Hotuba ya MB-Nassari (CHADEMA) baada ya kutangazwa imeliza wengi

Hongera kijana mwenzetu Nassari kwa kuwa nauthubutu na kumtanguliza mungu mbele hakika ushindi wako unamaana sana kwa watanzania na vijana. Tunakuomba ukawe sauti ya vijana na masikini wote wa nchi ili tunapokuona wewe tujione cc.
Bravo chadema
Mkuu wangu maneno yako ni hekima sana. Maelfu ya wananchi wa Meru walioshiriki uchaguzi jana na kumchagua Nasari na kuhakikisha hakuna hila wa hujuma inafanyika kuwakosesha ushindi ni wananchi masikini kama familia ya Joshua Nasari ilivyo! Naomba usisahau ulipotoka,watumikie wananchi wa Meru kwa nguvu zako zote! Hongera CDM na Watanzania wapenda haki wote.
 
msione simba amerowa mkadhani kafa, tumejihakiki na tunaendelea kujitathmini kuangalia mapungufu yetu.


tunajipanga tena kwa haraka sana. na msitarajie mteremko asilani

CCM bado iko imara na bado ina uwezo wa kukamata dola kwaa miaka kadhaa
 
Dogo Nasari furahia ushindi lakini ujue kwamba ubunge si lelemama.

Hatutarajii uige ya kule Arusha Mjini ya kujipeleka gereza la Kisongo na kupoteza muda wetu.

Pia upuuzi wa maandamano Arumeru mwiko, tuko bize na shughuli zetu za maendeleo. Usijaribu kutuvugua.

Tunadai ututatulie kero zetu fasta kama ulivyoahidi, vinginevyo 2015 inakula kwako kwani tutakupiga chini bila huruma.



anza na mafisadi wenzako wanaojambia viti vya bunge kwa kulala lala hovyo na kudai posho. idiot
 
Mungu bariki Magamba ili wajitambue wasituingize katika machafuko pale dola itakapokuwa inawaponyoka kwa nguvu ya umma
 
Ni vizuri kuwa kijana mwenzetu kuchaguliwa kuwa mbunge. Lakini jamani naomba niwakumbushe kuwa this does not mean everything is ok kwa vijana na wanamageuzi wengine. Lazima tujue kwa kila kijana na mwanamageuzi kama nasari ambaye amepata nafasi ya kutuwakilisha bungeni, maelfu wamekosa hiyo nafasi hata kama walisitahili. Kwa hiyo mambo yasichukuliwe kama yako shwari. Nawasilisha
Hao maelfu ni akina nani na walikuwa wapi? Kwa nini mambo yasiwe shwari? Mbona nahisi kama ulikuwa na kitu kizuri cha kusema lakini umeshindwa kujieleza? hebu fafanua mawazo yako basi!
 
Mungu akubariki kijana wetu nassari lakini kumbuka hatunabudi kuwa makini na tusiwe wepesi kumlaumu pale ahadi zake zitaposhindwa kutimizwa kwa wakati maana viongozi wote na mawaziri wote wa serikali waliofika arumeru walisema akishinda nassari watamnyima ushirikiano na watachelewesha maendeleo.mungu ibariki tanzania
 
anza na mafisadi wenzako wanaojambia viti vya bunge kwa kulala lala hovyo na kudai posho. idiot

Acha bangi wewe, huna hoja zingine isipokuwa kutukana!

Dogo lazima tumpe laivu nini tunataka, siyo baadaye atuletee ya kuleta.
 
"Tulianza na Mungu na Tunamaliza na Mungu...Sio tu kwa kura peke yake bali tutafanya hivyo hata kwa masuala ya maendeleo pia"
 
Kauri za aina hii uwa hazina vipingamizi wala vikwazo !!!!!!!!!!!!
 
Ndiyogi nadhani hujaelewa kaka. Mungu yupo na ndo injini katika nguvu ya umma. 2015 Tanaanza naye na kumaliza naye.Mungu ndiye aliyetupa hekima na busara katika kampeni,ujasiri wa kulinda kura na kujua hila za zote za wizi wa kura
 
Usicheze na mtoto wa mchungaji, kila kitu kimebarikiwa ndani ya hiki chama. Ndo maana vijana wamepokea upako na kuwezeshwa kulinda kura zao......Sauti ya watu ........nguvu ya umma .........
 
Tuwekee basi hio hutuba kwa urefu ya Mh Mbunge baada ya kutangazwa kua yy ndio mshindi,tuone jinsi ilivyo athiri nyoyo za wapenda mageuzi TZ,kwa maneno hayo tu machache ulio yaandika mbona sioni kama yana msisimko wowote kiasi cha kumtoa mto machozi?au ndugu yangu mapenzi yamekuzidi?maana jicho la kupenda halioni kasoro
 
Back
Top Bottom