Hukumu Kesi ya Mgomo wa Walimu: Mgomo ni batili

Tunasubiri Mkuu Japo Mwajiri lazima ataibuliwa kidedea as Usual....Ndiyo maana JK jana alisema tusubiri kesho.Mgomo haukuwa halali na kwa amri ya mahakama walimu wote watakiwa kurudi kazi bila masharti yoyote.Ni mtizamo/wazo:loco: tu wadau!

Confirmed....raba stamp
 
Hakuna ujanja, Tunarudi Kazini. Kikubwa "MESSAGE SENT" na tutaendelea na mgomo wa aina ya pili, na madhara yake yatakuwa ya muda mrefu. subirini, mtaona.
 
Tunajua tutafanya nini serikali ya ccm c mnajifanya hamnazo subirini mmetangaza vita na watanzania bila shaka mmepima uwezo wenu ni kweli mnaweza endelea kutawala lakini si kwa ridhaa ya umma wa walio wengi mtatawala kwa nguvu ya dola na mahakama lakini hiyo nayo hatakuwa siku zote ipo siku mtakosea mahesabu na ndipo mtakapojuta kama sio ninyi basi watoto wenu na kama sio watoto wenu wjukuu wenu hii ni dunia ole wenu wote wabunge na serikali
 
Mimi nilishakosa imani na mahakama zetu toka alivyofariliki jaji Lugakingira, he was the only judge you could trust, waliobaki ni proxy wa CCM na serkali yake.
 
Hakuna ujanja, Tunarudi Kazini. Kikubwa "MESSAGE SENT" na tutaendelea na mgomo wa aina ya pili, na madhara yake yatakuwa ya muda mrefu. subirini, mtaona.

huo ndo mgomo mzuri bhana,,,naupenda sana,,,atahr yake anaiona ndalichakooooooooo
 
Hakuna ujanja, Tunarudi Kazini. Kikubwa "MESSAGE SENT" na tutaendelea na mgomo wa aina ya pili, na madhara yake yatakuwa ya muda mrefu. subirini, mtaona.

Mama yangu!!

Mwalimu tafadhali tafadhali naomba usifanye mgomo huu wa aina ya pili. Tafadhali mwalimu.

Duh!!
 
Kama haitafika siku tukawa na sauti ya umoja na kusema pamoja, basi tusitegemee kutoka hapa tulipo..Taifa hili linapiga hatua moja mbele na kumi nyuma kila mwaka, sasa baada ya miaka 5 tutakuwa wapi? We must say NO and join together to fight against the corrupt system in power,the system that acts for minority and not majority. Members of parliament, ministers don't have to go to courts to have their salaries and benefits increased, they just press the buttons to achieve it. If leaders are for this country, why don't they act for the interest of the people? A true leader sacrifices for his people. It hurts alot!!

Kaka usije kulia mie mwenyewe leo nina uchungu zaidi yako sema basi natumia busara na heshima ya utanzania. Inabidi wanajamii forum wote twende msituni. Au wananchi wote tugome mana vyombo vya habari havina uhuru, vinatangaza kwa hofu kuna mwananchi mmoja kapiga simu katka kipindi fulani cha TBC fm Akisema kuwa Mungu kaidhinisha kwamba kuna kuzaliwa na kufa na hata chama hichi hakukitaja jina kwamba kinataka kufa kwahiyo iwejuhudi toka kwa wanainch kuinusuru serikali yetu. Wale maoperata waka mkatia simu. Sasa hapa kaka kuna uhuru. Na kama upo je kunahaki ya kuendelea kukumbatia Chama Cha Majivuno, Chama Cha Mafisadi, Chama Cha Manyonyaji, Chama Cha Mateso Magwepande. Chama Cha Madudu, Chama Cha Magamba. Chama Cha Migongano. Chama Cha Maozo. Chama Cha Majizi, Chama Cha Majambazi. Chama Cha Mataira. Chama Cha Makunguru. Chama Cha Miguno. Chama Cha Matekanyara. Chama Cha Majangili. Hiki chama kinamwisho na lazima kife ili kijione upuuzi kilio nacho.
 
Kwani Tanzania tuna Majaji ? si hawa waliosomea ST KANUMBA wewe mtoto kasomea chini ya mwembe na kamaliza darasa na wakaingia form one bila kujua kusoma na kuandika wakapewa ujaji wa kishikaji unategemea nini ? Ndio Jaji wetu hao !!!!!!!!!!!!!

Mkuu wala tatizo siyo hilo bali mahakama sasa iko chini ya serikali ya ccm na njaa za majaji
 
Inasikitisha maamuzi ya mahakama zidi ya walalamikaji na serikali. Mahakama na walimu, mahakama na madaktari, mahakama na wafanyakazi,mahakama na maskini, mahakama na wachimbaji wadogowadogo inatia hudhuni.

