Hotuba ya Mhe Moh Dewji: April 25, 2009

Umetoa mfano wa Bloomberg. NYC ina matatizo mengi sana ya kifedha, mwaka jana kwa mfano, hela ya kusafisha snow iliisha kabla ya wakati, walimu wanakimbia inner city schools kwa sababu hawalipwi vizuri, police wengine wa NY wanaondoka kwenda PD za miji ya jirani wanakolipwa vizuri zaidi. Yote haya ni matatizo ambayo Bloomberg angeyatatua kwa kutoa tu hata robo ya utajiri wake lakini hajafanya hivyo, kwa sababu siyo njia muafaka ya kutatua tatizo. Leo MO anajenga mashule, mahospitali, visima nk, ikitokea akaamua kutogembea tena, au kushindwa uchaguzi na akaja mbunge hohehahe itakuwaje?
Dawa ni kufanya kazi bungeni kama alivyoomba kura kuwakilisha wananchi. Yeye si fisadi, lakini atunge sheria kwamba hela zote zilizoibwa na akina Chenge zirudishwe na mikataba mbali mbali ya kifisadi isainiwe upya. Akifanya hivyo zitapatikana hela nyingi za kujenga shule, barabara, visima na mahospitali na yeye hatatoa hela mfukoni mwake, badala yake hela zake atatanua biashara zake zaidi, ataajiri watu wengi zaidi na atalipa kodi zaidi. hivi ndivyo atakavyoleta maendeleo.

Kwame:

Matatizo yako, unalinganisha matango na ubuyu. Sheria za nchi zinazoweza kuwafunga Chenge na mafisadi wengine zipo. Kinachoshindikana ni ufuatiliaji wa sheria hizo. Na hilo sio suala la mbunge. Ni swala na vyombo vinavyosimamia sheria.

Sheria za nchi ambazo zinaweza kufunga jela mwizi wa kuku kwanini zisiweze kumfunga Chenge? Hapa haiitajiki sheria mpya. Huu ni ukosefu wa nidhamu za kiutawala ambazo zinafanya sheria zitumike kwa wanyonge tu. Lakini walionacho wakifanya makosa, wanapeta.

Hivyo basi hata kama sheria mpya zitatungwa, hakuna kitakachosaidia iwapo watu watakuwa hawana nidhamu.
 
Balantanda said:
Basi si vizuri kumhusisha Mohammed na tuhuma hizi(kuziweka tuhuma hizi kwenye habari hii ni sawa na kumhusisha moja kwa moja na tuhuma hizi) maana kipindi zinatokea dogo alikuwa zake shule na kampuni(kama sikosei) ilikuwa chini ya baba yake mzee Ghulam Dewji,kumhusisha Mohammed na tuhuma hizi ni kumuonea tu...Cha msingi ni kumpongeza kwa haya aliyowafanyia wananchi wake,ni tofauti kabisa na wabubge wengi(hasa wa CCM)

Balantanda,

..tayari nimeshampongeza Mheshimiwa Mohamed kwa juhudi na michango yake.

..lakini baada ya kumpongeza ndiyo nikakumbuka haya mambo ya michele mibovu.

..ni vigumu kutofautisha kati ya kampuni na wenye kampuni. naweza kukubaliana na wewe kwamba Mo alikuwa shuleni miaka ya 90, lakini kampuni anayoiongoza sasa hivi ni hiyohiyo iliyokuwa ikituhumiwa wakati ule.

..I am trying to find the facts, na inawezekana kabisa zinaweza kuisafisha kampuni ya mheshimiwa mbunge.

NB:

..kuna makampuni leo hii yanachunguzwa kwa kushirikiana na Nazi Germans in the 40s.
 
Nimekusoma mkuu...Pamoja
 
Bill Gates hakutaka kuzitumia haki zake za kiraia lakini sio kweli kuwa utajiri wake umemkataza kuingia kwenye siasa.

Zakumi, Zakumi, Zakumi nani kasema utajiri wa Bill Gates umemkataza kuingia kwenye siasa. Yeye ameamua kuutumia utajiri wake kuwawezesha wasio na uwezo bila malipo kama ya kupewa cheo tofauti na huyu Dewji anayeutafuta ubunge kulinda biashara zake. Pesa anazozitoa kutoka mfukoni mwake akiwa mbunge na mfanya biashara ni aina nyingine ya uwekezaji - kuna namna atazirudisha tu, huo ndio ukweli.

