Huu ni baadhi tu ya ufisadi mkubwa ndani ya CHADEMA; ni kuhusu mamilioni ya Sabodo

Nauliza hivi!
1.Uadilifu wa viongozi wa chadema uko wapi?
2.Je huu sio ufisadi? au ufisadi ni EPA,MEREMETA na DOWANS?
3.Hivi unapo wadanganya watanzania kuwa umerudisha gari wakati nyuma yake umelichukua kimya kimya inaleta picha gani?
4.Hivi kunautofauti gani kati ya mwamvita makamba aliyejenga nyumba hapa TZ na MBowe aliyekwenda kununua nyumba nje ya nchi ?
5.Hivi hatari ya kuwaamini viongozi kama hawa ambao machoni niwasafi,moyoni wanaroho ya mbwa mwitu mwisho wake itakuwaje?
6.Hivi kunaulazima gani kuweka walinzi kanisani anakosali mchumba wa Dr.slaa kwa kutumia ruzuku ya chama?
7.Hivi CHADEMA watachukuaje nchi,ikiwa pesa iliyoazimishwa na kamati kuu baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 kuwa asilimia 25% ya ruzuku yote kwa kila mwezi iwekwe kwenye account ya uchaguzi kwaajili ya 2015,lakini mpaka sasa hakuna hata shillingi zote zimechukuliwa na wajanza wa chache?

Naomba kiongozi wa CHADEMA yeyote yule aliyemo humu JF aje akinzane na ukweli huu...ili tuweze kuweka data kamili hapa.
NI mwanzo tu wa MWANAHALIS kueleza uozo wa CHADEMA,tusubiri makala ijayo.


Ulivyouliza tu hapo nimegundua wewe ni mla rushwa na mnafiki manake unapiga vita wapiga vita.
In red uliza uambiwe hiyo nyumba kajenga nani acha kuropoka. Nyumba imejengwa na Quentin na ni fisadi la ki Australia ambalo makamba ametumia madaraka likapata tenda ya kupima mafuta bandarini na kuyawekea dawa. Alikuwa mkurugenzi wa SGS na Makamba aliruhusu mwanae afunge ndoa bomani na kafiri nishangaa kuona na sehemu ya kuswalia ipo ilhali ndani anaishi na kafiri. Hapo ndo ujue CCM linapokuja ufisadi hata imani za kidini zinawekwa pembeni.
 
Hii ni vita ni mapambano; katika vita - hasa classical warfare - lengo ni kuwashambulia majemedari. Tumeshaona kuwa CDM wanashambulia viongozi wa juu wa CCM na hiyo ni sehemu ya mapambano na anayefikiria kuwa watu wa CCM watakuja na kutoa pongezi kwa viongozi wa CDM anakosea. Tumeshaona toka mwanzo wa kampeni za Arumeru na kwingine viongozi wa CDM watashambuliwa siyo kwa mambo ya utendaji tu bali hata kwenye mambo binafsi. Hili limekuwa likifanyika kwa viongozi wa CCM vile vile.

Ni jukumu la watu kupima kila wanachokisoma na kupima uzito wa ukweli wake - au hata kupima uwezekano wa ukweli wake. Kama mtu anaweza kuyumbishwa na simulizi la kufikirika kwa sababu linasomeka vitamu atakuwa na matatizo.

Mwanakijiji,

Bravo...! ! Ni muda sasa kwa wale wapambanaji wa kweli kuelekeza nguvu na akili zetu kwenye chaguzi ndogo tulizo nazo.Let us move on....!!!
 
pia ni vizuri mh MNYIKA akaijibu hii tuhuma ambayo sisi tushaiona kama haina ushaidi wa kutosha

WanaJF,
Upotoshaji si vema kuuchia. Mnyika yuko Joeburg kikazi hivyo naomba kufafanua mwenyewe.
1. Fedha za Sabodo ni kweli zimepokelewa kwa awamu mbili @100m. Hizi zilikuwa kwa ajili ya Kampeni Uchaguzi Mkuu na tumezitolea taarifa ya matumizi mara kadhaa hadharani. Taarifa pia ipo kwa Msajili wa vyama kama mhusika anataka kujua zaidi.
2. Fedha za Sabodo ahadi ya 150m kwa ajili ya ujenzi wa Chuo. Ilikuwa ahadi na hatua tuliyopo sasa ni ku process "title Deed" eneo la ekari 100m Soga, Kibaha. Fedha za Sabodo bado ziko kwa Sabodo kwa kuwa ujenzi haujaanza. Sijui kama Sabodo anaweza kujifisadi mwenyewe.
3. Fedha za visima 200m toka Sabodo. Wajibu wa Chama ilikuwa kuomba. Wajibu wa Sabodo ni survey, design, kuchimba na kukabidhi visima vilivyokamilika( turn key). Sijui kwenye Turn key project ufisadi una sura gani. Labda mimi sielewi.
4. Nyumba ya Dr Slaa. Hivi mhusika alitaka niishi Abla milele au alitaka nikope kwake ili ajue siyo ufisadi. Anaruhusiwa kupekua pote na aanike hadharani ushahidi wake
4. Sihitaji kumtetea Mbowe. Ni mfanyibiashara asiyejificha. Sources za ujenzi wa Bilicanas si siri aache uvivu wa kufikiri na kutafiti kisayansi.
 
]Alafu Mi ningemshauri Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Kamanda Wilfred Lwakatare afanye uchunguzi wa huyu mtu anayejiita TUNTEMEKE, MWANAHALISI, PAA, PII, nk tumfukuze Chamani. Ni Mpuuzi sana. Yani mtu kushindwa uchaguzi wa BAVICHA ndio akengeuke kiasi hiki?!

[/QUOTE]Acha utope ww uchunguz wa nn na ushasema alishindwa bavicha?.........jibu hoja usiuukimbie ukwl
 
quote_icon.png
By MWANAHALIS

Nauliza hivi!
1.Uadilifu wa viongozi wa chadema uko wapi?
2.Je huu sio ufisadi? au ufisadi ni EPA,MEREMETA na DOWANS?
3.Hivi unapo wadanganya watanzania kuwa umerudisha gari wakati nyuma yake umelichukua kimya kimya inaleta picha gani?
4.Hivi kunautofauti gani kati ya mwamvita makamba aliyejenga nyumba hapa TZ na MBowe aliyekwenda kununua nyumba nje ya nchi ?
5.Hivi hatari ya kuwaamini viongozi kama hawa ambao machoni niwasafi,moyoni wanaroho ya mbwa mwitu mwisho wake itakuwaje?
6.Hivi kunaulazima gani kuweka walinzi kanisani anakosali mchumba wa Dr.slaa kwa kutumia ruzuku ya chama?
7.Hivi CHADEMA watachukuaje nchi,ikiwa pesa iliyoazimishwa na kamati kuu baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 kuwa asilimia 25% ya ruzuku yote kwa kila mwezi iwekwe kwenye account ya uchaguzi kwaajili ya 2015,lakini mpaka sasa hakuna hata shillingi zote zimechukuliwa na wajanza wa chache?

Naomba kiongozi wa CHADEMA yeyote yule aliyemo humu JF aje akinzane na ukweli huu...ili tuweze kuweka data kamili hapa.
NI mwanzo tu wa MWANAHALIS kueleza uozo wa CHADEMA,tusubiri makala ijayo.

Kwa mimi naona Mwamvita ana afadhali kubwa sana, kwanza ana kazi inalipa vizuri, pili anaweza akaonesha mikopo, tatu anaweza akaonesha kuwa kajengewa na bwanake, nne kajenga hapahapa nchini kwa hiyo hata kama kapata kwa njia ya udanganyifu au ubadhirifu mali hiyo inaweza kuzuiliwa na au kuchukuliwa.

Ya Dubai Jee? Mzalendo haswa aliyefanya hivyo? Utakuta huyo si Dubai tu, ikichunguzwa pengine na London pia, maana huko alikuwa akienda sana huyo kijana. Jee, na huko hajawekeza kwenye nyumba?
 
Mh. SLAA hujajibu tuhuma kuwa chama kinawalipa walinzi wa kanisa analosali (mkeo Josephine) sh. 500,000/= kila mwezi. Hizi tuhuma ni serious kuliko zote!
 
Lakini leo hii inashangaza sana kuona Mbowe na Slaa ndio haohao wanaoongoza kwa ufisadi mkubwa ndani ya chama na kwa watanzania kwa ujumla wao
.
Hardly one week hapa JF umeshaanza kumwaga sumu. Yaani huu ni "Ushigongo kweli kweli". illi tu upate wachangiaji! afadhali basi ungetoa ushahidi kidogo uonekane unajua walau kidogo. "Where we dare to talk openly" we this before we talk. Ooops! nilisahau kuwa uko kwenye campaign huko arumeru na unafikiri "Siasa Uchwara" za chama cha mafisadi, zitafanya Chama cha mapinduzi kishinde! Amka, ulikuwa unaota ndoto, kumekucha nenda kajenge taifa!
 
Hivi Million mia tatu zinaweza kununua nyumba Dubai halafu zikabaki za kujengea nyumba Kunduchi na kukarabati Billcanas??

Hivi keli mwandishi anajua gharama ya nyumba au flat Dubai au amesikia story mtaani na anataka kuja na thread ili tumjue??

Na za ruzuku, umezisahau? hizo ni baadhi tu.
 
KIMSINGI NAONA KAMA MADAI NA SHUTUMA UNAZOTOA HAZINA MASHIKO YOYOTE,NI JANA TU UMEJIUNGA UMEANZISHA THREAD YA KUSHAMBULIA VIONGOZI WA CDM.SAWA TUNAOMBA UTUPE DATA KAMILI ZA HIYO NYUMBA YA DUBAI YA MH MBOWE.JE UNAFAHAMU AU UNAJUA FINANCIAL BACKGROUND YA MBOWE JUU YA UKUMBI WA BILICANS?AU UNAONGEA ILI MRADI NA WEWE UONEKANE KWENYE JF?TRY TO PRESENT VIVID EVIDENCES TO PROVE YOUR ALLEGATIONS AGAINST MBOWE NA DR.NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK.:scared::A S 13::A S crown-2::lock1::lock1:
 
nawasikitikia watanzania wenzangu mimi.
nani wa kutukomboa tena?.
slaa njoo ujibu hizi tuhuma. its too much aisee. duh!.

WanaJF,
Slaa hana cha kuficha kwa kuwa utaratibu uko wazi.

1. Kulipwa Mke wa Dr Slaa aweke ushahidi wana Jamvi waupime.

2. Ni kweli Josephine ambaye Professionally ni pamoja na System Analyst ali volunteer ku design Reporting System. Inawezekana mhusika ameona sasa atabanwa vilivyo hivyo anapiga vita. Nilidhani anayejitolea anapongezwa!.

3. Kabla ya Junior kwenye kesi tulikuwa tukilala Sky Link au Miami 40،000 per night. Baada ya Junior akiwa miezi 3 Impala at 280،000 per night bila chumba cha yaya na extra za mtoto na chakula. Kesi ni za Chama alitaka tumwadhibu Junior? Inawezekana hajui maana ya kusafiri na mtoto wa miezi 3! Tungekuwa fisadi tungelala Naura Sring, Kibo Palace, Mt. Meru etc. Inawezekana hajui rates za Luxury hotels.

Wakuu;- ule msemo wa usiyapamie maji usiyojua kina chake kwa mti hivi sasa umetimia baada ya viongozi wakuu wa upinzani wenye bahati ya kupendwa na vyombo vya habari vya Tanzania Bw. Freeman Mbowe, Bw. John John Mnyika, Bw Tundu Lisu na wengine sasa wameanza kuumbuka kutokana na matendo yao yasiyosadifiana na maneno yao.

Wote tunakumbuka mapema mwaka jana wakati wa bunge la bajeti Dodoma kulizuka mjadala mkubwa uliogusa nyoyo za watanzania wengi wa kukataa posho ya vikao (Sitting Allowances) ulioasisiwa na naibu kiongozi wa upinzani bungeni ndugu Kabwe Zuberi .
Ni katika mjadala huo ndipo viongozi hawa waliropoka maneno wasiyoyafahamu madhara yake kwa jamii siku za usoni.
Wakati JOHN MAGALE SHIBUDA yeye aliweka wazi kuwa kwake yeye si sahihi kuacha kupokea posho kwa kuwa inamsaidia kujikimu kwa shuhuli zake mbali mbali ikiwemo kuwasaidia wapiga kura wake na kuliomba bunge liongeze kiasi hicho cha elf 80 kwa siku mpaka laki 5.Na kusema kuwa wanaopinga posho ama ni wanafiki au waongo ama wana agenda ya siri.
1. FREEMAN MBOWE;- akiwa kama kiongozi wa Upinzani bungeni aliutangazia umma wa watanzania kuwa hakuna haja ya kupokea posho kwa kuwa ni dhuluma kwa wananchi masikini na hivyo akasisitiza kuwa msimamo wa chama chao ni kuwa hawachukui posho na kamwe hawatachukua posho. Na kumtangaza Shibuda kama msaliti mkuu wa chama.
Mbowe alikwenda mbali zaidi akarudisha hadi gari alilopewa na serikali la kutembelea kama kiongozi wa upinzani KUB kwa kusema ni matusi kwa viongozi kutembelea mashangingi wakati watanzania wanazeeka kabla ya umri wao kwa umasikini mkuu uliokithiri.
2. Dkt. Slaa yeye alianza kulisemea swala la posho tangu mwaka 2008 na kusema ni hatari kwa wabunge kuchukua kiasi kikubwa hicho kwa kukaa bila ya kuchukua maamuzi yoyote.(Slaa alisema tu hakuchukua hatua yoyote na posho aliendelea kupokea) na hata lilipokuja swala la posho kwa mara ya pili baada ya kuibuliwa na Kabwe Zuberi alimkemea Shibuda kuwa anakwenda kinyume na maamuzi na msimamo wa chama chao na kuwa atachukuliea hatua kali za kinidhamu.

3. Tundu lissu yeye alitoka hadharani na kutangaza kuwa ni mwiko kwa viongozi wazalendo kuchukua posho na kuahidi kumchukulia hatua kali za kinidhamu na kuwa ameshamkab8idhi barua ya kujielezea ndugu Shibuda na wapo tayari kama chama kumfukuza uanachama kuliko kuendelea nae mpinga msimamo wa chama.


4. John John Mnyika yeye kipindi hiki chote alikuwa ndio katibu wa wabunge wa Chadema na kuwa alikuwa mstari wa mbele kusema kuwa wabunge wote wa chadema wanapinga poisho na kuwa yeye kama katibu wao atahakikisha wanamshuhulikia nduigu shibuda kwa makosa ya kikatiba aliyoyafanya.
KUMBE NI WANAFIKI.
Mungu si Athumani tayari sasa kila mmoja ameonyesha jinsi gani viongozi hawa wote kwa pamoja ni wanafiki na walikuwa wanaongea mambo ambayo kamwe wameshindwa kuyasimamia.
1. FREEMAN MBOWE;- Bila aibu wala soni kiongozi huyu wa upinzani ameendelea kuiramba posho ya kukaa (Sitting Alowance) tangu siku ya kwanza mpaka leo na zaidi ya yote ametoa kituko cha mwaka pale ALIPOJIRUDISHIA KIMYA KIMYA GARI LA KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI (KUB) WAKATI ALILIRUDISHA KWA MBWEMBWE NA VIGERE GERE.
2. Dkt. Slaa yeye amedhihirisha ni jinsi gani mnafiki kwani pamoja na kujidai kupinga posho lakini bado ameshindwa hata kuusimamia mfumo wa posho ndani ya chama chake nitatoa mfano;-
i. Amelazimisha chama kumlipa mke wake milioni kumi kama malipo ya kutengeneza mfumo wa komputa wa kusimamia mahesabu ya chama.
ii. Anajilipa posho ya shilingi 250000/= kwa siku kila aendepo ziara na kwenye kesi yake kule Arusha ambapo yeye, mke wake pamoja na yaya wao husafirishwa kwa ndege kila safari na wote wanalipwa 250,000/= ya kujikimu wakati wote wanalala chumba kimoja?. Haya ni matumizi mabaya ya ruzuku ya chama ambazo ni kodi za wananchi.
iii. Amejikopesha pesa ya chama kujengea nyumba yake kule kunduchi ambapo yeye mwenyewe ndio msimamizi mkuu wa pesa za chama na ndio mlipaji mkuu na wala hajafuata mfumo wowote wa malipo na ukopeshaji na haijulikani ni lini atarudisha fedha hizo za wanachama na kwa utaratibu upi?.

3. JOHN JOHN MNYIKA. Yeye ameshindwa kuusimamia msimamo alioutangaza wa kutopokea posho na mpaka leo anairamba kama kawaida na ukimuuliza anasingizia kluwa eti zinaingizwa kwenye akaunti moja kwa moja bila ridhaa yake na ukimuuliza zaidi anakwambia nimemwandikia barua katibu wa bunge kuomba maelezo kwa nini wananiingizia pesa bila ridhaa yangu.(MWONGO;- wabunge wa chadema wanaokaa nae jirani bungeni wanasema huwaga anaiita karatasi ya kusaini ikiwa amechelewa kusaini ili apate posho ).

4. TUNDU LISSU – yeye ameshindwa kusimamia kabisa msimamo wake na mpaka sasa anaramba posho na amewahi kukaririwa katika kukao kimoja cha wabunge wa chadema akisema ''sijagombea ubunge ili niwe masikini, mimi posho nachukua kama kawa''.

Wakuu kwa uchambuzi huu mdogo ninamwomba sasa SLAA kama kiongozi mtendaji wa kila siku wa chama aseme ni hatua gani walizomchukulioa shibuda mpaka sasa kama kweli alip[ingana na msimamo wa chama?.
Ninaona ni jinsi gani ukombozi wa pili wa taifa letu ulivyotekwa na matapeli wa kisiasa.
Hongera zake shibuda kwa kutuonyesha watanzania ngozi yake halisi na sio hawa wanafiki wengine.
Wasalaam, karibuni tujadiliane.
 
nawasikitikia watanzania wenzangu mimi.
nani wa kutukomboa tena?.
slaa njoo ujibu hizi tuhuma. its too much aisee. duh!.
 
Sasa nimeamini yale maneno ya Jenerali kuwa wakati wa uchaguzi kuna watu wanapeleka akili zao likizo.
Na bado tutasikia mengi sana mwezi huu
 
Ninaimani na chadema


UNAIMANI NA CHADEMA AU NA MBOWE?.
kama mtindo wenyewe ndio huu sasa naona hawa wapinzani wetu wamepoteza uelekeo rasmi.
hivi ni kweli mbowe kalirudia gari la KUB au anasingiziwa tu kamanda wtu?
 
Yaani Lissu alitumia Neno KAWA?!?!?!

Maadam wewe ni Mtaalam mzuri hivyo, waweza kutuambia aliyehusika na kifo cha Nyerere? Soma Sahihi yangu na ujibu.
4. TUNDU LISSU – yeye ameshindwa kusimamia kabisa msimamo wake na mpaka sasa anaramba posho na amewahi kukaririwa katika kukao kimoja cha wabunge wa chadema akisema ‘’sijagombea ubunge ili niwe masikini, mimi posho nachukua kama kawa’’
 
hehehheheh....CHADEMA mko wapi mjibu tuhuma hizi,Dr.slaa inakuwaje unalazimisha chama kumlipa mke wako?
Hivi ile tenda ya Million mia tatu aliyojipa Mh,Mbowe nayo imepitia kamati kuu?
 
.

hehehheheh....CHADEMA mko wapi mjibu tuhuma hizi,Dr.slaa inakuwaje unalazimisha chama kumlipa mke wako?
Hivi ile tenda ya Million mia tatu aliyojipa Mh,Mbowe nayo imepitia kamati kuu?

John Heche ndiye Mwenyekiti wa Bavicha.
 
Back
Top Bottom