HR Managers wenye tabia hizi mshindwe na mlaaniwe

bornagain

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
3,383
1,354
MaHR wote mnaowaita watu kwenye usaili wakati kuna mtu wenu mmeshamuandaa mlaniwe na Mungu, machozi ya wale wote waliopoteza nauli zao kutoka Katavi, Kibondo, Namtumbo na kwingineko mbali kufuata interview za post ambazo nyie HR mnajua kuwa mmeshawapatia watu au ni za watu flani wenye ushawishi nakuapia hayataenda bure, ipo siku machozi hayo yatawarudia tena mara zaidi ya watafuta ajira.

Cha msingi cha kufanya sio lazima kuweka matangazo yenu kwenye magazeti wakati mnajua kabisa kuwa ni geresha, nyie kaeni kimya msiudanganye umma wa waTanzania kuwa mnatoa ajira tena bila upendeleo wakati sio kweli. Cha kufanya chukuaneni kimya kimya kama wanavofanya baadhi ya makampuni then acheni kuwasumbua watoto wa watu, acheni kabisa mtindo huo wa kusafirisha watu safari za mbali wakati moyoni mnajua mnalolitenda ni kinyume na maadili ya kikristu au iwe hata ya Kiislam. Kwa HR yeyote anaefanya unayama huu mshindwe na mlaaniwe na mtakuja kulipia machozi ya watafuta ajira siku moja, acheni na mkome kabisa
 
if u are a believer muombe mungu atakuongoza pale penye nafasi yako, mungu ana kusudi la kila mtu hapa duniani amekupangia mambo mema, usiapply kila kazi ukiona tangazo just pray muulize mungu kama ni yako then uapply kwa imani,hata kama kazi ina mtu ukimuomba mungu kwa imani unaweza ukapata wewe.
 
na wale wote wenye kutaka rushwa ya ngono hasa kwa wake za watu, wewe Oscar wa ofisi za mazingira acha ufuska.
 
hapo kwenye red

Nafikiri ujumbe unamfika bila chenga.
ngoja watu walifanyie kaz alaf tuone mwisho wake.

Hata tume ya ajira mie sijaielewa, wanatangaza nafas 2, then wanaita watu 267 kwenye intvyu, mtu unakata tamaa kabla hata ya kwenda, ni kama vile hawajui wanataka nn, au wanaondoa lawama?
 
Hebu funguka zaidi mkuu, ni Oscar wa Mazingira wapi, ofisi gani? na hata kama majina yote mawili unayo, huenda ikasaidia/ikatusaidia kumfunza adabu.
 
if u are a believer muombe mungu atakuongoza pale penye nafasi yako, mungu ana kusudi la kila mtu hapa duniani amekupangia mambo mema, usiapply kila kazi ukiona tangazo just pray muulize mungu kama ni yako then uapply kwa imani,hata kama kazi ina mtu ukimuomba mungu kwa imani unaweza ukapata wewe.

Soledad kusema ukweli una imani ya kuhamisha milima, asante kwa upako na Mungu aendelee kukuongoza zaidi na zaidi
 
Hii tabia imekua kama ya kawaida kumbe sio ya kawaida,malalamiko mengi sana kwa NHIF pia,wana tabia ya kutoa watu namtumbo kufanya intavyuu kumbe wana watu wao,dunia hii jamani!!!??
 
Siyo tu NHIF, hata TASAF, PPF,TRA, NSSF, TTCL, TANAPA na makampuni mengine mengi tu, lakini kwa ujumla mtindo huu upo serikalini na kwenye taasisi za serikali. Ndo maana kwa mfano kama ikitokea kazi EWURA ya IT na nyingine ya IT labda USAID zote zihitaji watu wenye qalification sawa nakuambia ukweli application za EWURA zitakuwa 300 wakati za USAID zitakuwa kama 50 tu. Hii ni kwa sababu hata wale wasio na qualifications wataambiwa na ndugu zao we aply tu kuna jamaa namfahamu pale ntajaribu kupiga ndogo ndogo
 
MaHR wote mnaowaita watu kwenye usaili wakati kuna mtu wenu mmeshamuandaa mlaniwe na Mungu, machozi ya wale wote waliopoteza nauli zao kutoka Katavi, Kibondo, Namtumbo na kwingineko mbali kufuata interview za post ambazo nyie HR mnajua kuwa mmeshawapatia watu au ni za watu flani wenye ushawishi nakuapia hayataenda bure, ipo siku machozi hayo yatawarudia tena mara zaidi ya watafuta ajira.

Cha msingi cha kufanya sio lazima kuweka matangazo yenu kwenye magazeti wakati mnajua kabisa kuwa ni geresha, nyie kaeni kimya msiudanganye umma wa waTanzania kuwa mnatoa ajira tena bila upendeleo wakati sio kweli. Cha kufanya chukuaneni kimya kimya kama wanavofanya baadhi ya makampuni then acheni kuwasumbua watoto wa watu, acheni kabisa mtindo huo wa kusafirisha watu safari za mbali wakati moyoni mnajua mnalolitenda ni kinyume na maadili ya kikristu au iwe hata ya Kiislam. Kwa HR yeyote anaefanya unayama huu mshindwe na mlaaniwe na mtakuja kulipia machozi ya watafuta ajira siku moja, acheni na mkome kabisa

Leo unalalamika ulivyofanyiwa lakini huwa hamchelewi kusahau, siku na wewe ukipata nafasi ya HR mahali fulani utawafanyia ubaya hata wa kupitiliza wenzio na hata ya kudai rushwa ya ngono.
 
umenena mkuu,BOT.TRA.TCAA ndio mchezo.wanasema eti ni procedure tuu wanafuata lakini wameshawajua waajiriwa wapya
 
if u are a believer muombe mungu atakuongoza pale penye nafasi yako, mungu ana kusudi la kila mtu hapa duniani amekupangia mambo mema, usiapply kila kazi ukiona tangazo just pray muulize mungu kama ni yako then uapply kwa imani,hata kama kazi ina mtu ukimuomba mungu kwa imani unaweza ukapata wewe.

hapa umenena,kweli kabisa sio kila sehemu unatakiwa uaapply kazi kwa sababu tu una shida ya kazi! tukiifanyia kazi maneno haya tutaokoa nguvu zetu,mali,na muda ambao mara nyingi tumeupoteza kunatokana na kufanya mambo kwa kukariri utaratibu wa kibinadamu,badala ya kutumia hekima.
 
Leo unalalamika ulivyofanyiwa lakini huwa hamchelewi kusahau, siku na wewe ukipata nafasi ya HR mahali fulani utawafanyia ubaya hata wa kupitiliza wenzio na hata ya kudai rushwa ya ngono.

distazo usingepungukiwa na chochote kama ungemwambia mtoa mada hivi: UKIPATA NAFASI SIKU YA KUWA HR UKAYAKUMBUKE MANENO YAKO KWA KUTENDA HAKI KWA WOTE USIISHIE TU KUNENA!kuliko ulivyofika mbali kwa maneno yako makali wakati mwenzako kaongea kweli tupu!
 
How can you interview watu wote hao! Heeh!
Msikate tamaa, Mungu yupo.
hapo kwenye red

Nafikiri ujumbe unamfika bila chenga.
ngoja watu walifanyie kaz alaf tuone mwisho wake.

Hata tume ya ajira mie sijaielewa, wanatangaza nafas 2, then wanaita watu 267 kwenye intvyu, mtu unakata tamaa kabla hata ya kwenda, ni kama vile hawajui wanataka nn, au wanaondoa lawama?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom