Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,471
Umetoa mfano wa Bloomberg. NYC ina matatizo mengi sana ya kifedha, mwaka jana kwa mfano, hela ya kusafisha snow iliisha kabla ya wakati, walimu wanakimbia inner city schools kwa sababu hawalipwi vizuri, police wengine wa NY wanaondoka kwenda PD za miji ya jirani wanakolipwa vizuri zaidi. Yote haya ni matatizo ambayo Bloomberg angeyatatua kwa kutoa tu hata robo ya utajiri wake lakini hajafanya hivyo, kwa sababu siyo njia muafaka ya kutatua tatizo. Leo MO anajenga mashule, mahospitali, visima nk, ikitokea akaamua kutogembea tena, au kushindwa uchaguzi na akaja mbunge hohehahe itakuwaje?
Dawa ni kufanya kazi bungeni kama alivyoomba kura kuwakilisha wananchi. Yeye si fisadi, lakini atunge sheria kwamba hela zote zilizoibwa na akina Chenge zirudishwe na mikataba mbali mbali ya kifisadi isainiwe upya. Akifanya hivyo zitapatikana hela nyingi za kujenga shule, barabara, visima na mahospitali na yeye hatatoa hela mfukoni mwake, badala yake hela zake atatanua biashara zake zaidi, ataajiri watu wengi zaidi na atalipa kodi zaidi. hivi ndivyo atakavyoleta maendeleo.
Kwame:
Matatizo yako, unalinganisha matango na ubuyu. Sheria za nchi zinazoweza kuwafunga Chenge na mafisadi wengine zipo. Kinachoshindikana ni ufuatiliaji wa sheria hizo. Na hilo sio suala la mbunge. Ni swala na vyombo vinavyosimamia sheria.
Sheria za nchi ambazo zinaweza kufunga jela mwizi wa kuku kwanini zisiweze kumfunga Chenge? Hapa haiitajiki sheria mpya. Huu ni ukosefu wa nidhamu za kiutawala ambazo zinafanya sheria zitumike kwa wanyonge tu. Lakini walionacho wakifanya makosa, wanapeta.
Hivyo basi hata kama sheria mpya zitatungwa, hakuna kitakachosaidia iwapo watu watakuwa hawana nidhamu.