Housigeli’ anataka kuniharibia ndoa

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,148
‘Housigeli’ anataka kuniharibia ndoa


!


habari yako. Nategemea mzima wa afya na hutasita kunisaidia kunipa ushauri unaonifaa. Mimi ni mwanamke mwenye watoto wawili. Tangu nimeolewa miaka sita iliyopita, nimekuwa na msichana wangu wa kazi mmoja ambaye nimempenda sana hasa kwa kuwalea vizuri watoto wangu na kuwa mwepesi wa kazi. Kutokana na kuishi vizuri na ‘housigeli’ huyu, amekuwa kama mtoto wa nyumbani na hata ndugu zangu na wa mume wangu wanampenda sana na wamemzoea kupita kiasi.

Tatizo hili la kuwazoea ndugu wa mume wangu sasa naona linataka kuharibu ndoa yangu kwani huyu msichana ameanza tabia mbaya na amemweleza mkwe wangu kuwa mimi situlii nyumbani na sina muda wa kumshughulikia mume wangu kwani kazi zote anafanya yeye, mimi kazi yangu kusafiri na kushinda kazini. Huyu mama mkwe wangu kusikia hayo, amekuja juu na sasa anamshinikiza mume wangu aniache eti nashindwa kuhudumia nyumba na badala yake amuoe ‘housigeli’. Mume wangu ameshtuka na amenieleza kila kitu hali iliyonikasirisha sana.

Sasa naomba ushauri wako kwani mama mkwe bado yupo kwangu, je, nifanyeje kabla hajaondoka kurudi kwake? Mama Kelvin Tabata, Dar es Salaam. Mama Kelvin pole sana kwani inaonekana huyo mama mkwe wako hajaelimika vya kutosha. Uzuri wa mwanamke haupimwi kwa kazi za nyumbani pekee, bali kuna mambo mengi na mkwe wako anapaswa kutambua kuwa wewe unafanya kazi hivyo huwezi kukaa nyumbani muda wote na ndiyo sababu ukatafuta msaidizi.

Lakini pia ni vyema ukiwa nyumbani ufanye kazi zilizopo ikiwamo kumpikia mumeo na kumhudumia ipasavyo. Usiwe na hasira za haraka kwa msichana wako wa kazi kwani inawezekana aliulizwa kimtego naye akajibu vizuri tu lakini mkweo akawasilisha kwa mumeo vibaya. Nadhani mumeo pia anapaswa amweleze mama yake kwa upole kuwa wewe unafanya kazi na huwezi kufanya kazi zote za nyumbani. Pia amweleze kuwa huyo msichana wa kazi kamwe hawezi kuwa mke wa mtoto wake.

Naamini mtoto wake akimwelimisha na akawa na msimamo, mama mkwe wako ataelewa au hata kama hataelewa, atashindwa kuendelea kusisitiza anachotaka. Ni vyema pia ukakaa na mshichana wako na kumhoji ilikuwaje hata wakazungumza hayo na mkweo na ukiona kama alichokonolewa basi mtahadharishe akae mbali na mama mkwe na asiwe mwepesi kueleza mambo ya ndani ya nyumba kwa mkweo.

Hata hivyo fanya uchunguzi wako kwa siri na ukiona msichana wako anapalilia ili aolewe yeye, basi ni vyema ukatafuta msichana mwingine wa kazi na huyo kumwondoa ili asije kuharibu ndoa yako. Haina haja kugombana na mtu yoyote kwani naamini huyo mkweo ataondoka na nyinyi mtaendelea na maisha yenu. Pia jifunze kuvumilia kwani wakwe wengine uelewa wao ni mdogo.
 
hako ka maid kimeo eeh kwa staili hiyo mie ningekapiga kibuti tu
kwanini avuruge ndoa yangu eeeh
 
Thanks kwa kujua kumbe pdidy ni SHE! Majina mengine bana! LOL!
 
Tatizo la nyie akina dada pindi mnapoolewa na kupata housegirl mnamtelekezea kila kitu. Hiyo ni mbaya sana. Yawezekna housegirl anakutandikia hadi kitanda, kukuwekea neti, kukufulia nguo za ndani za kwako na mmeo kwa ujumla anafanya kazi zote, kazi yak ni kula, kusafiri na kwenda kazini.
Hali hiyo ni mbaya sana kwenye ndoa, hasa unapomwamini hausegirl katika kila kitu adi kulea watoto wako! kumbuka housegirl siyo permanent, akikuharibia watoto? Kwa hiyo kama mama kumbuka majukumu yako ya famia hata siku moja, jitahidi kumuanda mmeo na hata mala mmbili kwa wiki kuwaandalia dinner. Zaidi ya hapo housegirl asiruhusie kukufanyia kazi za chumbani kwako. hapo ndoa yako itaimalika. mama mkwe ameishaona kuwa wewe ni kimeo hasa kwenye kucare mmeo na familia. badilika.
 
Thanks kwa kujua kumbe pdidy ni SHE! Majina mengine bana! LOL!
Sidhani kama ni SHE, maybe amecopy & paste hii habari. Kuna siku alikuja na habari ya kuonyesha kwamba yeye ni HE.
...mnaokumbuka nilikuja na mada ya"nifanyeje kuongeza hormones za kiume""...
...nilipopewa dawa za kurekebisha sperms nikapima tena nikaambiwa nipime rate za hormnoes ndipo nikakuta za kiume ni 1.6 wakati zinatakiwa 2.2-10% nilimwomba sana mungu na kuamini kama ni makusudi yake kuoa basi ni makusudi yake kunipa mtoto thanx much kwa mkewangu aliekwa pembeni yangu muda wote kunikumbusha kwenye maombi...
...niliamua kwenda kupima baada ya madadazangu kuanza kumtukana mkewangu mpendwa oooohhh anajaza chooo...
 
Sidhani kama ni SHE, maybe amecopy & paste hii habari. Kuna siku alikuja na habari ya kuonyesha kwamba yeye ni HE.

Au Semenya huyu? Manake dah! Leo anaonyesha yeye SHE, juzi katoa thread yeye dume! LOL!
 
Au Semenya huyu? Manake dah! Leo anaonyesha yeye SHE, juzi katoa thread yeye dume! LOL!


Huyu ni dume ila naogopa kuandika hapa tabia nayohisi anayo, kwa mwanaume huwezi penda kujizungumzia wewe ni SHE hata siku 1, pia avatar nayo utata kidogo kwa wewe mchambuzi wa mambo ya jinsia naomba utumie dk chache kupitia thread zake utaniambia.
 
Mimi nadhani hauna haja ya kuuliza ushauri kwenye hapa unless wewe mwenyewe una mapungufu yako na unayajua. Are you afraid of getting another housemaid? Kitu cha kwanza ingekuwa kutafuta replacement asap kuokoa/kulinda ndoa yako. Unaogopa kuwa matatizo yako yataonekana pindi huyo housemaid akiondoka.
Mume wako vilevile anaweza kuwa anakutegea.
 
Huyu ni dume ila naogopa kuandika hapa tabia nayohisi anayo, kwa mwanaume huwezi penda kujizungumzia wewe ni SHE hata siku 1, pia avatar nayo utata kidogo kwa wewe mchambuzi wa mambo ya jinsia naomba utumie dk chache kupitia thread zake utaniambia.

Nyie rudini kwenye mada!
 
Huyu ni dume ila naogopa kuandika hapa tabia nayohisi anayo, kwa mwanaume huwezi penda kujizungumzia wewe ni SHE hata siku 1, pia avatar nayo utata kidogo kwa wewe mchambuzi wa mambo ya jinsia naomba utumie dk chache kupitia thread zake utaniambia.

Hahaha! Nimeenda kwenye profile yake! LOL! Kaazi kweli kweli! Na avatar yake basi burudani tupu! Si nchezo; wacha turudi kwenye mada sasa kama mdau Radical anavyotutaka! LOL!
 
Huyu jamaa ni MAN ila inaelekea ame-paste hii bila kutujulisha ameitoa wapi. Anayeomba ushauri hapo amejitambulisha kama Mama Kelvin wa Tabata ambaye naamini sio huyo Pdidy. Chini yake kuna ushauri unatolewa ambao pia hajaeleza umetolewa na nani. Hebu ondoa huo utata kwanza Pdidy.
 
pdidy ni mwanaume na hii Topic kacopy sehemu na kuiwasilisha hapa ijadiliwe
Mama kevin kama una mapungufu ya kupika ,usafi wa ndani na mengineyo jitahidi uvijue fasta ili beki tatu wako atakapoondoka ujue namna ya kumuhudumia mmeo
kaa na mmeo muongee wewe ni binadamu bwana sio mungu
 
pdidy ni mwanaume na hii Topic kacopy sehemu na kuiwasilisha hapa ijadiliwe
Mama kevin kama una mapungufu ya kupika ,usafi wa ndani na mengineyo jitahidi uvijue fasta ili beki tatu wako atakapoondoka ujue namna ya kumuhudumia mmeo
kaa na mmeo muongee wewe ni binadamu bwana sio mungu

Ahsante FL1 kwa unabii wako. Then, kama ni mambo ya kukopi na kupesti, angepaswa kutuambia hivyo mapema ili tujue tuchangieje. Otherwise yatakuwa yaleyale ya Gudboy. Watu wanatunza kumbukumbu humu jamvini wacha mchezo. Haya tuendelee na mada.
 
hako ka maid kimeo eeh kwa staili hiyo mie ningekapiga kibuti tu
kwanini avuruge ndoa yangu eeeh
Hivi ukiamka asubuhi ukajiangalia kwenye kioo na ukakuta kuna matongo tongo, utakiondoa kile kioo? je utakivunja?

Naamini majibu ni hapana, huyo h/g ni kama kioo, cha msingi ni kujirekebisha tu.
 
Kama hausi geli wamekubaliana na Mr. wako wawe wanamegana si uwaache wasisitizie watumie sox tu.
 
Back
Top Bottom