Tram Almasi
JF-Expert Member
- Feb 26, 2009
- 749
- 226
kama miezi miwili hivi nilishuhudia hili tukio la gari kuzama(Angalia picha). Ilikuwa kama tunaangalia movie vile. Kilichonisikitisha ni kuona kwamba hata wale amabao tunategemea kwamba wangesaidia kutoa taarifa katika vyombo vya usalama na uokozi, hawakuonekana kuguswa kabisa na tukio lile mpaka wavuvi na baadhi ya wananchi walipoamua kujitosa na kusiadia kuiopoa gari iliyozama kutoka majini.Bahati nzuri ni kwamba, mwenye gari alipoona inazama aliamua kufungua mlango na kuruka baada ya kuona pantoni inafunga lango lake akiwa nusu ndani na nusu nje.
MY TAKE:
Ni jana tu nikiwa ktk pantoni nimejaribu kuchunguza na nikaona kwamba hakuna jitihada zozote za kuhakikisha kuna huduma za uokozi iwapo ajali kama hiyo itatokea tena.inasikitisha na kutisha kwa kweli. au tunasubiri kuunda tume ajali ikitokea?