BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,015
Date: 6/20/2009
Spika aweka kiporo kombora la Dk Slaa
AITAKA SERIKALI ITOE MAELEZO IFIKAPO JUMATATU
Spika aweka kiporo kombora la Dk Slaa
AITAKA SERIKALI ITOE MAELEZO IFIKAPO JUMATATU
Ramadhan Semtawa na Tausi Mbowe, Dodoma
Mwananchi
Mwananchi
ALIANZA na mbunge wa Nzega, Lucas Selelii na jana Spika wa Bunge la Muungano, Samuel Sitta aliahirisha majibu ya swali la Dk Willbrod Slaa aliyehoji sababu za kutokaguliwa kwa makampuni ya Buhemba Gold Mine (Meremeta) na Tangold.
Selelii alihoji kama serikali imeshaanza kutumia fedha za bajeti ya mwaka 2009/10 kwa kutekeleza mradi wa upanuzi na ukarabati wa barabara ya Chalinze-Segera kabla ya kupitishwa wakati alipoomba mwongozo, na Sitta alijibu kwa kuitaka serikali impe maelezo, lakini hadi leo majibu hayo hayajatangazwa.
Jana Sitta aliahirisha majibu ya swali la Dk Slaa, ambaye ni mbunge wa Karatu aliyerejesha Bungeni suala tata la kampuni hizo mbili wakati alipouliza sababu za kutokaguliwa kwa Meremeta na Tangold.
Katika swali hilo namba 76, Dk Slaa alisema kuwa hotuba ya waziri mkuu kivuli kwa Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), aliyoitoa bungeni Juni, 2007 ilieleza juu ya ubadhirifu mkubwa uliofanywa na makampuni ya Meremeta na Tangold.
Dk Slaa pia alisema kwamba ubadhirifu huo ulibainika kwenye makampuni ya Mwananchi na Deep Green Finance Co., na kwamba kiasi kinachodaiwa kufanyiwa ufisadi ni zaidi ya Sh215 bilioni.
Na baadaye alihoji: "Ni lini kampuni hizo zitafanyiwa ukaguzi wa kina kama ilivyofanyika kwenye akaunti ya EPA ili kubaini ubadhirifu huo uliohusisha uhamisho wa fedha kutoka Benki Kuu (BoT) na vyombo vya umma kupitia NBC Corporate Branch DSM na Ned Bank ya Afrika Kusini."
Dk Slaa aliuliza ni sababu gani za msingi zilizofanya kuchukua muda mrefu kuanza ukaguzi wa kina hata pale tuhuma hizo zilizopigiwa kelele na jamii na hata kamati mbalimbali zilizoundwa kuchunguza tuhuma hizo.
Baada ya kuuliza swali hilo la msingi, Spika Sitta alitoa maelezo badala ya kumruhusu Waziri wa Fedha na Uchumi kulijibu.
"Hili swali lililoulizwa na Dk Slaa ni zito, inabidi serikali ipate muda wa kuandaa majibu ya kutosha, kwa hiyo naliahirisha hadi Jumatatu liweze kujibiwa," alisema.
Hatua hiyo ya Spika Sitta ni mwendelezo wa danadana za kutoa maelezo kuhusu kampuni hizo mbili Tangold na Meremeta, ambayo inahusishwa na Jeshi la Ulinzi wa Wananchi (JWTZ).
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, aliapa kutotoa maelezo kuhusu suala hilo la Meremeta hata kama akisulubiwa.
Tayari pia ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mwaka huu imeshindwa kukagua Meremeta na Tangold.
Utata mkubwa uliopo Meremeta ambayo inamiliki mgodi wa dhahabu Buhemba, pamoja na tuhuma za ufisadi ni utata wa wanahisa.
Kamati ya rais ya kuishauri serikali kuhusu usimamizi wa sekta ya madini ilitilia shaka malipo kwa kampuni hiyo na kuitaka serikali kufanya uchunguzi wa kina juu ya uanzishwaji wa Tangold na umiliki wake katika kampuni hizo.
Pia serikali ilitakiwa ichunguze uhalali wa malipo ya dola 132 milioni za Marekani yaliyofanywa na Benki Kuu (BoT) kwa benki ya Nedbank ya Afrika Kusini.
Kamati hiyo pia ilipendekeza serikali ichukue jukumu la kuhakikisha mgodi wa Buhemba unafungwa kwa kuzingatia sheria na taratibu zinazohusu ufungaji wa shughuli za migodi na kuhakikisha kuwa taratibu za kurejesha mazingira katika mgodi huo zinafanyika.
Kamati hiyo iliundwa na Rais Jakaya Kikwete, Novemba 12, mwaka jana na kuipa muda wa miezi mitatu kukamilisha kazi yake.
Ilikuwa chini ya uenyekiti wa Jaji Mark Bomani ambaye ni Mwanasheria Mkuu mstaafu na Wakili wa Kujitegemea na ilikuwa na wajumbe wengine 11, wakiwamo wabunge wanne.
Hotuba yenyewe hii hapa:
(download attachment)