Hosea ameathiri maisha yangu na familia yangu!

Wakuu watu wangapi iwa tunashuhudia wanabambikiwa kesi??Mbona mnataka kuleta mijada isiyo ya lazima tunaona watu wanabambikiwa bangi mfukoni na polisi kesi kibao za kubambikiwa.........cha mhimu hapa tufanyaje kumkoma Hosea aliye mwalibia maisha Zephania ...huku yeye akipeta.Hivi na kwa nini hili swala la huyu mwandishi halipewi uzito wa aina yake naona vyombo vya habari vimekaa kimyaaaaaa....


Kwa ufupi msicheze na Hosea!!! Ni Mafia ni hatari!!!! Pamoja na yote mnayolaumu huyu mwandishi but Hosea alijua anachokifanya!!! Na for sure ni case iliyotengenezwa.

Kwa taarifa ni kwamba Hosea as among the Fisadi's in the list of shame na wale wote waliotajwa kuwa mafisadi kwenye vyombo vingi vya habari wako katika mpango mzito sana wa kuwatafutia kesi owners of the media houses and their editiors. So please, kwa wewe unayeitwa mwandishi wa habari au owener au kama umewahi kutoa habari mbaya za fisadi kaa chonjo sana. They are plannig for a remarkable revenge. Take it from me.

Do not accept the so called cheap invitations!!!! Always ishi kimachale machale hasa pale ambapo unajua unafanya kazi ya kugusa binadamu mwingine ambayo ni sensitive kama issues zote za ufisadi and the like.

Pia kuwa makini na wale wanaokuzunguka ikiwemo marafiki. Fisadi huwa anatunia mbinu nyingi kwa sababu ana pesa. Na fahamu pesa ni kishawishi kikubwa sana kwani wengi wetu tuna mahitaji mengi na pesa yetu ya halali haitoshelezi. Be blessed and take care.
 
--- sijui kama huku ni kutaka kukata rufaa baada ya kutumikia kifungo, au ni personal encounter stori iliyoandikwa kwa ajili ya kuuzwa na mtu kujipatia kipato kama vile ambavyo matabloid ya ughaibuni huwa yanafanya kwa baadhi ya watu wanapotoka jela...

--- kama ni stori iliyolenga kuingiza visenti hapa bongo, basi wameiwahisha kuitoa. wangekaa chini na kuiandika vizuri kisha kutoa kitabu tu, hapo nami ningekinunua.

--- hata hivyo katika sakata lote hili kitu ambacho nina uhakika nacho ni kule kwa ndugu Musendo kwenda jela na kurudi uraiani ghafla kukutana na some of the new Big BOYZ in town; JF na KLHNews!!!! Trial (post-trial) by media couldn't be better!!!
 
kama hii habari ya kubambikiziwa kesi ni kweli inauma sana!!! na kwa nini ukubali kwenda kuonana na Hosea? kama alikuwa na shida angekuja ofisini kwako. na kama ilithibitika alitoa rushwa basi hiyo habari ilikuwa ya ukweeli

Ukiwa mwandishi wa habari huna mipaka

Kwani kuitwa hotelini sio hoja, ziko issue nzito na kibao ambazo huwa haziibuliwi kwenye ofisi ya gazeti bali sehemu fulani.

Na huo ndio uandishi wa habari.
 
kama hii habari ya kubambikiziwa kesi ni kweli inauma sana!!! na kwa nini ukubali kwenda kuonana na Hosea? kama alikuwa na shida angekuja ofisini kwako. na kama ilithibitika alitoa rushwa basi hiyo habari ilikuwa ya ukweeli

nadhani alikubali kwenda kuonana naye kwa kuwa alikuwa na habari inayomhusu, eneo la kukutana hiyo sio tija lakini mwisho wa siku alitakiwa apate uthibitisho wa habari aliyonayo.

na suala la kesi za kubambikiwa sio kitu kigeni, watu wanahangaika magerezani kwa kesi sizizokuwa zao na watuhumiwa halisi wanapeta mitaani,. Sheria inaweza ikawa upande wako lakini haki ikanyang'anywa na walioshikilia mpini.
 
Nimetaka kujua huko nyuma kama waandishi wengine na watetezi wa haki walimsusia mzee Musendo hii kesi ama la, bahati mbaya hakuna aliyejibu, labda hawapo wenye habari zaidi miongoni mwetu. Nikakumbuka pia kuwa wakati mwandishi Adam Mwaibabile "mwana" alipobambikiwa kesi na mkuu wa mkoa Nicodemus Banduka, waandishi wenzie walisimama kidete kumtetea hadi akaachiwa huru licha ya kuwa alishaanza kutumikia adhabu yake ya kifungo jela. Sasa hapa kwa mzee Musendo nini kilitokea, alisuswa? Na kwa nini ikawa hivyo?
 
