Milioni 5 kwa goli na 10% mikopo kwa wanawake/vijana/wenye ulemavu ni Mbingu na Ardhi

Songambele

JF-Expert Member
Nov 20, 2007
4,695
2,553
Bravo Madame Presidaa kwa kuhaidi na kutoa sh. 5 M kwa kila goli linalofungwa katika mashindano ya CAF. Beyond reasonable doubt matokeo tumeyaona na timu zetu ziko robo fainali, hii kitu ilifanyika kwa wakati sahihi na timu nzima ya utekelezaji ilisimama katika malengo, niungane na watanzania wenzangu kumpongeza raisi wetu na kiukweli anaupiga mwingi mno na ametutendea haki na Imani yetu moto huu akauwashe kwenye zile 10% za vijana, wanawake na walemavu. Gari lishawaka hili safari iendelee.

Nawaza kulinganisha ubunifu huu na swala zima la mikopo ya asilia 10% kutoka kwa halmashauri kwenda wanawake, vijana na walemavu, haki ya Mungu Madame Presidaa ingilia kati huku sasa watendaji ni wale warasimu na wahafidhina ambao kuona wananchi wananufaika na serikali yao ni machozi jasho na damu. Huku ni sababu lukuki za kwanini watu hawakupewa hizo pes ana mipango mkakati.

Mie nina kesi ya Ilala hapa kuna vikundi viliomba mikopo toka 2021 lakini sababu ndio zimejaa kwa nini hawakupewa, na waliopewa ni vikundi vichache tena toka waambiwe wanapewa pesa ni Zaidi ya mwezi pesa hazijasoma katika account zao. Zaidi ni Tambo za wanasiasa na viongozi, kwa segerea alianza Diwani kujinasibu wametoa mikopo baadae katika siku ya wanawake waliona dummy cheques nyingine lakini mpaka leo pesa hazijasoma. Hili la million tano kwa goli acha kabisa mpira unaisha watu wanachukua pesa zao, na Jana presidaa kasema mzigo bado upo.

Mh. Madame presidaa wengi wanashindwa kulisemea sababu zimeingizwa siasa na UCCM katika mikopo matokeo yake ni mupe muruke, ashakum si matusi mpaka tumeingiwa hofu na hao maofisa wenu wanataka nini kwa wake na dada zetu ili waachie hizo pesa kwa wakati. Biashara nyingi ni za msimu na kupata pesa kwa wakati ndio sababu muhimu ya kuweza kurejesha kwa wakati. Nyie kutoa pesa mpaka muandae mikutano ya hadhara na viongozi ambao kila kukicha kuwapata taabu.

Mwaka jana Julai walisema wameanzisha mfumo wa kujisajili kidigitali na wale wote walioomba maombi yalifutwa na wakaanza upya, mwezi huu wa Machi ndio kundi lakwanza limeaanza kupewa sasa mbona imebaki miezi michache mbele na urasimu uliopo hizo 10% zilikusanywa nyie wahafidhina mnataka kuzifanyia nini wakati watu hawana kazi na mitaji kuanzisha biashara zitakazoleta ajira.

Msigwa ubunifu wako unatakiwa sana katika hii mikopo ya 10% kwa hivi sasa ni vuta nikuvute, itilieni wepesi Maisha yawe rahisi mmelundika warasimu na wahafidhina wana milolongo mirefu mno kama mlivyoupiga mwingi CAF hata huku kwa wajasiriamali na wenyewe watatoboa. Mnake hii ni double standards kutoka watu wale wale.

Mama yeye hana baya wala mbambamba shida ni wasaidizi wake ngazi ya halmashauri.
 
Back
Top Bottom