Hotuba ya Mhe Moh Dewji: April 25, 2009

KAMARADE

Member
Nov 18, 2009
63
3
HOTUBA YA MHESHIMIWA MOHAMMED DEWJI YA MKUTANO MKUU WA CCM WILAYA YA SINGIDA MJINI TEREHE 25/04/2009.

ASSALAAM ALAYKUM ! BWANA ASIFIWE ! TUMSIFU YESU KRISTO !

HABARI KII , AMUCHA , MWAFANGANA

Mhe. Mwenyekiti
, Niruhusu nianze na shukrani, shukrani zangu za kwanza ni kwa Mwenyezi Mungu aliyetujalia uhai na afya na akatuwezesha kukutana kwenye mkutano Mkuu huu wa CCM Wilaya, shukrani pia kwa Secretarieti nzima ya Wilaya kwa kuandaa mkutano huu, nasema ahsanteni sana.

Mhe. Mwenyekiti
, naomba nichukue tena nafasi hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa wajumbe wote wa mkutano mkuu huu wa CCM, pamoja na wageni waalikwa kwa mahudhurio yao , nasema ahsanteni sana .

Mhe. Mwenyekiti
Naomba nitoe pongezi zangu za dhati kwa uongozi wa serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na mhe. Jakaya mrisho Kikwete rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kutokana na jitihada inazozifanya za kutatua kero za wananchi na kuiletea nchi yetu maendeleo endelevu.

Mhe: Mwenyekiti
; Naomba niwapongeze viongozi wote wa jumuiya za chama cha mapinduzi ndani ya mkoa wetu kwa kuchaguliwa kwao kuziongoza jumuiya hizo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. Mhe. Chilolo hongera sana kwa kuchaguliwa, Mhe. Hussein Nagi hongera sana kwa kuchaguliwa, Mhe. Amani Nyekele hongera sana kwa kuchaguliwa. Majukumu mliyokuwa nayo ya kuziongoza jumuiya hizi ni makubwa mno lakini naamini kwa kushirikiana na viongozi wenzenu mtayatekeleza kwa ufanisi zaidi. Nawatakia kila la kheri.

Mhe. Mwenyekiti
nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipomshukuru ndugu yangu Dr. Raphael Chegeni mbunge wa jimbo la Busega kwa kuja kushirikiana nasi katika mkutano huu wa CCM, asante sana Dr. Chegeni, na hii imefungua ukurasa wa ushirikiano kati yetu. Nami nakuahidi kuwa pindi utakaponihitaji ndani ya jimbo lako la Busega nitakuwa tayari kushirikiana nawe.

Mhe. Mwenyekiti
naomba tena nitoe shukrani zangu ingawa nilishazitoa mapema mwezi Januari 2006 na February 2008 lakini siyo vibaya kuzirudia tena kwa wananchi wote wa Jimbo letu la Singida Mjini kwa kunichagua kwa kura nyingi dhidi ya wagombea wenzangu kupitia vyama vya upinzani kuwa Mbunge wa Jimbo hili. Katika hili ningependa kuwashukuru wananchi wote wa Jimbo la Singida Mjini hata wale wasio nipigia kura kwani ni haki yao ya kidemokrasia kuwa na mawazo mbadala na pia ni changamoto kwangu “ Nasema ahsanteni sana wananchi wa Singida Mjini”.

Mhe. Mwenyekiti
pia naomba nitoe shukrani zangu na pongezi zangu za dhati kwa wananchi wote wa Jimbo la Singida Mjini kwa jinsi wanavyonipa ushirikiano wa kuitekeleza vyema Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi, wananchi wa Singida Mjini nasema ahsanteni sana “ Mwajifya Sana ”.

Mhe. Mwenyekiti
, baada ya mimi kuchaguliwa, niliapishwa tarehe 29/12/2005 pale katika ukumbi wa Bunge Dodoma na nikawa tayari kuwatumikia wananchi wa jimbo letu la Singida Mjini, kitu cha kwanza nilichofanya niliwaalika madiwani wote kwa niaba ya wananchi ili waje washuhudie kuapishwa kwangu, na nikafanya nao kikao cha kazi ili tuweze kugawana majukumu ya kuwatumikia wananchi. Niliwaomba madiwani waniainishie vipau-umbele vya kero za wananchi vilivyopo kwenye kata zao, ili kwa kushirikiana na wananchi tuweze kuvitatua vipau-mbele hivyo, napenda kutumia nafasi hii kwashukuru madiwani wote kwa kazi kubwa waliyoifanya kwa kushirikiana katika jambo hilo, na mpaka sasa tumeweza kufanikiwa kutatua kero za wananchi kwa kiasi fulani.

Mhe. Mwenyekiti
, baada ya pongezi na shukrani naomba sasa nitoe taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi na ahadi nilizotoa kwenye mikutano yote ya kampeni za Chama Cha Mapinduzi mwaka 2005, kwa kipindi cha miaka mitatu ya Ubunge wangu kwa jimbo la Singida Mjini kama ifuatavyo:-

Mh. Mwenyekiti
, kwenye secta ya Kilimo, Chakula na Ushirika :- Serikali ya awamu ya nne iliingia madarakani rasmi mapema Januari, 2006, huku ikikabiliwa na janga la njaa lililoikumba nchi yetu kutokana na ukame uliojitokeza, hata mimi kwa nafasi yangu ya ubunge changamoto hizo zilinigusa hasa ukizingatia kwamba wilaya yetu ipo mjini, ambapo kimsingi wilaya za mjini huwa hazipati msaada kutoka hifadhi ya Taifa ya chakula (SGR), ilibidi mimi mbunge wenu pamoja na kuiomba serikali ilete chakula cha bei nafuu lakini pia nilijitolea tani mia moja za mahindi zenye thamani ya Shilingi Millioni Arobaini kwa wakati huo (T.shs.40,000,000/-).

• Kutokana na janga hilo mahudhurio ya wanafunzi darasani yakadorora, hivyo kama mbunge wa jimbo kwa kushirikiana na wenzangu tukaamua kutoa unga wa uji kwa shule zote za Msingi zilizoko ndani ya manispaa ya Singida kwa miezi minne mfululizo. Unga huo uligharimu takribani Millioni Thelathini (T.shs. 30,000,000/-).
Kwa kweli nilijifunza mengi kutokana na tukio hilo hivyo nikapata wazo la ufumbuzi wa kudumu ambalo ni kuleta tractor ili kurahisisha kazi za kilimo kama ifuatavyo:-
• Tractor hili lifanye kazi ya kulima mashamba ya shule ili mazao yatakayopatikana yawekwe kwenye maghala ya shule, inapofika wakati wa uhaba wa chakula, akiba hii izisaidie shule zetu kwa kuwapikia watoto wetu uji, na kwa jambo hili nilitaka uwe ni mpango wa kudumu, kwani wakati wa njaa watoto walipopatiwa Uji, mpango huo ulifanikiwa sana kwa kurejesha mahudhurio ya wanafunzi darasani. Sote tunafahamu kuwa tumbo likiwa halina chakula kamwe hautapata usingizi wala usikivu kwa mwalimu.
• Tractor hili lifanye kazi ya kulima mashamba ya vijiji, ambapo pia tungepata nafasi nzuri ya kuwatumia wataalamu na maofisa Kilimo wetu walioko vijijini kwa kufundisha njia bora za kilimo cha kisasa kwenye familia zetu. Mazao yatakayopatikana kutoka kwenye mashamba hayo, yawekwe kwenye maghala ya vijiji na wakati wa uhaba wa chakula, serikali ya kijiji iweze kusaidia familia zilizo na upungufu wa chakula.

