KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,590
- 4,603
Kuna mambo ukiyaangalia kwa undani sana Tena kwa jicho la tatu utagundua kuna kaupepo fulani kana mchanganyiko wa joto na baridi kakivuma upande wa kiti Cha Spika. Je, upepo huu una madhara kwake?
Mambo fulani fulani yanatoa picha ya vuguvugu la upepo huu. Kwanza, kitendo Cha Shabiby kusema kauli yenye kuashiria Jambo zito, nanukuu sehemu ya kauli yake "...hata wewe Spika ukileta siasa zako tutakuazimia". kwa wenye kuangalia mambo kwa jicho la tatu watagundua kauli hiyo imebeba kusudi na dhamira. Je, ni siasa zipi Spika anazifanya? Je, zipo kinyume na sera za CCM?
Jambo la pili, Punde tu baada ya kupokea ripoti ya CAG kamati kuu ilikaa na kutoa maazimio kwa Serikali kuchukua hatua za haraka kwa wote waliohusika na ubadhirifu. Spika ni mjumbe wa vikao vya kamati kuu na azimio hilo aliridhia. Kama mchakato wa kuchukua hatua ,unaanzia bungeni huku Spika amesema kwamba Ripoti itajadiliwa mwezi Novemba. Je, utekelezaji wa maazimio ya kamati kuu utakuwaje?
Jambo la tatu, wakati wa mjadala wa mambo ya ushoga , Spika aliagiza Serikali ifanye mabadiliko ya sheria. Kwa uelewa wangu mdogo, sioni kama spika ana mamlaka ya kuiagiza Serikali. Kwa sababu katika mchakato wa kubadili sheria , serikali hupeleka muswada bungeni na mwisho bunge huufanya muswada kuwa Sheria. Je, Spika ana hayo mamlaka?
Nne, kitendo cha Waziri Mkuu na Makamu wa Rais kwa nyakati tofauti wameweka mkazo wa kuchukua hatua kali kwa haraka kwa wahusika waliotajwa na ripoti ya CAG. Je, hiyo inaashiria nini?
Hapa ndipo akili ya ziada inatakiwa itumike katika kuona kilichopo katikati ya mstari. Nimalizie kwa kusema ,huu ni upepo mbaya sana kuelekea kwenye kiti Cha Spika. Je ,upepo utapita naye au utavuma na kutulia ?