Imani yetu kwa serikali ya Kikwete

Bado una imani na serikali ya Kikwete?

  • NDIYO (YES)

    Votes: 215 19.4%
  • HAPANA (NO)

    Votes: 834 75.1%
  • Sijui (Undecided!)

    Votes: 64 5.8%

  • Total voters
    1,111
Quote:
Bunge likishindwa kulinda katiba ambayo lenyewe limeitunga halina budi nalo litimuliwe. Na kama halitaki kuondoka wananchi wana haki ya kuwashinikiza wajiuzulu kwa kulizingira jengo la bunge.Wakiendelea kugoma hata baada ya kuzingirwa basi kinachofuata hapo mimi sitakuwepo nitakuwa nawahi Moscow kwenye mtaa wa machinga wa silaha kuuliza kama bunduki za AK 47 za mitumba wanazo na zinauzwa bei gani na zaweza wasili kwenye jengo la bunge lini na kwa usafiri upi wa haraka.Yatakayofuata sijui naachia walenga shabaha walenge chochote wanachoweza kulenga kile ambacho roho zao zinapenda kulenga.Shenzi type.

Kaka Netanyau Hiyo Lugha yako ngumu na imejaa Jazba....Mwenyezi Mungu apishilie mbali na tusifike hapo unapokusudia...Tutumie njia ya kidemokrasia kumuondoa huyu Mkwere,Uchochezi wa kidini utatugawa zaidi,kwani vita ya akina Mwawado na Rev.Kishoka kutokana na imani zao za kidini ni mbaya sana haifai kuiona!!!
 
Mkuu Mwawado inaonekana ndio hali halisi ya wabongo na ndio maana wanarusha mawe tuu.

Sasa na mkuu wa nchi anaenda kulala mapema kwa kuhofia usalama wake....Sasa ukisema maneno hayo ni ya jazba na wakati mtaani ni vitendo vya jazba then utakuwa ume ignore reality...Reality kwamba ni kweli wananchi sasa wana jazba sana.

Hata hivyo Netanyahu alianza na kauli hii hapo chini...

Naunga mkono hoja hiyo kama njia mbadala ya kuiepusha nchi katika vita.
Raisi kashindwa kwa baadhi ya mambo yafuatayo yanayomfanya apoteze sifa za kuwa Raisi mwenye hadhi.
 
Mambo yanayotokea sasa Tz yananikumbusha miaka ile ambapo masheik na maaskofu walikuwa wanapeana zamu za kutoa "matamko". Wakitoa maaskofu tamko dhidi ya serikali, masheikh nao wanainuka kutoa tamko kupinga lile la maaskofu.

Nakumbuka kipindi fulani hata Rais aliibuka na kuhutubia "wazee wa Jiji la Dar es salaam" kujibu waraka wa baraza la maaskofu, akiwakumbusha kutenganisha ya "Mungu na Kaizari", lakini hapohapo hadhira yake ikimwitikia kwa vibwagizo vya "takbiir!"
 
Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikifuatilia mambo ya ufisadi yanayofanywa na baadhi ya viongozi wetu.

Inakatisha tamaa kuona kwamba watu wakijitokeza kuwataja, au kufichua madhambi nchini mwetu, ni viongozi wetu wa chama tawala na serikali ambao wanajitokeza kwa kasi kubwa sana kutetea ufisadi huo. Ingekuwa vizuri wao kukaa kimya na kuacha hao waliotuhumiwa walalamike kwa kutumia vyombo vya sheria. Utetezi huu wa watuhumiwa wa ufisadi umeleta kwangu hali ya kutokuwa na uaminifu kwa viongozi, chama tawala pamoja na serikali kwa ujumla katika kutetea maslahi ya wananchi wa Tanzania.

Sijafanya utafiti wa kitaaluma, lakini baada ya kupitia humu jamvini, kusoma habari za magazeti mbalimbali na kukusanya hoja za watu mbalimbali, nimeona kuwa ni wengi tu ambao hawana tena imani katika vyombo hivyo.

Katika nchi zingine kumekuwa na kitu kiitwacho 'Vote of no confidence´, ambapo kura inapigwa na kama wananchi hawana imani na vyombo tawala, basi vyombo hivyo vinaenguliwa. Sidhani kama katiba ya Tanzania imeundwa ikiwa na kipengele hicho, lakini, kwa mawazo yangu, naamini kuwa iwapo kutakuwa na mabadiliko ya kikatiba, kipengele hicho kiwekwe ili kuhakikisha kuwa viongozi wetu hawavimbi vichwa na kukingiana vifua, wakati wananchi ambao ndio waliowapa wadhfa wa kuongoza, wanaumbuka na kupata shida.
 