Mayor wa New York City ni Billionare na ni mwanasiasa. Hivyo utajiri haumnyimi mtu haki zake za kikatiba.

Zakumi, Zakumi, Zakumi Mayor wa New York hawezi kutoa hela mfukoni mwake kutatua matatizo ya wana New York kwa mipango ya zimamoto. Wana New York wanalipa kodi na wanataka kuona kodi zao zinatumika ipasavyo kama ilivyopangwa. Mayor wa New York analipa kodi na vyanzo vya mapato yake viko wazi kwa yeyote anayetaka kujua. Duh, Zakumi wewe ni Mtanzania kweli kweli.
 
Mag3,
Sidhani kama Zakumi kasema hivyo. nachoelewa mimi kasema Bill Gate anaweza kuingia Siasa akipenda! hapendi kuingia siasa hayo ni maamuzi yake hakuna sheria inayomzuia..Hata hivyo wapo matajiri wengine wakubwa US wameingia siasa...na wanavuta tu hela za walipa kodi. Mo sii tajiri mkubwa ranked 1, nchini kumfananisha na Bill wa duani nzima.. Kisha tunachomsifia ni kwamba wapo matajiri wakubwa kuliko yeye Tanzania na wengine ni wanasiasa lakini wameshindwa kufanya hata robo ya kile alichofanya..
Huyu ndio mwanasiasa tunayemhitaji sisi, Mtu ambaye yupo tayari kugawa Utajiri wake kuwawekea wananchi vyanzo muhimu vya maendeleo yao japo sii makubwa hivyo..Rostam na kina patel ni matajiri kuliko Mo mara 10 lakini ndio kwanza wanatafuta kutumaliza zaidi..Vingozi wengine ndio kwanza wanataka tugawane umaskini kama mirathi ya nyumba za Kariakoo..matokeo yake familia nzima inarudi ktk umaskini kuliko hata hali waliyokuwa nayo zamani..
Jamani mpeni sifa zake
 
Zakumi, Zakumi, Zakumi nani kasema utajiri wa Bill Gates umemkataza kuingia kwenye siasa. Yeye ameamua kuutumia utajiri wake kuwawezesha wasio na uwezo bila malipo kama ya kupewa cheo tofauti na huyu Dewji anayeutafuta ubunge kulinda biashara zake. Pesa anazozitoa kutoka mfukoni mwake akiwa mbunge na mfanya biashara ni aina nyingine ya uwekezaji - kuna namna atazirudisha tu, huo ndio ukweli.

Zakumi, Zakumi, Zakumi Mayor wa New York hawezi kutoa hela mfukoni mwake kutatua matatizo ya wana New York kwa mipango ya zimamoto. Wana New York wanalipa kodi na wanataka kuona kodi zao zinatumika ipasavyo kama ilivyopangwa. Mayor wa New York analipa kodi na vyanzo vya mapato yake viko wazi kwa yeyote anayetaka kujua. Duh, Zakumi wewe ni Mtanzania kweli kweli.

Mag3:

Nchi inaongozwa na katiba na sheria. Naona mnamuhukumu ndugu Dewji bila kuangalia kuwa kavunja katiba au katiba ya nchi.

Katiba ya nchi inampa mtanzania mwenye profession yoyote ikiwemo kufanya biashara kugombea nafasi za uongozi.

Sheria za mtu hazimkatazi mtu kutumia mapato yake kwa shughuli za maendeleo ya nchi hata kama matumizi hayo yatakuwa ni kujifagilia.

Na tukirudi kwenye Mayor ya NY, Jamaa alitumia 200 Millioni USD kwenye kampeni.

Na wafanyabiashara wengi kukwepa tax hapa Marekani, pesa zao wanatoa kwenye huduma za jamii.

Nakuomba toa hukumu kwa mtu kwa kufuata misingi ya sheria na katiba na sio hisia zako.
 
Kama ametayayarishishiwa na watu fulani,kwa alivyo awezi fanya mwenyewe taarifa hii-lakini ni mfana wa kuigwa Mahanga tupe yako uliyafanya Ukonga.
 
Duh, jamani lakini mkuu wangu anatisha!.. kuwa na fedha au tajiri sii sababu ya kufanya yote haya ni MOYO wa kuipenda nchi na wananchi wako.

Angekuwa anawapenda wananchi wake asingeweza kujiingiza kwenye biashara ya kuagiza chakula kibovu ambacho hakifai kwa matumizi ya binadam. Wenye kumbukumbu watakumbuka kwamba aliwahi kuingia kwenye kashfa hiyo na kibaya zaidi mashahidi wote muhimu walipotea mmoja baada ya mwingine na kesi ikaisha. Kwa anayetaka details aende ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali aulizie.

Ni mfanya biashara, yuko hapo anafanya biashara na kulinda maslahi yake. Kwa kitendo cha kuwa Mbunge anakuwa na access ya kumuona Waziri yeyote na hata akitaka kwenda Ikulu kuonana na Mkulu anaweza kupata access kirahisi ukilinganisha na akiwa mfanya biashara wa kawaida tu.

Hivi kuna mfanya biashara anaweza kumwaga hela zote hizo bure bure tu, kisa eti anawapenda wananchi wake? Mbona mishahara ya wafanyakazi wa Kampuni yake ni duni? Angeanzia kuboresha mishahara ya wafanyakazi wake ambao wanamzalishia ndipo aende kumwaga hizo hela.

Mwisho kabisa, hakuna ambaye anaweza kuverify kwamba vitu alivyofanya vina thamani ya fedha hizo alizoandika, Wengi wamekuwa waki-inflate bei ya vitu wanavyochangia ili waonekane wamechangia hela nyingi sana na kumbe ni utapeli mtupu. Kuna kipindi tuliwahi kuletea news kutoka kwenye gazeti kwamba dawati moja lina gharimu shilingi laki 4! Kwa kutumia mbao za kutoka wapi? Sana sana mbao zinazohitajika ni 2 au 3, ambazo haziwezi kufika shilingi laki moja na ufundi bei ya dawati haiwezi kuvuka laki moja na nusu, hata kama hilo dawati limechongwa Dar.
 
Keil,
Kula tano mwanawasu. Naona huyu mbunge anatanguliza hela kwanza.
Yaani ni lazima ataje ametumia fedha ngapi kusaidia na kuwakarimia
watu wake?Na kama sote tutaingiwa na kasumba ya kuwaona watu kama hawa kuwa ni wakombozi na muhimu katika siasa zetu basi nchi imekwisha.
 
Keil, hizi ni tuhuma hata kama ingekuwa yeye kaingiza nchini, huyo Mkemia alikuwa wapi kuzuia chakula hicho kisiingie. Hii habari hata Bakhresa aliwahi shutumiwa na ngano wakati hakuna sheria wala wahusika wanaoweza kuwa responsible.

Wewe umewahi kuagiza mali toka nje?..Mkuu wangununaweza agiza mchele leo hii toka Thailand au India ukabambikwa ulooza. Marekani na wajuzi wa kila sheria wenyewe waliingiza maziwa ya watoto ambayo hayafai kwa matumizi ya binadamu. lakini tazama tofauti baina yetu. Wenzetu hawakuishtaki kampuni iloingizxa mali hiyo bali walifuatilia chanzo cha mzigo huo hadi kutambua ni China na kuna kundi la watu waliokuwa wakifanya mchezo huo... Mchina hakuwakawiza kawapa hukumu ya Kifo..imetafutwa source na sii kuvamia kesi maadam jamaa ni tajiri basi tumkamue.

Hivyo Mo yeye ni muagizaji ambaye mali yake ilitakiwa kuzuiwa pale bandarini na uchunguzi ufanyike na sii kumhukumu yeye kama ameagiza mali isiyofaa pasipo kuwa na ushahidi huo. Kwanza pa kufuatilia ni wapi mali ile imetoka na shirika gani linafanya biashara hiyo haramu nasii kkurukia gari moshi kwa mbele. Ndio maana uagizaji mali nchi bado tunaletewa mali isiyofaa kabisa kwa matumizi ya binadamu.

Huyo mkemia atasema anavyotaka lakini ndiye asiyeweza kazi yake.. NI mtu alotakiwa kufukuzwa kazi kwani wakati wa sakata hili mali zote nchini zilikuwa zinaingia feki na mbovu toka madawa hadi chakula..Ni majuzi tu serikali kwa msisitizo mkubwa toka juu ndio wamevamia maduka ya watu na kukusanya mali za kijinga kijinga (feki) toka kwa walalahoi na sio kufuatilia swala la Madwa na vyakula. Mkuu wangu hadi leo hii tunavyozungumza vyakula vingi ktk supermarkets nchini ni expired product ambazo wafanya biashara baada ya muda kupita kugongesha mhuri mpya..Just in case na they get away with it!..Nakupa haswa dataz za wabangaizaji mjini mkuu wangu hakuna cha Mkemia wala baba yake mkemia.. Huyo Mkemia alikufa kwa kihorohoro cha kesi iliyokuwa ikimkabiri yeye mwenyewe..
 
Ngoja nichukue calculator nijumlishe hizo hela alizotoa masaada !!

ukishajumlisha na kupata jibu lake toa $25m ya kodi ya edible oil ambayo hajalipa.
jibu lake ndio faida ya ubunge wake

hizo hela ukipiga mahesabu ametumia 1.6bil ambayo ni sawa na $1.3m kwa hiyo ukitoa unapata $23.7m.
 
Hawa waheshimiwa CV zao kwa sasa zimeleta mushikeli ndani ya nchi hii kwahiyo hata wakitoa kitu tunajua kwamba wanaturudishia kile kidogo chetu.
 
Adaiwe vipi tax ikiwa mliweka exemption!
hakupewa exemption babu ila kwa ajili yeye ni mchangiaji mkubwa ndani ya ccm basi kodi halipi
siwezi kuamini bob unatetea peanuts huku ukiibiwa mahela kibao
hizo ndio faida anazozipata za kuchangia na kuwa mmbunge
 
Nifahamishe mkuu, navyojua mimi mafuta yalifutwa kodi na serikali kuingia mkataba na mashirika yote ya mafuta, hivyo najaribu kuelewa hoja yako!
 
So jibu unalo kuwa ni za ufisadi ama???.Kaka/dada unaijua vizuri kampuni ya Mohammed Enterprises??
Inajulikana kama kampuni iliyojaa harufu ya damu ay Watanzania.

HOTUBA YA MHESHIMIWA MOHAMMED DEWJI YA MKUTANO MKUU WA CCM WILAYA YA SINGIDA MJINI TEREHE 25/04/2009

hakuna haja ya kujadili leo,imepitwa na wakati hii.
Habari usiyoijua ni mpya. Nikimaanisha kuwa kama ulikuwa unalifamu hili ungekuwa umeshaliweka hapa siku nyingi.
..lakini hawa Mohamed Enterprise si walikuwa wanatuhumiwa kuingiza na kuuza mchele mbovu nchini?

..nakumbuka kulikuwa na mjadala mkali sana bungeni miaka ile. hivi mmesahau maelezo ya mheshimiwa Semindu Kisange Pawa bungeni kuhusu mchele wa Mohamed Enterprise?

..halafu kuna kifo cha Dr.Fupi, aliyekuwa Mkemia Mkuu wa serikali wakati ule. wako wanaodai kifo chake kilitokana na maamuzi yake kuhusu sakata ya mchele huo mbovu.

..hivi kuna anayefahamu kesi ile ilikwisha ktk mazingira yapi?

Mh... Pesa zote hizi kazitoa wapi?! Kama siyo za ufisadi????

Siyo hilo tu hata ile ilikuwa ikiitwa sukari kijiko kimoja ilikuwa ni kashfa kubwa tu lakini kwa sababu ni Tanzania Rupia ilipenyezwa mambo yakamalizwa kimyakimya. Kwa wasiofahamu ni kwamba ile sukari ilichanganywa na kemikali fulani kuiongezea utamu. Waliotoboa siri sasa hivi wako futi saba chini ya ardhi. Pia kuna mkemia Mashimba naye alipotezwa sikumbulki kama ndiye huyo Fupi.
Jokakuu:

Kulikuwa na kesi moja kuhusu unga wa ngano uliooza. Kesi hii ilikwenda kwa Mrema na bungeni. Kwenye kesi hiyo Mohamed enterprise ilikuwa victim ya extortion ya tapeli mmoja ambaye nina undugu naye. Siwezi kutoa details zaidi kwa sababu zangu mwenyewe.