Sasa tufanyaje wajameni
 
Hii nchi ni ya kipuuzi, mimi uwa nashangaa wakati gani ambapo uwa atuingilii mamlaka ya mahakama...mafano, tangu mgomo wa madaktari umeanza serikali imekuwa ikisema kuwa mgomo ni batili, sasa sijui ilikuwa inapata wapi mamlaka na nguvu ya kuisemea mahakama muhimili tofauti kabisa. Nchi yetu inaongozwa kipuuzi sana wakuu, yani mpaka wakati mwingine unapandwa na hasira na kutamani kupiga vibao hawa watawala wetu wadhaifu.

unaposema nchi inaendeshwa kipuuzi inamaana viongozi wake niwapuuzi?
 
Mahakama za wakati wa ukoloni zilisema ni batili maandamano ya wapiga uhuru Dar na hata Nyerere akajikuta anapigishwa faini huku akiangala kifungo cha miezi mitatu. Mahakama hizo hizo zilipinga migomo ya waokota takataka wa Alabama wakati wa MLK Jr na kusema ni batili; mahakama hizo hizo zilitoa maagizo kuwa maandamano ya wapigania uhuru na migomo ya vyama vya wafanyakazi Afrika ya Kusini ilikuwa batili... Mahakama zilizokosea! Kudai haki hakuhitaji kibali kwani siyo hisani au chonde kinachoombwa!

'Uhuru wa mahakama' ni neno la kisiasa. Kwa Tanzania hakuna kitu kama hicho, ni lini mahakama zetu zimewahi kutoa hukumu kinyume na serikali katika masuala yanayohusu migogoro ya maslahi? Sasa hivi 'mahakama' imegeuzwa kichaka cha kuficha ukweli usijulikane. Wakati serikali ikiendelea kujadili 'masuala yaliyoko mahakamani', wengine wanazuiwa wasiyazungumze.

Tuna wabunge dhaifu, serikali dhaifu na wananchi dhaifu sana.
 
Mama yangu!!

Mwalimu tafadhali tafadhali naomba usifanye mgomo huu wa aina ya pili. Tafadhali mwalimu.

Duh!!

Kama kawaida mie nilikuwa cijamaliza sylabus na nimeshikilia masomo mawili Chemistry na Biology shule nzima haina mwalimu wa Chemistry na Biology hata mmoja na Kuna mkondo kutoka form I yani A, B, C na D hadi form four shule fulani XXXXXX na mshahara wangu kama vle mnavyojua serikali nundu hii. Inabidi nijitolee kwa wiki vipindi zaidi ya 80, na wanategemea nini. Nakuja na mgomo wangu yani kupiga story na wanafunzi na Kuwafundisha jinsi ya kuing'o serikali pumbavu kama hii. Sitarajii kushika chaki. Itakuwa ni story darasani maana matoto yenyewe matikiti maji yanapenda Topic ya REPRODUCTION tu. Zingine wanaona usenge nami ntawafundisha hyo hyo. Ukiwaleta ktk EVOLUTION NA GENETICS anabaki MMOJA tu Darasani yani topic ngumu. CHEMISTRY Ndo usiseme MAJANGA TU. Wataona WANAFUNZI NI STORY KWENDA KUSHOTO.
 
Hukumu ya mahakama za ccm siyo za kuaminika. Hukumu ilishatolewa tangu jana, Kweli tutarudi kazini, lakini ufaulu wa mwakani, hasa Form four wa mwaka huu, mtaniambia. Hii ni kwa sababu watoto wao hawasomi nchini. Za kuambiwa, watz changanyeni na zenu 2015,
 
'Uhuru wa mahakama' ni neno la kisiasa. Kwa Tanzania hakuna kitu kama hicho, ni lini mahakama zetu zimewahi kutoa hukumu kinyume na serikali katika masuala yanayohusu migogoro ya maslahi? Sasa hivi 'mahakama' imegeuzwa kichaka cha kuficha ukweli usijulikane. Wakati serikali ikiendelea kujadili 'masuala yaliyoko mahakamani', wengine wanazuiwa wasiyazungumze.

Tuna wabunge dhaifu, serikali dhaifu na wananchi dhaifu sana.

Mahakama zina uhuru lakini serikali imeweka mataira wao katika mahakama hizo kujaji uupuuzi usio unamaendeleo. Jamani Tanzania inabidi tuungane tugome wote kwa pamoja watupeleke magwepande wakatu torture wote.
 
Niliposikia suala lipo mahakamani nikajua kwamba nwisho wa siku serikali lazima ishinde.
 
Back
Top Bottom