Houthi wanatumia mbinu za kivita ambazo zitaichosha Marekani kama ilivyotokea Ukraine

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,186
10,922
Tamko kwamba Marekani haina tena pesa kuisaidia Ukraine limekuwa ni la wazi na hata taifa hilo limesema jukumu la kuendelea kuisaidia Ukraine kupigana na Urusi imewaachia wenzake 50 wafanye hivyo.

Pamoja na tamko hilo kutokana na uchofu katika vita hivyo, Marekani pia imesema haina mpango wa kwenda kutengeneza silaha za kivita ambazo zimeharibika.

Mbinu za kivita zinazotumiwa na wanamgambo wa Houth katika kuendelea kuzuia safari za meli za mataifa yanayoisaidia Israel kuleta janga Gaza zinazopita bahari nyekundu, nazo zimetajwa huenda zikapelekea kuchoka kwa Marekanini kwa mara nyengine kupambana na wanamgambo hao.

Mpaka juzi Marekani ilikuwa imeshafanya mashambulizi dhidi ya maeneo ya wanamgambo hao kwa siku 8 tofauti.Katika kila siku ya mashambulia Marekani ilitoa takwimu za mafanikio ya mashambulio hayo na kusema ilikuwa imeharibu rada za kufuatilia safari za meli na za kuongozea mashambulizi ya kundi hilo.

Pamoja na matangazo ya mafanikio hayo mashambulio ya Houth bado hayajasita ambapo juzi hiyo hiyo walifanikiwa kuzilenga na kuzipiga bila madhara makubwa meli mbili za mizigo zilizokuwa zikipeperusha bendera ya Marekani.

Wanamgambo hao wa Yemen wameelezwa kuwa kutokana na vita vyao na Saudi Arabia vya miaka kadhaa kabla ya kusitishwa mwaka 2022 wamepata uzoefu mkubwa wa kuficha silaha zao.

Sehemu kubwa ya wapiganaji wa jeshi hilo huwa wanapata mafunzo na kusambaa maeneo mbali mbali bila kuwa na kambi maalumu. Teknolojia za kivita wamekuwa wakipata kwa msaada kutoka wataalamu wa Hizbullaha na wale wa Marekani.

Rada na silaha zao muhimu huwa wanaziweka kwenye gari ndogo ndogo ambapo mara baada ya kufanya shambulio moja huondoka eneo hilo na kuelekea kituo kingine. Marekani tayari ina droni za upelelezi aina ya Reaper juu ya anga la Yemen kufuatilia mienendo ya kundi hilo. Hata hivyo kutokana na mfumo wa kupiga na kuhama imetajwa kuwa droni hizo hazitoweza kuleta tija kubwa katika kuzuia mashambulio ya Houth.

Kuhusu silaha wanazotumia Houth ni uhakika kuwa nyingi zinatokea au kupitia Iran baadae kusafirishwa kwa meli ndogo ndogo kupelekwa Yemen. Kutokana na wingi wa meli hizo na pamoja na ujasusi mkubwa inaofanya Marekani kufuatilia silaha hizo nako kumeelezwa haitokuwa rahisi kuzipekua meli zote hizo kuzuia silaha hizo zisiwafikie Houth.

Wiki mbili zilizopita jaribio la kuzuia silaha kutowafikia wanamgambo wa Yemen zilipelekea askari wawili wa Marekani kuzama na kupoteza maisha. Haikuwekwa wazi mazingira yaliyopelekea askari hao kuzama na hatimae kupotea moja kwa moja

Mwisho wa yote matarajio ni kuwa katika vita baina ya Marekani na wanamgambo wa Houth kutapelekea hasara kubwa kwa Marekani na hatimae kuchoka bila kufanikiwa kuwazuia wanamgambo hao kuendelea kuzichagiza meli za mizigo zinazopita kwenye lango la bab Mandeb kuelekea au kutoka mfereji wa Suez.
 
Umepiga mdomo mtupu tu huna chanzo, hivyo tunaweka kwenye takataka
Kila kitu chanzo.Hayo ni matamko ya watu wasio na akili timamu. Ndio maana imekuwa ni muhimu tuanze kubadili mifumo yetu ya elimu.Watu wanakuwa na digrii mpaka tatu lakini hawana lolote.

Kwani mawazo yako baada ya kusoma na kufuatilia mambo huwezi kuchambua kitu ukaweka kwa wenzako.
 
tumia akili ndugu, Us na Israel kuichakaza Iran ni suala dogo sana. Wanatafuta sababu tu hapo subiri aje
 
hapo ni iran vs america.... hao houth ni proxy wa iran, fully funded, trained and supplied by iran... kwahyo msidhani ni wajiwanamgambo.
Lakini hapo Iran kapiga mahesabu vizuri sana.
Marekani hawezi kulala nyumbani kwake huko mbali halafu kila siku akawaletea watu tabu.
 
Kila kitu chanzo.Hayo ni matamko ya watu wasio na akili timamu. Ndio maana imekuwa ni muhimu tuanze kubadili mifumo yetu ya elimu.Watu wanakuwa na digrii mpaka tatu lakini hawana lolote.

Kwani mawazo yako baada ya kusoma na kufuatilia mambo huwezi kuchambua kitu ukaweka kwa wenzako.
Ungeandika basi kwamba ule ni mtazamo wako, tungejua tukusaidie vipi kwenye comments
 
Kuiondoa utawala wa mahayatollah nchini Iran ndio mpango mzima. Huo utawala hauna mustakbali wowote huko tuendako.
Mpaka 3000 na ngapi mtakua mshauondoa
Dunia haiwezi kua na multi-player(multipolar) bila kua na sirikali imara pale iran kama iliopo sasa
Iran ndio nchi pekee inayojitambua pale mido ist
Ili uiangushe iran kwanza hakikisha hakuna hams hakuna Hizbullah hakuna houthi hakuba qatai Hizbullah nk
Yaani wamagharibi pamoja na imeloa mliisha feli zamani sana kuiangusha iran na march sijui feb hapo iran inaenda kufanya uchaguzi wa karne mkiwakosa kwenye uchaguzi wa mara hii kuivuruga iran kutokana na tension iliipo pale mashariki ya kati labda muombe tu Mungu awapelekee gharika bila ya hivyo mtakua rasmi mshashindwa zaidi kuiangusha sirikali ya tehran
 
tumia akili ndugu, Us na Israel kuichakaza Iran ni suala dogo sana. Wanatafuta sababu tu hapo subiri aje
Suala dogo sana si kama vile walivyoichakaza hamas
Kila siku mnatafuta visingizio kwani walitumia sababu ipi kuichapa iraq na Afghanistan?
Americant anaiogopa iran kama kufa yaaani
 
Kama Hadi Leo hawajaiona sababu ujue wanagwaya US akiwa anakuweza huwa ni kichapo tu kwenda mbele sema saivi US tangu awekewe dole la kati na Putin kule Ukraine amekuwa mdebwedo
United Shits Of Americant kwa sasa hata wewe ukieka nayo mbili unaikalisha
Jamaa anashangaza sana eti marekani itafute sababu ukiona inatafuta sababu ujue haikuwezi
 
Ungeandika basi kwamba ule ni mtazamo wako, tungejua tukusaidie vipi kwenye comments
Kama uko vizuri kichwani ungechukua baadhi ya mistari niliyoandika ukatafuta ukweli wake halafu ukanisaidia pale ambapo ungeona nimekosea.
Nadhani modi wa JF wananiamini na wanafanya kazi ya kutathmini.Wewe huna uwezo huo.
 
Mpaka 3000 na ngapi mtakua mshauondoa
Dunia haiwezi kua na multi-player(multipolar) bila kua na sirikali imara pale iran kama iliopo sasa
Iran ndio nchi pekee inayojitambua pale mido ist
Ili uiangushe iran kwanza hakikisha hakuna hams hakuna Hizbullah hakuna houthi hakuba qatai Hizbullah nk
Yaani wamagharibi pamoja na imeloa mliisha feli zamani sana kuiangusha iran na march sijui feb hapo iran inaenda kufanya uchaguzi wa karne mkiwakosa kwenye uchaguzi wa mara hii kuivuruga iran kutokana na tension iliipo pale mashariki ya kati labda muombe tu Mungu awapelekee gharika bila ya hivyo mtakua rasmi mshashindwa zaidi kuiangusha sirikali ya tehran
✍️ Sasa mtu mpaka aombe Muungano na Nchi zingine ndio waende Frontline, sasa huyo kweli ana nguvu...?

✍️ Na kuhakikishia hata Kama Iran haina Hizbullah,Houth na Hamasi, huyo US hati pua hao hapo Iran.

✍️ Na siku zinavyodi kwenda hao Iran wanaendelea kujiwekea utawala hapo Middle East.
 
tumia akili ndugu, Us na Israel kuichakaza Iran ni suala dogo sana. Wanatafuta sababu tu hapo subiri aje

tumia akili ndugu, Us na Israel kuichakaza Iran ni suala dogo sana. Wanatafuta sababu tu hapo subiri aje
✍️ Unapo sema US na Israel hapo bado sijakuelewa, we ukisema US inatosha maana Israel ndio huyo huyo US.
✍️ Iran ya sasa utaitafutia sababu ipi mkuu...?
~ Vikwazo umeshindwa
~ Kumuundia vikundi vya uasi ndani ya Iran umeshindwa
~ kumvamia umeshindwa
~ Ukimletea ubabe na yeye anakuletea ubabe.

✍️ Itoshe kusema Iran ya sasa ni mkubwa mwenzao sema jeuri tuu zimewajaa.
 
Back
Top Bottom