Humu JamiiForums hakuna wife material, kijana usidanganyike

Mohammed wa 5

JF-Expert Member
Jun 20, 2022
1,215
2,995
Inawezekana Nina pasaka chache na eid chache humu JF lakini kwa uchunguzi wangu mke bora hayupo JF, wanawake wengi wapo JF kwa ajili ya stress zao za mahusiano au ndoa.

Embu niambie Kuna member gani waliwahi kukutana JF mpaka wakaoana, na kuwa na familia kabisa, mtakaonijibu mje na ushaidi.

Mwanamke anatumia ID fake anaweza kweli kuwa mama Bora wa familia, washazoea kuigiza maisha. Vijana wa JF acheni kwenda PM mtapigwa na kitu kizito, humu kila mtu yuko single.

Kama umeshindwa kupata mke uko mtaani kwenu usijidanganye uje JF kutafuta mchumba, umeishaaaa.
 
Kama hakuna mwanamke wa kuolewa kwa kigezo chakutumia ID fake basi tukubali pia hakuna wanaume wakuoa humu kwasababu pia tunatumia ID fake. Kuoa na kuolewa ni fumbo la Imani ndugu.

Kuna watu wameoana wakiwa walokole na wacha mungu haswa ila ndoa zimewashinda na wamewaacha wanawake waliotolewa bar na kuolewa wanaendelea na familia zao.

Hivi umekaa ujajiuliza kuwa waliomi humu jf ndio walioko mtaani huko na makanisani?, Vipi huyo mkeo au demu wako ndio ana id fake hapa na hujui!!.

Usihukumu kundi la watu wote kwasababu zako binafsi aidha umepigwa za uso au umeamua tu. Mke/mme anapatikana mahali popote kutegemeana na mitazamo na udhati wenu katika Jambo hilo..!
 
Lemme share the closely withness from my blood brother..alipata mchumba hapa JF akaoa na mpaka sasa ana miaka 10 ya Ndoa na huyo huyo Mke wake..wamejaaliwa watoto 3 and are happy changamoto hua hazikosekani popote pale..but sio members wote wa JF ni wazinguaji kuna member’s wanaojitambua humu humu JF

Wapo WANAUME Smart humu wenye visions za maana na vile vile wapo Wanawake wenye kujitambua wanataka nini

Another witness nina best friend wangu BFF alipata Mume Instagram wameoana na wamejaaliwa watoto wawili wana mwaka wa4 kwenye Ndoa yao

Hizi Social media ukizitumia vizuri unapata connections za maana in your development carrier and in your relationship..it’s how you use them and how to put on your profile tells alot about you.

Wish every of you best of Lucky 🙏
 
Kama hakuna mwanamke wa kuolewa kwa kigezo chakutumia ID fake basi tukubali pia hakuna wanaume wakuoa humu kwasababu pia tunatumia ID fake. Kuoa na kuolewa ni fumbo la Imani ndugu... Kuna watu wameoana wakiwa walokole na wacha mungu haswa ila ndoa zimewashinda na wamewaacha wanawake waliotolewa bar na kuolewa wanaendelea na familia zao.
Hivi umekaa ujajiuliza kuwa waliomi humu jf ndio walioko mtaani huko na makanisani?, Vipi huyo mkeo au demu wako ndio ana id fake hapa na hujui!!. Usihukumu kundi la watu wote kwasababu zako binafsi aidha umepigwa za uso au umeamua tu. Mke/mme anapatikana mahali popote kutegemeana na mitazamo na udhati wenu katika Jambo hilo..!
fact
 
Humu hakuna wanaume wanaume wengi wanaolewa na wanataka bandoo . Na huku wewe upo serious akuambie mnaanzaje maisha mtaishije mtu afanyaje , yeye anasema toka kwenu ukapange chumba nije nikaishi halafu unadai wadada wabaya mlitaka tuwatunze nope aisee maisha nikusaidiana na Kwa mwanamke anakufanyia mengi , kukupa k hadi uridhike , akupikie , akufulie aweke nyumba safi , na bado akuzalie mbwa nyie , na bado utegemee akulishe akuvishe roho mbaya mnatoa wapi?

Tuacheni tuishi kaeni nahao wanaonekana na bado mbona mmewashindwa basi wakaka mmeshindikana sana wanaume saivi . Mnashida sana badilikeni mmekuwa vipuri hamtaki kucheza sekta yenu ya utafutaji . Hamtaki majukumu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom