Huu wa Kukiri mapungufu ni uungwana kaka Zitto! Hongera sana!

Honey K

JF-Expert Member
Sep 14, 2008
629
72
Maelezo ya Bajeti Kivuli

Katika mjadala unaoendelea Bungeni kuhusu Bajeti, baadhi ya wabunge wameeleza kwamba Bajeti Kivuli haikuonyesha vyanzo vya mapato na hivyo kuita ni vyanzo sifuri. Ukweli ni kwamba tumeweka vyanzo vya mapato ya ndani kwa ujumla bila kuainisha mapato ya kikodi ni ngapi, mapato yasiyo ya kikodi ni ngapi na mapato ya Halmashauri ni kiasi gani. Hivyo tunakiri kosa hili na tumechukua hatua ya kuainisha mapato hayo Kama inavyoonekana kwenye jedwali hili hapa chini.

Mapato haya yamo ndani ya Hotuba ya Bajeti Mbadala lakini kwa makosa ya *kihariri hayakuonyeshwa kwenye jedwali na hivyo kuleta usumbufu kwa Wabunge na Watanzania wengine waliopata fursa ya kusoma Hotuba yetu. Tunaomba radhi kwa usumbufu. Nawashukuru walioona tatizo hili na hii inaonyesha kuwa wabunge wanasoma kwa makini Bajeti ya Upinzani.

Ninawatakia mjadala mwema wa Bajeti.
JUMLA YA MAPATO YA NDANI
Tshs. Millioni 11,889,078/-

MAPATO YA KODI
Tshs. Millioni 10,232,539/-

MAPATO YASIYO YA KODI
Tshs. Milion 1,163,533/-

MAPATO YA HALMASHAURI
Tshs. Milioni. *493,006/-

Kabwe Zuberi Zitto,Mb
Waziri Kivuli wa Fedha
 
..sasa na nyinyi CCM kwanini hamkiri mapungufu na makosa yenu na kuyarekebisha?

..mngekuwa na uungwana kama wa Zitto na CDM msingekuwa na wakati mgumu kama mlionao sasa hivi.
 
Maelezo ya Bajeti Kivuli

Katika mjadala unaoendelea Bungeni kuhusu Bajeti, baadhi ya wabunge wameeleza kwamba Bajeti Kivuli haikuonyesha vyanzo vya mapato na hivyo kuita ni vyanzo sifuri. Ukweli ni kwamba tumeweka vyanzo vya mapato ya ndani kwa ujumla bila kuainisha mapato ya kikodi ni ngapi, mapato yasiyo ya kikodi ni ngapi na mapato ya Halmashauri ni kiasi gani. Hivyo tunakiri kosa hili na tumechukua hatua ya kuainisha mapato hayo Kama inavyoonekana kwenye jedwali hili hapa chini.

Mapato haya yamo ndani ya Hotuba ya Bajeti Mbadala lakini kwa makosa ya *kihariri hayakuonyeshwa kwenye jedwali na hivyo kuleta usumbufu kwa Wabunge na Watanzania wengine waliopata fursa ya kusoma Hotuba yetu. Tunaomba radhi kwa usumbufu. Nawashukuru walioona tatizo hili na hii inaonyesha kuwa wabunge wanasoma kwa makini Bajeti ya Upinzani.

Ninawatakia mjadala mwema wa Bajeti.
JUMLA YA MAPATO YA NDANI
Tshs. Millioni 11,889,078/-

MAPATO YA KODI
Tshs. Millioni 10,232,539/-

MAPATO YASIYO YA KODI
Tshs. Milion 1,163,533/-

MAPATO YA HALMASHAURI
Tshs. Milioni. *493,006/-

Kabwe Zuberi Zitto,Mb
Waziri Kivuli wa Fedha
Mbona nyie magamba hamtaki kukiri kuwa Kikwete ni dhaifu?!!
 
SAWA ZITO KAKUBALI MAKOSA

Je na CCM mnakubali kwa haya mawili?

1-ukosefu na usumbufu wa kukosa umeme kwa wananchi mwaka wa fedha uliopita ilikua ni hujuma mahususi ya makusudi ili kuja kujitetea mbele ya bunge la sasa kuwa matumizi mabaya ya bujeti iliyopita ilisamwaka uhaba wa umeme???

2-je mabadiliko ya baraza la mawaziri lililopita ilikua ni strategy ya kufanikisha upitaji wa budget hii ya sasa na kufunika madhambi ya ubadhirifu wote wa pesa ya budget ya mwaka uliopita usijadiliwe kwenye bunge hili la budget??

Ukijibu hili usikurukupe fatilia utetezi wa serikali khs kutotekelezwa kwa matarajio ya budgeti iliyopita

Asante
 
Haya sasa CHADEMA wamekiri udhaifu japo kuwa ni mdogo, kama hili limewafaa CCM mbona hamkiri udhaifu ? badala yake mnaweka propaganda hata kwenye mambo ya msingi.
 
Maelezo ya Bajeti Kivuli

Katika mjadala unaoendelea Bungeni kuhusu Bajeti, baadhi ya wabunge wameeleza kwamba Bajeti Kivuli haikuonyesha vyanzo vya mapato na hivyo kuita ni vyanzo sifuri. Ukweli ni kwamba tumeweka vyanzo vya mapato ya ndani kwa ujumla bila kuainisha mapato ya kikodi ni ngapi, mapato yasiyo ya kikodi ni ngapi na mapato ya Halmashauri ni kiasi gani. Hivyo tunakiri kosa hili na tumechukua hatua ya kuainisha mapato hayo Kama inavyoonekana kwenye jedwali hili hapa chini.

Mapato haya yamo ndani ya Hotuba ya Bajeti Mbadala lakini kwa makosa ya *kihariri hayakuonyeshwa kwenye jedwali na hivyo kuleta usumbufu kwa Wabunge na Watanzania wengine waliopata fursa ya kusoma Hotuba yetu. Tunaomba radhi kwa usumbufu. Nawashukuru walioona tatizo hili na hii inaonyesha kuwa wabunge wanasoma kwa makini Bajeti ya Upinzani.

Ninawatakia mjadala mwema wa Bajeti.
JUMLA YA MAPATO YA NDANI
Tshs. Millioni 11,889,078/-

MAPATO YA KODI
Tshs. Millioni 10,232,539/-

MAPATO YASIYO YA KODI
Tshs. Milion 1,163,533/-

MAPATO YA HALMASHAURI
Tshs. Milioni. *493,006/-

Kabwe Zuberi Zitto,Mb
Waziri Kivuli wa Fedha

Nimekukubali kama kijana wa Tanzania ya leo. Mungu akutangulie usiteteleke kwenye ukweli
 
Mbona nyie magamba hamtaki kukiri kuwa Kikwete ni dhaifu?!!
Swala la Kikwete sio la Magamba, Yule ni Rais wetu wote, Hivyo Kama tunakubaliana Rais ni Dhaifu ni dhaifu tu haihitaji opinion za watu, lakini maana yake ni kwamba sisi wote ni Dhaifu pia.

Kuna post nimeweka hapa nahoji juu ya usalama wetu katika msingi wa kuwa na rais anayeheshimika na kuaminika katika Taifa kiasi cha kwamba, akisema tunaingia vitani, basi wote tunafurahia kauli hiyo na kuingia vitani kumtandika hadui, watu wengi hawajapata mantiki ya post ile, lakini maana yake inapanuka mpaka kwenye mawanda kama haya.

Kama Rais ni Dhaifu maana yake Taifa zima ni Dhaifu, na Jinsi CHADEMA wanavyoendelea kumdhoofisha ndio tunakuwa dhaifu zaidi.
YANGU NI HAYO
 
Nafurahi Katibu Mwenezi umeliona hili na utaanza kulifanyia kazi na kulihimiza hasa ndani ya Chama chako pia
 
Nape Umerudi Dar?Karibu Sana ingekuwa Vema kama ungejibu hoja za wadau kwa muda mrefu umekuwa adimu kama sharubu za kambare!
 
Lini magamba waliwahi kukiri waliokosea wao ni malaika hupatia tuu! wanaosema ndiyo ........ ccm wote ..ndiyooooooooooo hata waliolala basii hiyo ndo kazi yao!
 
Swala la Kikwete sio la Magamba, Yule ni Rais wetu wote, Hivyo Kama tunakubaliana Rais ni Dhaifu ni dhaifu tu haihitaji opinion za watu, lakini maana yake ni kwamba sisi wote ni Dhaifu pia.
Mkuu, Kikwete alipitishwa na magamba kugombea urais and then akatumia madaraka yake ya "Imperial presidency" kuchakachua kura na matokeo ya uchaguzi 2010. CCM ndio walimuona the best na si watanzania.
 
viongozi wa hivi ndio wanaotakiwa...kuna hotuba moja ya nyerere na yeye anakiri madhaifu yake kama kiongozi wa AFRICA kwa kukopi kila mfumo wa maendeleo kutoka ulaya bila kuutafakari namna ya uendeshaji..alikiri hadharani
lakini hwa wenzetu wa leo huezi sikia hii kitu
BIF UP SANA ZITTO...
 
Swala la Kikwete sio la Magamba, Yule ni Rais wetu wote, Hivyo Kama tunakubaliana Rais ni Dhaifu ni dhaifu tu haihitaji opinion za watu, lakini maana yake ni kwamba sisi wote ni Dhaifu pia.

Kuna post nimeweka hapa nahoji juu ya usalama wetu katika msingi wa kuwa na rais anayeheshimika na kuaminika katika Taifa kiasi cha kwamba, akisema tunaingia vitani, basi wote tunafurahia kauli hiyo na kuingia vitani kumtandika hadui, watu wengi hawajapata mantiki ya post ile, lakini maana yake inapanuka mpaka kwenye mawanda kama haya.

Kama Rais ni Dhaifu maana yake Taifa zima ni Dhaifu, na Jinsi CHADEMA wanavyoendelea kumdhoofisha ndio tunakuwa dhaifu zaidi.
YANGU NI HAYO

Mkuu kwa maneno mengine ni kwamba kutokana na huo "udhaifu" wa Rais wetu kama Taifa hatuko salama! Akitokea adui akaishambulia nchi yetu kwa sasa, Rais wetu hana "ubavu" wa kuwavuta wanachi wote kuunganisha nguvu dhidi ya huyo adui! Na hii ni hatari sana kwetu sote bila kujali "itikadi"!!!
 
Nappe nini mbona hujachangia chochote zaidi ya kukopi na kupasti.!
 
Back
Top Bottom