Iko wapi Tanzania yangu? Ipo wapi CCM yangu; wapo wapi wazee wangu wenye dhamana ya chama na nchi yangu?

Mkirindi

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
6,750
4,958
IKO WAPI TANZANIA YANGU; IKO WAPI CCM YANGU: WAKO WAPI WAZEE WANGU WENYE DHAMANA YA CHAMA NA NCHI YANGU.

Ndugu Watanzania na wanajamvi, nawaombea kila la kheri wakati huu mgumu. Mola atatupa neema zake na tutavuka hili janga tukiwa salama wa afya.

Ninaleta uzi huu nikiwa na majonzi na wasiwasi na chama changu au chama kikongwe nchini, kinavyo tetereka na huku wale walezi na washauri, waliopewa jukumu na Mungu wako kimya na wala hawajaribu kufanya wajibu wao.

Watanzania tusijidanganye, kutetereka au anguko la CCM, litakuwa na effect kubwa sana kwa nchi na wananchi.

Je, tatizo la hizi ishara mbaya ndani ya chama changu, lina sababishwa na nini?

Mimi sio mwandishi mahiri, na wala sio fani yangu. I am a very good Administrator but not a Writer; nitajaribu kueleza maoni yangu, ubovu uliopo ndani ya chama changu.

Tokea enzi na enzi, vyama vikubwa ustawi wao sio mali au wingi wa wanachama, bali ni siasa safi, uongozi wenye busara, uadilifu, na muhimu zaidi WALEZI WAZOEFU NA WASIO NA TAMAA. CCM ilikuwa na sifa nyingi kama hizi na Zaidi. Mfano mzuri ni vyama vya upinzani Uingereza au USA, vinaweza visishike dola kwa miaka zaidi ya 10-20, lakini bado vina nguvu, sauti na vinazidi kukuwa.

Kama Rais wangu asemavyo: MSEMA KWELI NI KIPENZI CHA MUNGU. Ukweli ni kuwa walezi wetu kama akina Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Malecela, Msuya, kinana, nk. wamekuwa na dosari nyingi sana, ambazo zimemuwezesha Rais Magufuli kukiteka chama na kukibadilisha kuwa tofauti na asili ya chama. Huwezi kubadilisha mwenendo au siasa za chama bila ya ridha ya chama, na chama sio wale wachache wanaounga lolote MK atakacho, ila ni wale watakaojadiliana naye na kuja na mbinu vumbuzi na zenye tija na manufaa kwa chama nchi na Africa. Nitazungumzia baadhi ya hawa walezi wachama na kwa machache:

1. MZEE MWINYI: Heshima kwako Mzee wangu, Mungu akupe afya na maisha marefu. Mzee wetu ukweli ni kuwa wewe ndiye aliyetokea kuwa janga kubwa la CCM leo, sijui ni uzee, Alhamdulilah imani yako ni kubwa sana, na unajua dini vizuri sana. Lakini kwa sasa uyafanyayo ni maovu sana kwa dhamana ya chama na kwa umma uliyopewa na Mola wetu. Mzee wetu, wewe kama Babu yetu, leo uko tayari kukaa kimya huku unayaona maovu yakifanywa ndani ya chama, Babu unajua fika ya kuwa mwanao atapata alichoandikiwa na Mola wake, na ambacho hakuandikiwa hatakipata.

Kama ameandikiwa kuwa Rais wa Zanzibar, ataupata huo urais bila ya uvumba wala ubani, lakini CCM wala Magufuli hawawezi kumpa Hussein kila ambacho Mola hakukiridhia. Babu mwanao Hussein, ni kijana mzuri, mwenye hekima na heshima, anapendwa na sifa zake binafsi ndizo zitakazo mpitisha kuwa na cheo chochote hapa duniani. Mzee wetu, tunakusihi ujirudi na kufanya wajibu wako kama Quran ilivyokufundisha.

2. MZEE MKAPA: Heshima kwako Mzee wangu, Mungu akupe afya na maisha marefu.

Mzee wangu, mimi ni mfuasi wako wa kisiasa na nilipenda sana namna ulivyoirudisha Tanzania kwenye ulimwengu wa biashara, you did very well during your tenure. Mheshimiwa kuna taabu sana kuhusu hii awamu ya 5, kila mtu anakuona wewe ndio the strongest kati ya walezi wote walio hai leo, tena mwenye uwezo wa kumshauri Rais wetu anapohitaji ushauri, japokuwa inasemekana ni Rais asiyependa kushauriwa na asiye na shukrani.

Inasemekana kuwa hata simu zenu mara nyingi hazipokelewi. Mzee wangu, wewe bado unapendwa na kuheshimiwa na wengi sana, na neno lako bado lina uzito mkubwa sana. Mzee wangu, una power kubwa sana kumshinda kiongozi yoyote hapa nchini, na wananchi wanakuangalia wewe ufanyavyo.

Tafadhali sana jitahidi na wazee wenzako kuja na mbinu ya kurudisha chama chetu kwenye mistari na misingi yake. Hivi kinavyokwenda ni ileile staili ya Marehemu Rais Moi na KANU, na leo tunaiona KANU ilipo. Unalo jukumu kubwa sana, na USIJIFICHE KWENYE GLASS. Your legacy highly depends on hii awamu ya 5.

This will be on you Sir

3. MZEE KIKWETE: Heshima kwako Mzee wangu, Mungu akupe afya na maisha marefu. Duh kaka yangu kipenzi Pole sana tena sana, Lilahi kila ninaposwali ninakuombea Allah akukinge na macho na midomo ya wanyonge, Maanake kila zuri lifanywalo na awamu hii ya 5 linasheherekewa kama la kwao peke yao, lakina kila baya au lenye maumivu linakuwa lako kaka yangu, na Ukweli ni kuwa yenye maumivu ni mengi sana awamu hii.

Chama chetu kinaendeshwa kichokorachokora, vijana wamepewa dhaman bila ya kuwekewa check n balance, wanafanya watakavyo, Sheikh ukienda Magerezani kila Mkoa waliobambikizwa makesi ni wengi sana, tena kwa jina la Rais, na Rais hana habari nazo. Kuna viongozi wanamtumia Rais vibaya sana. Awamu hii imekuwa awamu ya visasi, na hilo sasa limerudi nyumbani. Chama kinavurugwa kuwabambikia kesi viongozi na kuwaadhibu. Rushwa ni aina mbili -- ya pesa/fursa na ya vitisho.

Kaka yangu bado u kipenzi cha UMMA, hebu funga safari uende Mbeya, Arusha, Kigoma au Mwanza kama mtalii tu, uone kama watu hawakufunga barabara kwa mapokezi yako, YOU ARE STILL LOVED TO THE HILT.

WAZEE MWINYI/MKAPA/KIKWETE: Ushauri wangu ni kama ufuatvyo, na kama nisemayo yana ukweli wowote tutaona wananchi wengi sana bila kujali itikadi ya vyama, wataniunga mkono na kuwapa wazee wetu moyo wa kuweza kufanya mema na mazuri, yatakayo nyoosha njia nzuri nchi yetu inayohitaji kupita, na pia mtamu weza kumsaidia Mheshimiwa Rais wetu mpendwa kuusikiliza ushauri wenu mzuri na kufanya mema kwa wananchi.
  • Kama wazee wenye dhamana ya chama na nchi, dhamana hiyo mlipewa na Mola, mulipochaguliwa kuwa Ma Raisi wa Tanzania, wajibu huo mnao hadi pumzi yenu ya mwisho hapa duniani. Jialikeni mkutane pamoja bila ya kuficha, kiwe hata chakula cha mchana kwa Mzee Mwinyi. Hicho kikao kwanza kitawafungua macho wengi sana, na kutakuwa na maneno mengi, yalio ya busara, hekima na upendo, na yaliyokuwa na unafiki na fitna. Sisi ni watu wenye busara tutayafuata ya busara na hekima, ya kinafiki yataendelea kuwa ya kinafiki. This will be a wake up call, and will prove that you still matter in this nation.
  • Katika kikao hicho, muanzishe a forum ya viongozi wastaafu ambao hawana tena nia za URAIS, it should include only Ex-Presidents & Ex- Prime Ministers wasiokuwa na ambitions za URAIS, na kila mmoja a sing an undertaking.
  • Muwe na uwezo wa kuweza kukutana na Raisi kwa pamoja sio zaidi ya mara 3 kwa mwaka, na kumshauri a jirekebishe kama kuna jambo muhimu sana na hatari kwa nchi na chama.
  • Muwe na uwezo kuitisha kikao cha kamati kuu ya CCM, kukielezea hoja yenu na kuitaka kamati ichague committee ya chaguo lenu kufuatilia jambo hilo, na kama litaekewa pingamizi, mtakuwa na uwezo kwa jina la chama kuwafikia wananchi kupitia media na kwa kufanya press conference. CCM sio chama cha mtu bali watu.
  • Ajenda yenu sasa ambayo ni muhimu sana ni namna sasa hivi nchi na chama vnavyoendeshwa, viongozi wanavyodhalilishwa.
Ndugu wana CCM,Wantanzania na JF Huu ni ushauri na maoni yangu, nitafurahi kukosolewa na kuungwa mkono. Nia yangu kubwa sio kuona mtu anatukanwa, kebehiwa, bali nitafurahi kama tuna rekishana. Tanzania nz hata chama changu sio mali ya mtu, ni mali ya Watanzania. Lazima tujirekebishe, tunaanza kuona ukabila na udini ukishamiri.

