mageuzi1992
JF-Expert Member
- Apr 9, 2010
- 2,503
- 253
Ndugu KITIA boksi ya kupigia kura ipo wapi?
Michango mingi inayotolewa humu ukiangalia kwa makini kinachosababisha madhaifu yote hayo ni UDHAIFU WA KATIBA YETU. vote of no confidence ilipaswa iwepo kwenye katiba, sio kwa Rias tu hata Wabunge na Madiwani. Kipengele hiki kingemfanya Kiongozi aliyechaguliwa kujituma na kuwafanya waliomchagua kumu-asses mara kwa mara.
CHANGAMOTO: Tunapoimizana kuchagua wabunge wa upinzani wengi lengo la msingi ni kwenda kubadilisha katiba. Sasa hivi inakuwa ngumu kwani Mbunge wa upinzani akipeleka changamoto ya kubadili Katiba kitaitishwa kikao cha wabunge wa CCM na kuelezwa madhara ya kuingizwa kipengele hicho kwa CCM bila kuangalia madhara yake kwa wakulima na wafanyakazi.
SHIME SHIME WANAJAMII TUONGEZE WABUNGE WA VYAMA VYA UPINZANI.
Sipaoni pa kupigia kura au ballote boxes zimeibiwa nini?Sina imani hata kidogo na Serikali ya JK kwa sasa.
Wale wote wenye mtazamo kama wangu kuwa JK ameshindwa kuongoza nchi, hivyo asipitishwe tena kugombea 2010 kwa maslahi na usalama wa nchi yetu wagonge thanks hapa.
Tunaye tu JK wetu. Tatizo ni kwamba wengi mnaomkataa mlikuwa na "Marais" wenu ambao hawakuwa! Ajaribu tu kupunguza nguvu za kisiasa za wanafamilia wake wanazotaka kuwa nazo.
Unajua chini ya makubaliano ya serikali iliyo madarakani hivi sasa kule Kenya, Waziri anapoteuliwa ni lazima aidhinishwe (yaani going through CONFIRMATION process - ambayo Bongo hakuna kitu kama kama hicho) na Bunge la Kenya. Hivyo basi inapotokea Waziri yule akavurunda au Wabunge kukosa imani naye katika utendaji wake wana uwezo wa kumpigia vote of no confidence. Na Waziri Mkuu (Kama Kiongozi Mkuu wa Serikali ndani ya bunge) atalifikisha suala hilo kwa Rais (ambaye ndiye Mteuzi) na kufanya maamuzi juu ya Waziri husika. Na ndio kesi ya Waziri Amos Kimunya.Nimekuwa najiuliza kuhusu kura ya kutokuwa na imani (a vote of no confidence) Hii kura iko applicable kwenye sheria zetu za Tanzania au haipo. Lini bunge au baraza la mawaziri laweza kuitumia against waziri mwenzao au bunge juu ya waziri mkuu au raisi wa nchi. Katika matukio mbali mbali kama vile Israel waliishawahi kumpigia waziri mkuu Nentenyahu kura ya kutokuwa na imani http://findarticles.com/p/articles/mi_qn4158/is_19970625/ai_n14101252. Kenya leo wabunge wamempigia waziri wa fedha Amos Kimunya kura ya kutokuwa na imani baada ya kuuza hoteli ya kitalii kwa siri Reuters.com. Katika nchi yetu hasa wabunge wetu je inawezekana kwa wao kupiga kura ya kutokuwa na imani bungeni kwa Rais, Waziri Mkuu au Waziri yeyote kama wanafikiria hawako effective kutekeleza majukumu yao?
JF kama kuna mtu anaweza kutupa sheria na mazingira ya kura ya kutokuwa na imani rusha msaada basi!