Huyu mke wa mtu ananitafutia matatizo!

Huyo ni mke wa mtu,muache na acha kumsaidia,maana unavo endelea kumsaidia anazidi kumdhalilisha mwanaume wake.

~Kumbuka yale unayotaka utendewe uwatendee wengine,maana maisha ni kupanda na kushuka,wewe muoe halafu uchumu wako ukija yumba atapata mtu nje na atakutangaza na kukudharau km mara 70 ya huyo mwenzio

~Huyo dada muogope km ukoma
 
Mke wa mtu kaa nae mbali.Wengi wana chuma ulete.Hivi inakuaje unakula kiapo na mwenza wako alafu mkifika ndan unamgeuka kisa hana kipato kikubwa ina maana unakua hujaona kwenye mahusiano kabla ya ndoa?wanawake tupunguze tamaa.
 
Habari zenu ndugu,

Nakumbuka kwa mara ya kwanza nilikuja humu JF kuomba ushauri katika jambo lililonitatiza kwa wakati ule na kweli wana JF walinishauri na ushauri ulinisaidia na kwa sasa niko poa.

Leo nimekuja tena na jambo hili linalonitatiza naomba ushauri wenu nifanyeje!

Kuna binti nilisoma nae O-level miaka kadhaa iliyopita na tukapotezana kwa miaka mingi lakini kwa vile milima haikutani ila binadamu hukutana basi tulikutana miezi kadhaa liopita kwenye harusi ya jamaa yangu mmoja hivi.

Ki ukweli kwa vile tulipotezana miaka mingi hata hatukua na mawasiliano hivyo tulipokutana tulifurahi sana kwa vile tulikua marafiki sana enzi za O-level na nakumbuka nilimtongoza kipindi kile akanikataa kabisa hivyo tukawa ni marafiki wa kawaida tu, baada ya kumaliza O-level tulikua katika contact ila baada ya miaka kadhaa kupita akawa hapatikani kwenye namba yake na mimi kuna wakati ilifikia nikabadili namba hivyo tukawa tumepotezana rasmi! Hivyo baada ya kukutana tulifurahi tukakumbushana enzi zile na kuelezana our current situation kisha tukabadilishana namba. Moja ya vitu alivyoniambia ni kua kwa sasa keshaolewa na ana mtoto mmoja. Basi nikampa hongera kisha tukaachana siku ikapita.

Siku iliyofuata alianza kunichatisha akiniulizia mke wangu na watoto, nikamjibu ki ukweli bado sijabarikiwa kuoa ila nilikua na mchumba aliyenisaliti sana na nimeachana nae si kitambo sana hivyo kwa sasa bado sijaingia tena kwenye commited relaltionship. So tukachati ila kilichonishangaza akaniambia anahitaji tuonane sehemu tuongee zaidi basi na mimi nikamkubalia.

Jioni tukakutana kwenye hoteli fulani aliyoipendekeza yeye, tuliongea mengi ila akaniweka wazi kua mambo yake kiuchumi si mazuri kama nina weza kumsaidia apate kazi atashukuru sana, na mimi nikamwambia nitajitahidi, basi tukaachana siku ikapita. Ila kuanzia siku hiyo akawa ananichatisha sana na simu kila mara, mara anakumbushia nilivyomtongoza akanikataa na kusema ule ulikua utoto n.k. basi tunacheka na kutaniana.

Kuna siku akaniambia ana shida na nimkopeshe kiasi flani cha hela, basi na mimi kwa vile nilikua nayo nikampatia. baada ya siku kadhaa kupita akaniambia tena kua amekwama nimsaidie kiasi fulani cha hela, kumbuka hapa lugha haikua nimkopeshe hapa alisema anaomba, basi na mimi nikatoa kwa vile nilkua nacho. Siku zikapita akaanza kunisimulia matatizo ya mumewe sasa mimi kama mwanaume sikupendezwa na hilo nikamwambia unaponiambia kua mumeo haudumii familia ni kumdhalilisha so usimfanyie hivyo but akawa hajali, sasa mara akaanza kuniomba hela za salon, mara mtoto wake amepungukiwa ada nimsaidie basi mimi nikawa natoa ninapoweza kwa upendo tu.

Ila sasa nikaanza kujisikia vibaya kwa sababu mda mwangine ananiambia dhahiri jinsi anavyomchukia mumewe na kila udhaifu wa mumewe anaumweka bayana na hadi mda mwingine ananiomba hela ya matumizi nyumbani. Sasa kuna siku nimemwambia mumeo hua hakuulizi unatoa wapi fedha hizi, akajibu kua hawezi kumuuliza coz anajua kua anajishughulisha na vikoba.

Sasa kilichofanya niandike uzi huu ni kwamba huyu binti amenitamkia kabisa kua anataka aachane na mumewe ili awe ana mimi, nikamuuliza kwanini ufanye hivyo? akajibu eti jamaa hawezi kumhudumia yeye na mtoto wake! nimejisikia vibaya sana kwani mimi nimekua nikimsaidia kwa upendo kama rafiki ila kwa sasa amekua akiniomba hela kama vile mimi mumewe na kunitaka kimapenzi.

Kwa jinsi nilivyosalitiwa najua ni jinsi gani inauma mke wako kuliwa na mtu mwingine, na hapa nikiangalia kigezo kikubwa kwanini huyu binti anafanya hivyo ni kwa sababu jamaa ana hali ngumu kimaisha.

Hivyo naomba ushauri wenu maana nimetamani kukata mawasiliano nae ila kuna siku kanipigia simu kua mtoto wake anaumwa sana yuko hospital but amepata changamoto ya fedha, ikabidi niende hospital kuhakiki nikawakuta kweli, na mtoto alikua amedhoofu sana, ikabidi nimsaidie.

Sasa nawaza nikiendelea kumsaidia anakua ananitaka niwe nae kimapenzi na nikisema nikate msaada nakua namuonea huruma mtoto, na ki ukweli jamaa ambae ni mumewe yupo katika wakati mgumu sana coz amepoteza ajira yake na bado hajapata ajira.

Je nifanyeje? Maana sitaki kumlia jamaa mke wake, but as long as naendelea kuwasiliana na huyu mwanamke ni kwamba anafanya mazingira ya mimi kua kama mume wake na anaushawishi mkubwa ki ukweli maana ni mrembo sana.

Asanteni.
Utamtafuna tu, imagine ukifa ataishije au before kumjua aliishije. Huruma zitakuponza.
 
Hadith nzuri sna inaendelea lini
 
Achana nae! Huruma kasaidie walemavu na wasiojiweza au wasaidie Ndugu zako waliokulea kule namanyere na kazulamimba....
Kwanza alishakukataa hapo mwanzoni, je alitathimini athari ambazo zingekupata pindi alipo kukatalia? Ungekuwa chizi au ujinyonge kwa ajili yake Leo ungekuwepo hapo ulipo? Isitoshe huyo ni mke wa mtu na wakati anaolewa alikiri kuwa atakaa na mumewe wakati wa shida na raha! Sasa kwa nini aikwepe shida wakati anajua kuwa shida ipo? Huoni kuwa kuna walakini hapo?
Sasa hivi unajifanya unajua kumsaidia je, akimpata anayemsaidia zaidi yako Wewe unauhakika atakukumbuka na kuuthamini mchango wako? Wewe unavyomsaidia unafikiri utapata faida gani zaidi ya kufanya zinaa? Wewe hujui madhara ya kufanya zinaa tena na mke wa mtu? Unafikiri ulivyomtongoza kipindi kile mnasoma yupo vilevile! Hujui kuwa wahuni walishamharibu kabisa miundombinu yake ya chini?
Tumia akili yako vizuri.....
NASIKITIKA SANA IDADI YA WANAUME WANAOWEZA KUFANYA MAAMUZI YENYE TIJA IKIPUNGUA SIKU HADI SIKU.
 
Hana nia mbaya, anataka tu kulipa fadhira kwa unayomfanyia!!
Anahisi ndio kitu pekee kwake kuonyesha shukrani zake kwako!
Kazi unayo!
 
Hiyo kaz ulohaidi kumtafutia Hugo mwanamke ni bora umtafutie huyo mume wake.
 
sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, chukua tahadhari mkuu usimle please utaandamwa na mikosi, mi nakushauri kaa chini record namba zako zoote za kwenye simu yako kwenye notebook kisha badili namba, badili namba mkuu kabla ya jambo kubwa halijakufika.... wanaume tulio wengi hatujui lakini hakuna kitu kibaya kama ku take advantage ya shida za mwanamke na kufanya nae tendo la ndoa wakati yumo kwenye ndoa... ni mbaya mnooo tunapata mikosi bila ya kujijua..... achana nae haraka sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom