Ulongupanjala
JF-Expert Member
- Apr 9, 2013
- 7,718
- 12,372
Habari za asubuhi ya leo?
Naandika kwa masikitiko makubwa.
Jirani yangu hapa kwenye kota za Saruji Tanga amefiwa na mtoto wake wa kiume wa form four aliyekuwa anasoma Shule ya Sekondari ya Maweni kisa ni UZEMBE wa Madaktari na Manesi wa Hospitali ya Mkoa Bombo.
Mgonjwa alifikishwa Jumanne akiwa na upungufu mkubwa wa damu (damu 2) akawekewa damu akiwa mapokezi emergency baadaye akapelekwa Wodini na ndugu kuzuiwa kulala na mgonjwa wao. (Kwanini ndugu wa mgonjwa wazuiliwe kulala na mgonjwa wao huku mgonjwa mwe nyewe akiwa hajitambui kwa lolote)?
Pia kuna dawa zilinunuliwa nje ya hospitali nazo hakupewa kijana wa watu hadi amekufa.
Jumatano usiku majira ya saa 7 tarehe 18/19 kijana akafariki kutokana na kutoongezewa damu wala kupewa dawa.
Mwili bado upo mochwari kusubiria taratibu za kusafirisha kwenda Morogoro kwa mazishi hapo kesho.
Niwaombe kwa dhati kabisa Waziri wa Afya na timu yake kufanya uchunguzi wa kifo na kuwachukulia hatua Madaktari na Manesi wazembe sana wa Hospitali ya Bombo.
Yaani baada ya kuona hali yake mbaya wakazuga kumwekea oksijeni ambayo ilisababisha mishipa ya masikio na ngoma kupasuka na kuvujisha damu.
Yaani mtu ana upungufu wa damu uliosababishwa na malaria + UTI wao wanamwekea oksijeni ndio udaktari wa wapi?
Inaumiza sana watu kutothamini uhai wa wengine.
Familia imesema nao watatumia njia za asili kuwafikia wahusika.
Majibu ya Serikali soma hapa: Tanga: Serikali yaunda timu kuchunguza madai ya uzembe Hospitali ya Bombo yaliyosababisha kifo cha Mwanafunzi