Hii ni nchi yetu wote, tumebahatika sana kuwa na watu tusiokuwa na ukabila na udini, kwani kwa muda mrefu tulikuwa wakweli na wapenda haki, wanasiasa wasitufundishe mgawanyiko ambao hautatusaidia. 1982, palikuwa hakuna hata mfugaji mmoja wa Kimasai au Kisukuma akiishi Mtwara, Lindi au Morogoro, lakini leo mashala ni nyumbani, na hayo ni maendeleo. Lakini hizi siasa za kidini na kikabila zitatuchafua.
 
Mkirindi,
Ccm ilikufa na Mwalimu iliyopo ni certified gang criminal kama uonavo mafia gang,au terrorist group hii inapumua Kwa nguvu za dola na sio Hoja. Siku ikichokwa na dola haina mizizi pa kushikia tena.

Nchi ni katiba sio chama vyama vitapita Lkn nchi itadumu,nchi haiwezi athirika Kwa kufa Kwa chama kwani Kenya, Zambia tangu kufa Kwa vyama pacha wake na ccm kipi kilichoathirika.Ccm imejiua na mfumo wa katiba yake yaani Hakuna aliyejuu zaidi ya mwenyekiti maana ni mungu kamili haojiwi, apingwi, ashauriki, afukuziki, hata waasisi wake wangekuwwpo wasingefanya chochote kama uonavo waliopo sasa nyerere angekuwwpo angeishia jela angepewa uhujumu uchumi kama angenusurika na wasiojulikana.

Leo mnayaona japo mliweka pamba mlionywa sana juu ya madhara ya kofia mbili hamkusikia mkajiona mko Salama maajabu Leo mkapa,sumaye,lowasa,membe eti Leo baada ya kuwa nje ya mfumo ndo wanaona umuhimu wa tume huru na katiba mpya walipokuwa na nafasi ya kuweza kufanya mabadiliko walipopigiwa kelele waliweka pamba hayawahusu.

Mwafrika yeyeto asipowekewa mfumo au muundo wa kumdibiti ni lzm ataumiza wenzake. Ni faida Kwa chama na taifa kutenganisha Kofia Mbili mfano rais akikiuka katiba anafutwa uanachama na mwenyekiti wa chama.

Leo chama ni sawa na Mali binafsi ya familia Hakuna mwanachama yeyeto mwenye maamuzi juu ya chama kupinga,kuhoji zaidi atasalimiwa na wasiojulikana, uhujumu uchumi, au atajikuta ICU.Tz ipo sana wacha tu CCM ife.

Tanzania imekuwepo hata kabla ya mkoloni ikawa Deutsche ostafrica,Tanganyika na itaendelea kuwepo,ngoja kizazi hiki kipya kilichozaliwa miaka ya 90 wazidi ongezeka huku kizazi kile cha zamani kikizidi kupungua.CCM inahitaji kosa moja tu ilifutike kama KANU.
 
Mkirindi,
Hawa wazee jiwe kawapiga pin anawadukua mpaka vyumbani,

Wanajuta wakikumbuka tulivyoshauri mamlaka ya mfalme ni makubwa yapunguzwe walipuuza,

Kwa katiba yetu ni hatari madaraka yakiangukia kwa watu wasio sahihi kama ilivyo awamu hii

Waliomo wasiomo wote tunasubri gari ikate break atakapona sawa! atakayepotea sawa tu.
 
Mkirindi,
Nimesoma taarifa yako hadi mwisho lakini sijaona hoja ya maana bali blabla ndiyo nyingi. Nafikiri wewe utakuwa ni wale mlizoea kula bila kunawa ndani ya CCM sasa mnaisoma namba.

Hao wastaafu wapo nyuma ya serikali ya awamu ya 5 na wanashauri kila mara ila wewe kwa sababu ya masilahi yako binafsi ndiyo maana unalialia. Pole mkuu nakuomba ubadirike tu ili uendane na kasi ya awamu ya 5.
 
Hawa wazee jiwe kawapiga pin anawadukua mpaka vyumbani,

Wanajuta wakikumbuka tulivyoshauri mamlaka ya mfalme ni makubwa yapunguzwe walipuuza,

Kwa katiba yetu ni hatari madaraka yakiangukia kwa watu wasio sahihi kama ilivyo awamu hii

Waliomo wasiomo wote tunasubri gari ikate break atakapona sawa! atakayepotea sawa tu.
Wewe acha kujikweza! Eti ulishauri!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom