Ijumaa ya Fat-wah Mwanza; RC na RPC Si siku ya Kukaa Ofisini leo

Status
Not open for further replies.
pengine watawala wetu wanadhan chanzo cha vita hasa vya wenyewe kwa wenyewe lazima kiwe kikuuubwa kama tsunami, waweze kukiona kwa macho tokea magogoni, yaliyofanyika Mwanza na yanayoendelea Zanzibar hayana mustakbari mwema kwa utaifa na umoja wetu, kwamba sasa hatuwezi vumiliana tofauti zetu! hii inasikitisha na kuogofya sana. Mungu ibariki Tanzania
 
Inasikitisha sana kufikia hatua ya kuchoma Qur an inaonesha wenzetu mlivyo na chuki kali sana dhidi ya uislam.Naomba mamlaka zishughulikie jambo hili kwa ufasaha na umakin mkubwa.
 
Mkuu,

hili la kuchoma msahafu ni upumbavu na ujinga na it is unacceptable kwani msahafu haujawafanyia kitu chochote it is just book that express certain ideas na ideology of which to muslims it is believed to be a sacred book.
sawa kabisa (100%).
Hoja inayofuatia hapa ni je kuchoma kanisa ili kulipiza kisasi kwa kuchoma quran tukufu, ni sawa?
Hata kama itakuwa ni sahihi, je hapakuwa na kitu mbadala cha kufanyika (kama kuwapeleka mbele ya mkono wa sheria)?
Je kama huyu amechoma quran na huyu akalipiza kwa kuchoma kanisa, ikiendelea hivyo mzunguko utaishia wapi?
Waliochoma quran walifanya kosa kwani kitabu hicho kama ulivyoeleza hakina kosa; pia waliochoma kanisa wamefanya kosa kwani jengo hilo lina hatia gani?
Kosa kubwa zaidi ni kwa walioshindwa kuchukua hatua haraka/mapema kwa waliochoma quran. Na hili ni tatizo kubwa la serikali hii - kuchelewa kuchukua au kutochukua hatua kwa maovu mengi ndani ya jamii yetu.
 
Kosa la kuchoma Quran kisheria lipo wapi?
religious untorelance, ignorancee and lack of thinking is major problem!
Gaijin, hivi hawa wandugu wangeendelea tu na daawa kana kwamba hakuna kilichotokea kungekuwa na tatizo gani? Uislam ndio ungekuwa umefika mwisho? Naheshimu watu wanachokiamini ila ku react kwa hili tukio kwa fatwa, wameonesha utoto wa kufikiri. At least kama kuna jinai mahala wangeripoti vyombo husika. Fatwa ni kinyume cha sheria za nchi.
Na swali lako sidhani kama litapata jibu hapa!
 
Mikristu ya Kiafrika inajiona imefika kunako kwa kufata na kutetea dini iliyoletwa na migeni kwa nia ya kututawala. Miislam ya Kiafrika nayo hivyo hivyo...

Wee ngoja tu mimi niuchukue urais - I'll make sure that mapadri, wachungaji, masheikh, maimam and the likes are out of jobs!! Futilia mbali hii kitu iliyoletwa (hata iwe kwa nia njema) na kugeuka mwiba wa fikra na maendeleo!! Dini zirudishwe katika jamii yetu baada ya miaka 150 ya kujikwamua kisayansi!
 
Wote wajinga tu. Wameokoswa religous tolerance. Better be neutral rather than being fundamentalist. God is one.

Wajinga wa kwanza ni wale walioamua kuchoma Quran wakati haina kosa lolote. Kama ndugu zetu mnavyolinda utukufu wa Yesu kristo na dhana nzima ya utatu na waislamu kwao Quran ni kitabu kitukufu. Hivyo basi kitendo walichokifanya wale fundamentalist wa kilokole kuchoma moto quran lilikuwa kosa lisiloweza kuvumilika na kukosa hekima ni vema wakachukuliwa hatua hao kwanza kabla hamjageukia waislamu. ACHENI UNAFIKI WENU HAPA!!!