Kama unayozungumzia hiyo kesi, basi kuna mambo mengi sana yalikuwemo. Lakini utapeli ulitia chumvi kwa kiasi fulani.
Unakiri au unakataa?
Zakumi,Balantanda,

..I dont remember the exact details, lakini suala la Mohamed Enterprise lilifika mpaka Bungeni.

..Wabunge machachari kama Semindu Kisange Pawa walikuwa mstari wa mbele kufuatilia suala la uingizwaji nchini wa mchele mbovu.

..pia kulikuwa na kesi mahakamani, na inasemekana mashahidi kama watano hivi walikufa kabla hawajatoa ushahidi wao. Mkemia Mkuu wa serikali, Dr.Fupi naye alifariki, na kuna watu wanahisi alifanyiwa kitu mbaya.

..Jamii Forums ni jungu kuu hili, kwa hiyo nahisi kwamba tunaweza kupata ukweli wa kilichojiri wakati wa sakata/kashfa ile.

NB:

..kashfa hii ilitokea miaka ya 1990 -- 1994.
Wenye masikio yakusikia na wasikie

WeBalantanda,

..tayari nimeshampongeza Mheshimiwa Mohamed kwa juhudi na michango yake.

..lakini baada ya kumpongeza ndiyo nikakumbuka haya mambo ya michele mibovu.

..ni vigumu kutofautisha kati ya kampuni na wenye kampuni. naweza kukubaliana na wewe kwamba Mo alikuwa shuleni miaka ya 90, lakini kampuni anayoiongoza sasa hivi ni hiyohiyo iliyokuwa ikituhumiwa wakati ule.

..I am trying to find the facts, na inawezekana kabisa zinaweza kuisafisha kampuni ya mheshimiwa mbunge.

NB:

..kuna makampuni leo hii yanachunguzwa kwa kushirikiana na Nazi Germans in the 40s.

Huyo mkemia atasema anavyotaka lakini ndiye asiyeweza kazi yake.. NI mtu alotakiwa kufukuzwa kazi kwani wakati wa sakata hili mali zote nchini zilikuwa zinaingia feki na mbovu toka madawa hadi chakula..Ni majuzi tu serikali kwa msisitizo mkubwa toka juu ndio wamevamia maduka ya watu na kukusanya mali za kijinga kijinga (feki) toka kwa walalahoi na sio kufuatilia swala la Madwa na vyakula. Mkuu wangu hadi leo hii tunavyozungumza vyakula vingi ktk supermarkets nchini ni expired product ambazo wafanya biashara baada ya muda kupita kugongesha mhuri mpya..Just in case na they get away with it!..Nakupa haswa dataz za wabangaizaji mjini mkuu wangu hakuna cha Mkemia wala baba yake mkemia.. Huyo Mkemia alikufa kwa kihorohoro cha kesi iliyokuwa ikimkabiri yeye mwenyewe..
Mkandara,
Does another wrong right the other. Huyo mkemia alikufa kwa kesi gani gani vile?

Hawa waheshimiwa CV zao kwa sasa zimeleta mushikeli ndani ya nchi hii kwahiyo hata wakitoa kitu tunajua kwamba wanaturudishia kile kidogo chetu.

Hayo maneno. Ni kama RA anavyotaka kutuuzia mitambo ya DOWANS ambayo alaituibia hela zetu ati tu kwa sababu hakuna umeme.
 
Mkandara,
Does another wrong right the other. Huyo mkemia alikufa kwa kesi gani gani vile?
Mkuu unajua mimi habari za udaku siziwezi, nimeandika hivyo kwa sababu sioni la maana hapa. Kama wewe unaujua ukweli weka wazi.
Hizi habari ya sukari nusu ziweke wazi tupate kuona MO anahusika vipi maanake issue hapa isiwe yeye ila kile alichikifanya ndicho kieleze tabia ya biashara ya mtu huyu kufikia kuitwa fisadi na Ubunge kauchukua ili kuweka mambo yake karibu na Ikulu..
Nachofahamu mimi MO yupo na watu wengi sana hata kabla ya Ubunge, na anaweza fanya biashara zake pasipo kuwa mbunge wala kusaidia wananchi wa jimbo lake. Sioni connection ya Ubunge na madai yote haya ya kipuuzi..Hajaua mtu ila kama kweli wewe unao ukweli ubandike hapa sisi sote tuna machungu na mafisadi..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom