Hosea ameathiri maisha yangu na familia yangu!

Katika demokrasia ya kikatiba kuna kile kinachofahamika kama Penal Proportionality ambapo adhabu hupashwa ilingane na kosa linalodaiwa kutendeka. Kwa hiyo, inashangaza kwamba mtu anayedaiwa kupokea rushwa ya Tsh 100.000 anaweza kupata adhabu sawa na Afisa Mwandamizi wa benki (BoT), aliyehusika katika kashfa ya ujenzi wa minara-pacha ya benki hiyo na ambapo mamilioni ya fedha yalikwapuliwa. Hali hii inaeleza nini?

Pole sana Ndugu Musendo na wanataaluma wengine mliopata misukasuko ya namna hii katika utendaji wa majukumu yenu. Ingelikuwa vizuri kujua kama Ndugu Msendo ameisha mudu ku patch up maisha yake upya, baada ya jinamizi la kuwa jela miaka yote hiyo kwa mashtaka ya kughushi.

Ludovick S Mwijage
ludovick.mwijage@gmail.com
+ 45 50 29 04 27 (kiganja)

By the way huyu Bw. Musendo yuko wapi kwa saas na anafanya nini? Any update plz
 
Kwanini jamaa nae alikuwa anaenda kukutana nao hotelini, si angemwambia wakutane ofisini kwa Hosea au ofisini kwa huyu jamaa inaleta maswali mengi bana .wajifunze waandishi...
 
Ndugu Maundumula, kuna dhana kwamba kheri kukataa neno kuliko kutaa wito. Na siyo mara nyingi watu kuwa arresting officers katika kesi inayo wahusisa wao. Katika mazingira ya namna hii, binafsi ninaridhika kwamba uwezo wa Ndugu Musendo kufungwa kwa mashtaka ya kughushi ni mkubwa mno kuliko vinginevyo. Usisahau baadhi ya wanasiasa mashuhuri nchini mwetu walioyazungumzia masuala kama yale Ndugu Musendo aliyoyazungumzia kwenye makala yake, bado wanaendelea na matibabu huko India kwa maradhi ambayo huenda chanzo chake ni kulishwa sumu. Hapana, baadhi yetu tungelipenda kuona ushahidi zaidi kabla ya kuamini kwamba conviction ya Ndugu Musendo ilikuwa safe.
Kwanini jamaa nae alikuwa anaenda kukutana nao hotelini, si angemwambia wakutane ofisini kwa Hosea au ofisini kwa huyu jamaa inaleta maswali mengi bana .wajifunze waandishi...
 
bora ametoka salama huyu bwana,taasisi karibia zote za serikal hazifanyi kazi kusaidia wananchi,kila taasisi ina uchafu mkubwa sana-sasa huyu bosi ameamua kumbambikia kesi mhariri hadi akamsotesha mwenzie,jamani hii si dhambi kabisa.
ʞ@*&$##^& zao
 
Kwanini jamaa nae alikuwa anaenda kukutana nao hotelini, si angemwambia wakutane ofisini kwa Hosea au ofisini kwa huyu jamaa inaleta maswali mengi bana .wajifunze waandishi...
Yaani kwa maisha haya ya sasa-kama kuna mkulu au mtu yoyote ambaye yupo kwenye system akikuita mkutane hotelini kwa maswala ya kiofisi,ni bora ukatae,maana hotel kwao zimekua ndo "killing points"-maana hata kina gerry muro walimtega hivihivi
 
Ndio maana inchi hii imekuwa mwiba wa viogozi wetu, kumbe ndio ule msemo wa malipo ni hapa hapa unatimia.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom