hawa wazee wote ni mafisadi. Hapo wanawaza, sijui koplo chacha ataleta shs ngapi leo jioni.
kwikwi kwi .. hii imenikuna.. na koplo asipoleta za kutosha anahamishiwa mafya!! au pemba lol!
hawa wazee wote ni mafisadi. Hapo wanawaza, sijui koplo chacha ataleta shs ngapi leo jioni.
Niliogopa sana kumsikia huyu Mwema akitangaza mabaya. Hii ni hatari, unasimama unatangaza kupiga watu risasi za moto. TUNAELEKEA WAPI?
kwa kiasi fulani tunaweza kuangalia ni kwa nn akasema kuwa kuuwa halali ni mazingira yepi, mmh kwa spinning nyinyi mwisho na kuna watu liandikwalo basi sawa wanaanza kusupport usiwe ndondocha
mazingira yatahukumu, na sio utashi pekee mkjj, walivamiwa kituo wakamtoa mtuhumiwa na kisha kumuua sasa mazingira haya yaachwe yameee eeeh?
hata siku moja serikali na vyombo vya usalama kwa hapa hamna budi kukemea
mtu kawaambia ukweli mnasema kawatishia. Itawezekana vipi raia wachukue sheria mikononi kwenda kituo cha polisi na kumkwapua mtuhumiwa na kumuua kana kwamba Tanzania haina sheria? Je siku mmoja na ukichaa wa baadhi ya watu wakiamua kuingia ofisi ya Wizara au hata Ikulu na kumfanyizia "mbaya" wao si tutapiga kelele sana.
Hivi waungwana mnataka watu waanze kuvamia vituo vya polisi na kuchoma watu moto?
Lazima utawala wa sheria ulindwe kwa nguvu zote na hiyo ipo kila sehemu hapa duniani.
Hata kama polisi wameshindwa kazi yao lakini hata siku moja siwezi kutetea raia kujichukulia madaraka mikononi mwao. Madhara
ya hatua kama hiyo yanaweza kuwa makubwa mno.
Niliwahi kushuhudia sehemu, vijana wakamkamata jamaa na kuanza kupiga kelele za mwizi, watu wakaja na kumponda mawe mpaka kufa, kumbe jamaa alifumaniwa tu na mke wa mtu.
Tunapotetea utawala bora basi ni kwa kila mtu kuanzia raia mpaka rais wetu
Nadhani IGP mwema ametumia sentensi zisizo sahihi katika kufikisha ujumbe. Kusema kwamba watauwa sio jambo la maana at this point. However, police kokote dunia wana haki ya kujilinda this include uses of guns if necessary.
Kwa nchi za dunia ya tatu ambako police wengi wanafrustrations za maisha, kuwaambia kwamba wanaweza kuuwa ni kuongeza chumvi kwenye kidonda, kwani yanaweza lipuka mauwaji ya kishenzi shenzi na kiteteo kikubwa kikawa vipengele alivyo vitaja IGP.
Kada mpinzani. usigeuze JF kuwa uwanja wa mazuzu. Hizo sheria unazosema zinafanya kazi mbona hazijamgusa Ditopile??? Na kuna ushahidi wa kutosha kabisa kuwa Ditto alishiriki katika mauwaji ya marehemu Mbonde.
Kada mpinzani. usigeuze JF kuwa uwanja wa mazuzu. Hizo sheria unazosema zinafanya kazi mbona hazijamgusa Ditopile??? Na kuna ushahidi wa kutosha kabisa kuwa Ditto alishiriki katika mauwaji ya marehemu Mbonde.
Wanataka tujue kuwa kuna sheria za aina mbili, za watu wa kawaida na wale wanaojiona siyo wa kawaida (watawala).
We ushawahi kusikia mtuhumiwa mwingine anayepitia mlango wa
ma-Judge na siyo mlango wa watuhumiwa?
Ndo Tanzania hiyo.
By the way polisi walianzisha ulinzi shirikishi, ndo maana wananchi wameamua kushiriki kwenye ulinzi? Kama wenzao walivyowafanya wakenya, wakaamua na wao wafanye hivyohivo kwa Mbakaji!
kumbe kweli haya ya sasa bavicha wanayolalamikia sio mapya?Niliuliza "mko tayari"... ?