bornagain
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 3,383
- 1,354
MaHR wote mnaowaita watu kwenye usaili wakati kuna mtu wenu mmeshamuandaa mlaniwe na Mungu, machozi ya wale wote waliopoteza nauli zao kutoka Katavi, Kibondo, Namtumbo na kwingineko mbali kufuata interview za post ambazo nyie HR mnajua kuwa mmeshawapatia watu au ni za watu flani wenye ushawishi nakuapia hayataenda bure, ipo siku machozi hayo yatawarudia tena mara zaidi ya watafuta ajira.
Cha msingi cha kufanya sio lazima kuweka matangazo yenu kwenye magazeti wakati mnajua kabisa kuwa ni geresha, nyie kaeni kimya msiudanganye umma wa waTanzania kuwa mnatoa ajira tena bila upendeleo wakati sio kweli. Cha kufanya chukuaneni kimya kimya kama wanavofanya baadhi ya makampuni then acheni kuwasumbua watoto wa watu, acheni kabisa mtindo huo wa kusafirisha watu safari za mbali wakati moyoni mnajua mnalolitenda ni kinyume na maadili ya kikristu au iwe hata ya Kiislam. Kwa HR yeyote anaefanya unayama huu mshindwe na mlaaniwe na mtakuja kulipia machozi ya watafuta ajira siku moja, acheni na mkome kabisa