Ikulu yawajibu walimu, yasema mgomo ni Batili, kesi iko mahakamani

.
Hivi mgomo halali huwa unakuwaje? Maana walimu kama wanataaluma wamefuata taratibu zote zinazostahili kuzingatiwa. Na huko mahakamani sirikali imefuata nn na lini sirikali itasema mgomo huu ni halali..!!!!??
.
 
teh teh teh...the wretched ship has reached the deepest of the deep! Hakuna ujanja hata kama tutaleta makontena ya mapanga kama General Omar Mahita.
 
Ila walimu, hasa wa shule za msingi wamesahaulika sana. Tuone aibu kuwaweka walimu wetu katika hali duni. Jinsi mwalimu anavyokuwa na matatizo, fikra zake zinakuwa duni na fikra hizo anazipandikiza kwa wanafunzi, matokeo yake taifa zima linakuwa na fikra duni!
 
Kwani tangu lini selikali iliwahi kuwaambia wanaotaka kugoma go a head? Kama waalimu wanasubiri selikali iwaambie mgomo wao ni halali hivo basi gomeni watakuwa nimahayawani
 
yaani Ikulu imepotexa maana kabisa ...imekuwa ni sehemu ya kutoa matamko tu kila siku ..aibu sana sana
 
Ikulu ina mashetani, kwa kukosa huruma dhidi kundi hili linaloweka msingi maendeleo katika nchi hii. Walimu wanalipwa mishahara midogo hata akiwa na degree tofauti na wataalamu wengine katika nchi hii, Serikali gani isiyo na huruma na kundi hili muhimu kwa maendeleo ya nchi? Aibu kwao na rais asiye na huruma. Tpuuuuuu!
 
[h=2]Mgomo wa walimu[/h]
Nawashauri walimu hakuna kurudi nyuma, mgomo upo palepale. Mkoba zima simu zako sisi walimu tumeupokea mgomo kwa mikono miwili. Tumenyanyaswa kiasi cha kutosha, tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha, tumepuzwa kiasi cha kutosha, tumedharaulika kiasi cha kutosha, tumetukanwa kiasi cha kutosha, tumetishwa kiasi cha kutosha. TUUNGANE HATA IKIBIDI KUTEKWA KAMA ULIMBOKA TUWE TAYARI. WALIMU TUSEME HAPANA KUONEWA!

Hata kabla ya mgomo tulijua itakuwa hivyo kuwa watakimbilia mahakamani, waichukue mahakama ikafundishe. Hivi ni mgomo upi Tanzania wakasema huu ni mgomo halali? Tunaomba watanzania watuunge mkono. Hakuna mtanzania hata mmoja asiyejua umuhimu wa walimu na jinsi tunavyodharauliwa licha ya umuhimu wetu.

Rais, madaktari,mawaziri, wabunge na wataalamu wote ni yupi ambaye hakupitia mikono ya walimu? Leo iweje walimu ndo tuonekane wadhaifu kiasi hiki. Walimu tubadilike mabadiliko hayataletwa na mtu mwingine, hivyo ukombozi wetu walimu umo mikononi mwetu.

Tunadharaulika hata na watu wasio na elimu kwa sababu ya unyonge wetu TUSEME KWA PAMOJA YATOSHA.

Wito kwa mahakama tafadhali tendeni haki vinginevyo mahakama itakosa heshima usoni pa watanzania kwa kutetea serikali na kuminya haki zetu. Hata nyie mahakimu na majaji bila walimu msingekuwa hapo mlipo. Acheni unafiki wa kusikia kila amri tendeni haki. Vinginevyo hakuna sababu ya kuwa na mahakama. Maana mnatetea maovu ya serikali.


WALIMU WENZANGU TUPUZE TAMAA NDOGONDOGO ZA SENSA, KUSIMAMIA MITIHANI, KWENDA KUSAHIHISHA MITIHANI HUKU TUKIPANDA MAROLI KAMA TUNAENDA MINADANI. UKOMBOMBOZI UKO MIKONONI MWETU TUSIKUBALI KWENDA KAZINI JUMATATU HADI KIELEWEKE. TUWE TAYARI HATA KUPOTEZA KAZI YATOSHA KUNYANYASWA KATIKA NCHI YETU. HATA HAO WANAOJIONA LEO MIUNGU WATU NA KUTUONEA LEO WAKUMBUKE CHEO NI DHAMANA NA IPO SIKU WATAJIBIA UONEVU WAO.


MSHIKAMANO DAIMA NA KILA MWALIMU AWE MLINZI ILI TUWABAINI WANAOTUSALITI KWA KWENDA KAZINI JUMATATU.

MKOBA UKITANGAZA KUTOKUWEPO MGOMO UWE MWISHO WAKO WA KUITWA RAIS WA CHAMA CHA WALIMU VINGINEVYO USIJE UKATULAUMU WALIMU. WAKATI WA KUDANGANYWA UMEPITA.​


Edit Post Reply Reply With Quote


 
sina ufahamu sana na kama nitakosoea nielimishwe.
Mahakama na serikali zina tofauti gani?
Kwani mahakama inajiendesha yenyewe bila serikali?
Au mahakama haijawekwa na serikali?
Kama mahakama imewekwa na serikali(gharama za uendeshaji zinatoka serikali ) iweje itoe maamuzi kinyume na maazimio ya boss wake?(serikali)
kama nimekosea nielimisheni kwa upendo na upole ili nisijione kuwa na hatia kutaka maarifa zaidi.
 
kila jambo linazungumzwa na ikulu,wizara zimeshindwa majukumu?walim walishajigomea zamaniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
********iwasemi vibaya*********

wengi wanavyeti fake au vinatumiwa na mtu zaidi ya mmoja kunakugoma hapo
 
mimi nawashauri walimu wagome wasitegemee kwamba serikali itawaruhusu kufanya hivyo, gomeni ili heshima ipatikane
 
Mimi nafikiri serikali na mahakama za nchi hii ndio batili ila mgomo ni halali. Ni lini serikali ikasema mgomo ni halali, hii serikali ni ya kidikiteta maana ingekuwa ya kidemokrsia basi ingekuwa inakaa na watu wake kufikia muafaka. Walimu hakuna kwenda kazini hadi madai yetu yakubaliwe wasitufanye sisi ni wajinga tuna akili zetu ndiyo maana hata Kikwete ni Rais kwa sababu ya walimu, hata hao majaji na mahakimu wako pale kwa ajili ya walimu. alete virungu atupige kama walivyozoea hatuendi shuleni hata ikitokea tukaenda tutafundisha uongo labda mahakama zao ndio zifundishe. Watanzania tunawapenda ila sasa nasi tumechoka kuonekana wapuuzi.

TUMEGOMAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA. MKoba ukithubutu kuahirisha mgomo ujizulu kwanza vinginevyo amini utakuwa umetangaza vita isiyo isha na walimu hatutaki kubipiwa. Kwani watanzania wote ni walimu mbona wanaishi vizuri kuliko walimu. KIKWETE KUBALI KUTUSIKILIZA WALIMU TUMECHOKA KUONEWA VITISHO VYA IKULU HAVITAKUSAIDIA. MBONA WABUNGE MNAWALIPA HELA NYINGI KWA KUSINZIA WANAIMPACT GANI KATIKA JAMII. kWA NINI RAIS UNATAKA UCHUKIWE NA KILA MTANZANIA KWA UNAFIKI WA WATU WACHACHE WANAOJIPENDEKEZA KWAKO?
 
Kwa mara nyingine tena serikali imekimbilia mahakamani kupinga mgomo wa walimu huku Ikulu ikitoa taarifa ya kuwapiga mkwara walimu watakaogoma jumatatu ijayo. Hii ni taarifa zaidi toka Ikulu

TAARIFAKWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA YASERIKALI KUHUSU KUSUDIO LA WALIMU KUGOMA
____________________________________________
SERIKALI kupitia Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi leo,Ijumaa, Julai 27, 2012 majira ya saa tisa alasiri, imepokea notisi ya saaarobaini na nane (48) ya kusudio la walimu wanachama wa Chama cha WalimuTanzania (CWT) kugoma kuanzia Jumatatu tarehe 30 Julai 2012 saa moja na nusuasubuhi.

Kabla ya notisi hii kutolewa, Serikali imekuwaikifanya jitihada nyingi za kujadiliana na viongozi wa CWT kuhusu jinsi yakuboresha maslahi ya walimu kwa nia ya kumaliza suala hili kwa maelewano kwakutumia vyombo na ngazi mbali mbali za kisheria.

Kwa sasa, shauri hili liko Mahakama Kuu Divisheni yaKazi na leo hii siku ya Ijumaa tarehe 27 Julai, 2012 majira ya saa sita mchana pandezote mbili zilifika Mahakamani, na Mahakama ikaamuru kwamba pande zote zikamilishemaelezo yao ifikapo siku ya Jumanne tarehe 31 Julai, 2012 saa sita mchana, ilikuiwezesha Mahakama kuendelea kusikiliza shauri hilo na hatimaye kutoa uamuzi.

Kwa hiyo, Mgomo huu siyo halali kwa sababu shauri hilibado liko Mahakamani.Kwa msingi huo hatua ya CWT kutoa notisi ya kuanza kwamgomo kabla ya kukamilika kwa shauri hili ni kukiuka taratibu halali za Kimahakamaambazo kila mmoja anawajibika kuziheshimu.Serikali inapenda kuwafahamisha walimu wote kuwakujihusisha na mgomo huu ni kwenda kinyume cha Sheria, Kanuni na Taratibu zakazi.

Hivyo, walimu wanapaswa kupima madhara ya mgomo huu usiokuwa halali na Serikaliinawataka walimu kupuuza mgomo huo na kutokujihusisha nao. Walimu wotewanatakiwa waendelee na kazi kama kawaida.
Peniel M. Lyimo

KAIMU KATIBU MKUU KIONGOZI

Imetolewa na:
Kurugenziya Mawasiliano ya Rais,Ikulu.
Dares Salaam.
27 Julai, 2012

My Take: Inaonekana serikali imebaini namna ya kutumia mahakama kudhoofisha nguvu zote za wafanyakazi kudai haki. Iliwahi kutokea kwa wafanyakazi wa NBC, walimu, madaktari hivi karibuni, na sasa walimu tena.
 
Hali mashuleni ni mbaya sana. Walimu wanafundisha wakijisikia. Yaani walishagoma siku nyingi.

Impact yake inaonekana kwenye matokeo, na ya mwaka huu yatakuwa worse. Tutakuja hapa wakati ukifika.

Kuna watu wanakebehi taaluma hii ilhali watoto wao wako mashuleni wanafundishwa na hao hao walimu ambao serikali inawanyima haki zao za msingi kabisa.

Kumbukeni wao watoto wao wansoma nje au tz kwenye shule za gharama kubwa. Vitisho hivyo vya Ikulu havitasaidia chochote na havitajenga sbbu, yes wanawez wasigome sawa, wakarudi shule na wakaingia darasani lakini wasifundishe ipasavyo au wakawapa watoto wetu content out of kinachitakiwa kufundishwa.

Mwisho wa siku failures watakuwa wengi mno mtaani, wamemaliza kidato cha 4 kwa kukamilisha miaka na si kwa kufaulu, wingi huu utaongeza idadi ya vijana wasio na kazi, na kadri watakavyoogezeka impact yake wote mnaijua.

Obvious hawatakuja kuwadhuru walimu, watablame gvt, ndo watakuwa wachoma vituo vya polisi, watekaji mabasi, majambazi, na ndo watakaotumiwa kuchafua amani ya nchi as they are desperate, depressed n.k Mwisho wa siku ni vita ndani ya nchi.

Ushauri wa bure JK, wakati mwingine ku admit umeshindwa hutapungua kitu, pia hata once in your leadership jaribu kutekeleza maombi halali ya wafanyakazi hawa wanaodai haki zao possible utakumbukwa. Sbb naamini inawezekana kabisa.

Ubabe kwa watu wanaokujengea nchi na kuficha maovu yenu kwenye mwamvuli wa mahakama hautawasadia sana, you worsen the situation.
 
watafukuzwa kazi wote na kibaya zaidi vyeti vyao havitambuliwe kimataifa. Wataweza kuishi bila kazi?, ni bora waendelee na kazi huku madai yao yskishughulikiwa na serikali.
 
watafukuzwa kazi wote na kibaya zaidi vyeti vyao havitambuliwe kimataifa. Wataweza kuishi bila kazi?, ni bora waendelee na kazi huku madai yao yskishughulikiwa na serikali.

woga ni dhambi kubwa sana katika kudai haki mkuu
 
Back
Top Bottom