Hakika Kikwete siyo Jasiri, Kwa nini? anajua alifikaje hapo alipo na waliomfikisha wanajua ni kwa nini walimfikisha hapo. Hana ujasiri na ndio maana hata watumishi anateuliwa na hana ujasiri wa kuchukua maamuzi.

SINA IMANI
 
Inabidi uwe makini sana kuuliza maswali ya poll ili wengi waweze kushiriki.

Hapo ume assume kwamba awali tulikuwa tuna confidence naye. Si kweli. Wengine tunashindwa ku vote hapo.
 
Dilunga unataka swali liulizwe vipi??
 
Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikifuatilia mambo ya ufisadi yanayofanywa na baadhi ya viongozi wetu.

Inakatisha tamaa kuona kwamba watu wakijitokeza kuwataja, au kufichua madhambi nchini mwetu, ni viongozi wetu wa chama tawala na serikali ambao wanajitokeza kwa kasi kubwa sana kutetea ufisadi huo. Ingekuwa vizuri wao kukaa kimya na kuacha hao waliotuhumiwa walalamike kwa kutumia vyombo vya sheria. Utetezi huu wa watuhumiwa wa ufisadi umeleta kwangu hali ya kutokuwa na uaminifu kwa viongozi, chama tawala pamoja na serikali kwa ujumla katika kutetea maslahi ya wananchi wa Tanzania.

Sijafanya utafiti wa kitaaluma, lakini baada ya kupitia humu jamvini, kusoma habari za magazeti mbalimbali na kukusanya hoja za watu mbalimbali, nimeona kuwa ni wengi tu ambao hawana tena imani katika vyombo hivyo.

Katika nchi zingine kumekuwa na kitu kiitwacho 'Vote of no confidence´, ambapo kura inapigwa na kama wananchi hawana imani na vyombo tawala, basi vyombo hivyo vinaenguliwa. Sidhani kama katiba ya Tanzania imeundwa ikiwa na kipengele hicho, lakini, kwa mawazo yangu, naamini kuwa iwapo kutakuwa na mabadiliko ya kikatiba, kipengele hicho kiwekwe ili kuhakikisha kuwa viongozi wetu hawavimbi vichwa na kukingiana vifua, wakati wananchi ambao ndio waliowapa wadhfa wa kuongoza, wanaumbuka na kupata shida.

Hiiyaweza kuwa nzuri na hata kutoa majibu zaidi ya porojo za redeti. good move
 
Katika nchi zingine kumekuwa na kitu kiitwacho 'Vote of no confidence´, ambapo kura inapigwa na kama wananchi hawana imani na vyombo tawala, basi vyombo hivyo vinaenguliwa. Sidhani kama katiba ya Tanzania imeundwa ikiwa na kipengele hicho, lakini, kwa mawazo yangu, naamini kuwa iwapo kutakuwa na mabadiliko ya kikatiba, kipengele hicho kiwekwe ili kuhakikisha kuwa viongozi wetu hawavimbi vichwa na kukingiana vifua, wakati wananchi ambao ndio waliowapa wadhfa wa kuongoza, wanaumbuka na kupata shida.

Michango mingi inayotolewa humu ukiangalia kwa makini kinachosababisha madhaifu yote hayo ni UDHAIFU WA KATIBA YETU. vote of no confidence ilipaswa iwepo kwenye katiba, sio kwa Rias tu hata Wabunge na Madiwani. Kipengele hiki kingemfanya Kiongozi aliyechaguliwa kujituma na kuwafanya waliomchagua kumu-asses mara kwa mara.

CHANGAMOTO: Tunapoimizana kuchagua wabunge wa upinzani wengi lengo la msingi ni kwenda kubadilisha katiba. Sasa hivi inakuwa ngumu kwani Mbunge wa upinzani akipeleka changamoto ya kubadili Katiba kitaitishwa kikao cha wabunge wa CCM na kuelezwa madhara ya kuingizwa kipengele hicho kwa CCM bila kuangalia madhara yake kwa wakulima na wafanyakazi.

SHIME SHIME WANAJAMII TUONGEZE WABUNGE WA VYAMA VYA UPINZANI.
 
Sipaoni pa kupigia kura au ballote boxes zimeibiwa nini?Sina imani hata kidogo na Serikali ya JK kwa sasa.
 
Raisi kachangia kwa kiasi kikubwa kututo imani hasa watumishi kwa hotuba yake ya gadhabu, inaonyesha anapanic sana na manaagement yake ina ulakini
 
Mimi hata kabla ya kupiga kura 2005 Sikuwa na Imani Naye! Leo si kutokuwa na imani naye tu bali. IM TOTALY COMFUSED!
 
Back
Top Bottom