Hospitaiili ya wilaya Lushoto wakataa kumpa kitanda mgonjwa aliyevunjika mguu

Mzalendo120

JF-Expert Member
Jul 2, 2022
1,408
1,824
Yupo mgonjwa aliyepata ajali ya kugongwa na pikipiki na amevunjika nmguu. Tangu mapema saasita mchana hadi saa kumi na nusu hawataki kumpatia mama huyo kitanda wamemuweka mapokezi eti wanadai anatakiwa kupelekwa hospitali ya Bombo.

Mama huyo familia yake wamechelewa kupata taarifa na aliyesababisha ajali amewekwa ndani na polisi maana ndio mtu pekee kwasasa ambae angempatia hata huduma ya chakula Pale mapokezi wamemuanikatu mama wa watu anataabikatu. Hivi nikwanini nchi hii inawauguzi wenye mambo ya hovyo?

Mtu kama atapelekwa Bombo si mumpe kitanda wakati familia yake ikisubiriwa? Huyo mtu hapo mapokezi amekataa kabisa kutoa msaada kwa huyo mama. Mamlaka fanyeni ufuatiliaji. Mkurugenzi fuatilia uozo huo maana hiyo ni aibu kubwa kwenu viongozi na maumivu makubwa sana kwa huyo mama

Update
Mgonjwa alipata matibabu kama huduma ya kwanza na wamempa kitanda. Wamefikia hatua hiyo yakumpatia mgonjwa kitanda mara baada ya kuona habari hizi mtandaoni. Tena wamemuuliza mgonjwa nani aliyefikisha hizi habari mtandaoni? Yupo wapi? Nani alilalamika mpaka habari zikafika huko? Kwanini mamabo madogo yanafanywa kuwa makubwa?

Hiyo hospitali inasemekana wana nyanyasa sana wagonjwa,hakuna dawa badala yake zipo kwenye duka nje hapo. Mamlaka fuatilieni wizi wa dawa katika hospitali ya Lushoto,uongozi mbaya,unyanyasaji wa wagonjwa na ufanyaji kazi kwa mazoea.
 
Dunia ina mambo na walimwengu na mambo yao. Naswali na kuomba_ ehee Mungu mkuu wa mbingu na nchi naomba baraka nyingi sana niwe na safari nyoofu na salama hapa duniani.
 
Dunia ina mambo na walimwengu na mambo yao. Naswali na kuomba_ ehee Mungu mkuu wa mbingu na nchi naomba baraka nyingi sana niwe na safari nyoofu na salama hapa duniani.
Mungu abariki hiyo lakini ombea hao wauguzi pia
 
Back
Top Bottom