Imani hizi! Je, unajua kanisa linaitwa "Chanzo halisi?

Mfilisiti

JF-Expert Member
Apr 29, 2020
342
1,551
Leo baada ya kifurushi changu DStv kukata (mpira), nikashawishika kucheki hizi chanel za ndani, ile naweka star tv nakutana na kanisa linajiita "Chanzo halisi"

Cha kushangaza wanatumia bibilia ile ile

Wanaenda kuhiji kigoma, ndugu msomaji ni kigoma hii hii ya karibu na burundi😂😂
Na huyo kiongozi leo alikua anatoa tiketi 160 kwa ajili ya kwenda kuhiji huko kigoma.
Yule aliyekua mwanamuziki wa the mafiki nayeye sasa hivi yupo sauti ya chanzo halisi.

Katika mafundisho yao sijasikia neno Mungu wala Yesu,
Kauli mbiu ni " bila chanzo halisi hutoboi"

Waumini wa sauti ya chanzo halisi wapo wamejaa kweli na mavazi yao ni meupe

Dunia ina maajabu kweli kweli
PXL_20231224_072328547.jpg
 
Hili kanisa, si ndiyo lile lilikuwa linaitwa "THE POOL OF SILOAM?" Hawa jamaa wana aina ya "Injili" ya tofauti kabisa! Kuanzia saa, siku, wiki, mwezi hadi mwaka vina majina ambayo hata kwenye biblia hayapo!
Ni kweli kwa muda niliomsikiliza yaani wanaongea vitu tofauti kabisaa, na leo kasema siku ya kesho ambayo ni Christmas wao waniita family day na amewaambia waumini waende kesho kwenye family day😂
 
Leo baada ya kifurushi changu DStv kukata (mpira), nikashawishika kucheki hizi chanel za ndani, ile naweka star tv nakutana na kanisa linajiita "Chanzo halisi"
Cha kushangaza wanatumia bibilia ile ile,
Wanaenda kuhiji kigoma, ndugu msomaji ni kigoma hii hii ya karibu na burundi😂😂
Na huyo kiongozi leo alikua anatoa tiketi 160 kwa ajili ya kwenda kuhiji huko kigoma.
Yule aliyekua mwanamuziki wa the mafiki nayeye sasa hivi yupo sauti ya chanzo halisi.

Katika mafundisho yao sijasikia neno Mungu wala Yesu,
Kauli mbiu ni " bila chanzo halisi hutoboi"

Waumini wa sauti ya chanzo halisi wapo wamejaa kweli na mavazi yao ni meupe

Dunia ina maajabu kweli kweliView attachment 2851426
Linaitwa Kanisa halisi la Mungu baba. Lilianzishwa baada ya mpasuko kwenye kanisa la The Pool of Siloam.

Sasa hawa kanisa halisi la Mungu baba ndio wamewazidi nguvu wale Siloam na sasa wanajulikana zaidi wao.
 
Hao ni siloam baada Munuo kufariki wenyewe wana sema alipaa walibadilisha jina
Ni kama vile waligawanyika makundi mawili

Kwa kifupi tu ulokole una uraibu wa ajabu sana
Unaweza ambiwa ule majani ukatafuna majani kama mbuzi
Ua hachana na mkeo au mumeo ukaachana nae.

Muda si mrefu ulokole utakuwa ni mmojawapo ya magonjwa ya akili hapa nchini
 
Hao ni siloam baada Munuo kufariki wenyewe wana sema alipaa walibadilisha jina
Ni kama vile waligawanyika makundi mawili
Kwa kifupi tu ulokole una uraibu wa ajabu sana
Unaweza ambiwa ule majani ukatafuna majani kama mbuzi
Ua hachana na mkeo au mumeo ukaachana nae.
Muda si mrefu ulokole utakuwa ni mmojawapo ya magonjwa ya akili.
Walikuwa maeneo ya Mbezi enzi hizo, kuna jamaa yetu alijikuta anatoa uwanja wa familia yake sadaka.
Jua na mwezi kwao ni vyombo vya kutambikia
 
Back
Top Bottom