Sishabikii ujinga huu kabisa watu wanakosa hekima na logic na kuishia kufanya jambo kwa imani na emotion zao matokeo yake ndio hayo sasa.

Kwahiyo kosa lisilovumilika stahili yake ni kulijibu kwa kutenda kosa jingine? Mdau hapo juu ameyatazama makosa ya wahusika wote kwa jicho la haki na uzalendo lakini wewe umekuwa mbinafsi sana. Kosa moja haliwezi kufutwa ama kurekebishwa kwa kutenda kosa jingine, wote hao ni wahalifu na wanastahili kukabiliwa na hatua kali za kisheria.

Punguza jazba vuta pumzi then tafakari. Ni kweli hatua ianze kwa kosa la kwanza then na la pili pia lichukuliwe hatua. Hata lile la DC mbakaji wa demokrasia, sheria ichukue mkondo wake kwa kosa la kwanza la kufanya mkutano batili na la hijab lifuatie baadae.

Ndugu yangu, kosa haliadhibiwi kwa kosa. Wapo watu wanaojitahidi kumsemea Mungu kana kwamba Mungu hana uwezo. Kwanini wasimuachie Mungu mwenyewe aliyekosewa akawaadhibu wakosaji? kwani wao wanatumia kipimo gani chakujua Mungu amekasirishwa kiasi gani na wakosaji?

Ushauri mzuri sana huu, muhimu ni kuzingatia kwamba wote ni wakosaji aliyeanza kutenda kosa la kuchoma moto quran na aliyelipiza kisasi kwa kuchoma moto kanisa. Na wote hao wanastahili kukumbana na mkono wa sheria ili liwe funzo kwa wahuni wengine wa namna hiyo.

Mkuu,

Mie sina jazba ila nasema ifikie wakati watu wawe na logic na kutafakari haingiii akilini kuchoma msahafu haujakufanyia kosa lolote. Kama hukubaliani nao si uache kama ulivyo na sio kuchoma moto. Muanzishaji mada alitakiwa kwanza akemee kitendo cha watu kuchoma msahafu usio na hatia yeyote ndipo aje katika Fatwa ya waislamu.

Kuhusu mada ya DC mie hukunioa kuchangia wala kusema kitu chochote kwani nasubiria mahakama kwanza tujue ilikuwaje kuwaje hadi wakafikia hapo walipofika. Ila hili la kuchoma msahafu ni upumbavu na ujinga na it is unacceptable kwani msahafu haujawafanyia kitu chochote it is just book that express certain ideas na ideology of which to muslims it is believed to be a sacred book.

Hiyo logic unayoitumia mbona unaitumia kimakosa. Logic gani hiyo inayohalalisha watu kuchoma kanisa ili kulipiza kisasi cha kuchomwa kwa quran.

Ukizingatia kwamba waislamu wanaiheshimu sana quran, vivyo hivyo ukumbuke kuwa wakristo nao wanaiheshimu sana nyumba yao ya ibada.
 
Kisheria kuchoma moto Qur-an au Bible ni kosa?
Mimi niliweka jana thread kuhusiana na sheria zinasemaje iwapo mtu anachoma moto vitabu vyake ikiwemo Kuran na Baibo, cha ajabu hakuna aliyejibu watu waliishia kutupiana maneno yaliyojaa ushabiki wa kidini na Mods wakaiondoa bila idhini yangu (Kwa mara nyingine Mods wamenichezea rafu). Sasa hapa itakuwa ngumu kwa mimi kuchangia
 
makanisa kuchomwa moto, hasa Zanzibar inatokea sana lakini ukiangalia kesi huishia kituoni na hakuna hatua inayochukuliwa na bado hakuna anayetangaza vita. Na huwa sioni ndugu zangu akina Mdondoaji au Twahil et al wakisema positively. Hili nalo ni sawa kabisa na la mwanza. Tatizo ni zero torelance na ulegelege wa kikundi cha watu wanaojiita serikali.
 
Mikristu ya Kiafrika inajiona imefika kunako kwa kufata na kutetea dini iliyoletwa na migeni kwa nia ya kututawala. Miislam ya Kiafrika nayo hivyo hivyo...

Wee ngoja tu mimi niuchukue urais - I'll make sure that mapadri, wachungaji, masheikh, maimam and the likes are out of jobs!! Futilia mbali hii kitu iliyoletwa (hata iwe kwa nia njema) na kugeuka mwiba wa fikra na maendeleo!! Dini zirudishwe katika jamii yetu baada ya miaka 150 ya kujikwamua kisayansi!

Mkuu kwani wewe huhitaji kura zetu viongozi wa dini? sasa kama unatutisha mapema kiasi hiki hatutakuchagua kuwa kiongozi wetu ili tusijekukosa kazi kama utafutilia mbali hizi dini zetu za kigeni!
 
Mikristu ya Kiafrika inajiona imefika kunako kwa kufata na kutetea dini iliyoletwa na migeni kwa nia ya kututawala. Miislam ya Kiafrika nayo hivyo hivyo...

Wee ngoja tu mimi niuchukue urais - I'll make sure that mapadri, wachungaji, masheikh, maimam and the likes are out of jobs!! Futilia mbali hii kitu iliyoletwa (hata iwe kwa nia njema) na kugeuka mwiba wa fikra na maendeleo!! Dini zirudishwe katika jamii yetu baada ya miaka 150 ya kujikwamua kisayansi!
kwa hiyo utafuta imani za watu jwa kuwalazimisha waingie dini yako the so called 'sayansi'. You are then worse than them all!
 
Mimi niliweka jana thread kuhusiana na sheria zinasemaje iwapo mtu anachoma moto vitabu vyake ikiwemo Kuran na Baibo, cha ajabu hakuna aliyejibu watu waliishia kutupiana maneno yaliyojaa ushabiki wa kidini na Mods wakaiondoa bila idhini yangu (Kwa mara nyingine Mods wamenichezea rafu). Sasa hapa itakuwa ngumu kwa mimi kuchangia

Si Rafu na ndio kazi yao Mkuu, ni vema kuifunga kuepusha Malumbano ya Kidini hapa tunasaka muafaka kwa kushauriana meza moja waumini wa Dini zote bila Ushabiki. Ushabiki una mipaka yake.

Nasisitiza na humu ukianza ushabiki kama jana, Mkuu invissible funga hii thread.
 
Waliochoma kanisa ndio nawaona wajinga zaidi na muflisi wa mawazo/imani pia wakosa uvumilivu. suluhisho la matatizo/kosa c kulipiziana visasi. walitakiwa washirikiane kuhakikisha wale waliochoma kitabu kitakatifu cha kiislam wanafikishwa mbele ya sheria,wakatoa na ushahidi thabiti ku invite conviction, sasa unapokimbilia kulipiza kisasi ndio unaeneza moto mbaya wa vurugu
 
Baada maombezi mwenye nyumba akato kwa hiyari yake mwenyewe kutoa kuran ili ichomwe moto sababu aliona hizi haya za ki.....
 
Si Rafu na ndio kazi yao Mkuu, ni vema kuifunga kuepusha Malumbano ya Kidini hapa tunasaka muafaka kwa kushauriana meza moja waumini wa Dini zote bila Ushabiki. Ushabiki una mipaka yake.

Nasisitiza na humu ukianza ushabiki kama jana, Mkuu invissible funga hii thread.
GR,
ndugu yangu, kwa nini kama mtu anaona haki haikutendeka (kuchomwa kitabu cha imani yake) asichukue hatua za kisheria kama ambavyo kosa lingine lolote likitokea? Kwa nini waanze kuwapa pressure viongozi wao wakachome kanisa moto? Kama mambo yakienda hivi tuna haja ya kuwa na serikali?
 
kwa hiyo utafuta imani za watu jwa kuwalazimisha waingie dini yako the so called 'sayansi'. You are then worse than them all!
I could be worse than them all kiimani, but one thing I know for sure is that, hii kitu ni ya kuletwa na imetupotezea mwelekeo siye Waafrika , imetugawanya kwenye makundi tusiyostahili na tukiamua tunaweza kuishi bila uwepo wake! Na kama tunaruhusu uwepo wake; basi uishie majumbani mwa watu binafsi!!
 
Vita ya Panzi furaha kwa Kunguru, Kikwete lazima awe na Furaha hapo yeye ndio alioanzisha mambo ya udini. Kila akitoa hutuba anazungumzia udinoi sasa amechochea kuni kwenye moto. Lazima Watanzania tuwe na Hekima sio kila wanalolizungumza Wanasiasa tunalifuatisha
 
GR,
ndugu yangu, kwa nini kama mtu anaona haki haikutendeka (kuchomwa kitabu cha imani yake) asichukue hatua za kisheria kama ambavyo kosa lingine lolote likitokea? Kwa nini waanze kuwapa pressure viongozi wao wakachome kanisa moto? Kama mambo yakienda hivi tuna haja ya kuwa na serikali?
yes, tunahaja ya kuwa na serikali lakini si lazima tuwe mifanatics wa midini!!
 
Imefika mahali serikali iache ushabiki huu wa kipuuzi wa kidini maana itatuangamiza.. Inauma sana kuona wakristu na waislam wakishambuliana na kukashifiana tena kwa hasira mpaka imefikia hatua ya kuchoma maandiko matukufu pamoja na nyumba za Mungu. Serikali yetu iko kimya na wala hakuna hatua yoyote inayoichukua kwa hawa mafedhuli wanaotaka kutugombanisha.. Hakika na alaaniwe mtu anayejaribu kutupeleka huku, mwenyezi Mungu anamuona na hakika atamuangamiza kabla ya kuruhusu hiki kizazi chake kitukufu cha watanzania hakijaangamia..

Mimi ni mkristu na nimetoka kwenye familia yenye mchanganyiko wa watu wenye dini mbalimbali ikiwemo waislam..

Leo hii huwezi kupandikiza chuki baina yetu sie ndugu tulioishi pamoja kwa furaha na kuvumiliana kwenye imani zetu eti kwa sababu tunataka kutengenishwa ili watuongoze vizuri..

Naongea haya maneno kwa uchungu mkuu na machozi yanakaribia kutoka.. Sisi wote wenye mapenzi mema na nchi hii, naomba tuungane pamoja na kukemea huu upuuzi.. Wote katika dini zetu tumrudie Mungu na kufanya maombi ili atuepushe na hili janga ambalo linaweza kulikumba taifa letu wakati wowote sasa.. Na tuwakatae viongozi wote kwa umoja wetu (wakristu na waislam) wanaojaribu kupandikiza chuki kati yetu.. Hata kama tutabaki maskini, lakini tuendelee kujivunia Utanzania wetu pamoja na misingi mziuri ya kuishi kidugu tuliyoachiwa na baba ya wa Taifa.
 
GR,
ndugu yangu, kwa nini kama mtu anaona haki haikutendeka (kuchomwa kitabu cha imani yake) asichukue hatua za kisheria kama ambavyo kosa lingine lolote likitokea? Kwa nini waanze kuwapa pressure viongozi wao wakachome kanisa moto? Kama mambo yakienda hivi tuna haja ya kuwa na serikali?

Mkuu,
Tatizo la kuchomwa Quran na Kanisa kama sehemu ya malipizi tuyaweke Mezani na sheria ifuate Mkondo ili kujenga misingi ya kuheshimiana nan kuondoa matabaka miongoni mwetu yatakayodumisha Umoja. Sote ni ndugu regardless of our faith.

Leo hii tukishabikia Udini hakuna atakayebaki salama, si kila muislam katika uko wao ni waislamu tu na si kila mkristo katika ukoo wao ni wakristo tu, tumechanganyikana sana kwa hiyo maafa yanamaanisha tafaruku kubwa kwa familia zote.

Lengo la thread hii ni kuwaamsha RPC na RC mwanza wakifutika vichwa ofisini leo kama Mzee Kobe, matokeo ya fat-wah baada ya sala ya Ijumaa ni doa kubwa kwa utaifa na umoja wetu na si kingine mkuu.

Serikali isisubiri madhara wachukue hadhari na meza ya mazungumzo izae matunda si vurugu na hamaki
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom