Huu ndo ukweli toka moyoni mwangu!!!!

Ni wazi sababu zipo na chache kati ya nyingi ni ubinafsi, ukatili wa asili, kutokujali, na tamaa. Lakini kwa vile sababu zipo hiyo haina maana ya kwamba ni sawa. Kukiondoa kiumbe ambacho wala hata hakiwezi kujitetea ni ukatili wa kupindukia.

Nitajisemea nafsi yangu mwenyewe. Sijawahi na sitakuja kushiriki, iwe moja kwa moja au la, kwa hiari yangu, kuondoa uhai wa binadamu ambaye hajazaliwa. Huo ndiyo msimamo wangu na ninajivunia kuwa hivyo.

Hivi mkuu tumefanya tafiti na hao wanaotoa mimba wakatueleza hivyo au tunawawekea maneno mdomoni!

Hongera tena kwa msimamo wako huo.....Binafsi sina ugomvi na hilo!

Hivi mkuu tumefanya tafiti na hao wanaotoa mimba wakatueleza hivyo au tunawawekea maneno mdomoni!

Hongera tena kwa msimamo wako huo.....Binafsi sina ugomvi na hilo!

Kaka, kwani wewe hujawahi kukutana na wadada wanaotoa mimba kwa sababu za 'convinience'? Sidhani kama unahitaji kufanya utafiti rasmi kulijua hilo. Binafsi nina ndugu ambao walitoaga mimba kwa sababu za 'convinience'.

Nina watu wengine ninaowafahamu kupitia shule, kazini, na uraiani ambao pia walitoa mimba pasipo na sababu. Yaani kabisa wewe hujui mtu au watu waliowahi kufanya hivyo hadi uhitaji msaada wa utafiti rasmi?

kwa nini waota mimba wasiukumiwe kifo jamani

hilo ndo la msingi, huenda ukiwa hukumu kifo watasema kumuhukumu mtu kifo ni kinyume cha haki za binadamu wakati wao wanaua!!!

Sitaumia kuona anauawa kwa kumuua asielewa kitu, asie na kosa, asie sikia nk (kichanga)

naamini kungekuwa na hukumu ya kifo bila huruma kwa wanaoua bila huruma itakuwa afadhali.

Sawa mkuu,

Hivi sisi tulio pembeni tunachukua hata dakika moja kujiuliza kwa nini? Haiwezekana hawa watu wakawa wauaji na wakatili bila sababu!

Hata magaidi wanazo sababu kwa nini wanajilipua!

the problem is that, people are mercyless, they are killers and murderers.

General question!!!

Hivi huyu dada anaetoa mimba au daktari anaemtoa mimba mwanamke akipewa amuue mwanae kipenzi mzuri mwenye umri wa miaka 4 mwenye afya anaependeza na mwenye busara atamuua?

for real, but who can tell the exactly time for life to start?

Four years ago, I wrote this:

What is life? Life has many meanings but in this context, I will define it as the state of being alive as a 'human being'. When the sperm and the egg join together to form the embryo (which we all were at some point) and then implant itself in the endometrium, pregnancy occurs and that's the beginning of life because after 36 weeks a full-fledged human being will be born.

If implantation doesn't occur, then there is no pregnancy and consequently no life. Every human being (maybe with the exception of test tube babies) I know originated in this way and is now enjoying life that no other person has a right to take at any point, so what gives someone the right to end a life that is in it's early stages?

Therefore I must conclude that human life is sacred from the moment of conception, and that destroying that new life is never right, no matter what the purported good outcome would be. Therefore if you believe (like I do) that the conception of something is the beginning of something then life too, begins at conception.

1.Mwenzenu nikisikia tu flani kafanya hivyo, kuanzi hapo namchukia kabisa na
sitaki kumtazana hata filam au chochote anachokifanya.
2.Tatizo watu wengi wanmataka sana kujulikana kwa kufanya mambo ya kijinga.
3.Wameshindwa kuamini kama kuna Mungu, na wameshindwa kututangazia ili tujue.
Kama inawezekana kutoa, tutakuja kusikia wanatumia mimba hizo kama mboga.

Unataka kunambia binti wa miaka 14 anaweza kupinga wazazi wasimtoe mimba??? Si wote wana power ya kusema no.

Nina school mate wangu wa primary, alipata mimba akiwa form two na ilikuwa ni mimba ya teen mwenzake. Kwanza wazazi wa binti walikuwa wanamchunga sana. Nakumbuka tulifaulu wote kwenda shule moja hapa Dsm yeye wazazi wakamwamisha alivyofika form two ili aende boarding kuepuka kuwa ataharibika akisoma day school.

Kumbe binti akiwa likizo kuna kijana jirani anajimovuzisha nako. Akaja pata mimba. Huwezi amini wazazi wake walimfungia ndani mpaka kazaa. Na nina wasiwasi labda kulikuwa hakuna uwezekano wa kuitoa hiyo mimba. Alipozaa tu wakamrudisha shule mtoto akiwa sijuhi na siku chache tu.

What happened mtoto alikufa na ndio majirani wakajua kuwa kumbe binti alizaa. Maana hata mtoto alikuwa hatoki nje na hivyo nyumba yao ilikuwa ina geti na ina eneo kubwa si rahisi majirani kujua kinachoendelea ndani. Sasa nambie hao nao utawaweka kundi gani? Na binti kama huyu ana kosa gani?? Kuna wazazi wako over determined na maisha ya watoto wao kiasi kwamba hawafikirii cha nini wala nini.
Kwa vile mimba haitungwi na mtu mmoja, I place the blame squarely on both or all who take part in destroying it. Kama mdada akiamua mwenyewe kwenda kutoa kwa sababu zake mwenyewe basi na lawama abebe yeye. Kama anashawishiwa na huyo mwenzake na yeye anakubali halafu huyo mwenzake analipia, mbele yangu wote wanabeba lawama. Kama familia inatoa shinikizo na mdada anakubali kwangu wote wanabeba lawama. Katika hili pia siwa excuse waganga wanaozitoa. Matter of fact, ni wauaji tu na wenyewe.

This is a very, very weak and lousy argument! Mdada anayeenda mwenyewe kutolewa mimba yake huyo ni kaamua kufanya hivyo. Unless uniambie alifungwa kamba na akaburutwa kupelekwa huko wanakozitolea hizo mimba.

Mama mwenye mimba, ukiachilia mbali ajali zinazoweza kusababisha miscarriage, ndiye mwenye uamuzi wa mwisho kabisa wa kukibakiza na kukitunza hicho kiumbe tumboni mwake.

Kuna wasichana mimi nawajua ambao walikataa katu katu mashinikizo ya familia zao ya kutoa mimba na wakazibeba hadi wakazaa. Na walipozaa wazazi wa hao wadada mbona walisutwa na dhamiri zao!! Kila walipokuwa wanawaona wajukuu zao wakicheka na kutabasamu na jinsi walivyokuwa wazuri, najua kabisa dhamiri zao ziliwasumbua. Kwamba walikuwa wanataka hao viumbe waangamizwe kabisa na katu wasije na wao kuonja raha na karaha za dunia hii.

Sasa leo unakuja unakaona kajukuu kako, mashavu hayo yametuna, halafu na kenyewe kanatabasmu kila kamwonapo mtu yeyote yule. Wewe mzazi uliyekuwa unataka kukaangamiza hako katoto, kama una moyo lazima itakusumbua. Lakini kama una jiwe wala haitakusumbua.

Unataka kunambia binti wa miaka 14 anaweza kupinga wazazi wasimtoe mimba??? Si wote wana power ya kusema no.

Sikuwa nazungumzia watoto na wewe hukuweka bayana umri. Kwenye hali kama hiyo basi wazazi (kama wao ndiyo wanamshinikiza) ndiyo wanabeba lawama zote kwa ku promote mauaji!

What happened mtoto alikufa na ndio majirani wakajua kuwa kumbe binti alizaa. Maana hata mtoto alikuwa hatoki nje na hivyo nyumba yao ilikuwa ina geti na ina eneo kubwa si rahisi majirani kujua kinachoendelea ndani. Sasa nambie hao nao utawaweka kundi gani? Na binti kama huyu ana kosa gani?? Kuna wazazi wako over determined na maisha ya watoto wao kiasi kwamba hawafikirii cha nini wala nini.

Kuzaa katika umri mdogo si jambo zuri. Lakini pia, kama ndiyo imeshatokea mimi nitakubali matokeo na nitasaidia kulea. Siwezi kushiriki kuua kiumbe kisicho na uwezo hata wa kujitetea kisa tu eti nataka kusitiri heshima yangu. Siwezi kabisa. Uhai wa binadamu kwangu una thamani kubwa mno kuliko heshima yangu mtaani.

Na kuzaa kwenye umri mdogo si mwisho wa maisha. Wangapi wamezaa wakiwa ma teenagers lakini wakaja kufanikiwa kimaisha na hata watoto wao pia kuja kufanikiwa? Huyo raisi wa Marekani naye alizaliwa na mama teenager. Ona leo alipo. He is the most powerful man in the whole wide world.

Wazazi wanaoshinikiza watoto wao kutoa mimba ni wauaji tu na wenyewe.

ndo hapo sasa ambapo mwanamke anatakiwa asikate tamaa na kukimbilia kutoa mimba.

Mmmh.. naona wadada leo wamesepa mwee.. Niongezee sababu nyingine inayopelekea wadada kutoa mimba. Wengine huwa na mahusiano ya mtu zaidi ya mmoja at the same time (hii inainclude na walio kwenye ndoa), sasa mtu anapobeba mimba anakuwa hajui mwenye mimba ni nani.. sasa kuepuka yote anaona bora atoe tu ili yaishe!

Hiyo ni mbaya sana.

Similar Discussions

Back
Top Bottom