Hii habari haikuleza tu kama Hosea alikuwa shahidi kwenye hiyo kesi which I doubt. Nafikiri hii story iko twisted kidogo. Lakini pole sana kwa huyu bwana, ni kweli future yake imekuwa interupted sana.
 
Wandugu,

'Chifu' Musendo alikuwa kwenye malumbano na PCB kutokana na kuandika kwamba 'hata PCB nao wanakula rushwa'. Wakati malumbano hayo yakiendelea, ghafla tukasikia 'Chifu' kakamatwa kwamba ameenda kuwaomba PCB rushwa. Ni PCB na Musendo peke yao wanaoweza kujua ni nini hasa kilichotokea: lakini kwamba wakati wanalumbana, na kupelekana polisi, kutokana na kauli kwamba 'PCB nao ni wala rushwa', halafu Musendo aende kuwaomba PCB haohao rushwa waliokanusha vikali ulaji rushwa, itakuwa kweli kabambikiwa kesi, au Musendo ni kichaa kama baadhi ya watu walivyodai.

Nimefanya kazi na Musendo nikiwa mwandishi-Chinga, yeye akiwa mhariri (wa makala?). Inakuwa vigumu sana kwenda na nadharia ya kwamba kweli alienda kuomba rushwa PCB wakati wanalumbania madai kwamba PCB nao ni walaji. Lakini madaktari wanasema 'kila mtu ni kichaa, tunapishana 'digrii' ya huo uchaa!' Labda kama 'mgawo' wake wa ukichaa ulimtuma hivyo...

Natumia fursa hii kukupa pole nyingi Musendo.

Kusemaga ukweli, baada ya Musendo kukumbwa na kashkashi hiyo, ni moja ya sababu inayofanya nitundike daluga la uandishi wa kejeli, kwa vile siwezi kuvumilia kuona mambo yanapelekwa harijojo, jambo ambalo litahatarisha maisha, kwa vile itabidi kupayuka hata pale inapobidi kukaa kimya.
 
Jerry Muro angalia "scenario" hii hapa chini:
"Tulizungumza kwa muda na ghafla Hosea alinyanyuka na kulikuwa na watu kama sita walioingia na kuzunguka meza yetu na mmoja alimwingiza mkono mfukoni. "Wakaniambia nitulie nisifanye vurugu yoyote na kuwa walikuwa wanashuku nimepokea rushwa, wakaniamuru nitoe vitu vyote mfukoni na mimi nilitelekeza kwa kutoa kila kitu pamoja na pesa nilizokuwa nazo."Anasema baada ya kuweka mezani walikagua na kuweka pembeni baadhi ya pesa na kusema kuwa alikuwa na pesa zao kiasi cha Sh100,000 na hivyo aliamriwa kuwa yuko chini ya ulinzi. Baada ya hapo akasema kuwa walimchukua na kutoka naye nje wakidai kuwa na mahojiano zaidi.

"Tulipofika nje nikawaomba nimtaarifu dereva wangu ili arudi ofisini, lakini hawakukubali na waliondoka na mimi hadi polisi Oysterbay ambako nililala huko," anasema.

"Pia nilisikia kuwa hata dereva wangu alikamatwa baadaye na yeye alilala Central Police kwa kosa la uzururaji nadhani."Anasema kwa mlolongo huo wa matukio alijua kabisa kuwa hawa watu hawakuwa na nia njema naye na mpango huo ulikuwa kumkomoa, kwani dereva hakuwa na kosa lolote.

"Kesho yake nilipata dhamana na wakaniambia kuwa siku inayofuata niripoti ili nifikishwe mahakamani kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa."Tulipofika mahakamani nilitakiwa kuwekewa dhamana ya Sh500,000 taslim na kwa kuwa ofisini walikuwa wanashughulikia hilo, hawakusubiri na kunipeleka Keko ambako nililala kwa siku tano kabla ya dhamana kukamilishwa," anasema.

Kwa kuwa POLISI, WAENDESHA MASHITAKA, MAHAKIMU NI WALE WALE - My younger brother, hii case yako itakwenda mbali - inastahili ujiandae!
 
Hivi mtu ukiwekewa pesa mfukoni, si ina maana wewe hujawahi kuzishika hizo pesa. Je Tanzania hatuna utaalamu wa kuthibitisha kitu kama hicho?

Habari ya huyu mwandishi inaweza kuwa kweli lakini pia inawezekana kabisa alichukua hiyo laki moja toka kwa Hosea na hivyo kuishia pabaya.

Kama ni kweli alibambikiziwa hizo pesa basi Tanzania tunaelekea kubaya sana.

Hivi sheria zetu za kumpekua mtu zikoje? Yaani mtu anaweza kuja bila kibali chochote na kuanza kukupekua? je ukikataa itakuwaje?

