Ibara ya 35 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

kaskas

Senior Member
Nov 1, 2010
158
137
WANASHERIA/WANASIASA NAOMBA MTAFSIRI HII IBARA YA KATIBA YA TANZANIA

35.-(1) Shughuli zote za utendaji za Serikali ya Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na watumishi wa Serikali kwa niaba ya Rais. (2) Amri na maagizo mengine yanayotolewa kwa madhumuni ya ibara hii yatathibitishwa kwa namna itakavyoelezwa katika kanuni zilizowekwa na Rais, kwa kuzingatia masharti ya Katiba hii.
 
Nyerere alisema hivi "kwa katiba hii tuliyonayo anaweza kutokea kiongozi na kuitumia kwa maslahi yake" hii ni nukuu ya mwl nyerere akizungumzia uzuri na ubaya wa katiba tuliyonayo.
Suruhisho pekee kwa sasa ni kudai katiba mpya iliyopendekezwa na wananchi ili tuondoe u Miungu watu ambao umeliingilia taifa letu kwa sasa.

Swelana aka umtinki.
 
Nyerere alisema hivi "kwa katiba hii tuliyonayo anaweza kutokea kiongozi na kuitumia kwa maslahi yake" hii ni nukuu ya mwl nyerere akizungumzia uzuri na ubaya wa katiba tuliyonayo.
Suruhisho pekee kwa sasa ni kudai katiba mpya iliyopendekezwa na wananchi ili tuondoe u Miungu watu ambao umeliingilia taifa letu kwa sasa.

Swelana aka umtinki.
UKITAKA KUJENGA NYUMBA IMARA ANZA NA MSINGI IMARA.....sasa ili tuwe na katiba iliyo BORA tuanze kujenga kwanza katiBA zilizo bora ndani ya VYAMA VYETU ESPECIALLY VYA UPINZANI kwanza wanatakiwa waonje uchungu wa katiba unaoangalia MASLAI YA WANACHAMA WAO KWANZA WANATAKA NINI NA SI VIONGOZI KWANZA.....tukilifanikisha hilo ndipo tutaweza PATA KATIBA BORA KABSA YA NCHI HII maana tutatoka na uo msingi wa kuwaangalia wanachama kwanza then tutakuja KUDAI KATIBA INAYOANGALIA MASLAI WA WANANCHI KWANZA NA SI VIONGOZI KWANZA
 
Nafikiri ni muda mwafaka wa kupata katiba mpya.
Tatizo tafsiri na mtafsiri.
Hata mkiwa na katiba inayoelekeza mletewe hela nyumbani kila siku, asipotokea wa kuitafsiri hivyo, hamtaletewa hizo hela.
Tatizo ccm.
 
Je, Jaji Mkuu na Spika ni watumishi wa serikali wanaaoongoza mihimili miwili ya Mahakama na Bunge?
Interesting quiz ...naibu spika (spika) ameteuliwa na rais lakini sidhani kama spika na bunge lake wanaweza mteua rais. Hebu think deeply hapa kujua kiuhalisia nani ni mfanyakazi wa nani!
 
Back
Top Bottom