Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,504
- 113,620
Wanabodi,
Nikiwa ni mwanachama wa TLS, nimeisoma taarifa ya TLS kuhusu issue ya Bandari na DPW, kiukweli kabisa TLS inastahili pongezi za dhati!, imefunga huu mjadala, ingekuwa mimi ni Mnyamwezi, Kinyamwezi hii inaitwa "funga kalomo", yaani funga mdomo!. Taarifa hii ya TLS ni funga kazi, na huu ndio uzalendo!, hongera sana TLS kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa.
Kama mwanachama mwaminifu wa TLS, kwa heshima ya chama changu cha wanasheria wa Tanganyika, naomba nisikosoe jambo lolote kwenye taarifa ya TLS, ila sio vibaya kuzungumzia baadhi ya hoja ambazo TLS haikuzigusia kabisa!.
Ni baada ya kuisoma taarifa ya TLS, ndipo nikagindua mtu mwandishi wa habari kwanza, halafu ukaingia kwenye sheria, unakuwa na jicho kali zaidi kuliko jicho la mwanasheria mwanasheria tuu ambaye sio mwanahabari!.
Jicho la Mwanasheria linaangazia vifungu vya katiba, sheria, taratibu na kanuni, jicho la mwanahabari linaangalia mtazamo wa jamii, Mwananchi wa kawaida, anaona nini, anataka nini, hivyo jicho la mwanahabari linaona kuliko jicho la mwanasheria.
Baada ya Bunge letu kuridhia, niliandika makala hii, Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee! humo niliainisha mapungufu ya IGA hiyo kisheria kwa jicho la kiuanahabari.
TLS katika taarifa yao, kuna maeneo mengi wamepita mule mule nilimopita mimi, ila lile kubwa kuliko, "The Capacity" to contract, TLS wamelikwepa na kuliweka kiporo kusubiria wawasiliane na Dubai.
TLS hawakuyaona yale niliyo yaona mimi!. Tanzania ni nchi, inakwenda kuingia mkataba wa kimataifa wa nchi na nchi, yaani Tanzania na UAE, lakini signatories wa Tanzania ni nchi, halali signatories wa UAE ni kampuni ya DPW!, tena imesaini bila POA yoyote toka UAE!.
Kwa maneno mengine ni kampuni ya DPW imejigeuza ni nchi ya Dubai wakati ni kampuni binafsi!, sio nchi, Dubai sio nchi, nchi ni UAE!, nchi yetu haiwezi kuingia mkataba wa kimataifa wa kuwa ratified na Bunge letu kama an international Treaty wakati signatories ni kampuni na sio nchi na hakuna POA yoyote ya UAE kuruihusu DPW to transact an international Treaty on behalf of UAE!.
Nimeipongeza TLS kwa uzalendo kwenye hili, ila nikiri kuwa nimeshangazwa na umakini huu wa TLS katika hili la Bandari.
Sheria Kuu kuliko zote nchini kwetu ni katiba, katiba ndio sheria Mama, sheria nyingine yoyote inayokwenda kinyume cha katiba ni sheria batili!. Kinachoibatilisha hiyo sheria yoyote kinyume cha katiba, ni katiba yenyewe!.
Nimalizie kwa pongezi tena, TLS kwa hili la Bandari, ila kuna makubwa kuliko hili la Bandari, TLS bado hamjachelewa!.
Mungu ibariki TLS
Mungu Ibariki Tanzania
Paskali
Rejea
1. Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law! Kuendelea Kuitumia ni Ujinga? Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!
2. Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
3. Mgombea Kudhaminiwa na Chama ni Ubatili Uliochomekwa Kiubatili na Bunge Letu Ndani ya Katiba Yetu!. Tuache Ubatili Huu Uendelee Ndani ya Katiba Yetu?

- Serikali yetu ime draft sheria batili, inayokwenda kinyume cha katiba, ikaipeleka Bungeni kutungwa kuwa sheria!, kwanini TLS walikaa kimya?!.
- Bunge letu likaitunga hiyo sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba, kwanini TLS walikaa kimya?.
- Rais wa JMT akaisaini hiyo sheria batili kuwa ni sheria!, kwanini TLS walikaa kimya?!.
- Mahakama Kuu kupitia kesi ya Mtikila, ikatamka sheria hiyo ni batili na kuitaka serikali iifute. Kwanini TLS walikaa kimya?!.
- Ubatili wa sheria batili yoyote unabatilishwa na katiba, Mahakama Kuu ikiisha tamka sheria fulani ni batili kwa kwenda kinyume cha katiba, automatically sheria batili hiyo inakuwa imebatilika from there and then. Kazi ya serikali ni procedures tuu za kuifuta!. Kwanini TLS walikaa kimya na sheria batili hiyo mpaka sasa bado iko kwenye sheria zetu licha ya Mahakama Kuu kutangaza ni batili?.
- Serikali yetu ikakata rufaa kupinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu, ikashidwa!, kwanini TLS walikaa kimya?!.
- Serikali yetu baada ya kubwebwa, ikafanya kubwa kuliko, ikapeleka Bungeni mabadiliko ya katiba kwa hati ya dharura, batili ile ikachomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu!. Kwanini TLS walikaa kimya?!.
- Bunge letu likafanya mabadiliko ya katiba na kuichomeka hiyo batili ndani ya katiba yetu!. Hivyo katiba yetu imenajisiwa kwa kuchomekewa ubatili!, kwanini TLS walikaa kimya?!.
- Mchungaji Mtikila hakukubali katiba yetu inajisiwe, akafungua shauri kupinga mabadiliko hayo ya katiba, Mahakama Kuu ikampa ushindi na kutangaza mabadiliko hayo ni batili!, kwanini TLS walikaa kimya?!.
- Serikali yetu ikakata rufaa Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu, serikali ikashinda, kwanini TLS walikaa kimya?!.