Ndugu zangu tutofautishe kati ya sheria na haki. Watu wanaweza kutumia vifungu vya sheria halali za nchi mtu akapatikana na hatia au kuachiliwa huru, lakini bado ikawa haki haijatendeka kwa mhusika. Hivi ndivyo majambazi wanavyoachiliwa huru na waliobambikiziwa kesi wanavyofungwa. Wanasheria wanatumia vipengele vya kiufundi vya sheria na jinsi ya kucheza na maneno. Unaweza kushuhudia kabisa kwa macho yako mtu akitenda uhalifu, lakini unapoutoa ushahidi huo mahakamani unashangaa wanasheria wanaugeuzageuza hadi inaonekana kuwa ushahidi huo hauna nguvu, hakimu anautupilia mbali! Vivyo hivyo mtu anapobambikiwa kesi, kama mbambikaji ana utaalamu wa kutosha, ataubambika kiufundi kiasi kwamba mahitaji yote ya kisheria ya kumtia mtu hatiani yanakuwapo. Kwa nafasi kubwa aliyokuwa nayo Bw Hosea kipindi hicho na utaalam wa sheria alionao, sishangai hata kidogo kuwa alifanikisha kumfunga huyu Mzee Zephania, kwa hakika inasikitisha sana.
Ningependa kujua pia kama Mzee huyu alikata rufaa na majibu yake yalikuwaje. Na kama hakukata rufaa, nini kilimzuia kufanya hivyo? Nakumbuka mwandishi mmoja kwa jina Adam Mwaibabile aliwahi kubambikiwa kesi huko Songea na mkuu wa mkoa Nicodemus Banduka, akafungwa jela mwaka mmoja. Waandishi wenzie waliishikilia bango kesi ile na kukata rufaa, akaachiwa baada ya muda mfupi tu. Sasa sijui kwa huyu mzee Musendo waandishi wenzie na wanaharakati wa haki za binadamu walimsusa au ilikuwaje?