Mbeya: Serikali yawasilisha pingamizi dhidi ya kesi iliyofunguliwa kupinga mkataba wa DP World

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,753
15,227
KESI YA KIKATIBA NA.5/2023:
Majaji wameingia ukumbi Na. 04 muda huu saa 6:05

MAWAKILI WANAJITAMBULISHA
UPANDE WA SERIKALI:
1. Mark Muluambo - Wakili wa Serikali mkuu
2. Edson Mweyunge
3. Alice Mkulo
4. Edwin MubiloWote watawakilisha Wajibu Maombi.

UPANDE WA WALETA MAOMBI
1. Adv. Boniface MWABUKUSI
2. Philip Mwakilima
3. Livino Ngalimitumba.

Wakili wa serikali SA: Waheshimu Majaji, tulipokutana tarehe 3.7.2023, Mahakama ilitoa amri mbalimbali ikiwa ni pamoja na kwamba Wajibu Maombi waweze kuleta majibu yao tarehe 14.7.2023, na kwamba kama Waleta maombi watakuwa na majibu ya ziada, waweze kujibu tarehe 19.7.2023.

Waheshimu Majaji, sisi tulifanikiwa kutii amri ya mahakama na tulileta majibu yetu kwa muda uliopangwa.Wenzangu Mawakili wasomi upande wa Waleta Maombi hawakuwa na majibu ya ziada. Na hivyo Tumekubaliana kwamba pleadings are complete" yaani Nyaraka zote zimekamilika kama mahakama ilivyokuwa imeelekeza.Na pia Tumekubaliana kwamba shauri hili sasa linafaa kwaajili ya kusikilizwa.

Hivyo kama wenzetu hawatakuwa na mapingamizi, basi mahakama itamke kwamba shauri hili linafaa kuanza kusikilizwa.Naomba kuwasillisha.

Boniface Mwabukusi (Wakili mleta Maombi): Waheshimu Majaji, ni sahihi kama alivyosema Msomi Wakili Mkuu wa Serikali. Tumepokea majibu yao lakini katika majibu yao wameibua Mapingamizi Manne ya Kisheria.

Na ni taratibu za kisheria kwamba kunapokuwa na mapingamizi ya kisheria, Mahakama hii tukufu huanza na mapingamizi hayo kabla ya kwenda kwenye Shauri la msingi.

Kwa kuzingatia aina ya shauri lililoko mbele yenu na maslahi mapana ya jamii pamoja na mahakama kuweza kutenda haki; ni ombi letu kwenu Waheshimiwa majaji, muone kwamba inafaa kwamba, mapingamizi ya kisheria ya kisheria yaliyoibuliwa pamoja na shauri la msingi yasikilizwe yote kwa pamoja.

Na kwamba, wakati wa kutoa maamuzi; Mahakama hii tukufu ikiona kwamba mapingamizi yale yana mashiko, basi itaishia kutoa uamuzi hapo. Na kwamba kwama mahakama hii itaona mapingamizi yale hayana mashiko basi mahakama iweze kutoa uamuzi kwenye shauri la msingi.

Lengo la ombi letu, ni kuifanya mahakama kwama iweze kumaliza shauri la msingi kwa uharaka, na au kuweza kumaliza jambo hili kwa "Substantive justice." Ni hayo tu Waheshimiwa. I humbly submit.

Wakili wa Serikali: Iwapendeze Waheshimiwa Majaji, nimemsikia msomi mwenzangu. Ni kweli kwamba kwa kawaida kwamba Mahakama huwa inaanza na kumaliza kwanza mapingamizi ya kisheria.

Lakini kutokana na aina hii ya shauri, sina pingamizi kwamba shauri hili lisikilizwe kwa pamoja Mapingamizi na Shauri la Msingi. Hivyo, ikiwa mahakama itaruhusu, tunapendekeza kwamba siku ya Jumanne tarehe 25.07.2023, kama wenzetu hawana kipingamizi basi shauri hili liweze kusikilizwa Mfululizo.

Narudia tena, ni ikiwa wenzetu hawana kipingamizi na iwapo mahakama hii itaridhia. Ni hayo tu Waheshimiwa.

Jaji Ndunguru: Basi kwakuwa tumekubaliana kwamba Pleadings zimekamilika na kwamba shauri hili lipo tayari kwa kusikilizwa.Nasisi upande wa mahakama kwamba shauri hili litasikilizwe kwa pamoja shauri mama pamoja na mapingamizi.

Na kwamba shauri hili litasikilizwa mfululizo. Muda ni saa 3:00 Asubuhi.

Kesi imeahirishwa mpaka jumanne, Julai 25, 2023.

-------

Serikali imewasilisha pingamizi la awali dhidi ya kesi ya kupinga makubaliano ya ushirikiano wa kijamii na kiuchumi baina ya Serikali ya Tanzania na ya Dubai, yanayohusisha uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam, ikiiomba Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya isisikilize.

Kesi hiyo ya kikatiba namba 5 ya mwaka 2023 imefunguliwa na wanasheria wanne Alphonce Lusako, Emmanuel Kalikenya Changula, Raphael Japhet Ngonde na Frank John Nyalusi, wakipinga makubaliano hayo, wakidai kuwa baadhi ya ibara zina masharti mabovu ambayo hayana maslahi kwa taifa.

Wadaiwa katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na Katibu wa Bunge la Tanzania.

Sambamba na kesi hiyo ya msingi, pia wanasheria hao wamefungua maombi madogo ya zuio, wakiomba Mahakama hiyo itoe amri ya zuio dhidi ya wadaiwa kuwazuia kuendelea na hatua zozote za utekelezaji wa makubaliano hayo mpaka kesi ya msingi itakapoamuriwa.

Kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa leo Alhamis Julai 20, 2023 na jopo la majaji watatu linoloongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, akishirikiana na majaji Mustafa Ismail na Abdi Kagomba.

Hata hivyo Serikali katika majibu yake ya maandishi iliyoawasilisha mahakamani hapo yakiungwa na kiapo kinzani kujibu madai ya wadai hao, kabla ya kusikilizwa pande zote kwa mdomo, imeibua pingamizi la awali ikiiomba mahakama hiyo iitupilie mbali kesi hiyo kabla ya kuisikiliza.

Katika pingamizi hilo la awali, Serikali imeibua hoja nne za kisheria inazolenga kuishawishi mahakama hiyo kuwa haipaswi kuisikiliza kesi hiyo na badala yake iitupilie mbali.

Kutokana na kuwepo kwa pingamizi hilo la awali, kiutaratibu mahakama inapaswa kuanza kulisikiliza kwanza pingamizi hilo na kulitolea uamuzi

Hata hivyo Lusako, mmoja wa wadai, amelieleza Mwananchi Digital kuwa licha ya kuwepo kwa pingamizi hilo, wataomba kwanza maombi yao ya zuio la muda yasikilizwe kabla ya kusikiliza pingamizi akidai kuwa tayari hatua za utekelezaji wa makubaliano hayo zimeshaanza.

"Makubaliano hayo yanawaruhusu kufanya amendment (marekebisho) ya sheria za ndani. Na tayari wameshaanza kufanya hivyo. Kwa hiyo tunataka kuiomba mahakama kwanza tusikilizwe maombi yetu ya zuio," amesema Lusako.

Amesema kuwa kama watasubiri kusikiliza kwanza pingamizi kama taratibu zinavyoelekeza wakati utekelezaji wa makubaliano hayo, basi kesi hiyo haitakuwa na maana.

Makubaliano hayo baina ya Serikali ya Tanzania yalisainiwa Oktoba 25, 2022.

Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania yalisainiwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, kwa mamlaka aliyopewa na Rais Samia Suluhu Hassan yakishuhudiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.

Juni 10, 2023, Bunge la Tanzania lilipitisha azimio la kuridhia makubaliano hayo.

Hata hivyo makubaliano hayo yaliibua mjadala mkali unaoendelea mpaka sasa katika mitandao ya kijamii na hata viijiweni, huku wengine wakiyapinga na wengine wakiyaunga mkono

Katikati ya mjadala huo ndipo jopo Mwanasheria Lusako na wenzake walipoamua kufungua kesi Mahakama Kuu Kanda Mbeya, chini ya hati ya dharura kupinga uhalali wa mkataba huo.

Kwa mujibu wa hati ya wadai hao, wanadai kuwa makubaliano hayo ni batili kwa kuwa yanakiuka sheria za nchi za ulinzi wa raslimali na maliasili za nchi na kwamba yaliridhiwa na Bunge kinyume cha utaratibu bila kuwapa nafasi ya kutosha wananchi kutoa maoni yao.

Hivi sasa watu wanaofuatilia kesi hiyo wameshafurika mahakamani wakisubiri kuanza kusikiliza baada ya taratibu kukamilika.

Mawakili wa pande zote wako katika kikao na jopo la majaji wanaoisikiliza kesi hiyo Kwa majadiliano mafupi namna ya kuziendesha kesi hiyo.

Pia soma: Mawakili wataka Serikali ieleze sababu ya 'Kusaini’ Mkataba wa Bandari bila kushirikisha Wananchi
 
20 July 2023
Mbeya, Tanzania

FAULO ZA DOLA KUKWAMISHA KESI YA WANANCHI

Wakili msomi Mwabukusi : Vitendea kazi vyangu vilivyokuwa na mafaili vyazuiwa Polisi, katika mbinu ya kukwamisha kesi ya wananchi

N.B
Hoja ya masuala ya 'kiufundi' ndiyo hoja kubwa ya wanasheria wa upande wa serikali

Hoja ya kesi itupiliwe mbali kwa sababu za 'kufundi' ndiyo muokozi wa serikali katika kesi nyingi

Lakini katika kesi hii inayofuatiliwa na wananchi wengi kama ile kesi ya 'Mbowe' (Republic vs Halfan Bwire Hassan and 3 Others (Economic case 16 of 2021) itakuwa ni ucheleweshaji tu, hii kesi ipo na haiwezi kutafutiwa namna kuwa kamwe isisikilizwe.

Jambo hili la bandari halitapoa hadi hapo CCM na serikali yake watapoutupilia mbali mkataba huu mbovu.

More info : kutoka Mbeya, Tanzania

leo siku ya alhamisi July 20, 2023 jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu linoloongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, akishirikiana na majaji Mustafa Ismail na Abdi Kagomba.

Hata hivyo Serikali imekuja mbele ya Mahakama na majibu yake ya maandishi iliyowasilisha mbele ya mahakamani kuu yakiungwa na kiapo kinzani kujibu madai ya wadai hao, kabla ya kusikilizwa pande zote kwa mdomo, imeibua pingamizi la awali ikiiomba mahakama kuu iitupilie mbali kesi hiyo kabla ya kuisikiliza

Katika pingamizi hilo la awali, serikali imeibua hoja zake nne za kisheria inazolenga kuishawishi mahakama hiyo kuwa haipaswi kuisikiliza kesi hiyo na badala yake iitupilie mbali.

Kutokana na kuwepo kwa pingamizi hilo la awali, kiutaratibu mahakama inapaswa kuanza kulisikiliza kwanza pingamizi hilo na kulitolea uamuzi

Hata hivyo Lusako, mmoja wa wadai, amesema licha ya kuwepo kwa pingamizi hilo, wataomba kwanza maombi yao ya zuio la muda yasikilizwe kabla ya kusikiliza pingamizi akidai kuwa tayari hatua za utekelezaji wa makubaliano hayo zimeshaanza.

Toka maktaba : bandari za Kenya hatarini
Nchi jirani ya Kenya ilipona bandari zake kunyakuliwa pale wananchi walipopaza sauti na mradi wa kuchukua bandari za Kenya kuyeyuka kimya kimya
 
Watu wanaweza kusema ni shinikizo lakini kimsingi waleta maombi waliingia chaka kwa kufungua kesi ambayo Haina course of action. Wamepeleka mahakamani kitu tofauti na kilichojadiliwa bungeni. Wao wamepeleka mkataba wakati bungeni ilikuwa ni azimio la bunge. Wamekuja kushtuka mwishoni wameshapeleka maombi. Hivyo hiyo P.O ni sahihi kabisa na mapema asubuhi maombi hayo yanafukuzwa mahakamani kwa kukosa mashiko ya kisheria
 
Hoja ya masuala ya 'kiufundi' ndiyo hoja kubwa ya wanasheria wa upande wa serikali

Hoja ya kesi itupiliwe mbali kwa sababu za 'kufundi' ndiyo muokozi wa serikali katika kesi nyingi

Lakini katika kesi hii inayofuatiliwa na wananchi wengi kama ile kesi ya 'Mbowe' itakuwa ni ucheleweshaji tu, hii kesi ipo na haiwezi kutafutiwa namna isisikilizwe
The good thing ni kuwa,

Hakuna mkataba mwingine utasainiwa, Hadi kesi ipate ufumbuzi.

