Operesheni Haki ya CHADEMA, Hotuba ya Mbowe Mwanza, na Uharaka wa Katiba Mpya: Hoja za Mbowe zinabeba ukweli kiasi gani?

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,021
2,479
1626775636792.png

Jana, tarehe 19 Julai 2021, Mwenyekliti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe, aliongea na waandishi wa habari mjini Mwanza.

Katika kikao hicho Mbowe alilaani vikali uamuzi wa Jeshila Polisi mkoani Mwanza wa kuvunja kongamano la Katiba Mpya lililokuwa limeandaliwa na Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) ili lifanyike mkoani humo tarehe 18 JUlai 2021.

Baadaye, Mbowe aliongea kwa kirefu juu ya umantiki wa hoja ya Chadema kudai kwamba, kwa sasa, utengenezaji wa Katiba Mpya unapaswa kuwa kipaumbele namba moja ndani ya Tanzania, bila kujali ukweli kwamba ajenda ya Katiba Mpya ilikuwa sio ajenda ya chama tawala (CCM) au hapana.

Kwa ufupi, hoja ya Mbowe inao muundo ufuatao:

  1. Kama Katiba ya nchi tuliyo nayo isingekuwa na ubovu CCM wasingeweza kuitumia kuiba uchaguzi mkuu wa 2020, na hivyo kuinyima Chadema nafasi ya kuunda serikali ambayo ingekamilisha mchalato wa katiba mpya;
  2. Lakini, Katiba ya nchi tuliyo nayo inao ubovu uliowaruhusu CCM kuiba uchaguzi mkuu wa 2020 na kuunda serikali isiyo na uhalali wa kidemokrasia, na ambayo kwa Sasa inaongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan;
  3. Kwa hiyo, kutokana na ubovu wa Katiba ya sasa, Chadema haikuweza kupata fursa ya kuunda serikali ambayo ingeweka mipango ya kiserikali kwa ajili ya kutekeleza ajenda zilizokuwa kwenye Ilani yake ya 2020 ,ikiwemo kutekeleza ajenda ya kuundwa kwa Katiba Mpya;
  4. Lakini, kusudi serikali ya awamu ya saba iwe ni serikali ya Chadema, kunahitajika Katiba Mpya kabla ya uchaguzi mkuu ujao wa 2025;
  5. Kwa hiyo, kusudi Chadema iweze kuunda serikali ya awamu ya saba, viongozi na wanachama wa Chadema wanapaswa kutumia fursa za kikatiba na kisheria zilizopo ilikuendesha makongamano, mikutano ya hadhara, na maandamano kwa ajili ya kushinikiza utengenezwaji wa Katiba Mpya kabla ya uchaguzi mkuu ujao mwaka 2025.

Zifuatazo ni nukuu muhimu nilizozichukua kutoka kwenye vipande vya video nilivyovikusanya kutoka mitandao ya kijamii.

Nukuu hizi zinafafanua hoja ya Mbowe kuhusu umuhimu na uharaka wa Katiba Mpya,kama ilivyofupishwa hapo juu.

Baadaye, kupitia bandiko linalojitegemea, nakusudia kuhakiki hoja ya Mbowe, lakini kwanza nataka kuiweka bayana hapa chini,kupitia bandiko hili.


=========MWANZO WA NUKUU========

"Kuna siku itafika tipping point ... Kinachotokea South Africa ndio mtakiona Tanzania"
Watu wanadai Katiba. Ni kwa sababu inahusu maisha ya watu. Rais [Samia Suluhu Hassan] anaita chokochoko.

Na sasa wameibuka viongozi wa ajabu,mfano DC wa Ilemela aliita waandishi wa habari kuwaambia kuwa haruhusu mikutano ya hadhara wilayani kwake.

Kuna DC mmoja wa Ikunga anasema 'sitaki kuona mijadala ya Katiba wilayani kwangu.' Wewe una Wilaya yako?

Tutambue kuwa Katiba tunayoipigania sio Katiba ya Chadema. Ni Katiba ya Taifa letu. Ni kuitengeneza kesho yetu iliyo bora Zaidi.

Ni kulitengeneza Taifa lenye utengamano na kuachana na watu wachache ambao wanafanya maamuzi ya kuumiza watu milioni sitini na hawaoni hofu yoyote.

Ni katiba ambayo itaweka mipaka ya viongozi wetu kujua kwamba wana miiko na wana mipaka katika kutumia madaraka yao ya kiofisi.

Ni katiba ambayo [kwayo] jeshi la polisi linapaswa kujua kwamba linapaswa litoe huduma ya usalama kwa wananchi na sio jeshi la kupiga na kuwaumiza wananchi.

Wengine wana… wanatumiwa, kuna… kuna vikundi vinatumiwa kwenye mitandao. Vingine vinalipwa shilingi elfu tano tano na chama cha mapinduzi.

Vinataka eti kupiga propaganda, eeeh tozo mpya miamala ya simu, na katiba mpya sio priority (kipaumbele) ya CCM, ooh Katiba Mpya ni priority (kipaumbele) ya wapinzani, sio ya chama cha mapinduzi, ooh Katiba mpya haitusaidii kupata maji.

Ukiona mtu ana argument (hoja) ya namna hiyo jua huyo mtu ni mufilisi wa uelewa. Mtu ambaye haoni relevance (umuhimu), haoni mahusiano ya Katiba na maendeleo ya uchumi wa nchi, huyo mtu ni nincompoop, yaani ni mtu mbumbumbu.

[Hizi] ndio hoja dhaifu ambazo CCM wanazi-float (wanaziibua). Wanafikiri hoja ya Katiba ni hoja ya Mbowe ama hoja ya Chadema. Hii ni hoja ya Watanzania ambayo ilisimamiwa na Mzee Sinde Warioba.

Tulivunja Bunge la Katiba mwaka 2014/15 kwa sababu CCM waligeuza mapendekezo ya Warioba wakayakataa, wakaleta Katiba yao ambayo inataka matakwa ya chama chao, na sio matakwa ya wananchi yaliyokusanywa na Warioba.

Tulikataa kubariki unajisi ule, na ndio ule mchakato ulipofia. Kwa hiyo, tunataka mchakato huu urejee.

Na tunamwambia Mama Samia Suluhu [Hassan], anavyozidi kuchelewesha jambo hili, linazidi kuleta mpasuko katika nchi.

[Rais Samia] anapolichelewesha jambo hili anachelewa kuwaunganisha Watanzania. [Lakini sisi Chadema tunataka] tujenge Taifa moja lenye kupendana na kuheshimiana…

Tutafanya mikutano ya hadhara kwa mujibu wa sheria. Na sheria ya vyama vya siasa na Katiba ya nchi vinatupa ruhusa hiyo.

Na namna ambavyo mama [yetu Rais Samia] na CCM wanazidi kuchelewesha kutafuta mwafaka katika Taifa hili ndio tutatoka kwenye hatua ya mikutano ya hadhara na kwenda kwenye maandamano.

Tutajenga [na kutetea hoja yetu] hatua kwa hatua, kwa sababu tunawapa muda. Tunao wenzetu upande wa pili hawaheshimu [haki] kabisa, wala hawajutii [kuzivunja].

Tume ya uchaguzi ambayo imevuruga uchaguzi wote wa mwaka jana [lakini] leo bado kuna watu bado wako kwenye ofisi za umma. Wezi wa kura kabisa hawa.

Wamevuruga uchaguzi wa nchi nzima, lakini hadi leo wako kwenye ofisi za umma. Watu waliowatesa, waliowaua watu, waliompiga risasi Lissu, bado wako serikalini.

Hakuna hatua za maana zinazochukuliwa dhidi yao. Watu wanamwona Sabaya mmoja ametolewa kafara hapo.

Lakini huko serikalini wapo watu chungu mzima wamebambikizia watu makosa huko kwa DPP, wamehukumu watu kwa makosa ambayo ni ya kubambikiza.

Lakini hakuna hata mtu mmoja anayechukuliwa sheria. Tutaendelea na hali hii mpaka lini?

Kuna mambo mengi ya kihuni yanafanyika katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Yakiwemo kuwahifadhi wabunge wale ambao ni wabunge haramu wa chama chetu.

Mama [yetu Rais Samia] anayaona hayo anakaa kimya, halafu anataka Chadema wawe wastaarabu.

Anataka ustaarabu wa namna gani zaidi ya huo [wa kufanya makongamano, mikutano ya hadhara na maandamano]?...

Tutafanya kikao cha Baraza Kuu la Chadema mwishoni mwa mwezi huu, tarehe 31 JUlai 2021, mkoani Mbeya.

Na baada ya kikao hicho tutaanza kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima kwa mujibu wa sharia na Katiba.

Kama mama ananipa pole kwa kufiwa, pia anipe pole kwa wanachama wangu kufungwa, kufilisika na kuteswa.

Ni miezi minne sasa, Mama hajaona sababu ya kutuona ili kuzungumza na kutufuta machozi. Hatuwezi kumsubiria, tutakutana barabarani….

Napenda kuwatangazia wanachadema. Kazi ya kudai Katiba Mpya siyo lelemama. Hatuwezi tukaendelea na ule utaratibu wa zamani.

Tuna haki ya kukutana, tunakamatwa, tunapigwa, tunashitakiwa, tunasoteshwa mahakani miaka miwili, miaka mitatu, kisha tunakuja kuachiwa huru.

Au tunahukumiwa kifungo ambacho ni batili na rufaa zote tunashinda, halafu hakuna compensation (dhamana).

Nimesema kama wanataka kuwaweka wanachadema ndani kwa hoja hii ya Katiba wapanue kwanza magereza….

Tuko tayari wote tuwekwe ndani na wala hatutaomba dhamana….

Jana ndugu waandishi wa Habari tulikataa watu wetu wasitoke ndani kwa dhamana. Tuliwambia msitoke ndani kwa dhamana. Polisi wakaanza kuhaha, tokeo wenyewe mjidhamini wenyewe.

[Tukasema] khaa, nyie mliowakamata [twambieni] wana makosa gani hawa?

Hatutaondoka hapa Mwanza na wiki hii tutafanya kongamano kubwa hapa Mwanza, sisi viongozi hatutaondoka Mwanza.

Na kama polisi wanataka kutukamata basi waanze kunikamata mimi Mbowe. Tutafanya makongamano haya nchi nzima hadi tupate Katiba Mpya...

Tunatambua serikali ijayo itakuwa ni ya Chadema. Lakini, tunataka serikali ya Chadema iongozwe na Katiba Mpya iliyotokana na wananchi...

Nchi sasa hivi inaongozwa na decree za Rais [kauli za mdomo kutoka kwa Rais], wala sio executive orders [kauli za maandishi yaliyosainiwa na Rais ili yatumike kama sheria].

Rais Magufuli alisimama Dar es Salaam akasema navunja jiji la Dar es Salaam kinyume cha sheria kabisa. Hii ni impunity (kunajisi sheria).

Na akasema hakuna kumchagua Meya, hakuna kumchague Mkurugenzi, wewe utakuwa Meya, na wewe Mkurugenzi. Vitu vya ajabu.

Na hamna aliyesema [lolote] mpaka leo. [Rais] Samia ameningia madarakani [na hajarekebisha jambo hili]...

Rais wa nchi leo ana madaraka makubwa kama Mungu. Yaani kila kitu tunategemea aseme Rais. Haiwezekani...

Hapa Rais akisema kitu inakuwa ni amri. "Eeh, mikutano ya hadhara tusubiri kidogo" [Mbowe anamnukuu Rais Samia kwa kumgeza uongeaji wake lakini bila kumtaja jina].

Eti hiyo ni amri imeishatoka. Mfyuuu! [Mbowe anasonya, huku akionyesha uso wa mtu aliyeona kinyaa].

Kwa hiyo nasema, sisi tutaendelea na kudai mikutano, hatutachoka. Tutarudia, tutarudia, tutarudia. Kuna siku kitaita.

Tusifikiri maisha ya nchi yako static (yamesimama). Kuna movement (vuguvugu). Tunakwenda, tunakwenda, tunakwenda taratibu.

Kuna siku itafika tipping point (hatua ya nguvu ya umma kupindua nguvu ya watawala).

[Hatimaye] kinachotokea South Africa (Afrika ya Kusini) ndio mtakiona Tanzania.


======MWISHO WA NUKUU======

Haya ndiyo nimeweza kuokota kutoka kwenye video zilizosambazwa mitandaoni.

Kwa ufupi, sasa ni wazi kwamba, ajenda ya Mbowe sio Katiba Mpya pekee.

Katika urefu na upana wake, kinachotekelezwa ni zoezi la kupinga uhalali wa serikali ya awamu ya sita kwa kutumia mgongo wa ajenda ya Katiba Mpya.

Kwa hiyo, swalilinazuka: Kama Mbowe hatambui uhalali wa serikali ya awamu ya sita, anataka "mwafaka" upi hasa? Hili linahitaji ufafanuzi zaidi.

Amelalamika kuwa "Mama hajaona sababu ya kutuona ili kuzungumza na kutufuta machozi." Je, Mbowe anataka serikali ya mseto? Hili linahitaji ufafanuzi zaidi pia.

Lakini kitu kimoja kimenishangaza. Amekuwa kama mwanachama wake Mdude Chadema. Anataka kukaa meza moja na Rais Samia, lakini anamsonya hadharani.

Kitendi cha kusonya ni aina mojawapo ya offensive, insulting and abusive language (offinabus).

Kwa ujumla, kitendo cha mwanamume kumsonya mwanamume mwenzake, au mwanamke kumsonya mwanamke mwenzake, kinaweza kuwa kidogo.

Lakini, kitendo hiki kinapofanyika kati ya jinsi mbili tofauti, mwanamume dhidi ya mwanamke au kinyume chake, kinabeba maana kubwa. Kinageuka unyanyasaji wa kijinsia. Mbowe amekwenda mbali sana.

Kwa ufupi, ni maoni yangu kwamba, sasa Mbowe ametangaza "Operesheni Ukuta" Part Two, hata bila kutilia maanani sababu za kufeli kwa "Operesheni Ukuta" Part One.

Ameshindwa tena kutambua kisigino cha serikali ya Achile kiko sehemi gani katika mwili wa serikali hiyo.

Naona anarudia makosa yaliyofanywa na Chadema wakati wa "Operesheni Ukuta" Part One.

Nimefanya uhakiki hoja ya Mbowe kwa ukamilifu
HAPA.
 
Mbowe kama atafanikiwa kwa hii ajenda

Atakumbukwa na vizazi na vizazi kwa kusimama imala kwa muda mrefu kutetea haki.
 
Mbowe ameshindwa kabla hajaanza

Mama Amon kuwa mkweli kuwa CCM wanaifanya chadema iwe ndani ya kuti kavu kila uchao.

USSR
 
Back
Top Bottom