Hosea aligeuzia Bunge kibao

TAKUKURU wana wajibu wa kisheria kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma za kwamba Wabunge tumekuwa tukilipwa zaidi ya tunachotakiwa kulipwa kisheria. Wabunge hatuna kinga ya kufanya vitendo vya matumizi mabaya ya fedha za umma na hatua hii ya TAKUKURU itaondoa 'impunity'. Kwamba wanafanya hivi kwa visasi sio kweli. Ni wajibu wao. Uchunguzi huu unafanyika kwa Kamati zote za Bunge na sio hizi tatu peke yake. Hivi kama Mbunge analpwa pesa ili asafiri kwa siku 5, na yeye anasafiri kwa siku moja. CAG anagundua hilo katika ripoti yake, kwa nini TAKUKURU wasichunguze na kufungua mashitaka?

Tuwaache TAKUKURU wafanye kazi yao kwa mujibu wa sheria. Bunge pia tufanye kazi yetu ya kuwasimamia hao TAKUKURU ili watende mema. Hiyo ndio checks and balances.

Ndio maana umekuwa HERO kwa vijana wa kiTanzania...uko fair katika kila issue hata kama inakugusa wewe personally.
In my opinion naona PCCB waachiwe watimize wajibu wao na wabunge hawana immunity ya kushitakiwa iwapo watatenda criminal offence. And after all wao ndio wanaoisimamia serikali hivyo wanatakiwa wawe wasafi ili waweze kuisimamia serikali vizuri.
 
Back
Top Bottom