Ni mwanzo mzuri.
 
Watu wanaweza kusema ni shinikizo lakini kimsingi waleta maombi waliingia chaka kwa kufungua kesi ambayo Haina course of action. Wamepeleka mahakamani kitu tofauti na kilichojadiliwa bungeni. Wao wamepeleka mkataba wakati bungeni ilikuwa ni azimio la bunge. Wamekuja kushtuka mwishoni wameshapeleka maombi. Hivyo hiyo P.O ni sahihi kabisa na mapema asubuhi maombi hayo yanafukuzwa mahakamani kwa kukosa mashiko ya kisheria
Unadhani Kibatala,Lisu, Slaa, Mwambukusi nk nk ni vilaza?

Endelea kuota NDOTO za mchana!!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hoja ya masuala ya 'kiufundi' ndiyo hoja kubwa ya wanasheria wa upande wa serikali

Hoja ya kesi itupiliwe mbali kwa sababu za 'kufundi' ndiyo muokozi wa serikali katika kesi nyingi

Lakini katika kesi hii inayofuatiliwa na wananchi wengi kama ile kesi ya 'Mbowe' itakuwa ni ucheleweshaji tu, hii kesi ipo na haiwezi kutafutiwa namna isisikilizwe
Hayo sii matakwa ya serikali ni matakwa ya sheria

Hii inamtaka mtu yoyote anayepeleka kesi mahakamani asikurupuke ahakikishe kuwa anachokiomba atakipata kwa mujibu wa sheria, je ! Course of action Ipo? Je ❗ amefremu kesi yake kulingania na kile anachokiomba na sheria itampatia? Je! Amefanya taratibu zinazoelekezwa na sheria ?

Mahakama sio baba yako Wala mama yako, na Haina muda wa kufikiria huyu sijui alimaanisha nini. Wewe ukikosea maombi yako yanatimuliwa na unaamriwa kumlipa.garama uliyemsumbua kwa kumtuhumu
 
Watu wanaweza kusema ni shinikizo lakini kimsingi waleta maombi waliingia chaka kwa kufungua kesi ambayo Haina course of action. Wamepeleka mahakamani kitu tofauti na kilichojadiliwa bungeni. Wao wamepeleka mkataba wakati bungeni ilikuwa ni azimio la bunge. Wamekuja kushtuka mwishoni wameshapeleka maombi. Hivyo hiyo P.O ni sahihi kabisa na mapema asubuhi maombi hayo yanafukuzwa mahakamani kwa kukosa mashiko ya kisheria
Bungeni ilikua ni azimio la bunge?. Azimio la bunge kuhusu Nini?. Na Je Sheria inazungumza kupeleka bungeni nini, juu ya mikataba yote inayohusu rasimali za nchi?.

Naomba unieleweshe hapa mkuu.
 
Makosa ya kiufundi yanarekebishika au la? maana nakumbuka kwenye kesi ya mbowe, walilazimishwa wayarekebishe makosa ya kiufundi na hii ni precedent tayari.
 
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Watu wanaweza kusema ni shinikizo lakini kimsingi waleta maombi waliingia chaka kwa kufungua kesi ambayo Haina course of action. Wamepeleka mahakamani kitu tofauti na kilichojadiliwa bungeni. Wao wamepeleka mkataba wakati bungeni ilikuwa ni azimio la bunge. Wamekuja kushtuka mwishoni wameshapeleka maombi. Hivyo hiyo P.O ni sahihi kabisa na mapema asubuhi maombi hayo yanafukuzwa mahakamani kwa kukosa mashiko ya kisheria
Mkuu hawawezi kukuelewa na watakutukana lakini usiogope ukweli ndio huo
 
Wajinga hao wanaodai wananchi washirikishwe.

Wananchi walishirikishwa mkataba upi wa serikali toka tupate uhuru?

Au nchi ipi duniani inafanya hivyo?

Eti "wanasheria".

Uneducated fools from uneducated schools.
Shida mulizoea vyakunyonga...kiama kimefika kwa wala hongo wa Walodi include na wewe
 
Back
Top Bottom