Hebu tukitafakari kiapo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania

Kichuchunge

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
338
891
Mimi .............. naapa kwamba nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nitalinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilivyowekwa kisheria.

Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie.

Mimi ................ naapa nitatenda kazi zangu za Urais wa Jamhuri ya Tanzania kwa uaminifu kwa kutimiza wajibu wa kazi hizo kwa bidii na moyo mkunjufu na kwamba nitawatendea haki watu wote kwa mujibu wa sheria, mila na desturi za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila woga, bila upendeleo, huba wala chuki.

Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie.

Mimi ............. naapa katika kutekeleza madaraka niliyopewa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania....

Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie.

Kiapo cha kwanza Rais anaapa kuwa atakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuitumikia kwa moyo wake wote, ataihifadhi, kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ni kwa msingi huo, Rais aliapa kiapo cha pili kinachoeleza kuwa atatenda kazi zake kwa uaminifu na kutimiza wajibu wa kazi hizo kwa bidii na moyo mkunjufu.

Pia, atawatendea haki watu wote kwa mujibu wa sheria, mila na desturi za Tanzania bila woga, upendeleo, huba wala chuki, hii ni kwa mujibu wa kiapo cha pili alichoapa Rais.

Katika kiapo cha kudumisha Muungano, Rais aliapa kwamba ataitetea na kudumisha umoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Suala la rais kuapa ni takwa la kikatiba kwa mujibu wa ibara ya 42(5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Ibara hiyo inataka kila rais mteule na kila mtu atakayeshikilia kiti cha urais, kabla ya kushika madaraka ya rais, kuapa mbele ya Jaji Mkuu kiapo cha uaminifu.

Lakini, pia ataapa kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria itakayotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ibara ya 8(1)(a) ya katiba hiyo inasema “Wananchi ndiyo msingi wa mamlaka yote na Serikali itapata madaraka yake yote kutoka kwa wananchi”.

Serikali itawajibika kwa wananchi. Kwa hiyo utaelewa kwa nini rais anaapa kuilinda Katiba yetu. Anakula kiapo mbele ya Jaji Mkuu lakini anayemuomba amsaidie ni Mungu.

Mtu anapoapa hueleza umma au mamlaka husika kile anachoamini na kiapo huchukuliwa ndiyo ukweli halisi na kwa maneno mengine huwezi kuyakana maneno uliyoapa chini ya sheria. Je tunatekeleza?

Kiapo.jpg
 
Mmmmh,inafikirisha sana!Ukisoma hicho kiapo unapatwa na msisimko!Mimi naona kuna haja ya kutunga sheria ambapo kila mwaka Rais aapishwe!Hii itamsaidia kumkumbusha kiapo chake!
 
Back
Top Bottom