Huko CCM, nani mwenye ufahamu na/au Busara?

MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
4,009
2,173
Wana jf, nakiri kwamba ktk uhai wangu wa kuisikia CCM na kuona mbwembwe zake ktk siasa nilidhani kweli kwamba hiki chama ni ‘giant’. Kumbe ni giant kama Mbuyu. Mizizi dhaifu kabisa.

Kwa wale staunch supporters wa CCM, hebu nisaidieni kumpata mtu mmoja tu anayeweza kuwa ni muhimu kutoa mchango ktk mjadala muhimu kama huu wa sasa, wa Katiba. Pale UD aliletwa Ndimala(?), completely out of touch except those old theories. Mara ya pili tena hapo Dar kwenye public hearing kaja Tambwe Hiza!

Naangalia uongozi mzima nashindwa kuona nani mwenye uwezo zaidi. Katibu mkuu, Makamba, out! Makamu mwenyekiti, Msekwa, out with solid, gray jerry! Mwenyekiti, No comment!

UVCCM nilidhani enzi hizi za wanafunzi zaidi ya laki moja elimu ya juu wangeweza kuwa na thinkers, kumbe wamejaza 'misheni tauni'.

Hata kama hawakubali, ukweli wa enzi hizi za .com, walitakiwa wavutie watu wenye elimu bora na ufahamu.

Kama huko juu hali iko hivyo, vipi hali za hao wajumbe wa chini? Halmashauri Kuu, na hata Mkutano mkuu? Inakuja 2015, hakika hawataweza kutuletea mtu wa maana.
 
Nadhani CHADEMA ndio wanabusara zaidi na wengine woote ni wajinga, nadhani pia CDM ndio wa TZ zaidi ya watanzania wote na katika mijadala ya katiba ni vyema wakaachiwa hao wenye busara na watanzania zaidi ya wenzao kutoa maoni yao.
 
tatizo CCM wanatumia ubabe, na wanafanya wanachi wote ni kama wapumbavu.....
na siku zote busara ya ubabe ni ujinga
 
Mkuu mbona unaandika utadhani wewe ndo Tambwe Hiza mwenyewe!!! Au hujui kuwa wanaccm wengi haturidhishwi na mwenendo wa chama na chama kinasikiliza watu wanaofukuzia ulaji chamani tu!
Nadhani CHADEMA ndio wanabusara zaidi na wengine woote ni wajinga, nadhani pia CDM ndio wa TZ zaidi ya watanzania wote na katika mijadala ya katiba ni vyema wakaachiwa hao wenye busara na watanzania zaidi ya wenzao kutoa maoni yao.
 
Back
Top Bottom