Freelancer
JF-Expert Member
- Sep 22, 2008
- 2,965
- 2,141
Jamani kwa mtu yoyote ambaye anafahamu WEB API ambayo naweza nikaitumia for free kusend SMS anijulishe. Nimejaribu Google Voice ila sijui kama kutuma meseji ni bure maana natuma meseji hazifiki.
Kitu nachofanya sio kwa ajili ya faida. Nafanya for a good cause. Sasa habari za kuniambia napenda vya bure ndo nini. Unapotokea kwamba unaitaka kuisaidia community fulani na unatafuta cheaper solution ambayo haitacosdt hela ni kosa???
Nimeamua kutumia Clickatell wao wanachaji kama 0.027 USD per message.Mkuu binasfi sijawahi ona SMS provider wa bure online, wengi hutoa demo tu, zaidi ni kuchagua provider mwenye rates ndogo. Ukiweka 10$ tu unatuma sms nyingi sana.
Nimeamua kutumia Clickatell wao wanachaji kama 0.027 USD per message.
Nimecheki kuona jinsi gani tunawezapata hii service kule Tanzania kupitia Mobile Operator wa kule TZ, hadi sasa sijapata jibu.
Wewe unatumia technology gani kwenye application yako ambayo unataka ku integrate na SMS service?
Hizi mara nyingi zinakuwa ni based on REST API. Kwa hiyo any programming language yenye web support can do the job. Mfano Php, Python, Java etc. Hiyo kampuni inaitwa Clickatell wanafanya SMS dunia nzima. Na kama unataka bulky SMs unaweza negotiate nao wanaweza wakakufanyia bei ya discount kama utaingia contract ya kununua kila mwezi
Yes, I know.
Njia nyingine ni kupata access ya SMS Server/Gateway ya mobile operator katika nchi yako au nchi ambazo zina consumers wa application yako.
Mobile operator anaweza kukupa hostname, account name na password then una route message zako moja kwa moja kwenda kwenyeSMS server ya operator, wao wana foward kama SMS kwenda kwa consumers wako.
Hii approach unakuwa umeondoa another Layer katika communication Stack layers ikiwa utatumia SMS service providers kama hao wa USA, kwani wao pia wanachukua message yako, then wanacheki receiver's home SMS server ndiyo wana route kwenda huko. Sasa kwanini na sisi tusiingie agreement na operators wa tz tuka route message zetu moja kwa moja?
Inaweza kuwa nice idea. Kama SMS zote local then itakuwa poa. Ila kama SMS ni combination na local na international then in terms of cost hawa clickatell wanaweza kuwa bei rahisi zaidi.
Kwa dunia ya sasa hivi ni vizuri ukafikiria expansion beyond local boundaries has kama application yako ni kwa ajili ya biashara. Customers wanaweza kuwa popote pale.
Halafu sijui kama service providers wanatoa support za APIs kama hizi kampuni amabazo zimespecialize kwenye hayo mambo.