Hii ni Tanzania na kila kitu kinawezekana ukiwa na pesa au dola!!! sijui kwanini nashawishika kwamba huyu jamaa alibambikiwa na kama ni kweli then we are in deep shit!
 
I mean, ni vizuri kujua shuruba za wafungwa, lakini stori za prayer times au meal schedule za vyakula vya jela na daily regimen za lupango ni zile zile. Bondo na Ndondo. Kulima na Wanyampara. Funza na Uji. Kuhesabiwa na Kulala. Jumapili Nyama. Sigara ni dili. Kwishne. Wamarekani wanasema, same ol' shit!

Kwa hiyo Mwandishi cut that extraneous stuff, tuambie kesi ya Hosea mwenyewe iliishaje, na muulize ex-Mhariri atueleze vizuri alikamatwa kamatwaje?

.
Kuhani,
Mengi ya uliyouliza ni sawa na yanahitaji majibu, tunakubali kuwa mbinu za kupandikiza vielelezo (evidance planting) ni mashuhuri Duniani kote na zinatia fora katika nchi kama zetu, lakini muhusika nae (Mwandishi aliemaliza kifungo) anawajibika kuweka kila kitu wazi juu ya swala zima dhidi yake na Hosea badala ya kuchagua ni kipi atue na kipi azuie, aweke kila kitu mezani na sisi tuchambue na kutoa maoni yetu kwa ukweli huo.
 
Kama kweli ulionewa fungua kesi ya madai,lakini kumbuka sheria ni kipofu.
pole sana bro.Anza upya hakuna jinsi ya kurudi kama mwanzo.
 
Pole sana mzee Musendo, hili na mengine ya aina hii ndio iwe dira yake kutuelimisha kwa facts. Yote maisha mkuu Musendo
 
hivi ndugu yetu Hosea anajisikiaje kama kweli habari hii ni ya kweli? maana nasikia dhambi nyingine hulipwa hapa hapa duniani.............................

Hosea hawezi kujisikia vibaya. Tabia ya huyo jamaa ni ya ajabu sana. Tatizo ni nchi tu lakini ukifuata ukweli, Hosea hakustahili kuwa Mkuu wa taasisi kama PCCB.

Wakati ule ni kweli kabisa alikuwa mula rushwa mkubwa. Pamoja na cheo hicho alikuwa na ofisi yake binafsi ya kisheria na ilikuwa kwamba ukitaka kushinda kesi za PCB (wakati huo) lazima upate mwanasheria toka ofisi yake hiyo.

Labda tu Onyo kwa waandishi wa habari ni kwamba wasipende sana mazungumzo ya faragha na watu wanaowachunguza, ni Hatari. Mwandishi siyo spy kwa nini uende hotelini kwa mazungumzo mukiwa wawili tu na wakati huo huo umesha muandika? Hiyo ndo inatia wasiwasi kwamba waandishi wanaangukia mtego wa kutaka kufaidika kwa habari wazijuazo.
 
nchi hii ni ngumu, wanaweza kurusha kifuko cha heroin au bastola bustanini wakaja kusachi ghafla wakasema mzigo ni wa kwako....

hii kitu inaweza kuwakumba wazee wa hapa jamvini kama mko tz.....

ni kumwomba mungu....na kuacha kucheza na upuzi hasa ukiishakuwa bidhaa adimu....

mambo ya kunywa ovyo ovyo....kukaa na watuhumiwa mnajadili nini?

pole sana mzee....tumekusikia...tunasuburi kitabu

also see if there is a possibility ya kulianzisha na kudai compensation!
 
nimeisoma stori na kusoma michango ya wengine, kuna mengi ya kujiuliza ktk hii stori


kwa kweli, jamaa kama amechinjwa basi kuna mapungufu mengi ambayo na yy aliyafanya kuwarahisishia wachinjaji kumchinja kirahisi
 
Inasikitisha sana sana hii story na unyanyasaji mkubwa sana wa wakuu wa serikali na vyombo vya dola!!!hii stori ilitoka miaka 3 nyuma sasa imerejewa tena,sijajua kama jamii ilimsaidiaje bwana Musendo kurudi kwenye mstari japo si kama alipoachia alipofungwa hasa mwajiri wake wa zamani maana alikuwa anapambana akiwa kazini....
 
Ni kawaida kwa watu wasio na maadili kama Polisi, TAKUKURU na taasisi lukuki za serikali. Hili lililomapata huyo Mwandishi ni tone tu katika bahari ya unyanyasaji, dhuluma na uharamia ulioko ktk kila kona ya Tz.

Ni funzo kuwa hakuna raia aliye salama na wauaji hao. Na kama ni system basi hii ni mafioso
 
Haya ndio yanadhihirisha jinsi taasisi nyeti kama hizi hata uzipe meno ya sheria gani bado zimejaa watu wa ajabu sana!
 
Back
Top Bottom