subjects of the investigation. Jinsi Kamati Teule inafanya kazi, haijitungii utaratibu bali inafanya kile ambacho ina uwezo wa kufanya. Kudai kuwa Mwakyembe (a Constitutional Scholar) kuwa haelewi maana ya Principles of Fairness, Rule of Law and Due Process ni kutrivialize his dedication to judicial process.

Kama alitakiwa kumchunguza Lowassa halafu angeandika ripoti na kusema "Lowassa ndiyo Nguvu Kuu" iliyofanya hivi au vile bila ya kumuuliza then and only then your assertion would be with merit.Na kama wangeogopa kusema walichosema tungeendelea kuwa na Lowassa Waziri Mkuu na Baraza hili hili.

Alichofanya Mwakyembe na timu yake kilitakiwa kufanywa na TAKUKURU ambao ndio walimuogopa Waziri Mkuu. Ukitaka kuzungumzia woga ni wabunge wale wote ambao walishindwa kumnyoshea kidole Waziri Mkuu hadi pale Mwakyembe na timu yake walipofanya hivyo.
 
People are making this sound like a witch hunt towards Lowassa and that he wasn't questioned...there was no need to question because this Report was about the background and the process of how this compay won the contract. It was never a panel setup to investigate the Prime Miniter. It would have been unfair for Lowassa if the commission was investigating him without him being questioned. The fact kwamba kakurupuka moja kwa moja na kujiuzulu ni ameonyesha kwamba amehusika sana, maana angejitetea na kusema mimi simo. Na hawa wakina Mwakyembe I am sure they have more evidence against him than what is on the report and they will use that as leverage (Insuance policy) Just incase huyu Lowassa akikurupuka na kujaribu kuwadhalilisha. The paper trail speaks for itself. It was up to wabunge to make their own conclusions. They were just a fact - finding mission and all that was said about lowassa and people being Bangusilo, those were people being quoted and not the words of the members commission.
I challenge Lowassa to say in what aspects was he treated unfair other than not being questioned...because kwasababu hukuulizwa haimaanishi umeonewa, sema ni nini umeonewa hasa na mambo gani ya kwenye report yamefanya umeonewa...report imedanganya bunge kivipi...atuambie
 
Phil tunaomba source kwa sababu unachosema haki make sense, kwamba walishauri ripoti iwekwe bungeni bila kupendekeza chochote is hogwash because technically Mwakyembe hakusema Lowassa ajiuzulu (not in so many words anyway) ila alishauri Waziri Mkuu atumie busara zake, ambayo inaacha wazi option ya rebuttal.

Watu wote walio objective, Warioba included according to the above post, na wanaojua misingi ya sheria wanajua kwamba haki inapoonekana kuwa haikutendeka haki haikutendeka, kwamba siyo tu muhimu kwa haki kutendeka, inabidi haki itendeke na pia haki ionekane kutendeka.Tatizo ni kuwa nikisema hilo hapa naonekana Lowassa apologist which is a very narrow minded outlook.

Watu hawawezi ku reconcile facts kwamba one might be appalled by Lowassa's clear corruption and also be dissapointed that the Mwakyembe Committee did not question Lowassa.

There is this euphoria now that everybody should be happy now that Lowassa is out, and nobody should question the tenets of the procedures.I beg to differ on principle.That Lowassa had to go is as they say a "no brainer" but it would have been nicer to see Lowassa denied any reason to say he was not given a chance to clarify things.I understand the logistics may have been challenging for Mwakyembe but we have to set high standards and care about precedents.

Chief Pundit,

Nashukuru sana kwa careful evaluation of the whole Kamati Teule deal and how Lowassa was treated. Nafikiri umetoa mchanganuo mzuri, wa kina na wenye kuzingatia rule of law and the importance of precedents.

Naafikiana nawe kuwa ripoti ya kamati hii imeset precedent ambayo kisheria, si precedent nzuri. However, there is one point that I'm not sure whether most of us ignore or simply overlook it. This issue is a very unusual case with a lot of twists and turn. This point is, to treat the case strictly on the legal perspective was almost impossible because it was also very political.

Ni kweli kamati haikumhoji Lowassa kupata maoni yake. Lakini, Lowassa, japo alikuwa ni Waziri Mkuu, bado alikuwa ni mwananchi na angeweza kujitetea pale ambapo Kamati ilisema kuwa mtu yeyote anaweza kwenda kuzungumza nao. Kwa vile kazi ya kamati ilikuwa ni kuchunguza mikataba iliendaje, na kwa vile Lowassa role yake haikuwa kusaini hiyo mikataba, basi hakukuwa na clear link ambayo ingempasa kujieleza mbele ya kamati. Lakini, kulikuwa na kila ishara/dalili kuwa mkono wake ulikuwepo kwenye kashfa hii na kutokana na mazingira ya woga ambao ulioneshwa na wale waliotakiwa kujieleza mbele ya kamati, nafikiri ilikuwa sahihi kwa kamati kueleza kuwa Waziri Mkuu (au ofisi yake) imehusishwa kwa namna moja au nyingine na hivyo wakamwachia yeye mwenyewe atumie busara yake.

Kutokana na mazingira ya kisiasa yaliyotawala mfumo wa nchi yetu, nafikiri kwa jinsi ripoti hii ilivyokuwa presented ni sahihi kabisa. Sasa katika kuset precedent, hiyo bado haijakwisha. Kamati imetoa ripoti, Bunge linatakiwa kufanyia kazi na hapo ndipo Lowassa anaweza kujitetea. Bunge litaifanyia kazi kwa kumwagiza AG to formally charge all individuals who were implicated in this scandal in the court of law. Sasa kama Lowassa hataitwa kujitetea (kama yeye si mshtakiwa), then clearly huo utakuwa ni uonevu.

Binafsi nafikiri kulikuwa na makosa katika kujiuzulu kwa Lowassa. Angetakiwa afukuzwe kazi kwa kushindwa kuzuia uzembe ufanyike chini ya uangalizi wake. The same should have applied to Msabaha, Karamagi na wahusika wengine wote kwa kutokuwa responsible kiasi cha kusababishia taifa hasara. Lakini, kwa vile everything ni politiki, Lowassa kajiuzulu, atapata marupurupu, anakuwa treated kama mstaafu na kubakia matawi ya juu as if nothing has happened. Huu ndio uozo tulionao...kila kitu kuwa cha siasa na kupoteza uwajibikaji. Whether he was implicated or not, Lowassa, following the principles of good governance alitakiwa aachie ngazi kwani alikuwa na poor management.

I think it is about time our leaders should learn to be responsible and we need to hold them accountable. Kitu kikubwa tujifunze kutokana na hili ni kuwa, Bunge na Serikali Kuu (The Executive and Legislature) zinahitaji kuwa huru ili kuweza kuwa na checks and balance system nzuri. Without this, kila kamati itakayoundwa itakuwa forced kufanya kazi kisiasa na labda kisheria (kama kamati ya Mwakyembe) kwani hivyo ndivyo mambo yalivyo.

Mkuu Pundit, maji yameshamwagika, lakini hakukuwa na jinsi bali kwa Mwakyembe kutumia staili hiyo. Not a good precedent. The good thing is, precedents can be reversed. Just remember the case of Dred Scott in the US:
'Dred Scott Case" or "Dred Scott Decision", was a lawsuit, pivotal in the history of the United States, decided by the United States Supreme Court in 1857 that ruled that people of African descent, whether or not they were slaves, could never be citizens of the United States, and that Congress had no authority to prohibit slavery in federal territories. It was also ruled that slaves could not sue in court, and that slaves were private property, and, being private property, can't be taken away from their owners without due process. The decision for the court was written by Chief Justice Roger Taney.

Thank God for the 13th and 14th Amendments of the US constitution that nullified this precedent!
 
Maji yameshamwagika hayazoleki kama ameonewa aende Mahakamani, ana hela nyingi anaweza kupata Lawyer yoyote anayemtaka.
 
Watu tushamsema sana Lowassa kabla na baada ya ripoti, ukweli ni kwamba Mwakyembe na tume yake waliogopa kumuhoji Lowassa,wakapindisha the basic pinciples za fairness, rule of law na due process.

Wacha kutuzuga na ujinga wako bana! Kwanza ulianza na "obstruction of justice", sasa unakuja na madudu mapya. Unajua wewe tatizo lako ni kwamba una tabia ya kutaja legal phrases, concepts and whatnot ambazo huelewi hata zinamaanisha nini haswa kisheria. Kuna tofauti kati ya kazi tume na ile ya mahakama ditto tofauti kati ya dhana za kuwajibika (accountability) na kutiwa hatiani (innocence & guilt).
 
Naona sasa ishakuwa mambo ya for/against Lowassa, ukija na grey shades in between zinazochambua vitu unaonwa unamkingia kifua Lowassa.

Mwanakijiji

Pundit, hawakupindisha vitu hivyo, walifanya kile ambacho wanaweza kufanya ndani ya sheria

Hawakufanya yote waliyoweza kufanya ndani ya sheria.Hakuna sheria iliyowanyima uwezo wa kumhoji Lowassa.Wamefanya uamuzi wa kutomhoji na kutoa ripoti inayomnyooshea kidole Lowassa yenye maswali kibao ambayo tungependa kumsikia Lowassa akiyajibu under oath lakini hatujamsikia.Hatimaye wamempa msemo kuwa "hakupewa nafasi ya kujitetea" na kupoteza momentum ya kuweza kum-prosecute Lowassa.Sasa hivi, partly thanks to this fact, all we will get is "yaliyopita si ndwele, tugange yajayo".Lowassa ataendelea kudunda bungeni with no charges and this will be the last you will hear of the matter, unless an insurmoutible amount of pressure is brought upon CCM.Which judging from misifa anayopewa Kikwete hivi sasa I doubt will happen.People are already happy that Lowassa is out.

Mwanahabari

People are making this sound like a witch hunt towards Lowassa and that he wasn't questioned

I am not sure which people you are talking about, but for my case I have documented clearly here kwamba ninachoongelea siyo incident, bali ni process na precedent.Nimeeleza kuwa simtetei Lowassa, ninaonyesha dissapointment yangu na jinsi kamati ya Mwakyembe ilivyo-squander nafasi ya kum-corner Lowassa under oath tumsikie ange-zi explain vipi zile barua zilizosomwa na Mama Kilango bungeni.Yaani hapa Mwakyembe angemhoji Lowassa tusingemsikia hata huyu Pinda analeta ujinga wa "Yaliyopita si ndwele, tugange yajayo".Lakini sasa hivi kwa sababu ya Lowassa kutohojiwa there is little chance of prosecution na mambo badala ya kupelekwa kisheria, yanapelekwa kisiasa.

Mara nyingine nikifikiria sana naona kama Kikwete amempunguzia kikombe mshkaji wake kwa kuiamuru kamati ya Mwakyembe kutomhoji, kwa sababu hainiingii akilini mtu makini kama Mwakyembe kuacha kumuhoji mtu mzito katika deal hili.

Mpanda Merikebu

Bunge litaifanyia kazi kwa kumwagiza AG to formally charge all individuals who were implicated in this scandal in the court of law

Do you want to make a wager on this? I will put my honor where my mouth is what you heard last week is the last about this whole brouhaha.Tayari Pinda kashapindisha any possibility ya hili kwa kusema "Yaliyopita si ndwele, tujaze yajayo"

Avenue

Wacha kutuzuga na ujinga wako bana! Kwanza ulianza na "obstruction of justice", sasa unakuja na madudu mapya. Unajua wewe tatizo lako ni kwamba una tabia ya kutaja legal phrases, concepts and whatnot ambazo huelewi hata zinamaanisha nini haswa kisheria. Kuna tofauti kati ya kazi tume na ile ya mahakama ditto tofauti kati ya dhana za kuwajibika (accountability) na kutiwa hatiani (innocence & guilt).

Avenue,

Ninavyoelewa mimi hizi concept ni very basic na hzina bounds kwamba "mtu anapata haki ya rule of law anapokuwa mahakamani tu, au anapokuwa na shauri mahakamani tu".Hasha.

Kama concepts za rule of law, fairness,na due process zinatakiwa kufuatiliwa whether tunaongelea police arrest, a high court case, a schoolchildren's food fight brought before a headtecher or a parliamentary probe basi ilitakiwa zitumike hapa pia.

Kama unaamini kuwa hizi concept hazitakiwi kutumiaka katika cases ambazo ziko nje ya mahakama, then unaweza kuwa na argument.Watu wanaongea kama vile kuna set/standard moja ya fairness kwa issues zilizo mahakamani na set nyingine ya fairness kwa isues zilizo nje ya mahakama as far as those basic tenets are concerned.


Tatizo ni kuwa, Maradona akifunga goli la Mkono linaloishindia Argentina ubingwa watu wanalifumbia macho hata baada ya replay.Au hata mkono unaitwa "Mkono wa Mungu"

OK, ulikuwa mkono wa mungu!
 
Back
Top Bottom