Kinyume na matarajio yangu, nathubutu kusema kwamba mpaka leo hii hatujapata kijiji wala shule iliyo tayari kulitumia tractor hilo, na kwa jambo hili siyo tu kwamba tractor hili halitumiki kulingana na madhuni yake bali ni kitega uchumi kikubwa sana upande wa kilimo, tractor hili nimewekeza Millioni Ishirini na Tano (T.shs 25,000,000/-), ambazo hadi sasa hazizalishi na tractor limebaki bila kutumika, hizi ni fedha nyingi sana! ambazo tungeweza kuwekeza kwenye secta nyingine, hii ni changamoto kubwa sana ndugu Mwenyekiti, mimi nafikiri mpango huu wa kulima mashamba ya shule na vijiji utatusaidia kuondokana na matatizo ya upungufu wa chakula na kuwa na mpango endelevu wa Uji mashuleni. Lengo langu kubwa ni kuwa, watoto wakiwa na afya njema na mahudhurio mazuri darasani lazima watafanya vizuri katika masomo yao , na hatimaye kupata mafanikio ya maisha, ambayo si yao peke yao bali ya jamii yetu nzima ya Singida Mjini. Mara baada ya kikao hiki natarajia kufanya kikao tena na madiwani wote ili tupate ufumbuzi juu ya matumizi ya tractor hili ndani ya jimbo letu.


Secta ya Elimu na Ufundi Stadi:-
Mh. Mwenyekiti
, katika dunia ya sasa ukimpenda mtoto mpe elimu, kwani elimu ndiyo ufunguo wa maisha, na hata kama una mali ukimpa hela, akiwa hana elimu atazitumia zitakwisha, narudia tena kusema “hakuna kitu bora na muhimu zaidi kwa mtoto kama kuwekeza kwenye elimu yake” pia ni haki ya msingi kwa mtoto, hii inatokana na ukweli kuwa maendeleo ya sasa yanahitaji elimu na tekinolojia kubwa, hivyo bila elimu hatuwezi kupiga hatua yoyote ya maendeleo kwenye jimbo letu, Ndugu Mwenyekiti tukumbuke kuwa Jimbo letu tangu Uhuru mpaka 2005 kabla ya mimi kuwa mbunge wenu tulikuwa na Shule za sekondari mbili tu! ambazo ni Dr. Salmini na Chief Senge zilikuwa zinatoa wanafunzi 360 ukilinganisha na sasa tuna shule 15 ambazo zinatarajia kutoa wanafunzi 2,700 ikiwa ni zaidi ya mara nane. shule moja ina mikondo mine na kila darasa lina wanafunzi 45, hivyo kila shule ina wanafunzi 180 wanaomaliza na kufanya mtihani wa Taifa kidato cha Nne na ukizidisha mara shule 15 ni sawa na jumla ya watoto 2,700 wanaomaliza kidato cha Nne ndani ya wilaya yetu. Changamoto kubwa tujiulize kuwa hawa watoto 2,700 tunawapeleka wapi? ina maana waishie kidato cha Nne tu?! Hapana! Lazima tuweke mikakati ya ujenzi wa shule za kidato cha Tano na Sita ndani ya wilaya yetu, kama kwa muda miaka karibu Arobaini na Nane (1961 – 2009) tulikuwa na shule mbili na sasa ndani ya miaka mitatu tu tuna shule 15, hakika hatuwezi kushindwa kujenga ‘high school' hizi, tujipange vizuri na kushirikiana, nami sitasita kuchangia kama nilivyofanya kwenye shule zetu za Kata.

• Mh. Mwenyekiti, kama mnavyofahamu nilitoa ahadi ya kuanzisha mfuko wa Mbunge kwa ajili ya kuwalipia ada watoto yatima na wale ambao wazazi wao hawana uwezo wa kulipa ndani ya wilaya yetu, mwaka 2006 nililipia wanafunzi 100, 2007 wanafunzi 300, 2008 wanafunzi 550 na mwaka 2009 nimelipia wanafunzi 1,000 hii yote nafanya hivyo kwa vile najua umuhimu wa elimu. Jumla nimeshatumia shilingi milioni 36 kwa ajili ya ada, kwani elimu ni haki ya msingi kwa mtoto.
• Nimeshirikiana na wananchi wenzagu kujenga shule za sekondari za kata ndani ya wilaya yetu kwa kuchangia kama ifuatavyo:-

• Shule ya Sekondari Mitunduruni:-
nimejenga madarasa manne, jingo la utawala na vyoo vya kisasa pamoja na kuchonga samani (furniture) za madarasa hayo kwa thamani zaidi ya shilingi Milioni mia moja na thelathini (T.shs 130,000,000/-) na kesho natarajia kutoa cement yenye thamani ya milioni 2, Jumla nitakuwa nimetoa T.shs. 132,000,000/-.

• Shule ya Sekondari Mughanga :- nimemalizia madarasa manne pamoja na kujenga vyoo vya kisasa kwa thamani zaidi ya shilingi Millioni Arobaini na Tano (45 Milioni) na kesho natarajia kutoa vifaa vya ujenzi, cement na mabati vyenye thamani ya shilingi Millioni Tano, Jumla nitatumia Shilingi Millioni Hamsini (T.shs 50,000,000/-).

• Shule ya Sekondari Ipembe :- nimejenga madarasa manne, pamoja na vyoo vya thamani ya shilingi millioni sitini na Sita (66 Milioni) na kesho natarajia kuwapatia madawati yenye thamani ya shilingi millioni mbili (2 milioni). Jumla Shilingi Millioni 68.
• Shule ya Sekondari Kindai :-
nimejenga madarasa manne, jengo la utawala na vyoo vya kisasa pamoja na kuchonga samani (Furniture) za madarasa hayo kwa thamani ya shillingi Millioni Mia Moja na Thelathine (T.shs. 130,000,000/-)
• Shule ya Sekondari Utemini :-
shule hii kwa sasa iko kwenye hatua ya ujenzi wa madarasa manne kwa kushirikiana na Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Utemini, nimechangia vifaa vya ujenzi kama mabati 250 yenye thamani ya Tshs. 5 milioni, cement mifuko 600 yenye thamani ya T.shs. 10 milioni, mbao, misumari na nondo vyenye thamani ya T.shs 5 milioni. Vyote kwa pamoja vitakuwa na thamani ya Milioni 20.
• Shule ya Sekondari Majengo :-
nimechangia ujenzi wa madarasa manne shilingi Millioni Nne na Laki Nane (T.shs. 4,800,000/-) pamoja na vifaa vya ujenzi (Cement) vya thamani ya Shillingi Millioni Tano na Laki Mbili (T.shs. 2,500,000/-)
• Shule ya Msingi Misuna iliyopo Kata hii ya Majengo, pia nilishajitolea mchango wa kujenga madarasa mawili yaliyonigharimu ya shilingi Milioni Kumi na Nane (T.shs.18,000,000/-).
• Shule ya Dr. Salmini pia nimechangia shilingi Milioni Tano (T.shs 5,000,000/-) kwa ajili ya ujenzi wa maabara ya shule hiyo.
• Shule ya Sekondari Mandewa; - nilishachangia shilingi Millioni Tano 5,000,000/- na kesho nitatoa mabati yenye thamani ya 2 milioni. Jumla nitakuwa nimechangia shilingi millioni Saba (T.shs. 7,000,000/-).
• Shule ya Sekondari Unyamikumbi :- nimechangia uingizaji wa umeme katika shule hiyo. Na pia nimechangia fedha taslimu shilingi milioni Tano (T.shs. 5,000,000/-) katika ujenzi wa madarasa na ofisi yao ya Mtendaji wa Kata.
• Shule ya Sekondari Mwankoko (Unyianga) :- nimechangia shilingi Milioni Tano (T.shs. 5,000,000/-) na kesho naenda kukabidhi mabati 100 yenye thamani ya 2 milioni.
• Shule ya Sekondari Mtamaa :- nimechangia mabati yenye thamani ya shilingi Milioni Moja ( T.shs 1,000,000/-).
• Shule ya Sekondari Mungu Maji:- Naahidi nitachangia shilingi Milioni Tano (T.shs. 5,000,000/-).
• Shule ya Sekondari Unyambwa: - nimemalizia madarasa manne pamoja na kujenga vyoo vya kisasa kwa gharama ya zaidi ya shilingi Milioni Arobaini na Saba (T.shs.47,000,000/-) na ninatarajia kesho kuwapatia madawati yenye thamani ya shilingi milioni mbili (T.shs.2,000,000/-) Jumla nitakuwa nimechangia Milioni 49.
• Ndugu Mwenyekiti, shule za Sekondari za serikali na binafsi nimewapatia madaftari yenye thamani ya shilingi Milioni 7,550,000/- na mipira miwili miwili kila shule. Vyote kwa pamoja vimenigharimu kiasi cha shilingi 7,694,000/-.

• Nimewagharimia wasanii watano wa Kikundi cha SOT kwenda kwenye mafunzo Chuo cha Sanaa cha Taifa (BASATA) Dar es Salaam ambayo kwa ujumla imenigharimu kiasi cha shilingi Milioni Mbili (T.shs. 2,000,000/-).

Mh. Mwenyekiti
, kwa upande wa Secta ya Elimu pekee nimechangia na kugusa kila Kata iliyopo ndani ya wilaya yetu, kwa maana hiyo jumla imenigharimu shilingi 521,050,000/-.

Mh. Mwenyekiti
, Kuna changamoto nyingi zinazotukabili katika secta hii muhimu nazo ni kama ifuatavyo:-
• Tuna upungufu wa Waalimu tunaendelea na jitihada za kuitaka serikali kuendelea na mpango wake wa kutoa mafunzo kwa waalimu kadri iwezekanavyo ili tatizo hili la upungufu wa waalimu liweze kuisha na nina amini Serikali yetu imejipanga vizuri kukabiliana na tatizo hili.
• Upungufu wa Maabara, Majengo ya Utawala na nyumba za waalimu na hostel. Shule zetu za kata bado ni changa hazijakamilika, hivyo baadhi ya shule hakuna majengo ya maabara, nyumba za waalimu, majengo ya utawala na kadhalika.
Natoa wito kwa wananchi tusikate tamaa tuendelee kutoa michango yetu na serikali yetu itaendelea kutuunga mkono kama ilivyo kwa Mpango wa MMES na TASAF na hatimaye itafika wakati shule zetu hizi zitamalizika na kuwa shule kamili.
• Upungufu wa ‘high school' hizi tujipange na tuanze kuweka mikakati madhubuti ya ujenzi wa shule hizi mapema wilayani kwetu, tuonyeshe jitihada, nami sinta sita kuchangia kama ilivyokuwa kwenye sekondari za kata.
Mh. Mwenyekiti
, kwa mpango wa baadaye, ninafikiria kujenga kituo cha watoto Yatima ambacho pamoja na mambo mengine kitatoa elimu ya awali kwa watoto hao.

Secta ya Afya:-
Mh. Mwenyekiti
, kwenye secta hii kwa kipindi cha uongozi wangu nimefanya yafuatayo:-

• Macho
Ndugu Mwenyekiti
, katika mkoa wetu kuna tatizo moja kubwa la Mtoto wa Jicho. Gonjwa hili linasababishwa na vumbi na uzee , takwimu ya sensa ya mwaka 2001 inaonyesha kuwa Singida ina watu Laki moja kati yao asilimia 1% wana tatizo la mtoto wa jicho, hiyo ni sawa na watu 1,000.

Mwaka jana nilishirikiana na shirika lisilo la kiserikali la “Bilal Muslim Mission of Tanzania” kuwaleta wanganga wa macho walioendesha upasuaji wa macho na kutoa miwani ya bei nafuu katika hospitali yetu ya Mkoa. Mpaka sasa tumefanikiwa kufanya operation 240 na kutoa miwani kwa wenye matatizo ya macho zaidi ya 149 na ilinigharimu shilingi milioni 20. Mwaka huu natarajia tena kuleta waganga ili tufanye operation 280. Kuna msemo unaosema kuwa“ Kuona ni kuamini ” mfano, kuna mzee mmoja ambaye ni mmoja wa watu waliofanyiwa upasuaji wa macho, hakuweza kuficha furaha yake pale aliponiambia, nam-nukuu “ Mohammed, nakushukuru sana kwa huduma uliyoileta hapa, ya machonimeweza kukuona kwa macho yangu! tangu umechaguliwa kuwa mbunge nilikuwa nasikia tu sauti yako, ahsante sana ”. Hali hiyo ilinipa faraja kubwa sana na hatimaye nikaamua kutoa uamuzi wa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Hellen Killer International, tumejenga wodi ndani ya Hospitali yetu ya Mkoa kwa ajili ya kuwalaza wagonjwa watakaofanyiwa upasuaji wa Macho. Wodi hiyo nimechangia milioni 45, Hellen Killer International wametoa milioni 45, Jumla imetugharimu kiasi cha shilingi Milioni 90.


2. Malaria
Ugonjwa wa Malaria ambao umekuwa ukiendelea kushika rekodi ya kuua watoto wengi walio chini ya miaka mitano na akina mama wajawazito kwa kiwango cha juu kuliko ugonjwa mwingine wowote, takwimu zinaonyesha kuwa katika kila watoto 100 watoto watano wanapoteza maisha kwa ugonjwa wa malaria. Mh. Mwenyekiti , nimeshiriki kuhamasisha jamii juu ya matumizi ya chandarua kilichotiwa dawa na nimetoa msaada wa vyandarua zaidi ya 6,000 ndani ya vijiji vyetu 19. Vyandarua hivyo vilinigharimu Milioni 24 na nita uendeleza mpango huu wa kugawa vyandarua kwa awamu nyingine ya pili.

3. Ukimwi

Katika kukabiliana na gonjwa hatari la Ukimwi nimekuwa nikiwasiliana mara kwa mara na Wizara ya Afya ili kuona kuwa hospitali yetu ya Mkoa haikosi dawa zinazosaidia kurefusha maisha kwa waathirika wa Ukimwi na dawa hizo zinapatikana wakati wote, Napenda kuwatia moyo ndugu zangu, kuugua Ukimwi siyo mwisho wa Maisha, tusikate tamaa mapema, kuna mchezaji mmoja wa basketball anaitwa magic Johnson kwani alijitangaza kuwa ameathirika na ugonjwa ukimwi tangu mwaka 1984, leo hii ni miaka 25 tangu ajitangaze. Juzi nimemuona kwenye TV. Anaongelea mambo mbalimbali. Narudia tena kusema kwamba, ukiathirika usikate tamaa ya maisha kula vizuri, tumia vizuri dawa za kurefusha maisha na ufuate maelekezo ya madaktari kwani uitaweza kuishi kama mtu asiye athirika . Kitu muhimu kujitokeza kupima afya na kupatiwa dawa hizo.

Ni vyema akina mama wajawazito kwenda kupima afya zao ili endapo wakigundulika kuwa na ukimwi, watumie dawa kuzuia maambukizi ya virusi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Kila mtoto anayezaliwa ana haki ya kuishi, takwimu zinaonyesha kuwa dawa hizi zinasaidia watoto nane kati ya kumi kunusurika na ukimwi, hiyo ni sawa na asilimia 80.

Mh. Mwenyekiti
, mwishoni mwa mwaka jana 2008, nilimwalika aliyekuwa Balozi wa Mrekani Bwn. Mark Green kuja kutembelea Hospitali yetu ya Mkoa na kuahidi kuendeleza misaada mbalimbali hususani dawa za kurefusha maisha kwa waathirika wa virusi vya ukimwi, na dawa hizi zinapatikana katika Hospitali yetu ya Mkoa bure. Kila siku ya Alhamisi wale waliopima na kupata ushauri nasaha wanahudhuria hospitalini na kupatiwa dawa.

Ndugu Mwenyekiti,
tatizo hili la ugonjwa wa Ukimwi naomba nitoe wito kwa ndugu zetu wote wanaouguza wagonjwa wa Ukimwi, wasiwanyanyapae wala kuwatenga kwani hao ni ndugu zetu. Saidna Ally alisema namnukuu “ Kila binadamu kuishi bila mwili wake kupata maradhi anaweza kumkufuru Mungu, kwani mtu huyu anaweza kuwa na majivuno” mwenye busara huyo anatushauri kuyatazama maumivu yanayotokana na maradhi kuwa ni ibada kwa Mwenyezi Mungu na tuwe wenye subira ndipo tutakaposhinda mitihani ya kuugua na kuuguza. Jamani! kwa Waislamu na Wakristro kusubiri ni Ibada lakini nadhani ndiyo ibada ngumu zaidi, na ipo aya katika Quran Tukufu yenye kusema, INNALLAH Masswaaabriiiin, inamaanisha kuwa kila mwenye kusubiri yupo pamoja na Mwenyezi Mungu, hivyo ndugu zangu wenye kuelemewa na wagonjwa majumbani ama mahospitalini, tuyazingatie haya.
• Nimekuwa nikiwagharimia na kuwapeleka kwenye hospitali za rufaa watu mbalimbali ambao wanashindwa kukabiliana na gharama za hospitali za rufaa ndani ya wilaya yetu. Nimeshawapeleka kwenye hospital za rufaa za KCMC na Muhimbili, kwa mpango huu nimeshatumia shilingi Milioni 4,800,000/-.
• Nimekuwa nikitoa msaada wa chakula kwa wagonjwa wa Ukimwiwaliosajiliwa kwenye hospitali yetu ya Mkoa ambao kutokana na kuugua kwao uwezo wa kujitafutia mahitaji yao ya kila siku umepungua, hivyo nimeamua kujitolea kilo 60 za unga wa ngano na mchele kila siku ya Ijumaa ya kila wiki. Mpango huu mpaka sasa umegharimu shilingi Milioni 7,480,000/- kwa muda wa miaka mitatu sasa.
• Kwa kushirikiana na wananchi wa Kijiji cha MunguMaji tumejenga zahanati ya Kijiji hicho, na katika mpango huu mimi nimechangia kiasi cha shilingi 10,000,000/-. Kwani zahanati zilizopo sasa hazikidhi mahitaji ya wananchi tunao waongoza na nina mpango wa kujenga zahanati kama hiyo katika vijiji vingine. Naomba nitoe wito kwa viongozi na wananchi wa vijiji ambavyo havina zahanati waanze mchakato wa michango ya ujenzi wa zahanati.
• Nimekuwa nikijitolea chakula kila Ijumaa kwa ajili ya kuwahudumia watoto wanaoishi katika mazingira magumu waliopo katika kituo cha malezi Kititimo.

Secta ya Maji
Mh. Mwenyekiti
, kwenye secta ya Maji, kwa kipindi cha uongozi wangu nimefanya yafuatayo kwa kushirikiana na wananchi:-
• Mwaka 2006 kulikuwa na upungufu mkubwa wa maji ndani ya mji wa Singida kutokana na vyanzo vya maji kukauka, wananchi walikuwa wanalala nje kutafuta maji kwenye vioski vya maji, baada ya kuipata kero hiyo kwa wananchi niliwasiliana na uongozi wa mamlaka ya maji safi na majitaka (SUWASA) kujua kiini cha tatizo hilo, na wakanieleza kuwa tatizo kubwa ni kukauka kwa vyanzo vya maji na kusema kuwa iwapo watapata msaada wa kuwachimbia kisima kingine cha kusaidiana na visima vyao ingeweza kusaidia kupunguza tatizo lililokuwepo, nami bila kusita nilijitolea kuchimba kisima kirefu ndani ya mtandao wa SUWASA kwenye eneo la VETA ( Utemini) kisima kilichosaidia tatizo hilo kwa kiasi kikubwa, mradi ule ulinigharimu shilingi 22,000,000/-.
• Ili kuihamasisha jamii ianze mpango wa kuvuna maji ya mvua kwenye familia zao, nilijenga Tank la kuvuna maji ya mvua kwenye shule ya Dr. Salmini lenye ujazo wa lita 18,000, mpango ambao umeifanya jamii ya wanashule hiyo kuondokana na tatizo la maji kwa sasa, mradi huu ulinigharimu shilingi 18,000,000/-.
Mh. Mwenyekiti
, nimeanzisha mradi mkubwa wa uchimbaji visima virefu ndani ya Jimbo la Singida Mjini kwa kuwaleta wataalam kutafiti wingi wa maji ndani ya vijiiji vyetu, na baadhi ya mitaa yetu kazi hiyo imefanyika vizuri katika maeneno yafuatayo:-
a) Mtaa wa Manguamitogho , nimechimba kisima chenye urefu wa Mita 100 ambacho kipo tayari nimeshakabidhi na kinatumika.
b) Mtaa wa Kimpungua , nimechimba kisima chenye urefu wa Mita 70 nimeshakabidhi na kinatumika.
• Kijiji cha Unyambwa kitongoji cha Sanga , nimechimba kisima urefu wa Mita 68 ambacho nimeshakabidhi na kinatumika.
• Kijiji cha Unyambwa kitongoji cha Ipungi nimechimba kisima chenye urefu wa mita 70, nimeshakabidhi na kinatumika.
• Kijiji cha Unyambwa Kitongoji cha Mangua Mpyughu, nimechimba kisima urefu wa mita 70, ambacho nimeshakabidhi na kinatumika.
• Kijiji cha Mandewa , nimechimba kisima chenye urefu wa mita 107, ambacho nimeshakabidhi na kinatumika.
• Unyamikumbi kitongoji cha Ng'aida , nimechimba kisima chenye urefu wa mita 64 ambacho nimeshakabidhi na kinatumika kwa wananchi.
• Unyamikumbi kitongoji cha Nkhambi , nimechimba kisima chenye urefu wa Mita 40, ambacho nimeshakabidhi na kinatumika.
• Unyamikumbi ‘A' , nimechimba kisima chenye urefu wa mita 45, ambacho nimekabidhi na kinatumika.
• MunguMaji, nimechimba kisima chenye urefu wa mita 64, ambacho nimeshakabidhi na kinatumika.
• Mwankonko, kijiji cha Unyianga , nimechimba kisima chenye urefu wa mita 70 ambacho nimeshakabidhi na kinatumika
• Kijiji cha Mwankonko, nimechimba kisima kirefu chenye mita 60, ambacho nimeshakabidhi na kinatumika.
• Mtamaa ‘A' nimechimba kisima chenye urefu wa Mita 100, ambacho nimeshakabidhi na kinatumika.
• Kijiji cha Mandewa kitongoji cha Mwamtanda , nimechimba kisima chenye urefu wa mita 75, nimeshakabidhi na kinatumika.
• Kijiji cha Mandewa kitongoji cha Ititi , nimechimba kisima chenye urefu wa mita 70 ambacho nimeshakabidhi na kinatumika.
• Kijiji cha Mandewa kitongoji cha Manguanjuki , nimechimba kisima chenye urefu wa mita 60, ambacho nimeshakabidhi na kinatumika.
• Mandewa eneo la shule ya Sekondari, nimechimba kisima kirefu chenye urefu wa mita 100, ambacho nimekabidhi na kinatumika.
• Kijiji cha Mtipa, nimechimba kisima chenye urefu wa mita 60, nimeshakabidhi na kinatumika.
• Kindai mtaa wa Singida Munangi , nimechimba kisima kirefu chenye urefu wa mita 65, ambacho nimeshakabidhi na kinatumika.

Mh. Mwenyekiti
, mpaka sasa gharama ya kuchimba visima hivi pamoja na pump vimenigharimu shilingi milioni 255 na bado nitaendelea kuchimba visima vingine virefu takribani 20 ndani ya wilaya yetu. Mradi huu utanigharimu tena shilingi milioni 255. Jumla nitatumia milioni 510.
Kwa nafasi hii napenda kutoa wito kwa wananchi wa maeneno yaliyo chimbwa visima na pata kapo chimbwa waunde kamati ya uongozi maalumu ili pindi ita kapo tokea hitilafu katika visima hivyo waweze kusimamia na kutatua wao wenyewe.

3. Mh. Mwenyekiti , kuna mradi mkubwa wa maji ndani ya Wilaya yetu unaofadhiliwa na Bank ya BADEA na OPEC wenye thamani ya Bilioni Kumi na Mbili (Bilioni 12). Mradi huu utakapokamilika utabadili miundombinu yote ya Maji Safi na Maji Taka ya mji wetu wa Singida.

Nimekuwa nikiwasiliana na Wizara ya Maji kwa karibu zaidi na wamenieleza kuwa mradi huu umeshaanza kwa hatua za awali, na tangazo la kumpata mkandarasi limeshatolewa. Na hata bungeni nimewahi kuuliza swali kuhusiana na mradi huu.

Secta ya Mawasiliano

Mh. Mwenyekiti
, kwenye secta ya Mawasiliano kwa kipindi cha uongozi wangu nimefanya yafuatayo:-
• Nimeanzisha kituo cha Televisheni ambacho kimeanza kusambaza vipindi vya majaribio kwenye TV kwa channel mbalimbali kwa kutumia waya (Cable network). Kituo kitakuwa na uwezo wa kurusha vipindi zaidi ya Channel 30, na mpaka sasa kila kitu kimekamilika hatua tuliyofikia ni nzuri kwani tunafuatilia kupata leseni ya kudumu ya kurusha matangazo hayo kutoka Tume ya Mawasiliano (TCRA). Vifaa tulivyovifunga katika kituo hiki vimenigharimu kiasi cha shilingi Millioni 270,hivyo wananchi wata takiwa kuchangia gharama za uendeshaji pamoja na kuunganishwa kwenye mtandao huo kwa gharama nafuu.


Secta ya Miundo Mbinu
Mh. Mwenyekiti
, kwa kipindi cha uongozi wangu katika secta ya Miundo mbinu nimefanya yafuatayo:-
• Nimenunua na kukabidhi uongozi wa Manispaa nguzo za kisasa za taa za barabarani ambazo zimeshaweka kwenye kituo chetu cha mabasi cha Misuna na zingine zitawekwa kwenye barabara Kuu iendayo Dodoma . Nguzo hizo zilinigharimu shilingi Milioni Ishirini (T.shs 20 Million).
• Kwa kushirikiana na uogonzi wa Manispaa tumeweza kufanikisha kuletewa gari la Zima Moto katika wilaya yetu. Tatizo la kutokuwepo gari la zima moto lilikuwa kero kubwa sana kwa wananchi wa Manispaa, kero hiyo imekwisha.
• Pia nimeshawasiliana na wizara ya Nishati na Madini na wamehakikishia kuwa watasabaza umeme katika kata za Mtipa, Mwankonko, Mtamaa, Mungumaji na Unyambwa, Mh. Mwenyekiti , kama mnafuatilia vizuri, nimeshawahi hata kuuliza swali Bungeni kuhusiana na tatizo hili la umeme katika wilaya yetu, na Serikali kupitia wizara ya Nishati na Madini ilitoa majibu ya kuridhisha kuwa mpango huo wa umeme upo katika mpangilio mzuri.


Secta ya Ajira na Maendeleo ya Vijana
Mh. Mwenyekiti
, kwenye secta ya Ajira na Maendeleo ya Vijana kwa kipindi cha uongozi wangu, nimewatafutia vijana zaidi ya kumi kutoka wilayani kwetu ajira kwenye kiwanda cha nguo cha AFRITEX kilichopo Tanga. Na hata katika kampuni yangu ya Mohammed Enterprises katika suala la ajira huwa nawapa kipaumbele watu wa Singida, ndani ya kampuni hii kuna watumishi zaidi ya 400 kutoka Singida. Na bado nawasiliana na vyanzo vingine vya ajira ili niweze kuona tunakabiliana na tatizo hili mpaka tupate ufumbuzi wake, na tukifanikiwa kwa hili tutatupunguza idadi ya vijana wetu wanao maliza elimu ya sekondari kukaa vijiweni.

Secta ya Maendeleo ya Jamii
Mh. Mwenyekiti
, kwenye secta ya Maendeleo ya Jamii kwa kipindi cha uongozi wangu nimeweza kujitolea misaada mbalimbali kwenye jamii yetu kama ifuatavyo:-
• Nikiwa Diwani wa Manispaa ya Singida, nimeshirikiana na madiwani wenzagu wote wa Manispaa katika kufanikisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2005 ndani ya manispaa kwa kila kata.
• Nimetoa msaada wa baiskeli za walemavu pamoja na viti vya walemavu zaidi ya ishirini na tano (25) ndani ya wilaya yetu ambazo kwa pamoja vimenigharimu shilingi milioni saba na laki tano (T.shs. 7,500,000/-).
• Nimetoa msaada kwa vikundi vya wajasiriamali wa SIDO kiasi cha shilingi Laki Tano (T.shs 500,000/-).
• Nimetoa msaada kwa kikundi cha FARAJA Group kilichopo eneo la Kindai (CAPU) shilingi laki tano (T.shs 500,000/-).
• Nimetoa msaada wa mafunzo kwa kikundi cha akina mama wa Kisasida pamoja na kuendeleza mradi wao wa kilimo cha umwagiliaji kwa kuwanunulia vitendea kazi kwa gharama ya T.shs 2,500,000/-.
• Nimetoa Sare kwa vikundi vyote vya sanaa ndani ya wilaya yetu, na pia nimevichangia baadhi ya vikundi nauli ya kwenda Bagamoyo kwenye maonyesho mwaka jana 2008, nimekuwa nikijitolea michango ya kuimarisha Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake, mpaka sasa nimeshatumia shilingi Milioni 75,495,563/-. Mh. mwenyekiti , nimejitolea misaada mingi kwenye taasisi za dini kwa Waislamu na Wakristo kiasi cha shilingi milioni 22, ofisi yangu imepokea barua za maombi ya 5200 kutoka kwa watu binafsi na tayari zaidi ya barua 2100 zimeshajibiwa na nimesaidia milioni 26 na bado naendelea, naomba mvute subira katika hilo kwa wale mnaochelewa mniwie radhi.

Secta ya Michezo

Mh. Mwenyekiti
, kwenye sekta ya michezo katika kipindi cha uongozi wangu nimefanya yafuatayo:-
• Nilianzisha mashindano ya mpira na kunyanyua vipaji yajulikanayo kama “Mohammed Dewji Cup” yamefanikiwa vizuri mwaka jana 2008, kwani niliwapatia washiriki wake vifaa vya michezo na zawadi kwa washindi. Mashindano hayo yamenigharimu kiasi cha shilingi milioni 5,600,000/-.
• Kwa kipindi cha miaka mitatu sasa nimekuwa nikiyafadhili mashindano ya kumtafuta mrembo wa Singida (Miss Singida). Mpaka sasa imenigharimu kiasi cha Tshs.Milioni nne katika ufadhili huo.
• Nimechangia kiasi cha milioni kumi kufanikisha mashindano ya riadha yaliyofanyika kitaifa Mkoani kwetu kwenye Uwanja wa NAMFUA mwaka jana 2008.

Mh. Mwenyekiti
, nikiwa Mjumbe wa Halmashauri KUU ya CCM Taifa nilitoa ahadi ya kushirikiana na wana CCM wenzagu kujenga ofisi za chama za kata, kazi hiyo nimeshaanza kwa Mkoa mzima lakini kwa hapa kwetu Wilaya ya Singida Mjini nimeshakamilisha ujenzi huo katika kata za Kindai , Mandew a na Utemini . Mpango umenigharimu milioni 2 na utakuwa ni endelevu kwa kata zingine zilizopo kama tulivyojipanga.

Mh. Mwenyekiti
, Mafanikio haya tuliyoyapata kwa kipindi cha uongozi wangu na Serikali ya awamu ya Nne inayoongozwa na Mheshimiwa Jakayo Mrisho Kikwete ni ya wana CCM wote, kwa hiyo, hatuna budi kuyaelezea kwa wananchi tunaowaongoza kwa ufasaha ili kukabiliana na upotoshaji unaofanywa na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani.

Mh. Mwenyekiti
, na ndugu zangu viongozi wenzangu mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa, hivyo basi naomba tujipange vizuri ili tuweze kukifanya chama chetu kishinde uchaguzi huu kwa asilimia mia moja. Kwani mafanikio haya tuliyoyapata kwa kipindi cha miaka mitatu misingi yake ni uongozi wa Serikali za Mitaa yaani Vitongoji, Mitaa na Vijiji .

Mh. Mwenyekiti
na ndugu wajumbe wenzangu wa Mkutano Mkuu huu wa CCM, shughuli zote hizi za utekelezaji wa Ilani na ahadi zangu binafsi zimenigharimu zaidi ya kiasi cha shilingi Bilioni Moja na milioni mia tano. Nami nimesukumwa na moyo wa kutaka kuchangia maendeleo ndani ya Jimbo letu. Naomba nitoe wito kwa ndugu zangu wote wanaSingida walio ndani na nje ya Mkoa wetu kuchangia maendeleo ya Singida kwani bila sisi kujifunga mkanda kwa kujitolea michango ya maendeleo unafikiri ni nani atakayetuletea maendeleo hapa kwetu? kwa sasa Singida inaendelea kila siku, leo kunakojengwa kisima, kwingine wanajenga shule, wengine wanamalizia ujenzi wa zahanati na mahali pengine watu wanaanzisha vikundi vya uzalishaji mali yaani kila mahali wapo katika mchakato wa maendeleo, jamani ! ndugu zangu hamuoni kwamba Singida yetu inapaa?

SINGIDA INAPAAAA………. HAIPAI ?
Mh. Mwenyekiti
na ndugu zangu wajumbe wenzangu wa mkutano mkuu huu wa CCM napenda kuwahakikishia kuwa, mimi toka nimekuwa kwenye dhamana hii ya uongozi mlionipa hata siku moja sijawahi kuacha kuifikiria Singida, niwe hapa Singida, Bungeni au popote duniani. Nimekuwa nikitumia muda wangu mwingi kufikiria jinsi ya kushirikiana na wananchi wenzagu katika kujiletea maenndeleo endelevu. Naomba niotoe wito kwa wananchi wenzagu tujenge fikra za kuona mbele zaidi Kimaendeleo.

Mh. Mwenyekiti
na ndugu zangu wajumbe wenzagu wa Mkutano mkuu huu wa CCM, Chama Cha Mapinduzi na mimi mbunge wenu tumeahidi mambo mengi ya kimaendeleo katika jimbo letu. Na taarifa hii niliyoitoa hapa ni ya Utekelezaji wa hayo tuliyoahidi kwa kipindi cha miaka mitatu bado miaka mingine miwili inafuata. Kwa nafasi hii nawaombeni ndugu zangu wanaSingida Mjini muwe na subira kwani kuna msemo usemao “Roma Haikujengwa kwa siku moja” tunaomba ushirikiano wenu ili tuweze kufanikisha yote tuliyoahidi kwani nina amini kuwa tukidumisha upendo, mshikamno na ushirkiano kwa Singida yenye neema tele yote yawezekana. Lakini haya ndugu zangu mtambue ufanisi wake umerahisishwa na waheshimiwa, Mkuu wa Mkoa Comred Parseco Vicent Cone, Mkuu wa Wilaya Comredi Pasco Mabiti, Mkurugenzi wa Manispaa Robert Kitimbo, Msitahiki Meya Mzee Mahami, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa Mheshimiwa Joram Alute, Katibu wa Chama Mkoa Naomi Kapambala, Kamanda wa Polisi Mkoa Celina Kaluba, Mwenyekiti wa CCM Wilaya Hamis J. Ngui na Katibu wa CCM Wilaya Mama Marry J. Maziku.

Pia ningependa kuwashukuru madiwani wote kuanzia Mheshimiwa Twalib Kihara wa Ipembe, Yusuph Mwantandu wa Kindai, Ally Nkindwa wa Mughanga, Pantaleo Sorongai wa Mitunduruni, Salum Mahami wa Majengo, Shaaban Satu – Unyambwa, Said Chima – Mtipa, Hamis Ireme – Mandewa, Hamis Nkulungu – Mwankonko, Mbua Gwae – Mtamaa, Kipandwa Ipini – Unyamikumbi, Hassan Mkata – Mungumaji, Baltazari Kimario – Utemini pamoja na madiwani viti maalumu akiwemo Pili Satu, Lea Solomoni, Mwanjuma Shaha, Hadija Simba na Teddy Msuta, bila kuwashau wadau wote wa maendeleo ndani ya jimbo letu.

Pia nawashukuru wasaidizi wangu wote katika ofisi ya Mbunge Mwaduda, Esther, Miraji kwani bila timu hii kufanya kazi kwa pamoja na wanaCCM na wananchi kwa ujumla si rahisi kuyafikia mafanikio haya kama tunavyoshuhudia Singida yetu ikipaa.

Mh. mwenyekiti
na ndugu viongozi wenzagu katika kazi hizi mjue kuwa kunakupishana kwa kauli, kama kuna mtu ama kundi fulani nimewakosea katika lolote, mimi ni binadamu na kijana wenu, naomba radhi, lakini mkijua kwamba nia na dhamira yangu kuu ni kuiona Singida yetu inapaa, na kwa ushirikiano wenu mtarajie siku moja Singida inakuwa na madaktari bingwa, maprofesa, wahandisi, waalimu na wataalam mbalimbali waliobobea.

Baada ya kusema haya ndugu zangu hapa kilichobaki kuwaomba tule, tunywe, tucheze music na kufurahi kwa pamoja na leo nikiwa mwenye furaha nitatoa posho ya shilingi elfu kumi kama posho ya kikao kwa kila mjumbe. Ambayo kwa jumla itanigharimu kiasi cha shilingi milioni 21.


MUNGU IBARIKI SINGIDA
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU IBARIKI AFRIKA

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
AHSANTENI KWA KUNISIKILIZA
 
Ngoja nichukue calculator nijumlishe hizo hela alizotoa masaada !!
 
nimesoma hizo bold nimepata kitu.
Mheshimiwa anaonekana anafanya appeal kwa wapiga kura ili wamchague tena ingawa ni kweli amechangia bali pia asingepaswa kuonesha UMIMI ktk kauli zake. Namuunga mkono kwa kujitolea yeye binafsi kuchangia fedha ktk miradi ya msingi kwa maendeleo ya eneo husika. Ila tujiulize usafi wa hizo fedha (ingawa twamjua ni mfanyabiashara), kwani niwajuavyo wafanyabiashara hawawekezi mahala pasipo na faida. Je nia yake ni kusaidia kweli au anawekeza???

Namshauri mbunge angejiweka pembeni next election lakini ashiriki kumjenga mgombea (msikivu) ambaye atakuwa ni mkulima au mfanyakazi na si mfanyabiashara.
 
Ngoja nichukue calculator nijumlishe hizo hela alizotoa masaada !!

Utachoka, nimejaribu nikaachia njiani....yaani hapa nauguza kichwa, moyo na hata sura yangu iliyovimba kwa maumivu ya mawazo juu ya hili litanzania letu lilipofikishwa....tuna-outsource majukumu yote kasoro uheshimiwa tu.

Kwani kama huyu jamaa ameamua kuwa mfadhili kwanini asianzishe foundation yake halafu akawaachia wawakilishi wa wananchi kufanya majukumu ya kibunge...
 


Baada ya kusema haya ndugu zangu hapa kilichobaki kuwaomba tule, tunywe, tucheze music na kufurahi kwa pamoja na leo nikiwa mwenye furaha nitatoa posho ya shilingi elfu kumi kama posho ya kikao kwa kila mjumbe. Ambayo kwa jumla itanigharimu kiasi cha shilingi milioni 21.
Mh me nimeipenda hiii.....watz tutaendelea kununuliwa mpaka basi!!
 
Utachoka, nimejaribu nikaachia njiani....yaani hapa nauguza kichwa, moyo na hata sura yangu iliyovimba kwa maumivu ya mawazo juu ya hili litanzania letu lilipofikishwa....tuna-outsource majukumu yote kasoro uheshimiwa tu.

Kwani kama huyu jamaa ameamua kuwa mfadhili kwanini asianzishe foundation yake halafu akawaachia wawakilishi wa wananchi kufanya majukumu ya kibunge...

Give a man a fish and you feed him for a day. Teach a man to fish and you feed him for a lifetime.

Chinese Proverb


 
Mbona hasemi kwa kukifanya kiwanda cha magunia Moshi kuwa Gordown lake aliwanyima ajira vijana na wakina mama wangapi na ni shilingi ngapi hizo?
Aseme tenda ya kuingiza mchele alikwapua shilingi ngapi za walipa kodi?
Mbona haonyeshi kuwa aliwasaidia ? hivi kama kusingekuwa na njaa inamaana angefanya nini?
Wabunge wengine bwana ni vihiyo tuuu.

Kazi ya mbunge ni kusaidia wananchi kuweka miundombinu ili waweze kuzalisha na sio kusema aliwapa mahindi ya msaada wa njaa.

Alipaswa kuwasaidia wananchi wa kijiji cha kisasida kulipwa fidia zao ambazo kampuni la East Africa Power poll ltd wamegoma kuwalipa , na wangelipwa wangeweza kununua chakula wenyewe.
 
Jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni....Hakuna uthibitisho wa ufisadi kwa Mo so far! Kwa hiyo moyo huo wa kusaidia jimbo lake ni wa kusifiwa na kuigwa. Au mnataka tuwe na wabunge wanaolala usingizi bungeni hawachangii hoja, na wanakuja jimboni wakati wa uchaguzi tu? Tena kwa rushwa za shilingi 2,000 kwa kila mpiga kura?

Anawekeza kwenye elimu wa wapiga kura wake kwa kuwajengea miundombinu bora ya elimu na pia analipia ada za shule za watoto wasio na uwezo! What else do you want for a member of parliament? Au kwa sababu ni mbunge wa CCM? Angekuwa kafanya haya yote Dr. Slaa au Zitto Kabwe zingepigwa kampeni kwamba anafaa kuwa hata rais!
 
Asiwatishe cha mtoto tu hicho. Subirini vitu vya Mbunge wa Hai Mh Freeman Mbowe mwakani, atamwaga ma air ambulance na kumbi za disco (zenye hadhi sawa na Bilicanas) kila kijiji!
 
msaada kutoka hifadhi ya Taifa ya chakula (SGR), ilibidi mimi mbunge wenu pamoja na kuiomba serikali ilete chakula cha bei nafuu lakini pia nilijitolea tani mia moja za mahindi zenye thamani ya Shilingi Millioni Arobaini kwa wakati huo (T.shs.40,000,000/-).

KAMA KUSINGEKUWA NA NJAA ANGEFANYA NINI?
ASITAKE ADVANTAGE YA NJAA....KWANZA NI VIBAYA KUTANGAZA KUWA KAMA KIONGOZI ULIWAPA WANANCHI CHAKULA.

tokana na janga hilo mahudhurio ya wanafunzi darasani yakadorora, hivyo kama mbunge wa jimbo kwa kushirikiana na wenzangu tukaamua kutoa unga wa uji kwa shule zote za Msingi zilizoko ndani ya manispaa ya Singida kwa miezi minne mfululizo. Unga huo uligharimu takribani Millioni Thelathini (T.shs. 30,000,000/-).

ANGEWASAIDIA KUPATA MASHINE ZA UMWAGILIAJI TANGU 2005 LEO WASINGEKOSA CHAKULA.
 
Asiwatishe cha mtoto tu hicho. Subirini vitu vya Mbunge wa Hai Mh Freeman Mbowe mwakani, atamwaga ma air ambulance na kumbi za disco (zenye hadhi sawa na Bilicanas) kila kijiji!
Umeambiwa kuwa tatizo la wananchi wa Hai ni ambulance?
Umeambiwa kuwa wanataka kucheza disco? na wakitaka kumbi zipo nenda Bomangombe utakuta kumbi za kisasa kabisa.

Kumbe Bills ni ya kisasa hata wewe umekubali?
 
Hiyo hotuba ya tangu mwezi wa 4 inaletwa leo ,kampeni zimeshaanza?
 
Ningekuwa ni miongoni mwa hao wanaosikiliza hiyo hotuba ningeondoka mapema! Huyu Jamaa nadhani atakuwa Mbunge wa maisha hapo ukizingatia wapiga kura wake ni omba omba na wavivu kila mwaka wana njaa! wanajua MO yupo
 
Hongera Mh. Dewji! Mambo kama haya hii ndiyo wapiga kura wanataka kusikia siyo "mafanikio" ya kusaidia kupitisha Miswada na Sheria za Ruzuku na Madini bungeni (Ordinary folks don't relate to such crap)
 
HOTUBA YA MHESHIMIWA MOHAMMED DEWJI YA MKUTANO MKUU WA CCM WILAYA YA SINGIDA MJINI TEREHE 25/04/2009

hakuna haja ya kujadili leo,imepitwa na wakati hii.
 
Sioni kama alichofanya ni kibaya kwani ametatua matatizo ya kimsingi katika kuwawezesha wananchi wake kujiendeleza. Ametatua ya dharura (chakula cha msaada) na ya long-term (elimu, maji na afya). Kilichopo ni wananchi wamsaidie kutunza visima vya maji na watumie fursa hiyo kuwapeleka watoto wao kwenye shule hizo za upili. Naamini baadaye familia kadhaa zitanufaika na long-term investment ya Mheshimiwa huyu. Labda kwa nyongeza aibane serikali ktk huduma ambazo anaona hawezi ku-walk alone.
 
JK unayokazi kuwaondoa wafanyabiashara. Hakika ni kazi kubwa. MO ameishaanza kununua wajumbe sasa wewe na agenda yako ya kutenganisha biashara na siasa sijui kama itafanikiwa. Bado 2010 tutaona na tutasikia mengi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom